Mpwayungu Village
JF-Expert Member
- Jul 21, 2021
- 14,305
- 29,853
Uoga ni kitu kibaya sana kwenye hii Dunia. Ukitaka kukosa amani kwenye kila kitu unachokifanya hapa Duniani basi endekeza uoga. Umoja wa wakuu wa shule za sekondari Tanzanian (TAHOSSA) wiki jana walikuwa na mkutano wao jijini mwanza ukumbi wa Kwa tunza Beach jirani kidogo na Malaika Beach resort
Huu mkutano ulikuwa umejaa makada wa CCM tupuuu, yani viongozi wa serikali ni wachache ila viongozi wa CCM kama wote kuanzia shina, tawi mpaka taifa wote walijazana. Agenda kubwa ni Samia tuu mwanzo mwisho, yani mpaka semina inaisha Samia katajwa mara nyingi kuliko kitu chochote.. Mda wote waliweka mikakati ya kumpa sifa Samia huku shida zao zimetupwa kapuni
Walimu wakuu hawajitambui tu, yes nasema hawajitambui. Ebu fikiria huu mwezi unaenda wa tatu hawajapewa hata posho zao za madaraka (responsibility allowance), hapa Katikati kulikuwa na mitihani ya taifa form four na two, wasimamizi wa mitihani hulishwa chakula na mkuu wa shule Kwa kutumia pesa za mfuko wa shule (capitation grants), hizi pesa bado haijafika inabidi wakuu wa shule watumie pesa zao mfukoni kulisha wasimamizi kama huna pesa unaenda kukopa kausha damu
Hawa hawa wakuu wa shule wameenda kwenye semina lakini cha ajabu hawajalipwa pesa za semina (per diem). Kumbuka TAHOSSA wana mfuko wao ambao wakuu wa shule huwa wanadonate lakini cha ajabu semina yenyewe walimu wamechanga 60000 kila mmoja huku wengine wakitoka lindi na mtwara, songea na sumbawanga ni mbali saana wanakuja mwanza siku Tatu bila malipo yoyote Yale Kwa kigezo eti pesa watachukua kwenye mfuko wa shule, Kwa bajeti ipi Kati mfuko wa shule pesa zenyewe huwa kiduchu tu shule Zina madeni hadi aibu hapo hapo mpaka saizi pesa za elimu bure hazijaingia Sasa watachukua kwenye mfuko wa sweta au
Wakuu wa shule hawa hawa walipangiwa tarehe ya kikao itakuwa tar 10 mwezi huu lakini ajabu watu wamesafiri kutoka mikoa ya mbali wamefika mwanza wanaambiwa tarehe imeahirishwa Rais yupo na shughuli zingine (walikuwa wamemwarika awe mgeni rasmi) kwahiyo tarehe zikasogezwa, maanake inabidi ujue mwenyewe unaishi jiji la mwanza mpaka tar itakapofika ambayo ni siku nne zijazo au urudi ulipotoka huku nauli Zipo juu
Walimu wana matatizo kibao, mwisho wa siku semina yenyewe huyo Samia hakufika, wanashangaa anaingia Ndejembi, siku iliyofaya msonde baada ya hapo mchengerwa, waziri mwenyewe hata salamu za walimu hatoi anaanza na Samia oyeeee, nao panyabook wanaitikia, ajenda ni kumchukulia form ya urais Samia. Wakaanza kutoa akiba zao mfukoni hata pesa ya nauli wakakopeshana
Huu ni uonevu period!!