Samahani mume wangu: Halikuwa lengo langu...!

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,971
1,650
Wajemeni narudi tena jamvini...........watakaonuna au kufurahi kwa raha zao! Nimerudi toka mjini nimekutana na jambo la kusikitisha. Ile natia timu tu huku dodoma-eneo la chang'ombe, nimekuta kikao cha usuluhishi kati ya mpangaji mwenzangu na mkewe pamoja na ndugu wa mke na mume.

Kifupi ni kwamba mume amemtaliki mkewe baada ya jaribio la mke kumuua mumewe kwa kumuwekea sumu ktk chakula, wiki sita zilizopita. Baada ya mume kulazwa hospitali ya General kwa wiki 5, jana ndo katoka hospitali na kufikia kutoa talaka leo. Nami ndo nimefikia kuitwa kwa hicho kikao. Masikini bahati nzuri mume hajaathirika sana, ingawa morphology ya mdomo imeharibika kidogo. Habari ya mhusika haijafikishwa polisi kwa kuhofia watoto wao kukosa malezi ya mama-wamezaa watoto 4.

Wakati wa mjadala, mke alimuomba mume afute talaka kwani halikuwa lengo lake kumuua. Ajabu kila mume alivyokuwa akimkomalia, kutaka kujua lengo lake la kumuwekea sumu kwa chakula lilikuwa nini basi kama sio kumuua, mke alishndwa kujibu swali na kubakia kulia tu kila anapoulizwa jibu la swali hilo. Kwa kuhofia suala lisifike mahakamani, jamaa ameamua amuache mkewe kistaarabu kwa kutokwenda polisi kuwaambia 'source ya poisoning'. Kwa kuwa mume ameshikilia msimamo wa kumucha mke, sisi hatuna jinsi, mume kesha amua. Mjadala bado unaendelea jinsi ya kugawana mali, nyumba 1, daladala 2 na teksi 1.

naendelea kujiuliza, sijapata jibu-Hivi inawezekana kweli, unamuwekea mtu sumu kwa chakula halafu unadai lengo sio muathirka afe? Kama lengo halikuwa kumuua mume, alitegemea sumu imfanye nini mumewe?

Inahuzunisha sana!
 
Ndyoko ! Habari yako mbona imenistua hadi vinyweleo vimenisimama !.
Ama kweli MKE SIO NDUGUYO !
 
Sasa lengo lilikuwa ni ili iweje? Au labda siku hizi kuna sumu ambazo haziui? Ikishaitwa 'SUMU' itaachaje kuua! Amwache tu manake ni muuaji!
 
Labda alıtaka azıpate yeye hızo malı za ndoa baada ya mume wake kufa lakını Mungu amekataa.
 
Hayo ni mambo makubwa sana, lakini me naona kunajambo ambalo mdada kalipata ao kutoka kwa marafiki zake ao kalifikiria tu mwenyewe, pengine wazo kuu ni lile la kumwondoa mmewe ili arithi mali zote.
swala la adhabu huyo baba kafanya uamuzi wa busara sana tena ni wa kibinadam zaidi, haja taka kumrudishia ubaya kwa kumshtaki polisi afungwe na ataabike, kwa wototo isingalikua ni picha nzuri na pia wangekua na mazingira magumu sana katika maisha yao.

Kuhusu kugawana mali hizo mi naona mwanamke hakustahili tena kupata sehemu yake kwa kitendo alicho kifanya angalienda mahakamani angalipoteza vilevile kila kitu, hivyo basi naona ni vema sehemu yake ibakie kwa watoto kwa maisha ya baadae,
 
Abaki na watoto wake, huyo mama aondoke tu mwenyewe....asije kosea sumu akawawekea wao.....inauma aisee!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom