Sakata la Dr. Masau: Msimamo wa Serikali na Hatima ya Taasisi ya Moyo (THI)

- Hebu naomba ulete walau links zenye kuripoti kuwa Prof Masau anafanyiwa Fitna

-Kama hizo ftna zipo ni zipi?

-Zimefanywa na nani?

-Je huyo profesa kalalamika? kupitia authority zipi?

-Hizo authority zimetoa tamko gani?

-Kama si prof Masau, je hiyo THI imefanyiwa fitna vipi, na nani?

ni hayo tu kwa sasa walau tupate picha kamilimheshimiwa
DrWho wakati mwingine unaboa sana kama huna cha kuchangia ni afadhali kuwa msomaji tu. Umepewa articles usome hutaki labda sababu ni ndefu badala yake unakuja na maswali yako mara mia mia. Lunyungu unaweza kuja kutusaidia na huyu jamaa yako?
 
Majibu ya Mhe. Naibu hayahusiani na madai ya sasa ya Dr. Masau. Nilitaka kupata mtu ambaye anaujuzi wa mambo ya THI ambaye anaweza kuzungumza bila kuogopa na hivyo kuweza kubalance nitachozungumza na Dr. Masau. Hivi sasa ni maneno yenu wewe na KNKCU na sijui yana ukweli kiasi gani maana sijaona madai mnayoyatoa mahala popote kwenye maandishi. Hakuna mfanyakazi aliyejitokeza hadharani na kusema Dr. Masau hawalipi mshahara, na hakuna mahali ambapo wizara imesema hapo THI pana daktari mmoja tu? Wala madai ya ukabila sijaona mahala popote isipokuwa kwenye maneno yako. Hivyo, ningepata mtu ambaye anajua kwa hakika kinachoendelea. Hata taswira anayoiacha KNKCU kuhusu uwezekano wa kuwepo kwa matumizi mabaya ya fedha kitu ambacho hata kwenye maandishi yako unaashiria, sijawahi kuona hata kiongozi au wizara ikiulizia.

