Sakata la Dr. Masau: Msimamo wa Serikali na Hatima ya Taasisi ya Moyo (THI)

Sawa KNKCU nimekuelewa. Huhitaji kuwa Einstein kujua kwamba umaskini wetu
ni wa kujitakia!!. Bahati mbaya makali ya umaskini yanawadhuru ambao hawashiriki kwenye hayo maamuzi mabovu.

Simfahamu Dr. Masau na ndio kwanza nimemsikia wiki hii. I hope kuna siku
atafanikiwa.

Mwanakijiji, ninasubiri kwa hamu mahojiano hayo.
Nami ninamtakia kila la Kheri na Ninapenda akaze buti na asiwe tegemezi kwa serikali kwani taasisi yake ni taasisi isiyo ya kiserikali.Awe mbunifu wa kufikisha taasisi yake kule tunapotegemea wengi kuiona inafika na si kulalama kwenye Vyombo Vya Habari kwa kuilalamikia serikali kama vile ni muajiri wake.
 
KNKCU,

Dr. Masau anawakilisha kundi zima la wawekezaji wazawa. Sijadili hapa
kwasababu ni Dr. Masau na badala yake najadili kwasababu ndilo tatizo ninaliona likiwakabili wasomi wengi wanaoamua kutumia elimu zao kufungua miradi Tanzania. Walio wengi huwa hawakubaliana na mambo kama rushwa, kunyenyekea nk. Baada ya muda wanaambiwa ni arrogants na kejeli zingine nyingi.

Kama ilivyo biashara yoyote kuna watakaofanikiwa bila kuwa na matatizo na kuna wale watakaokuwa na matatizo. Uongozi upo kusaidia wale wenye matatizo.

Hao waliofanikiwa tunashukuru na kuwaombea waendelee kufanikiwa.

Binafsi nimewahi kukumbana na baadhi ya kashfa za wafanyakazi serikalini
katika kuhangaikia shughuli zangu TZ. Naongelea hili suala kwasababu ni true believer wa hili la kujaribu kuwasaidia Watanzania ili wamiliki njia kuu za uchumi.

Tatizo kubwa linakuwa ni wivu na vitu vingine ni visingizio tu. Huwa wanatumia ukweli mdogo kuhalalisha maamuzi mazito.

Makala zote nimesisitiza juu ya kama ana utaalamu, hilo ndio namba moja na mengine yote yanaweza kutatuliwa. Kitu ambacho binafsi siwezi ku compromise ni quality ya kazi. Kama Dr. Masau hana uwezo, mjadala wote huu hauna maana. Lakini hisia ninayopata ni kwamba ana uwezo wa kujua kazi lakini hana vitendea kazi equipment plus HR.
 
KNKCU,
Huna pesa, unahangaika hata kulipa loan, utawezaje kuajiri wataalamu wa kutosha? Suala ni lile lile la kuku na yai. Ingelikuwa wenzetu huku wangekaa naye na kumwambia, rekebisha hiki na hiki na sisi tutakupa tenda ya kutibu wagonjwa 100 kwa mwezi. Karatasi hizi hapa, kaombee pesa bank au jumuia nyingine ili upate vifaa vya kisasa na kuajiri madaktari wenye uwezo. Akiwa na
hizo karatasi zinazoonyesha kila mwezi serikali itakuwa inalipa kutibu wagonjwa
kiasi fulani, atapata tu hiyo mikopo ya interest nafuu.

Eti "kwanini wafadhili hawampi pesa za kutosha" Are you really serious kuamini kwamba THI itaendeshwa kwa fedha za wafadhili? Hivi kwanini wafadhili hao hao hawaipi Tanzania pesa za kutosha itoe elimu bure mlimani? Ndio maana nilisema status quo ina matatizo kweli kuibadilisha.

Kadri ninavyosoma hoja zako juu hili nazidi kupata uhakika juu ya fikra zetu na priorities zetu.

