Samaki wenye sumu ya mionzi ya nyuklia waingia Dar

ureni

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
1,261
526
Jamani nimesoma gazeti la Nipashe Jumapili, linasema kuna kontena 5 zenye uzito wa tani 25 kila moja,habari hizo zinasema samaki hao wametokea mji wa Fukushima ambao mji huo maji yake ndiyo yameathirika na mionzi baada ya vinu kulipuka.

Samaki hao walikataliwa Japan baada ya serikali ya Japan kubaini wamevuliwa kwenye maji ya mionzi, ndio ikaletwa Dar, imebainika makontena hayo yameshatolewa na TFDA, wizara ya afya na idara ya uvuvi walitoa vibali.

Kwa hiyo wana JF tujiandae wakati wowote tunakula sumu, tujiandae kupata saratani...


CHANZO: NIPASHE JUMAPILI said:
Na Moshi Lusonzo
24th July 2011

headline_bullet.jpg
Wadhaniwa kuwa na mionzi ya nyuklia
headline_bullet.jpg
Walaji kupata saratani, mimba kuharibika



DR%20Mponda%20Haji.jpg

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda

Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wapo hatarini kula samaki wenye sumu baada ya kumpuni moja (jina linahifadhiwa) kudaiwa kuingiza shehena ya samaki hao wanaodhaniwa kuwa na mionzi ya nyuklia.

Habari za uhakika ambazo NIPASHE Jumapili imezipata ni kwamba shehena hiyo ya samaki iliingizwa nchini wiki tatu zilizopita na kampuni hiyo ya jijini kutoka nchini Japan kupitia bandari ya Dar es Salaam.

Watoa habari hizo walisema samaki hao walikuwa wamehifadhiwa kwenye kontena tano zenye uzito wa tani 25 kila moja.

Aidha taarifa hizo zinaeleza samaki hao wametokea mji wa Fukushima ambapo maji ya bahari yaliyozunguka mji huo yameathiriwa na mionzi ya nyuklia iliyotokana na kulipuka kwa vinu vitatu vya mionzi.Japan tayari wamepiga marufuku uuzaji wa samaki wanaovuliwa eneo hilo la bahari.

Vinu hivyo vililipuka baada ya kutokea temekemo kubwa kwenye mji huo na kusababisha mionzi ya nyuklia kusambaa kwenye maji ya bahari.

Imedaiwa kuwa samaki hao kabla ya kufikishwa nchini, walikataliwa nchini humo baada ya Serikali ya Japan kubaini walitoka katika eneo linaloaminika kuwa na mionzi hiyo.

Hata hivyo, baada ya kukataliwa shehena hiyo ilisafirishwa hadi Bandari ya Dar es Salaam na nembo ya kampuni hiyo, ambapo kutokana na kuonekana itakuwa vigumu kukubaliwa kuuzwa sokoni kama itabainika inatoka Japan, kampuni hiyo ilibadilisha nembo na kuonyesha samaki hao wanatoka nchini Indonesia.

Ilibainika makontena hayo yalikaa bandarini hapo kwa wiki tatu wakati uongozi wa Kampuni hiyo ukihangaikia kupata kibali na walifanikiwa kuyatoa makontena hayo Ijumaa iliyopita baada ya kupewa vibali na vyombo husika.

Inadaiwa vibali vya kutolewa kwa makontena hayo vimetolewa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) iliyo chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii pamoja na Idara ya uvuvi iliyo chini ya Wizara ya Mifugo na uvuvi. Viongozi wa TFDA walipotafutwa hawakupatikana kwenye simu zao jana.

Kitu ambacho kinaleta hofu ni baada ya shehena hiyo kudaiwa wakati wowote itaanza kuuzwa kwa wananchi, kitu ambacho kinaweza kuleta madhara kwa binadamu.

Madhara yanayoweza kuwapata walaji wa samaki hao imeelezwa kuwa ni pamoja na kupata saratani, kuharibika kwa mimba pamoja na magonjwa mengine yanayoharibu neva za fahamu.

Aidha, athari endapo mtu atakanyaga mifupa yake kwa bahati mbaya anaweza kudhurika. Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda alipopigiwa simu yake ya mkononi kutoa ufafanuzi, alisema kwa upande wake hafahamu tukio hilo.

