robby one for really
Member
- Jan 17, 2013
- 29
- 8
Kwa kuanza naomba kuwapa pole woote wenye majukumu ya hapa na pale na Mungu wetu si mchioyo wa fadhira anaendelea kutujaaria uzima na afya njema. Naomba kwa wajumbe wa Jamii forum kufahamu mawazo pamoja na fikra zao juu ya mwenendo wa swala la Rasimu ya Katiba ambayo inaendeleza kuchanwa chanwa na wajumbe walio baki bungeni. Je kuna uhalali ya wao kuendelea kujadili kitu ambacho tayari rais na tcd walishafikia mwisho kuwa swala hilo litaendelea mwakani mara tu ya uchaguzi kumalizika. Hawaoni kuwa ni matumizi mabaya ya rasilimali za nchi yetu huku tukiwa na mambo rukuki ambayo yanatuhitaji kutumia fedha? Tena kwa kejeli kubwa nimemsikia Samweli sitta akisema kuwa hawa Ukawa ni Wacheza filamu za kuigiza huku akiwafannanisha na akina Anord Soziniga na wengineo kuwa wao hawawezi kuwababaisha kwa namna yeyote ile. Je huyu Samweli Sitta anamaslahi na Anahuruma na Wanyonge wa Nchi hii ambao hata hajui leo watakula nini na wataendeshaje maisha yao ya kila siku?