Sakata la Bandari: Serikali imepoteza mvuto na imani ya wananchi?

Aug 31, 2010
9
13
Tukiwa bado tunaendelea na mjadala wa uwekezaji wa bandari na kampuni ya DP World, lipo fundisho kubwa ambalo kama jamii tunapaswa kujifunza. Ukiachilia mbali suala la maudhui ya makubaliano haya, ambapo kuna pande mbili zenye mitazamo tofauti, kuna suala lingine ambalo kwa mtazamo wangu linahitaji kupewa uzito stahiki.

Suala hili limedhihirisha ni kwa kiwango gani kama jamii, tumepoteza uaminifu (trust) na imani (credibility). Sakata hili linadhihirisha wazi kuwa tumepoteza imani na uaminifu miongoni mwetu, katika taasisi zetu na serikalini. Hakuna mtu anayemuamini au mwenye imani na yoyote yule.

Nilitaraji, pale inapotokea mgongano wa mawazo, viongozi wakuu wanapotoa ufafanuzi, basi jambo hilo litaeleweka na litakuwa limekwisha. Kwa Bahati mbaya, hivyo sivyo, hata pale viongozi wakuu na taasisi mbalimbali zilipojaribu kutoa ufafanuzi bado hazikuaminika na bado maswali mengine yamezidi kujitokeza.

Kwanini hali hii?

Hali hii inatulazimisha tufanye tafakuri ya kina ni mambo gani yamesababisha tufike hapa tulipo?

Dhumuni la makala hii ni kujadili sababu ambazo husababisha kuvunjika kwa au kupotea kwa imani na uaminifu. Swali muhimu ambalo tunajaribu kulijadili ni mambo gani ambayo yamesababisha kuondoka kwa uaminifu na imani?

Zilongwa mbali na vitendo mbali: Viongozi wanapokuwa matendo yao na vitendo vyao ni mbingu na ardhi, hali hiyo husababisha kuondoka kwa imani na uaminifu. Wanasiasa wengi wamekuwa wanayohubiri si yale ambayo wanayatenda. Hali hii inaweza kabisa kupelekea wasiaminike tena. Hivyo kama tunataka kurudisha imani na uaminifu, ni vyema kwa wanasiasa wakapunguza pengo kati ya maneno yao na vitendo vyao.

Kutotimiza ahadi: Wanasiasa wengi wakati wa uchaguzi nahata wakati mwingine, husimama katika majukwaa na kutoa ahadi nyingi na kubwa. Bila kuangalia uwezo wa kutekeleza ahadi hizo. Ilani za vyama vya siasa mara nyingi husheheni ahadi na maneno matamu sana kwa wapiga kura. Kwa Bahati mbaya ahadi hizo kwa miongo na miongo huwa hazitekelezwi. Hayati Rais wa awamu ya tatu, Mheshimiwa Benjamini Mkapa alipoingia madarakani, alisema kuwa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) haitekelezeki na imesheheni ahadi nyingi mno. Alilazimika kuunda tume ili ifanye mapitio ya ilani hiyo.

Lakini pia mwaka 2010; Ilani ya CCM ya uchaguzi mkuu wa 2010, ilani ambayo ilinadiwa na Hayati Mh. Dr. John Pombe Magufuli, iliwaahidi Watanzania kuwa iwapo serikali ya CCM itapewa dhamana ya kushika dola basi watakamilisha mchakato wa kuandika katiba mpya, mchakato ambao ulianzishwa na mtangulizi wake Mh. Jakaya Kikwete. Ni jambo la kusikitisha sana! Baada ya kuingia madarakani, Rais Magufuli alisema kuandika katiba mpya sio kipaumble chake. Huu ni mfano mmoja tu wa namna viongozi hawatekelezi ahadi zao na kuondoa imani na uaminifu kwa wananchi. Baadhi ya kauli mbiu ambazo zinadhihirisha pengo kubwa kati ya maneno na vitendo: ‘Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania’; Maji safi na salama kwa wote ifika mwaka 2000, ‘Tanzania ya Viwanda’, ‘tutajenga uchumi wa gesi’, tumetaja mifano michache.

