Safi Sana: Marekani na ujanja wake kaingizwa mkenge na Venezuela kuhusu kuuziwa mafuta

Halafu tunaoongea sasa na kuanza kumwambia US atakoma tupo madongo kuinama huku Ulimwengu wa tatu kwenye dhiki tele hata kodi ya chumba kimoja kulipa ni shida.Nasoma comment za huu uzi huku nacheka sana
ha ha ha ha ha...
 
Habari yako haiko sawa na imekaa kichuki sana...
Sasa ni hivi...Marekani ina hifadhi kubwa ya mafuta kuliko nchi yoyote duniani
Mkuu wewe soma tu hii ni kama Comedy ya kina Masanja.Nchi ni Superpower kweli kweli in all aspects halafu mtu anakuja kutuletea blah blah za 'US watakoma" :)
 
Mr
Iko hivi, Marekani kwa kutaka kuikomoa Urusi wakapata mawazo ya kugomea kununua mafuta Yao. Lakini kabla hawajafikia muafaka wa kugomea mafuta ya Urusi wakaona watafuta chanzo mbadala Cha mafuta. Hapo ndio wakapata wazo la kuiomba Venezuela kwa Raid Maduro waweze kuànza téna kuchukia mafuta huko ambako mwanzo waliyagomea kwa kutokumtamvua Rais Maduro badala yake wakaamua kumtambua mpinzani wake aliyekuwa ameshindwa vibaya kwenye uchaguzi aitwaye Guaido.

Wakaona ni afadhali wameangukie Maduro kuliko kuendelea kununua mafuta ya Urusi. Ili kutekeleza sdhima hiyo, Marekani ikayuma ujumbe mzito kwa Rais Maduro wa Venezuela ambaye aliwaambia hakuna shida njoni tuyajenge (si unajua kwenye siasa hakuna sdui wa kudumu au rafiki wa kudumu, kinachoangaliwa ni maslahi!).

Kweli ujumbe mzito ukaenda na Rais Maduro akawapokea kwa bashasha na tabasamu la kufa mtu. Akawaambia hakuna shida mafuta nitawapatia. Wageni hao wa Rais Maduro wakarudi Marekani na moto wa kugomea mafuta ya Urusi maana wameshapata mafuta mbadala. Walipofika tu Marekani, Rais Biden wa Marekani akatoa amri ya kupiga marufuku ununuaji wa mafuta Toka Urusi.

Maduro akasubiri siku mbili Kisha akaioiga mkwara Marekani:

1. Nitawauzia mafuta lakini kwa masharti yafuatayo:
(i). Itabidi mnitambue rasmi kuwa Mimi ndiye Rais halali wa Venezuela tangu baada ya uchaguzi mkuu uliopita.
(Ii). Wakati nawaauzia mafuta Hilo halitaathiri ushirika wangu na Urusi na nitabaki mwamininifu kwa Nchi ya Urusi!!

Hayo masharti yakawa magumu Sana kwa Marekani na akashindwa kuyatekeleza wakati tayari ameshatangaza kugomea mafuta ya Urusi!! Bei ya mafuta Marekani ghafka ikapanda juu Sana!!

Rais Biden akaamua aiombe Saudi Arabia waongeze uzalishaji wa mafuta Ili kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya Marekani lakini mfalme wa Saudia akamchunia na hakukubali kupigiwa simu na Biden!! Sasa hivi huu ko Marekani Biden anahaha!

Kaingizwa mkenge na kiburi hakimruhusu kuyakubali téna mafuta ya Urusi. Mtamuua Babu yetu jameni
 
Bado nasisitiza tu kwamba vijana wa kitanzania bado ni shida sana kwani hawapendi kusoma na kutafuta taarifa ila wao ni kukariri tu na ushabiki kama wa Simba na Yanga.

Marekani ni taifa lenye watu "Think Tanks" na ni taifa ambalo vitabu walivyoandikia mipango yao ya maendeleo kwa miaka 200 ijayo vinaweza vikajaza semi trela hata kumi hivyo kutegemea kwamba mambo yake yanaweza yakakwamishwa na tu-nchi kama Venezuela au sijui Saudi Arabia ni kufikiria kitoto sana.

Sasa hivi wameshaanza mpango wa kutoa mapipa milioni mbili za mafuta ghafi kila siku kutoka kwenye akiba yao ya Strategic Oil Reserve ilioko Alaska na kufanya bei ya mafuta ghafi ipungue kwenye soko la dunia kutoka USD 124/bbd mpaka USD 106/bbd (High) na USD 98.6/bbd (Low) bei ya leo na bado itaendelea kushuka unafuu ambao hata sisi tutanufaika nao.

Wenzetu walishajipanga siku nyingi na kujiwekea Contingency Plans kwa kufahamu kwamba kuna kipindi lazima watakutana na taharuki fulani fulani.

Itakumbukwa kwamba Marekani ndio taifa la pili duniani, nyuma ya Russia, kwa kuwa na akiba kubwa ya mafuta ghafi kwa hiyo wanaofikiria kwamba wanaweza wakakwama kwa kukosa hiyo rasilimali watakuwa wanakosea sana.
Hasa hiki kizazi kilichojiunga JF kuanzaia 2015, 90% ni majanga makubwa sana.Unasoma Thread ina porojo nyingi unaamua kwenda nayo kimzaha hivyo hivyo.
 
Hivi, unafahamu kuwa Canada ndo supply namba moja wa mafuta kwa Marekani kwa zaidi ya 61%? Marekani hajawahi kununua zaidi ya 3% ya mafuta kutoka Russia, hivyo gap ya mafuta atakayohitaji haizidi hiyo 3%.
Soma hapa
Screenshot_20220316-202654.jpg
 
Back
Top Bottom