JERUSALEMU
JF-Expert Member
- Sep 19, 2012
- 3,106
- 3,523
Naam wanajamvi,
Ukisikia mtihani mkubwa ni kama hili Sakata la Mkataba wa DP World na serikali ya Tanzania juu ya uendeshaji wa bandari za Tanganyika. Ukisoma ule mkataba kwa ujumla mpaka hapa Tanganyika hatuna jinsi, kwa maana tukiendelea nao tutakuwa tumejipeleka utumwani kwa namna vipengele vya mkataba vilivyo tumekwisa.
Tukiachana nao tumekwisha pia. Kifupi mpaka hapa tulipo fika ni kwamba DP WORLD wametuweka kwenye 18 zao kila upande. Hata tukiachana nao leo, bado tutatakiwa kuwalipa fedha nyingi, nyingi , nyingi kwasababu watatushinda mahakamani mapema asubuhi.
Tumefikaje hapa? Kwa maoni yangu , kwanza ni tamaa za viongozi wetu, pili ni udhaifu wa Mwanasheria mkuu wa serikali, tatu ni udhaifu wa watu wanao msaidia Rais kuto kujiamini katika majukumu wanayo pewa na Rais. Nitafafanua kila udhaifu .
Ukiungalia huu Mkataba uko vile kwanza kwasababu inaonekana sisi ndio tulionesha kuwahitaji Waarabu kwasababu moja au nyingine na Sababu kubwa ni fedha. Kwanini? Katikati ya Sakata lenyewe unamkuta Rais Samia Suluhu Hassan pengine na Chama chake kwa mbali. Kwanini? Wanajiandaa kwaajili ya uchaguzi wa 2025 na hivyo wakaona namna nzuri yakuwawezesha kupata fedha ni kuingia huu mkataba kwa kisingizio cha kuboresha utendaji katika bandari zetu.
Nasema ni kisingizio kwasababu kama nia ingekuwa ni hiyo tu basi wangefuata namna bora ya kumpata mwekezaji bora kwa mchakato wa wazi kabisa. Ila kwasababu walikuwa na agenda binafsi ndio maana wakafanya haya makubaliano kwa kificho.
HUU MKATABA ULIKUWA NI SIRI KUBWA, UMEVUJISHWA NA WATU WEMA WASIO PENDEZWA NA VIPENGELE VINAVYO IPELEKA NCHI YETU UTUMWANI.
Hapa unaiona tamaa ya Rais wetu kutaka kushinda uchaguzi yeye na chama chake hata kwa njia haramu. Kimsingi amevunja KATIBA ya Nchi.
Udhaifu wa Mwanasheria Mkuu wa serikali. Huyu anatakiwa kuijua KATIBA ya Nchi yetu kinaga ubaga. Imekuwaje amekubali kuuza SOREINTY ya Nchi yetu kirahisi hivyo? Hajiamini, hakuwa tayari kumuudhi Rais, au na yeye fedha zilimfanya aseme Nchi nini bwana, nita a batana na fedha !!!
Waziri na watendaji wengine wa serikali tunaweza kuwalaumu lakini kwa mtazamo wangu hawakuwa na namna. Ukikataa huna kazi na ukikubali unakutana na fedheha kama hizi za kuingiza Nchi utumwani.
Nini kifanyike??
Kwa maoni yangu ni bora kuachana na huu Mkataba kabla hata hatujaanza kuutekeleza , halafu tusubiri kushitakiwa na kupigwa faini ya mabilioni ya dola kwasababu ya ukubwa wa mradi wenyewe.
MADHARA YA KUENDELEA NA MKATABA NI NINI?
Hofu kubwa ni kwanza ni kuligawa Taifa. Kuna watu wajinga wanachanganya Uarabu na uislamu ! Pili ni kuliingiza Taifa kwenye umasikini na utumwa mambo leo.
Kwanini ni The great ordeal?
Ukisikia kizungumkuti ndio hiki. Kifupi ni kwamba tumefika hapa kwasababu ya udhaifu wa USALAMA WA TAIFA. wajitathimini.
Lakini Rais Samia ni wakati sasa ajipime kama anatosha kuilinda, kuitetea na kuihifadhi KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
Kwa maoni yangu amepwaya.