Kauli za uongo: Si kiongozi tu, bali mtu yoyote anapokuwa si mkweli hupoteza Imani na uaminifu wake. Katika moja ya mafundisho ya Mtume Muhammad S.A.W. ni umuhimu wa kuwa mkweli na kusema ukweli. Katika mafundisho yake tunafundishwa kuwa Mtume aliwahi kusema kuwa: alama za mnafiki ni tatu. Anapozungumza husema uongo; anapoahidi hatekelezi ahadi yake na anapoaminiwa haaminiki. Iwapo tunataka kurudisha imani na uaminifu, basi ni vyema sote kwa ujumla na hasa viongozi kusema ukweli, kutekeleza ahadi na wanapopewa dhamana basi waheshimu dhamana walizopewa. Ni muhimu sana kwa kiongozi kutoa kauli thabiti na kuwa na msimamo na muendlezo kwa yale anayoamini na kuyatamka. Ugeugeu unaweza kuondoa imani na uaminifu.

Itakumbukwa, mwaka xxx wakati wa sakata la “makinikia” ambapo wananchi waliahidiwa na viongozi wa juu kabisa wa nchi – Rais wa wakati huo kwamba watapitia mikataba na kuhakikisha neema stahiki inarejea kwa watanzania na ikafikia hata kumithilisha na ahadi ya kila mtanzania kupata “noah”. Lakini sote tunatambua hivi karibuni tuliona mwenendo wa kesi ambapo Profesa Mruma alivyokuwa anabanwa katika Mahakama na hukumu ambayo imeigharimu nchi. Hivyo neema ile iliyoahidiwa imegeuka gharama kubwa zaidi kwa nchi.

Kutokubali kuwajibika au makosa: Wengi wetu hudhani kuwa kukubali kosa ni kuonyesha kuwa ni wadhaifu! Hivyo tunajipa sifa ya uungu kuwa sisi hatukosei, hatuna mapungufu, hatufanyi makossa na tunakataa kuwajibika kwa makossa tuliyotenda. Kwa kweli, ni ushujaa mkubwa kwa kiongozi au yoyote yule kukubali kosa, kukubalin kukoselwa na kuwajibika kwa makossa tunayoyafanya. Hakuna binadamu asiyefanya makossa. Ni Mungu tu ambaye sio mkosaji. Pale viongozi wanapokataa kuwajibika kwa makossa ya wazi wazi waliyoyafanya, hupoteza Imani na uaminifu kwa watu. Tabia hii pia hujenga kiburi na kuamini kuwa unajua kila kitu. Ni vyema viongozi na yoyote yule wakati wote ukakumbuka kuwa huwezi kuwa mkamilifu na pale unapokosea basi kiri makosa na ikibidi wajibuike kwa matendo yako. Hiyo itakuwa heshima, imani na uaminifu.

Ni muhimu sana kwa viongozi kukiri kuwa wanayo mengi ya kujifunza kutoka kwa wanaowaongoza. Ni muhimu wakawapa muda wa kutoa maoni yao na muhimu zaidi kuwasikiliza kwa mtazamo chanya wa kujifunza. Ni kiburi cha hali ya juu kuamini kuwa una majibu ya changamoto zote zinazowakabili wananchi. Sikiliza na jifunze kutoka kwao.

Mambo mengine ambayo yanamomonyoa imani na uaminifu miongoni mwa watu ni kushindwa kujibu hoja na maswali, kutoa maelezo ambayo yanajichanganya na kujikanganya, kutoa visingizio badala ya kukubali kuwajibika, kuacha kwa makusudi taarifa muhimu, kutoeleza pande zote mbili za shilingi yaaniza faida na hasara, kudhani kuwa ni mtalaam wa kila kitu, na kutoa taarifa ambazo hazina muendelezo, na hazina uhakika.

Katika suala hili la uwekezaji katika wa bandari na DP World, yapo mengi ambayo yamejitokeza. Lazima tukubali kuwa tumepoteza uaminifu na imani kwa taasisi, serikali na viongozi. Hali hii ni hatari. Tunatakiwa tuiamini serikali na viongozi wetu.

Ili tuweze kurudisha Imani na uaminifu ni vyema masuala hapo juu yakafanyiwa kazi. Serikali haina budi kuangalia tena mkakati wake wa mawasiliano. Ni nani mtu sahihi wa kutoa ufafanuzi? Anaaminika? Ana heshima mbele ya jamii? Na je taarifa zitolewe wakati gani? Na maudhui yake yawe ni yapi?

Lakini hili lifungue pia macho viongozi, wanapashwa wajihoji ni namna gani wanapashwa waenende kurudisha imani yao kwa jamii. Viongozi wajiangalie namna wanavyoishi, kauli zao, matendo nk.

Katika sakata hili kwa mfano, tumeshuhudia watoa ufafanuzi ni wengi sana na wote wamekuwa wakitoa ujumbe ambao unachanganya au unapingana. Ipo haja ya kuwa na mkakati madhubuti wa namna ya kuwasiliana na umma. Tuwe wanyoofu na wa kweli ili tuweze kurudisha Imani na uaminifu ambao unazidi kutoweka kwa kasi.