Madai ya wizara yamehusiana na vifaa na uwezo wa taasisi hiyo zaidi kuliko nani anatoa huduma hiyo. Kama serikali ingekuwa na mashaka juu ya nafsi ya Dr. Masau bila ya shaka wangesema hivyo. Na kama wangetaka ripoti ya matumizi ya fedha ya taasisi hiyo bila ya shaka wangepewa. Tatizo liko wapi? Hapa ndipo ninapotaka upande wa pili!
Mwanakijiji!
Unachopaswa kuelewa serikali haiwezi kuhoji Fedha ambazo si zao,Mimi kama mwananchi ambaye ninajua fika kwamba Dr Masau anatangaza ulalahoi wa Tanzania kujipatia Funds halafu bado anawalipisha watanzania kupata matibabu.Sijui unataka ushahidi gani?Muulize hayo maswali na tunasubiri!Haya hili lifumbie macho na yale matembezi ya mshikamano yaliyomshirikisha Mh.Getrude Mongela na kupatikana million 169 AMEZIFANYIA NINI?Hili nalo unaona ni sawa bado watu wakuchangie kiasi kama hicho cha fedha kwa lengo la kuwatibu masikini halafu bado unataka masikini hao walipe kuwapatia tiba?Hilo nalo kataa,Fikiria kwanini serikali haitaki kusaini makaratasi ambayo yatamuwezesha Dr Masau kupata hizo millioni 450 kutoka kwenye Taasisi ya kijerumani hili kalisema mwenyewe Dr Masau nalo likatae............Kwanini yeye Dr Masau haelezi wapi amepeleka zile dola 350,000 alizowahi kupewa na taasisi moja ya ulaya ili atoe huduma kwa wagonjwa ni wagonjwa wangapi wamefaidika na hilo?
Kuhusu la wataalamu ni kweli madai ya wizara kwani zaidi ya Dr Masau ,Je kuna wataalamu wengine wangapi wa fani yake kwenye hiyo Taasisi ambao wanatoa Huduma.Sasa ukitaka ukweli mwanakijiji Dr Masau pekee yake hawezi kufanya upasuaji mkubwa wa Moyo au kwa Lugha ya Kitaalamu (OPEN CARDIAC SURGERY),Ili upasuaji wa aina kama hii kufanyika unahitaji timu ya upasuaji sasa Dr Masau atufahamishe timu yake ya upasuaji mkubwa ni ipi na wamesomea wapi?Kinachofanyika pale THI ni upasuaji mdogo wa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu kwa Lugha ya kitaalaamu (Minor Cardiovascular Surgeries).Ninachokueleza ninafahamu mpaka hivi sasa Tanzania ina wataalamu wangapi wa fani ya kama ya Dr Masau na katika hao wenye utalaamu kama wake Hakuna hata mmoja ambaye ameajiriwa na Taasisi Yake au Kufanyakazi hata part time.Sasa wewe unataka wizara iseme THI Kuna Dr MMOJA Lakini kumbuka wizara imesema kwamba hakuna wataalamu wa kutosha.
Kuhusu vyombo kuwa chakavu hili pamoja na wizara kulisema hapa hawakumtendea haki kwani swala si uchakavu wa vyombo swali la msingi hivyo vyombo vinafanyakazi husika bila ya matatizo au kuleta madhara?Kama vinaweza basi kwa uwepo wetu Dunia ya tatu basi si mbaya kwa kuanzia na hivyo kwani at the end of the day what counts ni mgonjwa amepata huduma husika na kuokoa maisha.Kipi Bora mgonjwa kufa kwa kukosa huduma au kupewa huduma na vyombo vinavyoitwa chakavu na kuokoa maisha yake?
Muulize Dr Masau aliajiri Dr wa kichina ,je ni kwanini Daktari huyo wa kichina aliamua kuacha kazi?
Unasikia Mwanakijiji,Sipendi watu ambao wanaanzisha NGO zao na kuomba misaada na halafu walengwa hawanufaiki na misaada hiyo na Dr Masau ninamuona ni mmoja wapo Labda aje na Facts za watu aliowahudumia kutokana na funds za matembezi ya mshikamano Milioni 169 na zile dola 350,000 Hapo nitamtoa kwenye hilo kundi.Vile vile aje na vielelezo vya jinsi gani wananchi watanzania wanafaidika na msaada wa gari la wagonjwa aliloomba kwa serikali ya japan kupitia ubalozi wa Japan Dar kwa kivuli cha kutaka kuwasaidia watanzania yaani walalahoi.NATAKA ANIFAHAMISHE HIVI HII GARI ILISHAWAHI KUCHUKUA MGONJWA BURE SI KUTOKA HOSPITALI YAKE TU HATA KUMPELEKA HOSPITALI NYINGINE. au kam si bure hata kwa kuchangia tu gharma ya mafuta tu yaani kwa gharama nafuu.Muulize ni kwanini ameweka viwango vya ukodishaji wa hilo gari wakati alipoomba alisema ni la kusaidia wagonjwa?Je vifaa hivyo vyote vya upasuaji alipewa bure Marekani na Ujerumani kwa mgongo wa kusema watanzania ni masikini hawawezi kulipia matibabu sasa inakuwaje Leo anawadai malipo makubwa ya utoaji huduma hiyo? Kwanini basi kama nikuchaingia asiwatoze kiasi kidogo na kwa ambao hawana asiwafanyi bure kwani si ndio dhumuni kuu la kuanzishwa Taasisi Husika.
 
Majibu ya Mhe. Naibu hayahusiani na madai ya sasa ya Dr. Masau. Nilitaka kupata mtu ambaye anaujuzi wa mambo ya THI ambaye anaweza kuzungumza bila kuogopa na hivyo kuweza kubalance nitachozungumza na Dr. Masau. Hivi sasa ni maneno yenu wewe na KNKCU na sijui yana ukweli kiasi gani maana sijaona madai mnayoyatoa mahala popote kwenye maandishi. Hakuna mfanyakazi aliyejitokeza hadharani na kusema Dr. Masau hawalipi mshahara, na hakuna mahali ambapo wizara imesema hapo THI pana daktari mmoja tu? Wala madai ya ukabila sijaona mahala popote isipokuwa kwenye maneno yako. Hivyo, ningepata mtu ambaye anajua kwa hakika kinachoendelea. Hata taswira anayoiacha KNKCU kuhusu uwezekano wa kuwepo kwa matumizi mabaya ya fedha kitu ambacho hata kwenye maandishi yako unaashiria, sijawahi kuona hata kiongozi au wizara ikiulizia.

