Sakata la Mahujaji: Utendaji ATCL na Yaliyojiri Hadi Leo Hii

Je wanaweza kuondokea mji mwingine? maana ukiangalia gharama za kubakia mpaka 17th Jan na kusafiri kwenda mji mwingine zinaweza kuwa sawa au pungufu.

Yaah thats wat has been done. Mwakjj yupo sahihi Madina hakuna slots kwa msaada wa serikali wamepata slots Jeddah wataanza kurusi kwa mafungu kuanzia new year day
 
Rais amekwisha taarifiwa kuwa mahujaji wataanza kurudi tarehe 31 Desemba 07 hadi tarehe 2 Januari 08. Tarehe hizi haziwezi kubadilishwa na hivyo Serikali imeingilia kati suala la upatikanaji wa slots na ndege nyingine ili safari zianze kama ilivyopangwa.

Kwani ni sisi wenye maamuzi na hizo slots? Rais alielezwaje kabla ya uhakika kupatikana? Mimi naona ili kutimiza hii ahadi ambayo naona Kamati inaogopa kuitengua serikali itaingia gharama za ajabu. Hivi palikuwa na tatizo gani kumweleza Mheshimiwa Rais kuwa atataarifia uhakika utakapopatikana?

Kapteni Muze atakutumia taarifa za ndege hii nyingine. Suala la malipo ya ndege nyingine tutalijadili ili faida waliyopanga katika biashara hii isibadilike.

Mimi hapa pananitia wasiwasi. Malipo tutaelewana baadaye? Hii biashara gani!
 
mkjj.....

naamini JK ataingilia tena hili suala na kuokoa wa-tz haswa ukizingatia MZAA CHEMA wake au BABA MKWE WAKE yumo ndani ya kundi hilo.by the way inasikitisha sana.

i always nakumbuka maneno ya mzee ES kuwa JK amezungukwa na WAHUNI,wababishaji na matapeli watupu.
choveki...........

yes kwelikbs tumealaaniwa,tena ni laana za mungu.wewe fikiria mtu anatoka kijijini ame-save pesa yake miaka kibao ili aende akahiji makka then leo unamgandisha airport for 10days unampiaga kamba tu,lelo ameshamaliza hijja huko bado unamgandisha madina etc,wewe unafikiri MUNGU atawaacha?atawalipa tu taratibu.

unajua sifa ya mungu anaweza kukulipa hapo hapo au akakuaacha weee kwazna then ghafla akakulipa.


FUNZO KWA WANAOTAKA KWENDA MAKKA............

mie naona ushauri wangu ni bora kila mtu anayetaka kwneda makka,ni bora ugharamike utoe pesa nyingi mfano through ile jumuia ya MABOHORA etc lakini uwe na uhakika na safari kuliko kuwafuata hao washenzi wajinga na matapeli akina ATC etc.
unajua hivi vitu vya cheap sometime vina madhara yake,fikiria kama unaambiwa jumuia ya mabohora kwenda makka na kurudi inaku-charge dola 2500 while akina hao matapeli wengine wanaku-chargrge 2100 so ni bora ugharamike ndugu zangu lakini uwe na safari ya uhakika kabisa.
unafikiri wale waloenda makka walocholewa kwa 10days naamini tayari walikuwa wameshaa thirika kisaikolojia,wengi wao walikuwa wanafikria sijui itakuwaje kurudi etc.

any way nawatakia SAFARI NJEMA back home mola akipenda.
 
Unajua nini?

Bosi wa ATC alikataa na kusema shirika lao haliwezi safirisha Mahujaji.
Tatizo ni pale Mzee Nyang'anyi alipoingilia shughuli za kila siku za ATC na kudai wao wana uwezo wa kusafirisha mahujaji.

Mpaka sasa sielewi, sijui mzee huyu alitaka tengeneza fedha haramu kwa kuwapunyua Waislamu wenzie tena kwenye jambo muhimu kama Hijja au alitaka sifa tu?

Nao viongozi wa kuandaa hija sijui waliingiaje Mkenge na kuanza kuongea na mtu ambaye hana mamlaka na utendaji wa kila siku wa ATC?

Unajua huu Utamaduni wetu wa kuvuruga mambo na kupindisha taratibu kwa jeuri na kiburi hapa Tanzania umetufanya kushindwa kutekeleza mambo mengi na matokeo yake ni kutuzuria adha nyingi zisizo za msingi.

Hata kama jambo lenyewe ni jepesi kama kuweka chai kwenye kikombe kwa kutumia birika, usishangae kuona mtu na akili zake anazamisha kombe na kono lake chafu, tena la kushoto,ndani ya Birika ili achote chai. Ukimwuliza kwa nini anafanya hivyo anakunja ndita na ngumi kwa ununda.

Wako Akina Mustafa Nyang'anyi wangapi kwenye ofisi Muhimu za serikali na mashirika ya umma hapa Tanzania?

