Samuel Sitta aunda Kamati ya maridhiano ya kuwasikiliza waliopiga kura za HAPANA

Mwigulu anakumbukwa Kwa ushauri wake juu ya 2/3 tuangalie kama 2/3 inapatikana kama haipatikani tusitishe shughuli zote watu wakasema ametumwa na UKAWA.
 
Samweli Sitta amewaundia kamati watu waliopiga kura za HAPANA hii ina maana gani kwenye uhuru wa watu kuamua, haina maana kuwa mtu akikaa bungeni muda wote lazima akubali katiba pendekezwa. Sitta anafanya ubakaji wa democrasia wazi wazi.
 
waliopiga kura za hapana kwa sura zote ndiyo wameomba wasikilizwe sababu ni nni?
Mkuu, Chabruma ametudokeza kwenye uzi wa yanayojiri leo kuwa hawa wa hapana wamefanya hivyo kwa SHINIKIZO. Wakisikilizwa watabadili muelekeo
 
waliopiga kura za hapana kwa sura zote ndiyo wameomba wasikilizwe sababu ni nni?

Mjadala umeshafungwa,hakuna cha kusikilizwa tena, nahisi kuna ushawishi mkubwa na rushwa unaendelea hapo,kura ni hiyari ya mtu kwa nafsi yake,kwa nini ashauriwe,tena na jopo la wana ccm, ni maajabu, na duniani kote kura ni mara moja tu,vinginevyo iwepo kanuni ya kuvuka asilimia hamsini ambayo hapo haipo,hapo ni thelusi mbili, itakuwa aibu kubwa kama watabadilisha maamuzi yao na kupiga kura mara ya pili
 
Sitta Ni mpuuzi,kwanini asiunde kamati ya maridhiano ili wajumbe waliosema NDIYO wakubaliane kuikataa katiba ya kihuni hii?
 
Mwigulu anakumbukwa Kwa ushauri wake juu ya 2/3 tuangalie kama 2/3 inapatikana kama haipatikani tusitishe shughuli zote watu wakasema ametumwa na UKAWA.
2/3 lazima ipatikane. Pasco katuambia kuwa isipopatikana itapatilizwa
 
Sitta Ni mpuuzi,kwanini asiunde kamati ya maridhiano ili wajumbe waliosema NDIYO wakubaliane kuikataa katiba ya kihuni hii?
 
waliopiga kura za hapana wondoke dodoma haraka manake maCCM hayaaminiki..
 
Sitta Ni mpuuzi,kwanini asiunde kamati ya maridhiano ili wajumbe waliosema NDIYO wakubaliane kuikataa katiba ya kihuni hii?
Mkuu, kamati ya mashauriano imeundwa naada ya wajumbe wawili kuomba kusikilizwa
 
...Katika hali ya kuonekana kuanza kukwama kwa katiba, m/kiti wa bunge la katiba ndugu Sitta ameunda kamati ya maridhiano kwa ajili ya kujadiliana na wale waliosema HAPANA. Hii ni njia ya kutafuta 2/3 ya kura.

mbona waliopiga kura ya ndiyo hawaundiwa kamati?si walitegemea ipite?sasa kuna ndiyo na hapana.ikiwa hapana kwanini kamati?si ijulikane ni hapana?
 
Sitta Ni mpuuzi,kwanini asiunde kamati ya maridhiano ili wajumbe waliosema NDIYO wakubaliane kuikataa katiba ya kihuni hii?

Hapo ndipo maajabu,alifikiri mwewe huwa hawaombi dua, hatimaye mwewe wamemtikisa, ni uhuni tupu unakiuka principle ya free election,viongozi wa UKAWA wasiiache hii ipite,waitishe press conference na kutoa kauli
 
Sitta alipotangaza kamati tu nikampigia simu jamaa yangu aliyepo mjengoni dodoma kujua kulikoni.
Hawa waliopigia kura ya HAPANA wametengewa dau la 15m kila mmoja ili wakubali kuwa wametishiwa ili kuwalazimisha kupiga kura za HAPANA. Kwahiyo wataomba kupiga kura upya.
Watu wawili kati ya hao wamekataa mchezo huo na kuna mpango wa kuongezewa dau.
 
Watoto wa Bavicha, Acheni kupotosha umma!!! Kuna Wabunge wameomba kusikilizwa kama special case. Sitta ameunda
kamati ili wapate haki yao.

Acha ufala mandla jr
Hata kama wameomba kusikilizwa ndio kura zao za jana za hapana zitakuwa ndio baada ya kusikilizwa?
Acha ufala
 
Taarifa iliyotolewa hivi punde na Mwenyekiti wa bunge maalum la katiba Mb Samweli Sitta, ametangaza kamati maalum ili kwenda kuwasikiliza na kuwahoji kwa upya wajumbe wote waliopiga kura ya HAPANA katika kikao cha jana, waseme kwa nini wakapiga kura ya hapana na huku wamehudhuria vikao vyote katika bunge hilo maalum.
Naomba kuwasilisha.

#Source : TBC1.
 
Back
Top Bottom