Madai ya wizara yamehusiana na vifaa na uwezo wa taasisi hiyo zaidi kuliko nani anatoa huduma hiyo. Kama serikali ingekuwa na mashaka juu ya nafsi ya Dr. Masau bila ya shaka wangesema hivyo. Na kama wangetaka ripoti ya matumizi ya fedha ya taasisi hiyo bila ya shaka wangepewa. Tatizo liko wapi? Hapa ndipo ninapotaka upande wa pili!
Right on Mwanakijiji,
Mama Lao anaweza kuwa na hoja f'lani lakini ambazo zimejikita tu kwenye personal grudges. Labda ana ndugu yake ama yeye mwenyewe amewahi kutimuliwa pale. Sishangai kwa Masau kulalamikiwa na Watanzania kuhusu maslahi na mazingira ya kazi kwani WTZ ni wavivu na wababaishaji. Hawafanyi kazi ila wanataka malipo. Ukiwawajibisha watakwambia manyanyaso.
Hoja za serikali kuhusu THI zilikuwa ni kuhusu vifaa, na ndio suala ambalo Aisha Kigoda alipotoa tamko la serikali alisema. Dr Masau alijibu hilo na akatoa maelezo kuhusu vifaa walivyonavyo (latest technology) katika masuala hayo. Wakati waziri huyo anatoa tamko lake hakuwa hata ameviona vifaa vyenyewe.
Ni vizuri mwanakijiji utazungumza naye aseme mwenyewe. Katika masuala utakayomuuliza usisahau 1. Hoja za serikali kuipinga 2.Vifaa kwenye taasisi hiyo 3. Matumizi mabaya ya misaada na 4. Manyanyaso dhidi ya wafanyakazi.
 
Tabasamu, hilo la manyanyaso dhidi ya wafanyakazi limewahi kusemwa wapi kabla ya hapa JF? maana nisije kurukia treni lililoanza kuondoka!
 
Tabasamu!
Aliyozungumza Mama Lao yana ukweli kutokana na ufahamu wangu wa KARIBU.Kuhusu wizara ya afya kwenye swala la vifaa nafikiri wamemuonea kwasababu uchakavu si hoja kama vifaa ni imara na vinatoa huduma lengwa.Halafu pale wizara ya Afya Hakuna mtu mwenye utaalaamu wa kuvihakiki hivyo vifaa sasa sijui walielewa vipi kwamba havifai wakati hakuna mjuzi au mwenye ufahamu wa vifaa vinavyotoa huduma husika.Haya ni mapungufu ya upande wa wizara.Mapungufu ya Dr Masau ni kutokuwa na wataalamu wa kutosha kwenye Taasisi yake ni kweli,Kuomba misaada kwa kauli mbiu ya kutaka kuwasaidia wa tanzania lakini badala yake hasaidii anafanya biashara hili kwangu ni kosa.Si lalamikii taasisi yeyote inayouza huduma kwani tunaelewa kusudi kuu ni kufanya biashara ,Sasa Dr Masau naye ninaona ni vyema akaacha kuomba misaada chini ya kivuli cha kusaidia walalahoi na badala yake afanye biashara.Na kama bado anaona anataka kutoa msaada na kupewa misaada basi atoe huduma bure au kwa kuchangia gharama nafuu ili kuendesha taasisi kwa ufanisi na bado vile vile aajiri watalaamu waliobobea kwenye fani husika ili asaidane nao ktk kutoa huduma Bora na Si Bora HUDUMA.
 
