Naibu Waziri Sagini Azindua Shule ya Sekondari Kirumi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

NAIBU WAZIRI SAGINI AZINDUA SHULE YA SEKONDARI KIRUMI

Wanafunzi Kijiji cha Kirumi Kata ya Bukabwa katika Wilaya ya Butiama Mkoani Mara wamepunguziwa mwendo baada ukamilishaji wa Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kirumi iliyoanza kujengwa tangu mwaka 2003 kwa nguvu za Wananchi ambayo ilikuwa hitaji kubwa la muda mrefu kwa Wananchi.

Hafla hiyo fupi ya Uzinduzi wa Shule ya Sekondari ya Kirumi iliyofanyika Septemba 16, 2023 ilihudhuriwa na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi ngazi ya Wilaya, wadau mbalimbali wa elimu, Wanakijiji na vikundi mbalimbali vya burudani.

Akizungumza katika Uzinduzi wa Shule hiyo Mgeni Rasmi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Butiama na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini amesema kuwa Wananchi walimfuata wakilalamikia kuzuiliwa kuendelea na Ujenzi wa Shule hiyo huku Wanafunzi wakitembea umbali zaidi ya kilomita 15 mpaka Shule ya Sekondari Mmazami iliyopo kijiji jirani.

"Wanafunzi walikuwa wanapata matokeo mabaya sababu ya umbali na wale wakike baadhi yao ndoto zilizima baada ya kufanyiwa ukatili njiani, nikapata uchungu japo baadhi ya Viongozi walikwamisha ila nikatoa pesa kutoka kwa familia yangu ili Ujenzi uliokuwa umesimama uendelee hivyo Uzinduzi wa Shule hii ni ukombozi wa elimu katika kiijiji hiki". Amesema Mhe. Sagini.

Kwa upande wake Afisa Elimu wa Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Butiama Chacha Megewa, amesema katika kipindi cha miaka miwili cha Mbunge Jumanne Sagini tayari wamepata jumla ya shule nane za Sekondari.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Butiama Gosbert Bernard, alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Butiama na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini kwa kazi kubwa anayoifanya Jimboni kwake kwani mpaka sasa Wilaya hiyo imeongoza Mkoa, katika mwezi wa nane tumepokea fedha zaidi ya bilioni 5 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Aidha, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Christopher Siagi ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mbunge wa Jimbo la Butiama, Diwani wa Kata ya Bukabwa na Viongozi wengine walioguswa kuchangia Ujenzi mpaka leo imegeuka furaha na wanafunzi wameanza kupata elimu.

F6OXQTaWMAAqW_1.jpg
F6OXQQ_XcAAapen.jpg
WhatsApp Image 2023-09-18 at 14.16.57.jpeg
 
Back
Top Bottom