Watatuburuza na kutugaragaza huku wakitupa maumivu sisi watanzania kwa ujinga na kiburi chao na cha Aliyewateua hadi lini?

MH Rais Kikwete.
Hivi Ukurugenzi wa Bodi au Uenyekiti wa Bodi ni vyeo vya Vilaza walostaafu baada ya kuvurunda serikalini tu?

Mbona Watanzania wenye uwezo na moyo wa kufanya kazi walo staafu na vijana na nguvu zao zote sioni wakipewa vyeo ndani ya Bodi hizo?????

Au mwenzetu ndo unatekeleza sera ya SISIEMU kwa vitendo?
 
SITANII: Kuna mahujaji 14, akiwamo Muuza madafu mmoja wa Dar es Salama, ambao walisafiri kwa gari tani tatu Toyota pickup ambayo watarejea kabla ya hao waliokwenda kwa ndege. Taarifa zaidi za mahujaji hao nitawaletea kwa wakati mwafaka. Hii ni kutupa fundisho kwamba tunazidiwa hata na Somalia ambao hawana serikali. Hii ni aibu tupu
 
Hii hapa chini kanipenyezea mdau mmoja, nimeamua kuinakili na kuipachika:

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT

Telegrams: "MIUNDOMBINU", Dar es Salaam
Telephone: 2114425/2112858 P.O. BOX 9144,
Fax: 255 022 2112751/2116032 DAR ES SALAAM.


Ref: ATCL/HIJA/07 29th Desemba, 2007


Mark Manji
Mwakilishi wa ATCL Saudi Arabia,


Yah: KURUDI KWA MAHUJAJI

Kamati iliyoundwa kusimamia kurudi kwa mahujaji imepitia ripoti yako na kuwa na wasiwasi juu ya lini hasa mahujaji wa Tanzania wataanza kurudi hasa kwa kuzingatia kuwa shughuli za Irak zinaweza zikaendelea hata baada ya tarehe 1 Januari 2008 na hivyo tukawa hatuna uhakika wa slots ifikapo tarehe 2 Januari 2008.

Rais amekwisha taarifiwa kuwa mahujaji wataanza kurudi tarehe 31 Desemba 07 hadi tarehe 2 Januari 08. Tarehe hizi haziwezi kubadilishwa na hivyo Serikali imeingilia kati suala la upatikanaji wa slots na ndege nyingine ili safari zianze kama ilivyopangwa. Ndege ya Global Aviation itatumika kubeba mahujaji ambao watakuwa wamebaki wakati itakapomaliza shughuli ya Irak.

Hivyo unaagizwa ufanye yafuatayo:

1. Ongea na uongozi wa SAMEK ili kutumia angalau slot moja kati ya kumi walizopewa Irak.
2. Ongea na uongozi wa SAMEK ili kuwaarifu kuwa Serikali inaandaa ndege nyingine kuanza safari za kuwarejesha mahujaji wa Tanzania tarehe 31 Desemba 2007. Ndege DC10 ya Global aviation itatumika kumalizia mahujaji watakaokuwa wamebaki. Kapteni Muze atakutumia taarifa za ndege hii nyingine. Suala la malipo ya ndege nyingine tutalijadili ili faida waliyopanga katika biashara hii isibadilike.

Fanyeni kila linalowezekana ili mahujaji waanze kurudi tarehe 31 Desemba 2007.

Wako,



O. Chambo
NAIBU KATIBU MKUU
 
Kazi Kwelikweli::::hizo Ndege Za Serikali Zitakazoenda Kuwachukua Ni Community Airline???????
 
NDEGE ZENYEWE NDIO HIZO MMHHHHH MWENYEZI MUNGU TUHURUMIE WANAO

Dear XXXX



Please find details of additional aircrafts on which slots can be applied;
documents hijja 1 to 7 relate to Community Airlines. Docs Star Air 1 to 13
relates to an aircraft to be leased from Star Ailines (Peter Annear). I am
forwarding other docs.



Regards,

ZZZZZZ.
 
NDEGE ZENYEWE NDIO HIZO MMHHHHH MWENYEZI MUNGU TUHURUMIE WANAO

Dear XXXX


Please find details of additional aircrafts on which slots can be applied;
documents hijja 1 to 7 relate to Community Airlines. Docs Star Air 1 to 13
relates to an aircraft to be leased from Star Ailines (Peter Annear). I am
forwarding other docs.



Regards,

ZZZZZZ.

Pdidy mbona unatuacha hewani na hizo XXXX na ZZZZZZ? Unamficha nani? Weka mambo hadharani tumkome nyani mpaka giladi!
 
