Samaki wenye sumu ya mionzi ya nyuklia waingia Dar

Najiuliza, hivi bahari ya hindi na maziwa yote, katika miaka 50 tumeshindwa hata kuvua chakula chetu mpaka tunaagiza samaki.! Kama tunaleta wawekezaji wa madini na magogo kwanini tusilete mwekezaji wa uvuvi.

Hapa kuna watu wa kuuliza, TFDA, Bandari, wiazara ya afya, waizara ya uvuvi.
Nchi inakwenda kwa solar energy, hakuna human input! kila kukicha afadhali skendo ya jana. mhh
Uvuvi ni kitu kizuri sana lakini uvivu ni hatari kuliko hiyo mionzi
 
Yaani kumbe TFDA & TBS wanafanya kazi kwa kuamini "documents"? Leo ndio nimeelewa kwanini Tz tunafanyiwa majaribio mengi ya dawa za malaria etc kabla hazijawa dawa bila wataalamu wetu kujihusisha. HAWAJIFUTU / HATUJIFUNZI kwa wenzetu? Ingekuwja China tayari hukumu.

Intelijensia na wathibiti wa ubora na viwango vya bidhaa zetu wote wapo kwenye "bizinesi azi yuzo".
 
Najiuliza mbona asasi binafsi zina taarifa kalikali kuliko huo usalama wetu? Hebu tazameni jamani, kampuni ya jijini inapakia tani 125 toka fukushima! Vuuuuuuu, mpooooo, mpaka tanzania-dsm. Samaki waliwe na watanzania baada ya kukataliwa japan. "Baba yetu uliye mbinguni jina lako... ufalme wako ufike...Uwiiiiii
 
Nashauri wahusika wanyongwe bse nia yao ni kutupa vilema vya maisha.
Nijuacho ulika kinachotokea ni mutation katika mwili wako so yataanza kuja madhara kama yale ya hiroshima na nagasaki.
Sometimes we need to be serious this is life and death jamani
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Tuliambiwa hatukusiki,kumchagua rais legelege na serikali yake ni maafa SASA MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMA
 
Ilikuwa kupanda bei ya mafuta na gharama za maisha, baadaye ukaja mgawo wa umeme, juzi tu matumizi ya rushwa kupitisha bajeti bungeni. Leo kuingizwa samaki wa sumu nchini! Jamani Tanzania inaelekea wapi? nchi ina viongozi kweli?
 
Licha ya madhara makubwa yanayoweza kutokea kwa afya za watanzania iwapo samaki hawa wataliwa, hata kabla hawajaliwa athari za kiuchumi zinatokea tayari.

Kwenye mahoteli makubwa haiyumkinii samaki wanaliwa kwa nadra baada ya kujulikana ujio wa samaki hao wa Japan.
 
Mi na familia yangu kitambo kbs nimewapiga BAN ya ku2mia samaki na nguruwe,nilishtuka vi2 kama hivi vyaweza vikatokea na kweli yameshafika. Wa2miaji mtashangaaa na roho zenu.
 
Jamani nimesoma gazeti la nipashe jpili,linasema kuna kontena 5 zenye uzito wa tani 25 kila moja,habari hizo zinasema samaki hao wametokea mji wa Fukushima ambao mji huo maji yake ndiyo yameathirika na mionzi baada ya vinu kulipuka,samaki hao walikataliwa Japan baada ya serikali ya japani kubaini wamevuliwa kwenye maji ya mionzi,ndio ikaletwa dar,imebainika makontena hayo yameshatolewe na TFDA,wizara ya afya na idara ya uvuvi kwa hiyo wana JF tujiandae wakati wowote tunakula sumu,tujiandae kupata saratani
Mmmh! Nchi hii nayo sasa inatisha. Hivi hao TFDA role yao si kulinda afya zetu? Sasa kupokea hayo makontena ya samaki wenye sumu ya mionzi ya nuklia ndio kutulinda au kutuua!
 
KHERI YA JUMATATU WANA JF!

Naomba mnijuze nasikia dar sasa kuna samaki wenye mionzi ya nuclear! kwa sababu hii ni hatari kwa uhai wa wananchi
 
jamani hivi kwa nini Tanzania tunaingiza samaki toka nje bahari yote hii, maziwa kibao, naumia sana kwa kweli
 
Jamani nimesoma gazeti la nipashe jpili,linasema kuna kontena 5 zenye uzito wa tani 25 kila moja,habari hizo zinasema samaki hao wametokea mji wa Fukushima ambao mji huo maji yake ndiyo yameathirika na mionzi baada ya vinu kulipuka,samaki hao walikataliwa Japan baada ya serikali ya japani kubaini wamevuliwa kwenye maji ya mionzi,ndio ikaletwa dar,imebainika makontena hayo yameshatolewe na TFDA,wizara ya afya na idara ya uvuvi kwa hiyo wana JF tujiandae wakati wowote tunakula sumu,tujiandae kupata saratani

Sasa hao TFDA na wenza wake kazi yao ni kuangalia vyakula vyenye matatizo na kuviruhusu kuingia au kudhibiti??kama wameona kwamba samaki wana madhara hawakustahili kuruhusu kontena hizo zifunguliwe hapa kwetu.
 
Ikiwa kampuni inaeleweka kwa nini wasishtakiwe?

Leo jioni kwenye radio moja nilisikia kama kampuni yenyewe imeanza na jina Alpha ...... au nimekosea?
 
Back
Top Bottom