Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

He he heeeee!!!!!!!!!!!!!

UVCCM. Mmekuja moja kwa moja uwanjani. Jamani jamani jamani fani ya siasa inadhalilishwa sana.
Nasikitika sana kumjadili mtoto kama Isaac. Sijui kama wenzangu katika JF mnaona hiuli. tunaacha kujadili issues tunamjadili mfunga kamba za viatu. Ninajua Isaac ni jibaba lenye ndevu lakini kwa maneno yake nasikitika kuwa sishawishiki kutomwita mtoto mdogo

UVCCM wana kazi kubwa ya kutambua ukweli kuhusu siasa za nchi. Kwa kweli somo ambalo UVCCM hawalijui ni KUSOMA ALAMA ZA NYAKATI ZA KISIASA.

Kwa taarifa yenu UVCCM ninapenda kuwahakikishia kuwa zile nyakati za Kidumu Chama Cha Mapinduzi zimepita. alkini nina uhakika isipokuwa watu wachache wenye hekima sana ndani ya CCM na nje yake wengine wote hawawezi kuona ukweli huu.

Niwataarifu pia kuwa enzi za kutumia jeshi la polisi, dola, fedha za nchi nk. zitapita muda si mrefu. Hapo tutawapima akina Isaac kwenye mizani ya ujuzi wa siasa za kweli na uzalendo wao. Ulimwengu mzima utawatambua vijana katika siasa kutokana na input yao katika mustakabali wa nchi na wala si mbwembwe zao katika kuyalinda mitupora iliyojificha katika vyama vyao.

Nitaweka somo maalum katika Jamvi hili kwa ajili ya vijana wa CCM. Jiandae kusoma na kujifunza. Kama huna kipaji cha kujifunza, nakusikitikia, hutafaidi chochote.
 
... ni ulevi wa madaraka, hakuna kitu kingine hapo! Ulevi wa madaraka huondoa busara, akili na hata ujuzi!
 
kweli ccm muflis! yaani chama chenye dola kinashindwa kupata angalau kijana mmoja mwenye maarifa akaongoza vijana wenziwe!!

haya sasa, kiongozi wao kikwete alipokutana na wazungu mbona hakusema kama noma na iwe noma.......au ile si kauli ya kusikika nje ya tanzania, ni ya kuonea wanyonge tu
 
Nchimbi apata mpinzani uenyekiti Vijana CCM


Mwandishi Wetu
Daily News; Monday,May 19, 2008


MBIO za kuwania uenyekiti wa Taifa wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), zimeanza kupamba moto baada ya Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Mkoa wa Tabora, Hussein Bashe, kutangaza azma yake ya kuwania nafasi hiyo inayoshikiliwa kwa sasa na Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk. Emmanuel Nchimbi.

Bashe alitangaza azma hiyo Dar es Salaam jana katika mkutano wake na waandishi wa habari, huku akiahidi mabadiliko makubwa ya UVCCM Taifa endapo atafanikiwa kumrithi Dk. Nchimbi.


Kijana huyo aliyezaliwa Agosti 26, 1978 wilayani Nzega ambaye kwa sasa ni Meneja Mauzo na Usambazaji wa New Habari 2006 Limited, amesema kutokana na dhima kuu ya UVCCM ya kuandaa vijana kuwa raia wema, lakini pia kuwa tanuri la kupika viongozi wa Taifa, "hali ya mabadiliko katika umoja huu kwa sasa ni jambo lisiloepukika."


"Kuna haja ya kufanya mabadiliko makubwa ndani ya umoja wetu," alisema Bashe, ingawa anakiri kuwa historia ya jumuiya hiyo imejengewa misingi na viongozi waliopita na waliopo na msingi hiyo ni kama umoja na kujiamini, vitu ambavyo alisema ni vya msingi kwa jumuiya yenye dhima kama UVCCM.


"Hivyo basi leo natangaza msimamo na azma yangu ya kugombea nafasi ya uenyekiti wa UVCCM Taifa nikiwa na lengo la kufanya mapinduzi hayo na kuurejesha umoja huo kwenye chati yake kama ilivyokuwa enzi za TANU, kuwa chombo kinachobeba sura ya vijana wa taifa hili," aliongeza.