Tabasamu, hilo la manyanyaso dhidi ya wafanyakazi limewahi kusemwa wapi kabla ya hapa JF? maana nisije kurukia treni lililoanza kuondoka!
Mwanakijiji !
Mimi simjui Mama Lao,Lakini kwasababu ameongelea kitu ambacho ninakifahamu kipo ndiyo maana nimekuja kuikazi hoja yake!
Wewe si uliomba watu walete maswali yameletwa unaanza kuhoji hayajawahi kuzungumzwa kokote,Yamezungumzwa JF TU ni kwasababu yanafahamika.
Mimi mwanzoni nilisema ningeleta maswali yangu kwenye email yako LAKINI niliposoma Maelezo ya MAMA LAO Nikaona amegusia karibu kila upande niliotaka kujengea maswali yangu ndiyo nikaona hakuna tena haja ya kutuma maswali bali kuyaweka hapa kwasababu msingi wa maswali yangu ulishajengwa hadharani.
 
Tabasamu, hilo la manyanyaso dhidi ya wafanyakazi limewahi kusemwa wapi kabla ya hapa JF? maana nisije kurukia treni lililoanza kuondoka!

Mwanakijiji,
Si kila jambo lina mwanzo? Hata mimi pia ndio nimelisikia humu kwa mara ya kwanza tangua nianze kusikia kadhia hii. Bila shaka unaweza kumwuliza na tena ukamwambia limetoka jambo forums, kama hajawahi kupokea malalamiko kama hayo atasema.
 
Kulipa mishahara ni tatizo kwake,Mwanakijiji jaribu kuwapata baadhi ya wafanyakazi wake pale taasisi kuna wengine ni watoto wa dada zake pia wanafahamu mjomba ulipaji wake wa mishahara ni wataabu na wao wanafanya hapo hapo.
 
nawasikia... kitu kimoja bado hakijaniingia vizuri.. hivi hawa wataalam wa kaliba ya kina Dr. Cooley na wengine kweli wanaweza kujiassociate na institution ambayo ina vyombo chakavu, haina wataalamu wa kutosha na yenye ubadhirifu? au hawajui nini kinaendelea?
 
halafu namba waliyonayo kwenye website is a wrong number kuna mtu mwenye namba sahihi ya kituo?
 
nawasikia... kitu kimoja bado hakijaniingia vizuri.. hivi hawa wataalam wa kaliba ya kina Dr. Cooley na wengine kweli wanaweza kujiassociate na institution ambayo ina vyombo chakavu, haina wataalamu wa kutosha na yenye ubadhirifu? au hawajui nini kinaendelea?
Mwanakijiji unanifanya nicheke !!!
Hao wametoa msaada vyombo ambavyo vimeshatumika na hawakutoa vyombo au vifaa vipya.kwangu hakuna kibaya kwani hata magari tunanua second hand Kama nilivyosema awali cha msingi ni vinafaa kutoa huduma au la?
kwanini isiwezekane Dr Cooley kushirikiana na taasisi ambayo yeye mwenyewe si tu anashirikiana bali ameshiriki kikamilifu kuiunda na kuisajili kwa MAREKANI,Lakini hata usiamini ndiyo huyo huyo Dr Cooley na kundi lake waliotupa hivyo vifaa vya zamani(kwa mtizamo wa wizara Chakavu)
 
Kazi Kipimo cha Utu,

Hapo ndipo Watanzania tunapochemsha, kutegemea kwamba investor Mtanzania mpaka aje na maajabu ndio aonekane wa maana.

Kila nisomavyo baadhi ya maoni hapa yanazidi kunionyesha jinsi tusivyo na msaada kwa Watanzania wenzetu wanavyotaka kufanya mambo ya maana.

Huyu jamaa wala haitakiwi kulumbana naye kwenye vyombo vya habari badala yake inatakiwa kukaa naye chini na kujua ana uwezo kiasi gani? Anashindwa nini? Je ni kweli ana uwezo au ni tapeli tu? Kama ana uwezo je kwanini anakwama na asaidiwe vipi? Misaada sio lazima pesa na badala yake inaweza kuwa mawazo au kuambiwa lazima uajiri madaktari kiasi fulani wenye uwezo kama wako nk.

Jamani kuanzisha biashara sio kitu lelemama. Bila msaada wa kutosha watu wengi wanaamua kukimbia. Je wale jamaa wa google wangepondwa na kila mtu leo hii technology ya search engines ingelikuwa wapi? Walisota kweli kweli
kabla ya kufanikiwa, sasa kila mtu anaona wao poa.

