Sakata la mafao: Kuna harufu ya ubaguzi na ukiukwaji wa Katiba-tujadili

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,664
18,039
Wizara inayohusika imetunga kanuni na vikokotozi tofauti ndani ya sheria moja iliyounganisha mifuko ya jamii. wafanyakazi wote waliokuwa kwenye mifuko ya LAPF na PSPF walijiunga na mifuko hiyo chini ya sheria moja japo kwa miaka tofauti. Wale ambao ilipofika tareha 01/08/2018 ambapo sheria iliyounganisha mifuko ilipoanza kutumika walikuwa na miaka 55-59 wametungiwa kanuni na kikokotozi tofauti cha mafao yao.

Hawa watapewa asilimia 75 kama ilivyokuwa awali na mshahara wa mwisho ndio utakaotumika kwenye kikokotozi hicho. Hii itawafanya watoke na kitita kikubwa. Wale ambao ilipofika tarehe 01/08/2018 walikuwa na miaka 54 kurudi nyuma watapata asilimia 25 tu ya mafao yao kwenye malipo ya mkupuo na mshahara utakaotumika kwenye kikokotozi cha mafao ni wastani wa mishahara ya miaka mitatu "mizuri" ndani ya miaka 10 ya mwisho!!!.

Ikumbukwe kuwa kwa miaka mitatu mishahara haijapanda kama ilivyokuwa inafanyika huko nyuma. Kwa hiyo kundi hili watapata mafao kidogo kwenye mkupuo.

Kwa maoni yangu huu ni ubaguzi usiokuwa na sababu ya msingi, yaani kuwabagua watu kwa kigezo cha umri wao japo japo walijiunga na mfuko chini ya sheria moja!

Kwa mujibu wa katiba ya nchi yetu, ni marufuku kutengeneza sheria au kanuni za ubaguzi na kifungu hicho ni hiki hapa:

Usawa wa binadamu. Sheria ya 1984 Na.15 ib.6 12.-
(1) Binadamu wote huzaliwa huru, na wote ni sawa.
(2) Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake. Usawa mbele ya Sheria ya 1984 Na.15 ib.6 13.-
(1) Watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria. Sheria ya Na.4 ya 1992 ib.8 Sheria ya 2000 Na.3 ib.5
(2) Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake.
Karibuni wataalam wa sheria mtujuze kama kutumia kanuni tofauti na vikokotozi tofauti ndani ya sheria moja kwa kigezo cha umri ni ubaguzi kama hisia za wengi zilivyo?

Kungekuwa na ubaya gani kama watu wote bila kujali umri wao kama wangetumia kikokotozi kimoja? (yaani chochote kati ya hivyo viwili). Lengo si wanasema ni kuwianisha mafao kwa mifuko mbli mbali? Mbona kundi moja limeachwa(wenye miaka 55-59 by 01/08/2018). Au kundi hili ndo limesheheni vigogo? Karibuni kwenye mjadala huru lakini bila jazba!
 
Karibuni wanasheria mdadavue kile kinachoonekana kama uonevu na ubaguzi katika suala zima la mafao ya wastaafu
 
Waziri arudi mezani na watendaji wake washughulikie tatizo hili ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wadau...
 
Hapa kateleza mnoooo
Hapa kadondoka kabisa mzee..Pamoja na mzingira magumu ya streaa wanayofanya kazi Wafanyakazi wa serikalini tz bila hata kupandishiwa Mshaharaa mwaka wa nne huu unaenda....kazi kibaoo mzee leo hii bado unataka mtu akistaafu uendelee kumnyonya zaidi...!! Hii sio sawaa mtu apewe chake asepee... Ujambazi huu usifumbiwe macho
 
Huyu rais ni shetani!

Huyu Rahisi ni Shetani na maaluni mkubwa anayestahili kwenda motoni.Hivi huyu mtu anaisoma Katiba ya JMT na kuilewa au akiisoma ana LEWA Pombe ya Magufuli?
Nji hii kwa sasa inatawaliwa na Maatahira wakiongozwa na Taahira mkubwa aliyeshindikana,,,,!Chombo amekielekeza kwenye Maporomoko ya Maji maatahira wanashangilia badala ya kusikitika kuwa wanakwenda kuangamia...Inasikitisha sana.
 
Wanasheria pia mtusaidiye. Pale mtu anapoaga dunia iweje warithi kulipwa pension ya miaka 3 tu na kinachosalia cha miaka 9 kielekee. Je, sheria ya urithi inaitambua serikali kama mrithi wa raia? Msaada pia kwa hili
 
Jamani kuuliza si ujinga wengine Atujui hesabu kama mtu analipwa lakimbili 200000 asilimia 25% kwa mkupuo ngapi.
 
Suala la mafao sio kwa wastaafu pekee, kuna vijana wenye nguvu zao wamechoka kunyanyasika kwa wahindi.... mtu amejikusanyia 30M, ana miaka 35 or so unamwambia subiri endelea kuteseka miaka 20 iliyobaki tukupe 25% ya hiyo uliodunduliza na hiyo 75% tunakutunzia tutakupa kidogo kidgo..let alone loan board, makato heavy ya PAYEE, na ujinga mwingi mwing.....
Juzi DG wa SSRA anasema asilimia 90% ya hela zote zimewekwa kwenye miradi ya maendeleo..more than 11TR. ...hakuna anaeshtuka......
Waziri wa maliasili anajitokeza anasema kwanini utegemee serikali ikuwekee usiweke mwenyewe....(Sijui ana laana??)
Bado watu tunawaangalia tu..... siku itafika hakuna pa kujificha.....
 
Waziri arudi mezani na watendaji wake washughulikie tatizo hili ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wadau...
arudi meza ipi wakati amejifungia? DG wa SSRA anasema hizo hela hazipo zimewekezwa kwenye miradi, na ni 20% tu ndio wanalialia, wengine wameridhia kabisa kupewa hiyo 25%......nchi hii kaz kwel kweli...
 
Back
Top Bottom