Katika baadhi ya mambo anayokusudia kuyafanya akichaguliwa ni kuifanya jumuiya hiyo kuwa jukwaa la vijana wote; kubadili muundo wa utawala/oganaizesheni; kubadili kalenda ya vikao vya jumuiya; kuipatia uhai Idara ya Chipukizi na Uhamasishaji; kuifanya jumuiya kujitegemea kiuchumi; kudhibiti uhamisho usio wa lazima na kuboresha maslahi ya watendaji.


"Ili kusaidia vijana wafikie maisha bora kwa kila Mtanzania, nitafungua milango ya mijadala kwa wana CCM na wasiokuwa wana CCM ikiwa wote tutakutana kwa njia ya kutafuta majibu ya matatizo ya vijana wa Tanzania, pia nitasimamia kuwapa Wazanzibari nafasi katika kuongoza idara za jumuiya yetu," alisema Bashe ambaye anasema nafasi hizo zimetawaliwa na watu wa Bara na hilo kwake ni upungufu.


Kwa sasa, jumuiya za Chama Cha Mapinduzi zinaendelea na mchakato wa kuchagua viongozi wa ngazi mbalimbali, na kwa UVCCM wamefikia katika matawi na sasa wanaingia katika kata.


Mbali ya kuwa Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Tabora, Bashe ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa; Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Tabora; Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Mkoa; Mjumbe wa Mkutano Mkuu Wilaya ya Nzega; Mjumbe wa Halmashauri Kuu Wilaya ya Nzega na Katibu wa Uchumi na Fedha Kata ya Nzega Mjini.


HabariLeo
 
Nchimbi apata mpinzani uenyekiti Vijana CCM


.............................Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Mkoa wa Tabora, Hussein Bashe, ...............................

...............................................
Kijana huyo aliyezaliwa Agosti 26, 1978 wilayani Nzega ambaye kwa sasa ni Meneja Mauzo na Usambazaji wa New Habari 2006 Limited, ..............................................

..........................................................
Mbali ya kuwa Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Tabora, Bashe ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa; Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Tabora; Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Mkoa; Mjumbe wa Mkutano Mkuu Wilaya ya Nzega; Mjumbe wa Halmashauri Kuu Wilaya ya Nzega na Katibu wa Uchumi na Fedha Kata ya Nzega Mjini.

.......................................[/url]

Nadhani kuna mkono wa RA hapa.
RA ni mbunge wa CCM - Igunga (Tabora) na ni mmiliki hisa mkubwa wa New Habari Corporation 2006 (T) Ltd.

Patamu.
 
Nchimbi hagombei so far mpaka sasa kuna watu wafuato

Mhe. Jerry silaa
Benno Malisa
Isac <mropokaji>
Nape
na huyo aliyejitokeza,ila kuna vifaa vingine vipo mbioni kujitangaza
 
Nchimbi hagombei so far mpaka sasa kuna watu wafuato

Mhe. Jerry silaa
Benno Malisa
Isac <mropokaji>
Nape
na huyo aliyejitokeza,ila kuna vifaa vingine vipo mbioni kujitangaza

yupo pia Zainabu Kawawa
 
Yaani mtu mmoja ana vyeo vyote hivi ? Huko CCM hakuna wengine katika maeneo hayo ? Kama hawapo akiondoka nani atashika nafasi zote hizo ama ataendelea kuwakilisha hadi katani ? Huyu nadhani ana mambo kama ya six huyu kuna jambo hapa si bure .
 
Binafsi nampongeza Hussein Bashe kwa kitendo chake cha kujitokeza wazi kuonyesha nia yake, nawashauri na wengine wenye nia kama hiyo wajitokeze wazi bila kujificha, namjua vizuri bwana Bwana Hussein kwa umahiri wa kujenga hoja za msingi, tunahitaji vijana wa aina ya Hussein Bashe na si Remote Controlled Leaders ! vyovyote itakavyokuwa mwezi Desemba tutahitaji vijana wa aina ya Hussein na si wale wanaopangwa makao makuu kama si Husein basi yeyote yule ili mradi asiwe anaepigiwa upatu na vibosile wa Hq
 
Back
Top Bottom