Hakuna jipya hapa ni yale yale ya miaka yote ya kukomoana. Sasa wanataka kumkomoa Dr. kwa kuanzisha kitengo chao ambacho nacho matokeo yake kitayumba tu kama idara zingine za hapo Muhimbili.

kupitia Wizara hiyo hiyo serikali inalipa mabilioni ili akina Mkapa, Msuya, Hamad, Kawawa na wengine wengi waje ku check pressure mara mbili kwa mwaka na kukaa London mwezi mzima wakiongozana na wafanyakazi kama 10 wakiwemo hao hao watu wa Muhimbili. Kituo kama THI hakitasaidiwa mpaka siku tutakapowaambia hakuna kulipiwa nje tena.

Mkulima,
Niko nawe pamoja hapa. Ni zaidi ya kukomoana watu wa wizara husika wanajua kukiwa na taasisi inayofanya kazi basi safari za India zitpungua kama siyo kwisha kabisa. Je ni kiasi gani cha pesa watapoteza (utadhani ni halali yao kujipatia) endapo kamisheni wanazojipa hazitakuwepo kwa sababu hakuna safari? Ubinafsi, ubinafsi, ubinafsi tu. Watu wako radhi Watanzania wenzao wafe ilmradi wao wapate cha juu.
 
let me tell you firsthand my personal experience .I underwent open heart surgery in India at Madras medical mission.I was told by the doctor in charge that the children that was sent from Tanzania thru Lions club were operated on at a special discounted rate ;yet the organizers ????were demanding 10% .not only was I shocked but very ashamed,because I was being told how rotten we tanzanians were .since they were not in a position to pay the 10% because all that the hospital charged was for the nursing facilities .The doctors and surgeons waved their fees .They stopped sending children to Madras medical mission.The rest is history.
 
70mainrd;31646 let me tell you firsthand my personal experience .I underwent open heart surgery in India at Madras medical mission.I was told by the doctor in charge that the children that was sent from Tanzania thru Lions club were operated on at a special discounted rate ;yet the organizers ????were demanding 10% .not only was I shocked but very ashamed,because I was being told how rotten we tanzanians were .since they were not in a position to pay the 10% because all that the hospital charged was for the nursing facilities .The doctors and surgeons waved their fees .They stopped sending children to Madras medical mission.The rest is history.

Kuna vitu wewe naweza kusema umeviweka sawa, hao lions club si wizara walikuwa wanadai 10%, Na sikatai kwamba upande wa wizara vile vile huenda ukawepo na kitu kama hicho hasa kwa kulifumbia muda mrefu swala la kuwa na kituo chake cha upasuaji ili wananchi wakanufaika nacho, mimi ni mmoja wa watu waliokuwa wana advocate serikali kuwa na heart surgery insitution yake ili kuondoa usumbufu kwa watanzania waliowengi ambao wanasubiri foleni kupelekwa India pasi na kuwa na mafanikio yeyote.

Kuna Madaktari wazuri tu wa serikali ambao wamebobea kwenye fani hiyo ambao wengine walikuwa wanafanya KCMC Kama secondment na kuhamishiwa Mbeya baada ya kutofautiana na Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC mwaka 2005 na kwa kuwa wao ni waajiriwa wa wizara ya afya uongozi wa Hospitali ya Rufaa uliwarudisha wizarani. Arguments za walafi wa Wizarani dhidi ya Dr Masau ni Hizi :

1)Hana wataalamu wa kutosheleza kuweza kufanya Major Open Heart Surgeries.

2)Vifaa vichakavu na Havina uwezo wa kufanyakazi ipasavyo.

3)Bei ni ghali kuliko India.

1 na 3= Vina ukweli usiopingika na huko awali kwenye mjadala huu nilisema haya yanajadilika Lakini Dr Masau tangu ameelezwa haya na wabaya wake ameyatatuaje? Suluhisho ilikuwa ni kuajiri au hata kuomba wataalamu wa wizara ambao ni Madaktari Bingwa kwenye fani hiyo wapangiwe kituoni kwake kama secondment kwani wizara inafanya hivi kwenye taasisi mbalimbali yakiwemo mahospitali mengi ya kanisa ikiwemo KCMC, BUGANDO, IFAKARA NK.

Yeye hata hili hakujaribu na anakimbilia kwenye vyombo vya habari, hivi kukimbilia kwenye vyombo vya habari kuendeleza malumbano na hao wabaya wake ni njia muafaka ya kuwafanya wagonjwa wanufaike?