Kuaminiana na jambo muhimu sana katika maendeleo yetu.
 
Katika suala hili la uwekezaji katika wa bandari na DP World, yapo mengi ambayo yamejitokeza. Lazima tukubali kuwa tumepoteza uaminifu na imani kwa taasisi, serikali na katika maendeleo yetu.
Mvuto ulitoweka tangu 1995 hayati mrema alikua ashike kijiti kabla ya kuingiliwa kati na kupindua meza!!
 
1. Zilongwa mbali vitendo mbali.

Wanachosema sio wanachotenda.

2. Alama tatu za mnafiki.
-kusema uongo
-akiahidi hatekelezi
-akiaminiwa haaminiki.

N.k
 
Watanzania wanachohitaji ni maendeleo,na wepesi katika kila sekta ya kiutendaji, hayo ya kupoteza imani hayapo!,ni ya kimihemko tu.
 
Ikiwa Hali IPO kama ulivyoandika suala la ziada la kuongezewa ni je Mihimili mingine ya nchi nazo zitapoteza hiyo Imani au watazibakisha na kuwapa wananchi matumaini
 
Iko hivi, kila jambo lina wakati wake. CCM kwa sasa sio chama CCM cha kizazi hiki. Hapo ilipo imefikia mwisho ndio maana inatumia nguvu kubwa na sanasana kupora chaguzi kwa ushirikiano wa vyombo vya dola, na tume isiyo huru ya uchaguzi. Matokeo yake idadi ya wapiga kura inazidi kupungua maana watu hawaichagui, bali hulazimisha kukaa madarakani kwa shuruti. CCM ikubali tu kuwa wakati ukuta.
 
Mnagombana sana na Kaburi. Haya, kati ya mengi, ndio yale niliyoyanena sehemu "Wananchi hawajaridhika na Matusi na Kejeli" sijakosea, ni makusudi kabisa. Endeleeni na hayo matusi, dawa yenu ipo jikoni.

Makala hii kama makala mengi tu ipo kumsafishia njia SSH huku ikisahau kuweka madudu ambayo yametufanya kukosa imani naye na Serikali yake....CCM oyeee!
Amegawa Serengeti na Ngorongoro?
Ameangamiza Kabila la Wamasai?
Amegawa Bandari?
na mengine mengi tu!
Watu wanakufa njaa!
 
Pili limebebwa na harufu kuungwa mkono na udini na imani yake toka kwa wajomba.
Siku tu kapata uraisi na kwenda kwa mjomba wake omani tayari !?.
Usalama wakuona ili kuwa wapiga dili wamemtumia mtu wa karibu
 
Watu wote wenye akili timamu washa poteza imani na tumaini na chama Cha mboga mboga muda mrefu sana,ni wajinga pekee ndio wanaimani na hicho chama Cha tumbocracy
 
Mnagombana sana na Kaburi. Haya, kati ya mengi, ndio yale niliyoyanena sehemu "Wananchi hawajaridhika na Matusi na Kejeli" sijakosea, ni makusudi kabisa. Endeleeni na hayo matusi, dawa yenu ipo jikoni.

Makala hii kama makala mengi tu ipo kumsafishia njia SSH huku ikisahau kuweka madudu ambayo yametufanya kukosa imani naye na Serikali yake....CCM oyeee!
Amegawa Serengeti na Ngorongoro?
Ameangamiza Kabila la Wamasai?
Amegawa Bandari?
na mengine mengi tu!
Watu wanakufa njaa!
Wacha ujuha na wivu!

Amegawa wp Serengeti?
 
Ccm ina mvuto tuu kipindi cha kampeni. Baada ya hapo mvuto wanaamishia kwenye matumbo yao. Rushwa na upigaji
 
Binafsi huwa nashindwa kuwaelewa watu wenye nafasi zao kwenye jamii ya Watanzania. Hasa hasa wasanii, kwanini mnakubali kutumika kusahaulisha watu kufatilia suala la msingi la mikataba mibovu inayotufanya tuwe watumwa sisi na vizazi vyetu kwenye nchi yetu wenyewe.

Kwani nyie hamna Watoto au familia au mna nchi nyingine tofauti na Tanzania yenu?

Nini maana ya kuitwa kioo cha jamii? Au hiyo mirahaba mnayopewa mnadhani ni hisani?

Jigeshimuni nyie.
 
Back
Top Bottom