Sakata la Bandari: Je koti la Muungano linabana?

Zawadi B Lupelo

JF-Expert Member
Jul 19, 2015
2,549
3,722
Katika mazingira kama haya ndipo unapoona namna muundo wetu wa Muungano wa serikali mbili ulivyo mbovu na mbaya. Mazingira ambayo tuna Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka Zanzibar na waziri wa uchukuzi Prof Mbarawa kutoka Zanzibar pia halafu wanaingia mikataba kuhusu bandari ya Tanganyika huku watanganyika walio wengi wakihisi mkataba huo siyo kwa maslahi yao. Najua wengi hoja hii wanaichukulia kama ni ya kibaguzi lakini haiepukiki. Kitendo tu cha hoja hii ya uhalali wa Rais kutoka Zanzibar kuingia mkataba wa bandari ya Tanganyika kuibuka kunaashiria udhaifu mkubwa (Seriously malaise) katika mfumo wa Muungano wa serikali mbili.

Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania swala la bandari ni swala la Muungano kwa mujibu wa Katiba hivyo inatakiwa bandari zote za Zanzibar na za Tanganyika ziwe chini ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini kwa sababu zisizojulikana na kinyume cha katiba maswala ya bandari za Zanzibar yapo chini ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wenyewe huku maswala ya bandari ya Tanganyika ndiyo yapo chini ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Jaji Warioba hiki kitu aliita "Tanganyika kuvaa koti la Muungano", Mwanzo tusingeelewa vizuri lakini sasa ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni mzanzibar na waziri Mbarawa halafu wanakuja na mkataba huu ambao unaleta mashaka kwa Watanganyika walio wengi hii dhana inaanza kuwaingia Watanganyika walio wengi na ndiyo maana hoja hii imeibuka.

Jaji Warioba alipendekeza mfumo wa Muungano wa serikali tatu na katika hotuba zake mara nyingi ameweka wazi kuwa kwa muundo wa Muungano wa sasa wa serikali 2 Tanganyika imevaa koti la Muungano. Tuna serikali mbili serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar. Wakati serikali ya Zanzibar inatakiwa kushughulika na maswala yasiyo ya Muungano ya wazanzibari Serikali ya Muungano inashughulika na maswala yale yaliyo ya Muungano na wakati huo huo inashughulika na maswala ya Tanganyika ambayo siyo ya Muungano. Kwa vile watanganyika hawana serikali basi wanatumia serikali ya Muungano. Hapa ndipo koti la Muungano linapoonekana kwani serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inajikuta muda mwingi inautumia kushughulika na maswala ya Tanganyika badala ya yale ya Muungano kwani mambo ya Muungano ni machache.

Matokeo yake Watanganyika wanajiona ndiyo watanzania na wazanzibari wanabaki kuwa wazanzibari tu, hivyo serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inajikuta kama serikali ya Tanganyika zaidi ya kuwa serikali ya Muungano. Kutokana na dhana hii ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuonekana kama ni serikali ya Tanganyika zaidi matokeo yake Zanzibar inaanza kuondoa hata yale mambo ambayo kiuhalisia ni ya Muungano kama maswala ya Bandari na maliasili na kuyahamishia kwenye serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hivyo ni kama wanaondoa mamlaka ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya Zanzibar hili tusipoangalia tutajikuta tuna nchi mbili tofauti zinazojitegemea.

Kama wazanzibari watazidi kuondoa mambo ya Muungano na kuyasimamia wao wenyewe serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inajikuta inasimamia mambo ya Tanganyika peke yake na hapo ndipo sasa hisia za kwanini kuweni na Rais na mawaziri kutoka Zanzibar kuja kwenye Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati serikali hiyo inasimamia mambo ya Tanganyika zaidi? Hizi hisia haiwezi kuisha chini ya muundo wa serikali mbili.

Watanganyika wanaona koti la Muungano linabana. Shikamoo Jaji Warioba kweli tulihitaji serikali ya Tanganyika ili nasisi tuyakimbize huko mambo yetu ili yasimamiwe na sisi wenyewe huku kujifanya Tanganyika ndiyo Tanzania kumetuponza.
 
Mna waua sana Wazanzibar kwa sababu ya Muungano huu wa kifala mna tofauti gani na wakoloni ?

Nyerere alikuwa mkoloni mweusi na watawala wote walio fuatia ni wakoloni weusi.

Waacheni Wazanzibar wawe huru na nchi yao na nyie mbaki huru na nchi yenu.
 
CCM ndio adui wa taifa
 
Tuwaache waparurane huko kwao. Na walioko huku wapewe boti la ............
 
Kwanini waziri Mbarawa ambaye ni Mzanzibari ameteuliwa kuhudumu katika wizara isiyokuwa ya Muungano?
Inakuwaje mtu anahudumu katika wizara ambayo anakuwa anafanya kazi kama mtu anayefanya kazi kwa mhindi au mchina? Wakati yeye ni kiongozi wa kisiasa. Mbarawa anafanya kazi ambayo kwake ni kwa ajili ya kulipwa mshahara tu.
 
Back
Top Bottom