Bei hawezi kushindana na India, Bei za India ni za Chini tena bado pamoja na umasikini wao wanatoa Discount operesheni kubwa ya upasuaji Moyo kwa Dr Masau ni millioni 5 takribani Dola 4 za kimarekani na zaidi , India ni chini ya hapo na tiketi ni bei ya chini dola 400 kwani wanapata discount pia, ambapo gharama za usafiri na matibabu bado haifiki gharama za kwa Dr Masau Hili nalo linazungumzika kama angetumia misaada mengine anayopata toka taasisi mbali mbali kuwafanyia punguzo watanzania wenzake yaani kuwapa unafuu.

Hili Nalo Dr Masau, Hajafanya na kuzidi kuwapa mwanya wabaya wake. Rejeeni dhumuni kubwa la kuazishwa kwa hiyo taasisi. Hebu jiulizeni ni watu wangapi nje ya serikali ambao wamejitahidi kumsaidia Dr Masau ili Wizara iweze kumpa wagonjwa na kukwama. Rais mstaafu alielezwa akaahidi kumsaidia kalifikisha sehemu husika kwa Rais lakini Rais baada ya kuzungumza na watalaamu wa wizara wa kamueleza hayo mambo matatu akagwaya, Mke wa Rais amejaribu kagwaya, wengine wengi kama kina Mh. Getrude Mongela wamekwama.

Namba 2 hapo juu siamini kama hivyo vyombo ni vichakavu bali ninajua ni vya zamani (secondhand) Huko nyuma nilisema cha msingi ni kujiuliza vinafanyakazi yake ipasavyo au la? Bila ya kuleta madhara kwa wagonjwa Kama jibu ndiyo basi uzamani wake si tija nalo hili linazungumzika, nikasema wangekaa hata kutumia wataalamu huru wenye uwezo wa kuelewa ubora wa vyombo husika, Hili nalo amelifanyia vipi kazi? Unajua nini, unapokuwa ktk hali kama hii inabidi uhakikishe mapungufu yako unayafanyia kazi na kuyaondosha ili wahusika ambao wanakuwekea vikwazo wasiweze kupata upenyo wa hilo.

Lakini unapowapa upenyo ndiyo wanautumia kukumaliza huku wao wakiendeleza uovu kwani kupitia huo uovu wao ndiyo wanafanikisha azma yao.

Sasa 70MAINRD, Hivi leo hii ktk hali iliopo kwenye hiyo taasisi ukipewa choice ya kwamba ukafanyiwe open heart surgery ya pili India na Kwenye THI yetu utaenda wapi? Be honesty? Hasa ukizingatia umuhimu wa operation yenyewe?Hivi ulipofanyiwa hiyo operesheni yako kwenye ile hospitali kabla hujapewa dawa ya usingizi uliona Timu iliyojitayarisha kukupatia tiba kule chumba cha upasuaji kwa upande wa madaktari ni mmoja au zaidi? Kwa upande wa manesi, watoa dawa za usingizi, perfusionist Nk walikuwa wangapi? Halafu jiulize Dr Masau ana wangapi? Baada ya operesheni kule Chumba cha wagonjwa mahututi Madras ulikuonaje equipments zake, je Dr Masau ICU yake ipo equipt kuweza kukabiliana na dhoruba ya kuokoa maisha kwa wagonjwa wengi. Umeona Madras na Kama Upo Bongo Umeona na Dr Masau alivyoionyesha kwenye star TV, Je mlinganisho wako ni vipi?

Hebu tuwachane na wizara Ndugu Mengi anapeleka wagonjwa India kwa gharama zake Hivi kwanini na yeye asiwapeleke kwa Dr Masau? Wizara inamuonea na hawa wateja Binafsi nao inakuwaje? Huko nyuma nilizungumzia huduma kama hii inavyotolewa kwa ubora wa hali ya juu Kenya na Dr Masau aliwahi kutembelea kwenye hiyo taasisi wao hawapigishani kelele na serikali wamejipanga vizuri na ubora wao unawapatia wa teja ndani na nje ya kenya.
 
