tubadilike-sasa
JF-Expert Member
- Jan 31, 2012
- 681
- 167
Nani aliokudanganya?
Aliyenidanganya nini?
Nani aliokudanganya?
Hata aibu huna!!!!!!hivi waalimu 47 wanaweza kutoa elimu kwenye shule ngapi nchi hii?kwann asiboreshe maslah ya waalimu wazalendo walioko kwenye mgomo baridi ili wafanye kazi yao vizuri?kwann asijenge maabara zinazokidhi ili wanafunzi wa masomo ya sayansi wafanye practical?sasa hao wamarekani 47 wamekuja na maabara zao?hebu tubadilike tuwe na uchungu na mustakabali wa elimu katika nchi yetu,sio kusifia UJINGA.
Waalim wa sayansi 47 kutoka USA wameapishwa leo ubalozi wa Merekani. Wamejitolea kuja kufundisha shule za Sekondari za Tanzania baada ya kuombwa rasmi na Mheshimiwa Rais Kikwete.
Ahsante Kikwete. Inanikumbusha wakati nasoma, enzi hizo, tulikuwa na Waalim kutoka Australia, India, Uingereza kwa uchache na mambo yallikuwa swaafi kabisa,
Hii ni fursa kubwa kwa Waalim wetu kujifundisha mbinu za wenzetu nasi kuwaonesha uwezo wetu nao wajifunze kutoka kwetu.
Haya wanafunzi, kazi kwenu na Mungu awasaidie muwe wanafunzi wazuri wa kuigwa na hawa Wamerekani wapeleke salaam njema kwao ili waje na wengine wanaosuasua.
We Zomba kweli unaona ni sahihi kuleta mamluki wa kuiangamiza elimu yetu kabisa!! Curriculum ya Tanzania ni tofauti na ya US, hawa walimu watafundisha kitu gani walichosoma US? Ukitazama hawa walimu kutoka US, mara nyingi wanakuwa shallow sana. Bora wangekuwa wametoka UK! Kuna ugumu gani kuandaa hawa walimu wa science na kuwalipa vizuri ili waweze kuitumikia Nchi yao?? Huku naona ni kuwapoteza kabisa watoto wa maskini. Hawa walimu wengi wanakuwa wanafundisha mamichezo tu!! Je hawa walimu watalipwa au kujitolea?? Zomba jiulize swali moja, "watafundisha mjini au ni hadi vijijini"? Kama watafika hadi vijijini, mtawaweka wapi, ni kule walimu wetu waliozea shida wanakoishi au?? Hapa mnazidi kutupoteza ndg yangu!!
Tujadili kwa kina Mkuu!
Wale ni watalii sio walimu,wamekuja kuangalia namna bora ya kuvuna URANIUM toka kwenye nchi waliouziwa, fuatilia wanafunzi wanaokwenda kusoma marekani wa kidato cha tatu kwa mwaka mmoja wakirudi wanapelekeshwa sana na wenzao waliowaacha tanzania, timizeni na wapeni walimu wazawakipaumbele kwa kuwalipa stahiki zao na maslahi bora muone performance itakavyokuwa sio kupiga siasa tu
Waalim wa sayansi 47 kutoka USA wameapishwa leo ubalozi wa Merekani. Wamejitolea kuja kufundisha shule za Sekondari za Tanzania baada ya kuombwa rasmi na Mheshimiwa Rais Kikwete.
Ahsante Kikwete. Inanikumbusha wakati nasoma, enzi hizo, tulikuwa na Waalim kutoka Australia, India, Uingereza kwa uchache na mambo yallikuwa swaafi kabisa,
Hii ni fursa kubwa kwa Waalim wetu kujifundisha mbinu za wenzetu nasi kuwaonesha uwezo wetu nao wajifunze kutoka kwetu.
Haya wanafunzi, kazi kwenu na Mungu awasaidie muwe wanafunzi wazuri wa kuigwa na hawa Wamerekani wapeleke salaam njema kwao ili waje na wengine wanaosuasua.
Kama hujui aliyeiangamiza elimu, tuulize tuliokuwepo. Pitia juu huko tumeelezea kwa uchache.
Kwa kukujuza tu, somo la sayansi, ni moja uwe China uwe USA, uwe Tanzania, unaonesha hujui science ni nini.

Walikuwepo kabla ya Nyerere na Keneddy au hulijui hilo?
Nyerere alikuwa hafanyi ziara Nje tulikuwa na Waalimu wa Kinorway; Kiswidish; Australia; Kirusi; Kimarekani; Kidemnark
Sasa Unasema hizo trip 50 za US anapata waalimu 47? Oh, Tutafika kweli? Na ni Shule Gani hao 47 watafundisha?
Shule za Kata, Shule za Jamii, Shule za Serikali au Shule za Private?
Waulize waliosoma Mkwawa High School miaka ya 90 watakuambia vizuri habari za mwalimu mmoja wa kemia kutoka Uingereza Mr. Gordon alivyokua "mweupe" na kituko darasani. Aliiona syllabus ya A-level ya TZ kama Chuo kikuu kwao, mambo yalikuwa yanamwia vigumu.
Jenerali Ulimwengu said:TUNAWEZA kuteua, kama Taifa: ama tutafute elimu endelevu ama tutafute ujinga endelevu.
Ninasema tunaweza "kuteua" si kwa sababu jamii inaweza kuteua, kwa makusudi, kuendeleza ujinga, na kwa kweli kila mara itakuwa inasema kwamba inatafuta elimu.
Kinachoifanya jamii hatimaye ionekane kama iliyoteua ujinga ni jinsi inavyoenenda katika kutafuta hiyo elimu inayosema inaitafuta.
Kwa mfano, tunateua kuendeleza ujinga na kujenga misingi ya ujinga endelevu nilioujadili huko nyuma kwa kukazana na ujenzi wa vyumba vya "madarasa' katika "shule' zisizokuwa na walimu wenye sifa za ualimu wala vitabu.
Tunaweza tukaangalia majengo mazuri na tukaamini kwamba tumepata shule, kumbe ni majengo matupu ambayo yangeweza kutumika kama maghala ya tumbaku au vyumba vya kuhifadhia maiti (mochuari).
Kama hujui aliyeiangamiza elimu, tuulize tuliokuwepo. Pitia juu huko tumeelezea kwa uchache.
Kwa kukujuza tu, somo la sayansi, ni moja uwe China uwe USA, uwe Tanzania, unaonesha hujui science ni nini.
Tatizo letu ni zaidi ya upungufu wa walimu wa sayansi. Kama kungelikuwepo na incentives vijana wangi wangejiunga na masomo ya sayansi na kuwa waalimu bora wa kizazi kijacho. Wanafunzi sasa hivi hawataki kusoma masomo ya sayansi. Nani anataka kusomea udaktari kwa miaka 6 kwa mshahara huu? Hata kozi nyingine za sayansi, watoto wanakwepa.Upuuzi mtupu. Ukilinganisha gharama za safari za JK na kile watakachochangia utajua nimaanishacho kwa kusema upuuzi mtupu. Kwani rais ni waziri wa elimu? Hili la kuomba walimu laweza kufanyika hata hapa hapa Dar kupitia ubalozi wa Marekani. Ingawa mleta mada ni shabiki wa JK angetafuta kitu kinachoingia akilini badala ya habari hii ya kidaku na kinazi.
Na Mkwawa hiyo hiyo ndio kuligunduliwa the "mpemba effect", unaijuwa?