Kama huyu Dr. ana uwezo basi serikali inatakiwa imsaidie iwezavyo na wakati
huo huo kumpa ushauri juu ya nini arekebishe.

Kwa mawazo haya ya kutaka mpaka kila kitu kiwe OK ndio watu wajue unafanya la maana kweli tunapotoka.

Pia suala la kutibu bure linatokana na kama hicho kituo kinapata pesa za kutosha. Hata asipotibu bure, hata gharama zake ziwe sawa na India bado yeye ana create jobs directly and indirectly, bado yeye analipa kodi na pia bado yeye ni Mtanzania. Hivi Uzalendo umeishia wapi? Kitu tu ambacho hatuwezi ku compromise ni afya za Wateja wake, kama hana uwezo kweli hapo ni issue lakini haya mambo mengine yote naona anaweza kusaidiwa kwa faida ya nchi.
 
Unajua Hakuna kitu kibaya kama kutokuwa mkweli,Anachotakiwa Kufanya Dr NI KUREKEBISHA KASORO ALIZONAZO Kabla ya kutupa lawama kwa serikali au wizara.Vile vile anatakiwa kama anaomba misaada kwa ajili ya kusaidia walalahoi basi iwafikie walengwa na si vinginevyo.Kama umepewa milioni 169 kwa kusaidia wagonjwa kwa kuwapa huduma wape na si vinginevyo!
 
mkulima.. ulichosema hapo kinaitwa hekima! Hilo ndilo lilikuwa hasa lengo la mada hii, kwamba badala ya kulumbana naye na kumfanya aonekane "si kitu" serikali ingekaa mara moja na kuzungumza. Kama waliweza kukaa na Haki Elimu licha ya kuikandia hiyo taasisi kinawashinda nini kukaa na THI. Nakumbuka waliapa kuwa Haki Elimu haitafunguliwa hadi jamaa "waombe msamaha" watu wakakataa. Hadi ikawa ni aibu kwa serikali! Pia tukumbukue kuwa THI ndio taasisi pekee ya moyo Tanzania, kwanini tusingeiwezesha ili iwe ya kisasa zaidi? Baada ya muda si mrefu tutakuwa na taasisi nyingine mbili ambazo serikali itapeleka wagonjwa huko n.k na hilo litamnyima Dr. Masau wateja na hatimaye ataamua kuifunga!

Endapo Dr. Masau ataamua kuweka manyanga chini na kurudi kule anakohitajika, basi tujue Tanzania tumepoteza zaidi kuliko kugain. Inakuwaje tuwapeleke madaktari wanafunzi kwenda India wakati tuna mtaalamu ambaye anashirikiana na wataalam wa hali ya juu hapo hapo nchini. Kwanini Serikali isingefanya mpango na Dr. Masau ili madaktari wa Kitanzania wajifunze chini ya Dr. Cooley au mabingwa wengine hapo Texas Heart Institute kwa gharama yenye punguzo ukilinganisha na India?

Hofu yangu ni kuwa kuna kitu ambacho hakiko sawa.. and we are just scratching the surface!
 
Ifuatayo ni barua ya Dr. Masau kwa chama cha Thoracic Surgeons. Barua hii iliandikwa 2003, it give some insights kuhusu THI
 
Attachments

  • letterofmasau.pdf
    18.6 KB · Views: 126
Mzee Mwanakijiji,

Hapo umenena na ndivyo nchi inavyotakiwa kufanya mambo yake. Tusipoangalia tutaishia kulaumu watanzania wenzetu mpaka tutabaki na watu
wanaojali matumbo yao tu.
 
Mzee Mwanakijiji,

Asante kwa hiyo barua kweli naona inatoa mwanga kidogo. Hayo ndio
matatizo yanayowakumba wawekezaji wengi wa ndani. Hapo mkopo usije kushangaa interest ni 25% wakati angepata udhamini na kukopa nje
kama AB huenda interest ingelikuwa asilimia 5.

Watu wanaweza kudhani anapata misaada na kutumbua kumbe mwenzetu anaumiza kichwa kuhangaika na namna ya kulipa mishahara na kulipa madeni badala ya kutibu wagonjwa.
 