... Suluhisho ilikuwa ni kuajiri au hata kuomba wataalamu wa wizara ambao ni Madaktari Bingwa kwenye fani hiyo wapangiwe kituoni kwake kama secondment kwani wizara inafanya hivi kwenye taasisi mbalimbali yakiwemo mahospitali mengi ya kanisa ikiwemo KCMC,BUGANDO,IFAKARA NK...

KNKCU, unaona sasa. Kama serikali inajua jamaa hana madaktari wa kutosha na serikali inao kwanini isijitolee madaktari hao kufanya kazi hapo THI? Je serikali imewahi kutoa wazo hilo na Dr. Masau akalikataa?


kwa upande wa manesi,watoa dawa za usingizi,perfusionist Nk walikuwa wangapi?Halafu jiulize Dr Masau ana wangapi?Baada ya operesheni kule Chumba cha wagonjwa mahututi Madras ulikuonaje equipments zake,je Dr Masau ICU yake ipo equipt kuweza kukabiliana na dhoruba ya kuokoa maisha kwa wagonjwa wengi.Umeona Madras na Kama Upo Bongo Umeona na Dr Masau alivyoionyesha kwenye star TV,Je mlinganisho wako ni vipi?
Hebu tuwachane na wizara Ndugu Mengi anapeleka wagonjwa India kwa gharama zake Hivi kwanini na yeye asiwapeleke kwa Dr Masau?Wizara inamuonea na hawa wateja Binafsi nao inakuwaje?Huko nyuma nilizungumzia huduma kama hii inavyotolewa kwa ubora wa hali ya juu kenya na Dr Masau aliwahi kutembelea kwenye hiyo taasisi wao hawapigishani kelele na serikali wamejipanga vizuri na ubora wao unawapatia wa teja ndani na nje ya kenya.

KNKCU, kumekuwa na ziara kadhaa za madaktari kutoka nje na timu za upasuaji hapo THI ina maana zote hazina wataalamu wa kutosha? Mwaka jana mwezi februari timu ya "Project Open Heart" walikuja na kutoa mafunzo hapo THI waliwafundisha kina nani?
 
Tabasamu;31640 Mkulima,
Niko nawe pamoja hapa. Ni zaidi ya kukomoana watu wa wizara husika wanajua kukiwa na taasisi inayofanya kazi basi safari za India zitpungua kama siyo kwisha kabisa. Je ni kiasi gani cha pesa watapoteza (utadhani ni halali yao kujipatia) endapo kamisheni wanazojipa hazitakuwepo kwa sababu hakuna safari? Ubinafsi, ubinafsi, ubinafsi tu. Watu wako radhi Watanzania wenzao wafe ilmradi wao wapate cha juu.

Hilo la ubinafsi si upande wa serikali tu bali Hata Dr Masau Dhumuni la yeye kusaidiwa kuazishwa hiyo taasisi ilikuwa ni kuwasaidia watanzania wasio na uwezo sasa inakuwaje leo hii asiwapatie matibabu kwa unafuu na atake millioni 3.5-5, Mlalahoi atazipata wapi hizi? Bado wanaendelea kufa na Taasisi ipo. kwanini asipunguze gharama ili kuendana na kauli mbiu ya uanzishwaji wa taasisi hiyo. Pili kwanini asifanyie marekebisho yale mapungufu ambayo yanaweza kusababisha madhara kwa wagonjwa na kutoa huduma ambayo ni bora au salama angalau kwa level yetu ya Africa au Tanzania.

Sitetei ubinafsi wa Wizara na vile vile sitetei wa Dr Masau kwani vyote ni janga kwa wagonjwa. Lakini kwasababu ni mjadala ninavianisha. Unajua tusichangaye mambo kwasababu serikali haitutendei haki basi tukafumbia mapungumfu ya upande wa pili. Ni bora tukayaanisha ya pande zote mbili na kuona yanatatuliwa na wagonjwa kufaidika.
 
KNKCU,

Kadri unavyoandika ndivyo suala la ubinafsi linavyozidi kujionyesha.

Fahari wawili wapiganapo ziumiazo ni nyasi. Ni ndugu zetu wagonjwa ndio wanaoumia kwa kukosa matibabu. Nchi haina uwezo wa kupeleka wagonjwa wengi India. Ilitakiwa waweke kipau mbele kuongeza uwezo wetu hapo nchini lakini badala ya kufanya hivyo kwa kushirikiana na THI pamoja na kufungua kituo chao wenyewe, wao wameamua kumkomoa Dr. Masau.

