Safari ya JK Davos Pata Picha

Siku zote watu wanaona safari za JK hazina tija, hivi watanzania tunataka yote anayokwenda kuyafanya nje yawe yanatangazwa???? Huu ni utaratibu gani na tangu lini yaliwekwa wazi kwa awamu zote zilizopita?

Hata kama hamtangazi akina kameruni wanatangaza kile kinachompeleka nje.
 
kwa hiyo unataka kusema Jk aache kusafiri kwa sababu tu madaktari wamegoma.....are you kidding? tupate hasara mara mbili kwani amekwenda kutembea au kwa faida ya nchi? wabunge nao wakigoma abaki Ikulu, waalimu na wengineo vivyo hivyo...hapana haikubaliki Rais ni taasisi ndio maana chini ya Rais kuwa viongozi rukuki wa kumsaidia. kwani wakikutana na Pinda kuna tatizo gani?
Atalia bila kutoa suluhisho la tatizo. we humjui mizengwe nini?
 
Upuuzi wa Masoud kipanya, angalia hiyo documentary ndo utamjua jamaa ni kichwa.

Hiyo kitu inapatikana vipi? Nilienda Dar mwaka jana, nimezunguka kwenye madocho yote ya wauza majarida posta, sikuipata hiyo kitu. Mwongozo tafadhali anaejua.
 
Mungu wangu Mzee Kipanya ulifikiria nini mpiganaji wangu kabla ya kuchora Mhe Kikwete mawinguni??

Mkuu mbavu zinaniuma sana kwa kicheko. Nilipokua nafungua hii thread kwenye akili yangu nilikua natarajia picha kweli za mheshimiw na hata nikabaki kujiuliza kwamba safari hii ha Kamanda Ndallo kule A-Town safari hii naye katia timu ndani ya msafara wa rais?

View attachment 46103 Nilipata hii picha kwa hisani ya mzee mzima Masoud Kipanya safari ya JK kwenda Davos, bado naendelea kufuatilia matukio picha zitawadia baadae.
 
umasikini wetu kamwe hautaisha kama tutaendelea kuhoji safari za rais kwa ushabiki wa kisiasa. Kila safari ya rais na malengo tofauti na nyingine ni vema kila moja tukaipima faida yake kwetu badala ya ushabiki
 
We mama weee utakuja wehuka kwa kutetea mashetani. Hivi unapataga ngapi kwa kazi hiyo?

Na wewe unapataga ngapi kwa kumshambulia mama porojo? kila mmoja wenu ana mume anayemtetea sio bure. Tuache kila mtu awe huru katika jukwaa hili
 
Nadhani Vyuo vyote vilivyompatia degree za heshima huu ndio wakati wa kutathimi kumnyanganya
 
Amezikumbuka mbembea zake huko mamtoni!Mwacheni akabembee zake.

nyinyi ndio mnataka kutudanganya watanzania kwamba hakuna safari ya rais yenye manufaa kwetu eti anakwenda kubembea futa kauli yako ya kisiasa kwenye mambo ya uchumi.
 
Hawa majeruhi wa uchaguzi wa 2005, wanamtandao waliotegemea fadhila kutoka kwa jk akiwemo kipanya, Ngurumo na mwenzao sina imani nao
 
Nadhani Vyuo vyote vilivyompatia degree za heshima huu ndio wakati wa kutathimi kumnyanganya

Hata wewe unahitaji kujitathmini kama kweli una degree kwani hakuna msomi anayeweza kufanya hitimisho (conclusion) bila utafiti kama ufanyavyo wewe. Msomi unapita taarifa mtaa wa kongo bila hata kuchuja kisomi na kutafuta hoja za nyongeza unakuja hapa kwamba umepata chanzo cha taarifa cha uhakika
 
Kwa kawaida katika ziara yake huwa na watu wasiopungua 40. Na hutumia zaidi ya Tsh 300,000,000/- milioni mia tatu akitumia ile ndege maalumu ya Rais. Lakini kwa sasa anatumia Ndege za kukodi na za mashirika ya Kigeni. Piga hesabu. Madaktari wanadai nini kwa manufaa ya nani? Bila sha ni kwa manufaa ya taifa. Lakini yeye anatumia mihera yote kwa faida ya nani. Ni ya kwake na hao anaowatishia kuwashusha kwenye ndege. Tunahitaji Mapinduzi
 
nakumbuka mwalimu wangu mmmoja alisema 'wachoraji ni watu wenye IQ kubwa'

kama mazingira yakiwa'favour kufanya chochote akili inachowaaambia kufanya
 
Kama kuna mtu alisikiliza kipindi chake cha asubuhi leo hii walikuwa kama wako darasani na mwalimu alikuwa kipanya alikuwa na majina ya walioshiriki mkutano huo mwaka jana sasa katika kutaja majina jina la mkulu hal ikuwapo sasa dj q akawa anaulizwa wewe si uliaga kwamba unakwenda huko mbona jina lako halipo? Maana allikuwa amepata majina ya wote waliohudhuria sasa jina lake halikuwepo waafrika walitajwa Shangirai,Kagame na Mandela.
 
'Kipanya' anawakilisha wakosoaji wa serikali ya Jk ambao wanaamini katika maneno ya Dr Slaa kwamba angepata Urais asingesafiri angebaki pale magogono Ikulu na kula mihogo.

kwani KP amesemaje hapo?
Halafu wagombea 2010 si walikuwa wengi?
Kwanini usimtaje Peter Kuga Mziray? Kila siku Dr. Slaa...
 
Anajifanya anaenda kutupigania tupate hela maisha yawe sawa wakati huku nyuma anasababisha vifo vya watu wasio na hatia. Angekuwa anapenda wananchi wake si angebaki aokoe maisha ya maelfu ya watanzania anaojifanya anaenda kuwapigania huko Davos???For sure his trip to Davos ni kwa ajili yake na familia yake na sio watanzania. Huku nyuma ilitakiwa akute watu wote tupo viwanja vya jangwani tunatumia nguvu ya umma.
 
Back
Top Bottom