only83
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 5,343
- 2,525
Katika hali ya kuonekana kuanza kukwama kwa katiba, M/kiti wa bunge la Katiba nduguSamuel Sitta ameunda kamati ya maridhiano kwa ajili ya kujadiliana na wale waliosema HAPANA. Hii ni njia ya kutafuta 2/3 ya kura.
Wadau, amani iwe kwenu.
Muda mfupi uliopita, Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Sammuel Sitta ameunda kamati ya Mashauriano yenye Wajumbe 9 kuwasikiliza Wabunge wa BMK waliopiga kura ya HAPANA kwa Ibara zote siku ya Jana na leo. Anasema kuwa hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 36. Anasema kuwa kati ya wajumbe waliopiga kura za Hapana, Wajumbe wawili wameomba kusikilizwa. Kutokana na hali hiyo analazimika kuunda kamati hiyo ambayo amesema kuwa itaongozwa na Makamu Mwenyekiti Samia Suluhu Hassan. Wajumbe wengine ni;
Anawataka wajumbe kukutana mara moja ili wawasikilize wabunge walioomba kusikilizwa. Tuvute subira na kila kitu kitakuwa wazi kupitia mtandao huu wa Jamiiforums
- Rashid Mtuta
- Omar Yusuph Mzee
- Shamsi Vuai Nahodha
- Abood Mohamed
- Andrew Chenge
- Dr. Asha Rose Migiro
- Dr Francis Michael na
- Hassan Ngwilizi