Utasema hata Mengi hapeleki hapo, suala ni lile lile, kama serikali inatangaza wazi haina imani na hicho kituo Mengi atawezaje kupeleka wagonjwa wake hapo? Wakifa hata kama wangekufa hata huko India, lawama zote zitakuja kwake.

Serikali inatakiwa ikae na hao THI na kuwasaidia kwa faida ya Tanzania na hilo
ndilo tatizo.

Hata rais anapata ushauri kwa watu hao hao, akipeleka ombi wanakuja na dossier kubwa kubwa na lawama kibao juu ya THI, unafiri huyo rais mtaafu atafanya nini?

Hivi unaelewa kitu kinachoitwa economies of scale? Gharama ya kutibu watu 1000 kwa mwaka inaweza kuwa ni marambili ya ya gharama ya kutibu watu 100 kwahiyo ni rahisi bei kuwa chini kama unapata wagonjwa wengi wanaolipa. Kama kituo hicho kitapata vifaa na wataalamu wa kutosha na kuwa na wagonjwa wengi, gharama kwa mgonjwa itapungua sana maana kuna fixed cost ambazo ni zile zile whether wanatibu wagonjwa 100 au wagonjwa 1000.

Ndio maana nilisema tatizo hapo naliona ni moja tu, kama hana uwezo wa kutibu basi lakini hayo mengine yote yanaweza kutatuliwa kwa kuongea na yana solutions ambazo zinajulikana dunia nzima.
 
KNKCU, unaona sasa. Kama serikali inajua jamaa hana madaktari wa kutosha na serikali inao kwanini isijitolee madaktari hao kufanya kazi hapo THI? Je serikali imewahi kutoa wazo hilo na Dr. Masau akalikataa??
Unajua kwenye hali kama hii ili usaidiwe inabidi ukubali mapungufu yako wewe unaambiwa unamapungumfu unasema sina ,sasa kama huna unataka usaidiwe nini.Hivi wapi uliona wewe ndiyo mtoaji msaada halafu ukae kila kukicha kumbembeleza yule unayetaka kumpa msaada wakati yeye anaona hauhitaji.Halafu huyo unayetaka kumpa msaada kutwa anashinda kwenye vyombo vya habari kupotosha ukweli unaomuhusu.Watu wa makanisa wanaona wanauhitaji wanaomba na wanapewa.Na ndiyo maana kama KCMC Walipoukata msaada wa wizara ,wizara walichukua wataalamu wake na hakukaa kuwabembeleza KCMC.Wakati huko nyuma Mama watoto wangu aliajiriwa kama secondment kwenye hospitali ya kanisa na waliendelea kumtumia bila ya matatizo.Tena pamoja na kulipwa na wizara Kanisa Baada ya kumuona anatoa huduma wakampa na cha juu mbali na wizarani.Hili naomba umuulize na Dr Masau halafu muulize hivi ni kwanini hakai na watu wa wizara kujaribu kuondosha tofauti zao na badala yake anakimbilia magazetini,kwenye TV na Baadhi ya wakubwa kulalamika?Hivi kama anania nzuri ya kutatua tatizo lake kwanini asiwatumie hao wakubwa kuwa kama wasuluhishi wake wa kuweka mazingira mazuri ya mazungumzo na wizara Badala ya kuwafanya kama ni wanaotaka kupitia njia za kutoa Amri.