Ifuatayo ni barua ya Dr. Masau kwa chama cha Thoracic Surgeons. Barua hii iliandikwa 2003, it give some insights kuhusu THI

Mwanakijiji !
Hakuna mtu analumbana na Dr Masau bali yeye ndiye anayelumbana na Wizara na Kibaya zaidi kupitia vyombo vya HABARI Wakati akielewa anamapungufu. ktk hiyo Barua yake hapo ameeleza mapungufu yake Lakini tunachotakiwa kujiuliza TANGU 2003 Na sasa 2007,Je kati ya matatizo aliyoyaanisha ni mangapi yametatuliwa na hasa hilo la wataalamu.
Ninatahadharisha tusijenge mapenzi tu ya kuona Fulani anaonewa au hapewi msaada.Ninachouliza viongozi wa serikali wanapofuja fedha za walipa kodi au za misaada tunalalama Lakini tunapohoji Dr Masau ametumiaje fedha za Msaada dola 350,000 na zile za Matembezi ya mshikamano millioni 169 ambapo lengo ilikuwa kuwapatia wagonjwa msaada wa matibabu?Je watanzania ambao wanahitaji tiba na ndiyo lengo la msaada wa hizo fedha wamefaidikaje,Tukihoji hivyo ni kwamba tunalumbana na hatutaki watanzania wenzetu kunufaika au hatupendani.Kwa kifupi wizara ina mapungufu yake Lakini na Mtaalamu wetu naye ana ya kwake.Kama Unafikiri kurudi Marekani ni rahisi na kupata hiyo kazi kama unavyodai kwanini anashindwa kurudi MAREKANI,Wakati wagonjwa hapati na ana uwezo wa kurudi na kufanyakazi,Unafikiri akirudi marekani hizo Fedha za misaada atazipataje?Dr Masau anajua nini anafanya!Ninachotaka kusema ni kwamba ninayasema haya kwasababu ninataka watanzania wenzangu wanufaike kwani mnachosahau Mkulima na Mwanakijiji watanzania ni zaidi ya Dr Masau kwani hao walengwa wa misaada anayoomba ni Watanzania tena wenye shida na maradhi yanawanyungu'unya.
 
!

Endapo Dr. Masau ataamua kuweka manyanga chini na kurudi kule anakohitajika, basi tujue Tanzania tumepoteza zaidi kuliko kugain. !
Hebu niweke sawa watanzania wanafaidika vipi na kuwepo kwa DR Masau wakati misaada inapatikana Lakini haiwafikii na kuwawezesha angalau walalahoi kutibiwa bure,Kama ajira vile vile za kubabaisha toka kwake.
!Inakuwaje tuwapeleke madaktari wanafunzi kwenda India wakati tuna mtaalamu ambaye anashirikiana na wataalam wa hali ya juu hapo hapo nchini. Kwanini Serikali isingefanya mpango na Dr. Masau ili madaktari wa Kitanzania wajifunze chini ya Dr. Cooley au mabingwa wengine hapo Texas Heart Institute kwa gharama yenye punguzo ukilinganisha na India?

Hofu yangu ni kuwa kuna kitu ambacho hakiko sawa.. and we are just scratching the surface!
Madaktari waliopelekwa India si Madaktari wanafunzi ni Madaktari Bingwa ktk fani ya upasuaji wa Jumla au kwa Lugha ya kitalaamu (General Surgeons), watoa usingizi, perfusionist,manesi wa upasuaji Nk. hii ni timu ambayo imeenda kujinoa zaidi kwenye Moyo tu ili kuhakisha utoaji huduma bora za tiba na ufanisi unapatikana, na kwenye eneo hili ndiyo Dr Masau aliposhindwa.
Kuhusu Gharama za India ni nafuu ukilinganisha na kwa Dr Cooley.
 
Mzee Mwanakijiji,

Hapo umenena na ndivyo nchi inavyotakiwa kufanya mambo yake. Tusipoangalia tutaishia kulaumu watanzania wenzetu mpaka tutabaki na watu
wanaojali matumbo yao tu.
Vipi katika watu wanaojali matumbo yao Dr Masau hayumo au?kwanini anaomba misaada kwa jina la kuwasaidia watanzania wenye matatizo ya moyo lakini bado anawalipisha Huduma?
 
Back
Top Bottom