Hofu zilizopandikizwa ndani ya watu ndizo zilizorahisisha utawala wa wakoloni kudumu miongoni mwa jamii ya kiafrika. Ndugu zangu tusiogope viongozi wa dini bali tumuogope MUNGU. Kwani ni nani asiyejua jitihada za Lowasa kujisafisha kwa mgongo wa dini? Mi ningekua kiongozi wa dini hata nisingemkaribisha kwenye maswala ya dini kwa sababu bado hajajibu kashfa ya richmond na hivyo pesa aliyo nayo ni najisi na inachafua madhabahu ya mungu. Viongozi wa dini waache njaa kali kwani lowasa kwa sasa anatuhumiwa ni mwizi na hajajibu tuhuma. Arudishe kwanza alivyoiba ndipo labda asamehewe,. la sivyo yeye bado ni mtumishi wa shetani.
Unakosea sana unapomlinganisha EL na makahaba na watoza ushuru!! Yesu alikuwa anawaambia watoza ushuru wauze vyote walivyonavyo, waache vyote wamfuate. Sasa EL kahujumu uchumi wa Taifa na bado anataka kuendelea kujijenga kisiasa. Ni dhambi kubwa kumtetea Lowasa. Halafu yesu aliwafuata na wala wao hawakufanya kinafiki kama Lowasa anavyowarubuni hawa wa sasa. Yesu hakufuata wenye dhambi waendelee kuishi na dhambi bali alitaka watubu na kuanza maisha mapya ya utakatifu.Tatizo hapa ni either kutojua mafundisho ya dini hasa kikristo yanayohubiri UPENDO na MSAMAHA! pamoja na kuwa EL ana skendo mbalimbali au tuhuma nafikiri sio sababu ya viongozi kumfungia milango, kumbuka Yesu hakuja kwa ajili ya waliowasafi ila wenye dhambi wapate kutubu na kuungama or ukosefu wa elimu ya biblia kwani kuhusu matamasha ya makanisa hata Yesu alihudhulia matamasha yaliyokuwa na wadhambi kama makahaba na watoza ushuru hadi walimkaribisha nyumbanimwao kumbuka ZAKAYO!