KNKCU, kumekuwa na ziara kadhaa za madaktari kutoka nje na timu za upasuaji hapo THI ina maana zote hazina wataalamu wa kutosha? Mwaka jana mwezi februari timu ya "Project Open Heart" walikuja na kutoa mafunzo THI waliwafundisha kina nani?
Hiyo ni slogans,Hivi nikuulize kitu kimoja kwa mtu yeyote anayeelewa nini kusomea ubigwa ktk fani fulani Hivi unaweza kufundisha fani ya kuokoa maisha ya mtu tena ya kupasua moyo kwa wiki moja?Hii Labda niite workshop na workshop ni Continuing Education wanapewa wale waliokwisha kuwa na ujuzi huo Kama kuwakumbushia au kuwaelekeza kama kuna jipya katika fani fulani ndani ya Uganga au hata matumizi ya vyombo au dawa mpya , ambavyo havijawahi kutumiwa na wahusika sehemu zao.Kuna kipindi walikuja Madaktari Kutoka nje Marekani kutalii na kujitolea kutibia wagonjwa ni wakati Hospitali inaanza Baada ya hapo hawakurudi tena Prof. Doreen,Dr Cooley na wengine. Hivi kwanini asiwalike tena kwa ajili ya kubweresha Huduma mara kwa mara na kujenga Credibility yake ktk fani.............!
 
KNKCU,

Kadri unavyoandika ndivyo suala la ubinafsi linavyozidi kujionyesha.

Fahari wawili wapiganapo ziumiazo ni nyasi. Ni ndugu zetu wagonjwa ndio wanaoumia kwa kukosa matibabu. Nchi haina uwezo wa kupeleka wagonjwa wengi India. Ilitakiwa waweke kipau mbele kuongeza uwezo wetu hapo nchini lakini badala ya kufanya hivyo kwa kushirikiana na THI pamoja na kufungua kituo chao wenyewe, wao wameamua kumkomoa Dr. Masau.

Utasema hata Mengi hapeleki hapo, suala ni lile lile, kama serikali inatangaza wazi haina imani na hicho kituo Mengi atawezaje kupeleka wagonjwa wake hapo? Wakifa hata kama wangekufa hata huko India, lawama zote zitakuja kwake.

Serikali inatakiwa ikae na hao THI na kuwasaidia kwa faida ya Tanzania na hilo
ndilo tatizo.

Hata rais anapata ushauri kwa watu hao hao, akipeleka ombi wanakuja na dossier kubwa kubwa na lawama kibao juu ya THI, unafiri huyo rais mtaafu atafanya nini?

Hivi unaelewa kitu kinachoitwa economies of scale? Gharama ya kutibu watu 1000 kwa mwaka inaweza kuwa ni marambili ya ya gharama ya kutibu watu 100 kwahiyo ni rahisi bei kuwa chini kama unapata wagonjwa wengi wanaolipa. Kama kituo hicho kitapata vifaa na wataalamu wa kutosha na kuwa na wagonjwa wengi, gharama kwa mgonjwa itapungua sana maana kuna fixed cost ambazo ni zile zile whether wanatibu wagonjwa 100 au wagonjwa 1000.

Ndio maana nilisema tatizo hapo naliona ni moja tu, kama hana uwezo wa kutibu basi lakini hayo mengine yote yanaweza kutatuliwa kwa kuongea na yana solutions ambazo zinajulikana dunia nzima.
Mimi sielewi kipi kigumu kuelewa hayo mazingira wakuyatengeza ni Dr Masau na taasisi yake huoni anawakosa hata wateja wa mengi kwasababu hana credibility na labda mteja ambaye hajui matatizo yaliopo hapo ndiyo anaweza kumpeleka mtu kupasuliwa moyo sehemu ambayo ina matatizo.
Serikali kwa upande wake imefanya kazi ya kumjengea mazingira,mojawapo msamaha wa kodi wa vifaa vyake vyote,Pamoja na kuwa na mapungufu imempatia usajili ili kuweza kufanya operesheni ndogo ndogo zinazowezekana wakati akifanya marekebisho kwa ajili ya Operesheni kubwa kama hizo wanazopelekwa watu India, imemsainia documents za kwanza kwaajili ya msaada wa Dola 350,000 sasa wamegoma kusaini documents zingine za millioni 450 kutoka ujerumani na hapa ndipo Dr Masau alipoanzisha Bifu kwani Wizara wanaona wanatumiwa Lakini hawaoni wananchi kufaidika wala marekebisho kufanyika kwenye kila nyanja iliyotakiwa kubweresha.
Sasa serikali yenyewe imejitoa kwenye kuendesha huduma za afya kwa asilimia mia moja na ndiyo kuna kuchangia gharama kwa wananchi,sasa serikali hii mnataka tena ibebe mzigo wa Dr Masau wakati hata huko anakosaidiwa hatuoni wananchi wamefaidikaje?Sasa serikali isadie Dr Masau,Agakhan,Kariuki,Hindu Mandal, Tumaini Nk sasa si afadhali iendelee na jukumu lake la kutoa huduma na ndiyo Maana serikali inagharimia yake pale Muhimbili kwenye Pediatric Annex wing,na haiwezi kugharamia yake na ya Mtu binafsi. Swala la kwamba wanaoumia ni nyasi ni kweli LAKINI na Dr Masau ni mmoja ya anaoumiza hizo nyasi.Hili swala lilipoanza nilikuwa na sympathy na Dr Masau Lakini nilipolielewa kwa Undani nikafahamu ukweli na mimi ninapofahamu ukweli nitausimamia.Hii ni post yangu ya mwisho kwenye Hii Mada,ushauri mwengine achukue mkopo au aombe msaada wa kifedha,wanataaluma na vifaa bila ya kupitia wizarani,ambwereshe mapungufu then Aombe wagonjwa serikalini na kwa wadau wengine Lions Club ,mengi na NCHI JIRANI Kwa hali ilivyosasa itamuwia ngumu kuvuka kizingiti cha Wizara Labda apate msaada wa wakuu wa Nchi!
 