Mi Bado Najiuliza Nani Anatoa Hizi Hela Zinzotoka Kama Njugu,,atcl Nimesoma Wameingia Mkataba Na Samek Wa Kuleta Na Kurudisha,,na Nimesoma Wanadai Watapeleka Ndege Ok:::tunaombwa Tuelekezwe Yafuatayo

1))je Kama Mkataba Ni Kuwarudisha Kwa 3trips Na Ikatokea Badugu Wakakuta Kundi Zima Limesharudi Je Watarudisha Hizo Hela Walizochukua,

2))na Kama Hakuna Uwezekano Nani Awajibike Kwa Hili,,serikali Kupeleka Ndege Wakati Kuna Iliolipiwa Tayari Ambayo Haitafanmya Safari Zake Kama Ilivyo

3))kama Slots Zitachelewa Na Serikali Wanao Uwezo Wakulipia Hizo Ndege 2,,natumaini Wataenda Mara Mbili Mbili,,je Kwanini Tukubali Imeshatokea Wakatafutiwa Sehemu Nzuri Ya Kullala,,maana Nimeambiwa Na Mshikaji Guest House Ya 5000 Kipindi Hiki Ilikuwa 50,000,,imerudi ,then Zile Hela Za Kukodisha Ndege Nyingine Kila Hujaji Atakae Wasili Wampe Hata Dola 500 Ya Ahsante,,jamani Kukodi Natumaini Ni Zadi Ya Dola 50000,,so Hhizo Pesa Wakafutia Machozi Jamani,,,mungu Awalinde Uko Waliko

4)))serikali Tunaomba Mtupe Taarifa Kamili Mkishirikiana Na Atcl Ni Hasara Kiasi Gani Imeliingizia Taifa Kumbukeni Mlikuwa Mkitumia Pesa Za Walipa Kodi Kwa Kila Jambo,,,,na Kwa Hili Naomba Waandike Na Kusambaza Kila Gazeti Waliohusika Wamepata Adhabu Gani????maana Kuna Wengine Wameeenemeka Tumeambiwa Mpaka Inasikitisha Sana,,,

5)))tunaimba Chenge Ukishindwa Haya Yote Tunaomba Ujiuzulu Kabisa Na Tusikusikie Kwenye Magazeti Anymore
 
KWA KUMUHESHIMU MUNGU NA WANA JF WOTE

Dear Mark



Please find details of additional aircrafts on which slots can be applied;
documents hijja 1 to 7 relate to Community Airlines. Docs Star Air 1 to 13
relates to an aircraft to be leased from Star Ailines (Peter Annear). I am
forwarding other docs.



Regards,

Eliasaph.
 
Ahsante sana Pdidy, mpaka kieleweke kuhusiana na hawa viongozi uchwara wasioweza kufanikisha lolote ndani ya Tanzania.
 
Hii hapa chini kanipenyezea mdau mmoja, nimeamua kuinakili na kuipachika:....THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
.....Wako,.......O. Chambo........NAIBU KATIBU MKUU

Pokea tano Kithuku kwa kutulea hii, nyie ndo mashujaa tunaowahitaji (angalia usije mwanga unga lakini).
 
Nyie msiharibu taratibu za NCHI kwa kumkoma NYANI..taratibu za nchi ziachwe..HUu WIZI wa barua ni sawa na wizi mwingine...watu kama nyinyi MCHONGA alikuwa anawapoteza kabisa ktk Jamii..ila JK naona yupo COOL na watoaji wa siri za IKULU...
Naunga mkono kumkoma nyani mchana kweupe ila tuheshim taratibu..possibly wewe utakuwa NEXT President au PM after t years..
 
Mzee Ruksa alipokuwa waziri wa mambo ya ndani, ilitokea kashfa nzito kule eneo la Shinyanga. Ingawa yeye hakuhusika binafsi, lakini kwa kuwa yeye alikuwa kiongozi wa wizara husika, alijiwajibisha kwa kujiuzulu.

Sasa kwa mujibu wa taarifa tulizozipata kutoka kwa waandishi wa magazeti ni kwamba Mustafa Salim Nyang'anyi alijihusisha binafsi na hiyo ilikuwa bila ya kushauriana na Board yake wala uongozi wa ATC. Suluhisho, kwa upande wangu, lianze naye ema kwa kujiwajibisha au kwa kuwajibishwa.

Baada ya hapo, yaliyopita si ndwele, tugange yajayo. Mahujaji waombwe radhi na pia wafutwe jasho.
 
tuheshimu taratibu za nyaraka za utendaji wa serikali,ila zile zinazokwenda kinyume na maslahi yetu kama vile mikataba mibovu, au nyaraka za kukiuka haki zetu hizo tukiweza kuzianika hiyo itakuwa poa tu. lakini nyaraka mfano labda Muungwana kamuagiza fulani afuatilie kitu fulani(ambayo ni confidential na ni sahihi kiutendaji)sidhani kama ni vyema kukianika hapa barazani.
hayo ni maoni yangu tu, nipo tayari kukosolewa
 
Mimi nadhani tuondoe neno confidential kwenye msamiati wetu. mambo yote yakiwa wazi watu watakuwa makini zaidi.
 
Back
Top Bottom