Alisema ni kweli TFDA ndio wanahusika na utoaji wa vibali kwa bidhaa zote za chakula baada ya kuhakikisha ni salama, lakini kuhusu uingizwaji wa samaki hana taarifa.

"Bwana Mwandishi hilo jambo silijui lakini nashukuru kwa kunipatia taarifa hizo naanza kuzifuatilia sasa hivi," alisema Dk. Mponda.
Aidha alipopigiwa simu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, David Mathayo hakuweza kupatikana baada ya simu yake kuzimwa.
 
Kwahiyo itabidi tujihadhari na kitoweo cha samaki wa maji chumvi mahotelini.
Nakuambia watatuua manake makontena yameshatoka na kuingia mjini,mie nimekula samaki juzi tu nguvu zimeniishia sijui zitakua ndio hizo?
 
Daaaaa,,TFDA wamesemajeeeee???????jaman,,,,,,,wataalam wetu wa sasa ni sawa na mangungo wa msowero
 
Ebu kuweni serious jamani,usikute tfda wamewekwa sawa mbona yule mama anaonekana muadilifu sana
 
Hivi Tanzania inahitaji samaki wa kuagiza kutoka nje? Kwa upumbavu huu ndo tunategemea kukuza vipi uchumi wetu ilihali tunashindwa kulinda soko la bidhaa za ndani? Kweli samaki wetu hawatoshelezi mahitaji ya watanzania? Kama ndo hivyo ina maana zile nchi zisizo na maziwa wala bahari zenyewe zinaishije?
 
BBC wametangaza mda sio mrefu kuwa baadhi ya samaki wamezuiliwa kwenye maghala ya huyo mfanyabiashara na TFDA wamekiri kuwa inamionzi,wanaomba ushirikiano wenu wananchi,wanasema wao hawakujua kwa sababu mfanyabiashara huyo alikuja na document zote za kuonyesha usalama wa hao samaki.kazi kwelikweli
 
Samaki hao wa kuagizwa kwa ajili kuuzwa kwenye Supermarkets na kwenye Hotels mbalimbali kubwa hapa nchini... KAZI NI KWAKO!!! Nina wasiwasi kuwa wakizuiwa na TFDA wanaweza kupenyezwa hadi soko Ferry na kuuzwa kwa walaji wa kawaida... TUMEKWISHA!!! Nadhani serikali ya Japan ilimpa tenda ya kuwa-dump huyu supplier aliyezileta... kilichotokea ni tamaa ya Supplier pamoja na muagizaji... Naomba Muagizaji achukuliwe HATUA KALI!!! Serikali ya CCM mmeshindwa kila kitu hata hili la kumchukulia hatua muagizaji...??? SHAME ON YOU!!!
 
BBC wametangaza mda sio mrefu kuwa baadhi ya samaki wamezuiliwa kwenye maghala ya huyo mfanyabiashara na TFDA wamekiri kuwa inamionzi,wanaomba ushirikiano wenu wananchi,wanasema wao hawakujua kwa sababu mfanyabiashara huyo alikuja na document zote za kuonyesha usalama wa hao samaki.kazi kwelikweli
hivi ile intelijensia siku hizi haipo eenh?
 
Na viongozi wetu wasivyokuwa makini hakiyamungu twafaaa weeee, nafwaaa agweee, iweeee wagambire sitopu.
 
Kuna kipindi nilisikiaga samaki vibua wengi wanatoka china!huwa jamaa wanawavua wengi kama Chambo,then ndio wanaletwa huku kuuzwa!tokea siku hiyo mimi na vibua marufuku!sasa hii tena ya samaki wa mionzi ndio imeniacha hoi!nimesikiliza BBC jamaa wanasema kuna baadhi ya hao samaki tayari wapo sokoni,eti wanachi watoe ushirikiano!mm nilitegemea hata angesema ni aina gani ya hao samaki ili mtu awe makini nao!na sio kusema watoe ushirikiano wakati hata hawajui ni aina gani ya samaki!

Huyo aliyempa kibali cha kuingiza samaki kutoka Japan ilihali akijua kuna mionz ndio anatakiwa ashikishwe adabu!manake hapo kuna kitu kidogo kilitembea!
 
Back
Top Bottom