Mzee Mwanakijiji ,
Heshima yako.
I am interested to know what transpired in the interview na Dr Masau. Unfortunately sio wote tunaoweza ku acess radio yako.
 
Mama Lao...bado sikufanikiwa kumpata...nitawajulisha... hizi wiki chache zilizopita zimekuwa na mambo mengi sana..
 
Date::7/21/2008
Mtaalamu wa tiba ya moyo agoma kuhama jengo la NSSF
Jackson Odoyo na Saida Amini
Mwananchi

MWANZILISHI na Rais wa Hospitali ya Taasisi ya Moyo Nchini (THI), Dk Ferdinand Masau, amegoma kuhama katika jengo la Shirika la Taifa ya Hifadhi ya Jamii (NSSF) anakoendesha shughuli zake.

Dk Masau alisema hayo jana walipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Mikutano katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) mara baada ya kumalizika kwa semina ya madaktari wa moyo barani Afrika.

Dk Masau alisema hawezi kuhama katika jengo hilo kwa sababu NSSF imeshindwa kutimiza makubaliano walioafikiana walipompangisha na kwamba hivi sasa kuna wagonjwa pamoja na mali za THI.

''Kwanza siwezi kuhama katika jengo hilo kwa sababu kuna wagonjwa 15 wamelazwa, kati yao watano wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo wakati wowote.

Pia ndani ya jengo hilo kuna vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Sh1bilioni,'' alisema Masau na kuongeza kwamba alikubalina na NSSF kuwa watatengeneza jengo hilo ili liwe na hadhi ya hospitali ya moyo, lakini walishindwa kufanya hivyo.

Alisema baada ya makubaliano hayo NSSF walimpelekea taarifa kuwa kazi hiyo imeshamalizika hivyo anachotakiwa kufanya ni kukubali kusaini mkataba wa kulipangisha jengo hilo.

''Nilikubali kusaini mkataba kama mpangaji baada ya NSSF kunihakikishia kuwa wamenitengenezea jengo hilo kama nilivyowaeleza, lakini baada ya kusaini na kuingia ndani ya jengo nikagundua kuwa kuna baadhi ya maeneo hayakutengenezwa kama nilivyoyahitaji,'' alisema Masau,

Aliongeza kusema: ''Baada ya kubaini upungufu huo niliwasiliana nao na tukakubaliana kwamba niendelee kulitumia jengo hilo wakati marekebisho hayo yanafanyika, lakini hayo hayakufanyika badala yake nilishangaa wananipelekea taarifa ya kuitwa kwenye kesi mahakamani ikiwa ni miezi miwili baada ya kusaini mkataba.''

Alifafanua kuwa baada ya kesi hiyo kuanza kusikilizwa miezi miwili baadaye hukumu ilitolewa na mahakama ikaamuru aondolewe katika jengo hilo.

