Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,064
- 22,757
Geeque, kiwango gani cha lawama Nyerere apatiwe?
a. Jumuiya imevunjika
b. Kaanzisha mchakato wa kufuatilia mali na madeni ya EAC
c. Mchakato ukamalizika
d. Pesa zikawa tayari kabla yeye hajaondoka
e. Alipoondoka 1985 mchakato ulikwisha na fedha zilikuwa zianze kutolewa ndani ya miezi michache.
f. Wenzetu Uganda na Kenya wakaanza kuwalipa watu wao
g. Fedha zetu zikawa tayari 1987
h. Nyerere alishang'atuka na Rais alikuwa mwingine, baraza jingine na viongozi wengine waliotakiwa kutekeleza kitu kilishokwisha amuliwa.
i. Mwinyi hakutoa zile fedha ambazo Nyerere alisimamia mchakato wake toka mwanzo hadi anaondoka madarakani hakukuwa na malalamiko ya waliowahi kuwa watumishi wa EAC.
j. Ni baada ya Mwinyi kushindwa kutekeleza na kugawa fedha ilivyokuwa ndio minong'ono ilipoanza
k. akaja na Mkapa ni yale yale
l. Na sasa Kikwete ni yale yale.
Sasa Nyerere kosa lake ni kutokuwa na influence? Kama yeye mwenyewe alioneshwa kushangazwa kuwa fedha ambazo alijua tayari zipo na hazijagawiwa ilivyopaswa huoni kuwa ndio sababu ya yeye katika ile miaka ya tisini kuhoji sana mambo ya Ikulu? Aliposema kuwa "Ikulu kunanuka rushwa" yawezekana alikuwa anajua mengi kweli ambayo alijaribu kuyafuatilia (kuweka influence). Yawezekana alijaribu kufanya influence ya mambo lakini hatimaye alijua kuwa he was out of the loop?
Inawezekana alikuwa na influence lakini hakuwa Rais. Hakuwa na uwezo wa mambo mengi sana ndani ya serikali influence yake ilikuwa zaidi ndani ya chama. Na utakumbuka aliamua pia kuachia Uenyekiti wa chama kule Kizota na ninadhani ni mwaka huo huo 1987 au ilikuwa 1990 ile?
Lakini Mwinyi si bado yupo hai kwanini yeye hauulizwi kuhusu sababu zilizomfanya asiwalipe wale wazee na kama Nyerere alijaribu kumshawishi kwa namna yoyote ile.. Malecela yupo hai, na wengine waliokuwepo bado wapo kwanini hawa hatuwaulizi walihusika vipi kuhusu malipo ya wazee hawa?
Nyerere aling'atuka uenyekiti wa CCM mwaka 1987. Hata huko Kenya na Uganda wastaafu hawakuweza kulipwa mpaka baada ya mwaka 1987. Cha kujiuliza na kusikitisha ni kuwa wezi wa pesa za hawa wazee bado wapo na wanajulikana na Raisi wetu anafahamu hilo. Badala ya wanausalama kuwakamata wezi, wanawatawanya kwa virungu walioibiwa fedha zao na Kikwete anaangalia. Hili ndilo linalouma zaidi - wezi wanatanua, wazee wanarushiwa mabomu na Raisi, wabunge na mahakama wanashuhudia, kulikoni ?