Alisema baada ya amri hiyo alimfuata Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambaye aliwataka wayamalize nje ya mahakama chini ya usimamizi wa Wizara ya Kazi Ajira na Maendeleo ya Vijana.

Uamuzi wa kumuondoa katika jengo hilo lilitolewa juzi na shirika hilo katika vyombo vya habari iliyodai kuwa ameshindwa kulipa deni la pango la jengo hilo linalofikia Sh2.3 bilioni.

Sehemu ya taarifa hiyo ilisema kuwa NSSF ilisema inachukua hatua hiyo kwa muujibu wa amri ya Mahakama Kuu (Kitengo cha Ardhi) iliyotolewa Septemba 11, mwaka jana katika shauri namba 158/2007 kati ya NSSF na Taasisi ya moyo Tanzania.

NSSF itatwaa jengo lake lililojulikana kama Hosteli ya Tazara ambayo kwa sasa limepangishwa na THI na kufikia Julai 25, mwaka huu wagonjwa wote na familia zao wanashauriwa kufanya mpango wa mbadala wa hospitali ya kuhamia au kuwahamisha wagonjwa wao kabla ya tarehe hiyo kufika, ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Hata hivyo, kufuatia taarifa za ndani ya NSSF zilizonaswa na Mwananchi zimebaini kwamba serikali ilishawahi kutoa tamko kuwa haiwezi kingilia mgogoro huo na kuwataka waumalize mgogoro huo kama ilivyoamuliwa na mahakama.
 
hii kali!tatizo kodi pango? au ndio anataka kumalizwa ni kiprofessional? kweli watafika wajasiriamali wasio na majina?
 
Huyu vipi aliweka sahihi jengo hata kabla hajaliona? Au ndiyo yale ya waandishi wetu wa habari? Au ni mkono wa UFISADI kama siku zote.
Jamani haya mambo ya Dr. anakuwa mkuu wa sehemu hata chembe ya uongozi hajui haya ndiyo matatizo. Hata kama huna somo la uongozi, inajulikana kuwa hununui PAKA kwenye gunia eti. Inatakiwa hapa apelekwe au meneja au msaidizi wake atayeshughulikia maswala kama haya. Au hata awe na mwana sheria. Kusoma kasoma kweli ila kwenye uongozi mhh. Inanikumbusha yule bwana wa TANROAD anayesifiwa kwa kusoma.
 
GLORIA KRITKOS
Daily News; Tuesday,July 22, 2008 @00:03

The government has said it is ready to support efforts towards making heart treatment accessible and affordable by most Tanzanians. The Minister for Justice and Constitutional Affairs Mr Mathias Chikawe made the assurance to participants of the fifth African Heart Seminar at the Tanzania Heart Institute in Dar es Salaam yesterday.

He told over 150 medical experts from around the world at the seminar aimed to strengthening fight against cardiac diseases in Africa that Tanzanian government was ready to support any heart institute. Mr Chikawe warned that the recent medical reports, which suggested that cardiovascular diseases were likely to succeed HIV/AIDS as the major killer disease in Africa must be heeded and measures be taken.

He appealed to the participants to pay concerted efforts in creating adequate public awareness about the diseases '‘as a viable stage of the move towards wiping out the killer disease in Africa.'' He said the Tanzania Heart Institute is trying to develop its capacity to treat heart patients, who are unable to afford costs of being treated abroad.

Communities still find it hard to mobilize enough funds to assist their relatives undergo heart operations outside the country because of persisting poverty, according to heart specialists at the Tanzania Heart Institute (THI) THI's President Dr Ferdinand Masau said that although the problem existed for years, very few people have managed to develop strategic plans and strategies for financing treatment of heart patients. He appealed to African medical experts to pull their knowledge and resources together to fight the disease.
 
NSSF wametoa tangazo kwenye magazeti wakimtaka Dr. Masau na Taasisi yake waondoke kwenye JENGO lao na watafute pa kuwahifadhi wagonjwa waliolazwa pale wakisubiri upasuaji. NSSF ni TAASISI ya UMMA, huduma zinazotolewa pale ni kwa Watanzania wote, wameshindwa nini kuelewana na THI ili huduma hii muhimu na ghali sana kwa WANANCHI ikaendelea kutolewa?
 
Back
Top Bottom