Safari hii Mwalimu Mwakasege hajaita wadada wenye uhitaji wa kuolewa?

Issue ya pesa ni kila mtumishi brother, mwakasege anauza vitabu vyake kwa jina la Yesu, anachangisha semina kwa jina Yesu, anauza dvd zake kwa 30000, anachangisha forms, anapokea pesa kwa njia ya m-pesa, tgo na njia nyingine zote kama watumishi wengine.

Shida SADAKA na pesa zote tunazotoa zisipotumika kwenye kazi ya Mungu ndipo hasira ya Mungu itawawakia watumishi.
sawa mkuu izi pesa zitawachoma
 
Mungu amtunze huwa namuelewa sana.

Unasema Mwakasege unaongea kitu gani!!!
Ni NENO la Mungu linanena!!!!!

Hahahaaa long live Teacher.
 
Mwakasege ni Mtumishi wa Mungu kweli kweli. Mwaka 2002 pale Dodoma Warutheri wenzake wa mtaani kwetu walianza kumsema vibaya kuwa anapenda sana sadaka na anakula peke yake. Na mimi nikaingiwa na hayo mawazo mabaya nikaanza kumchukia. Mungu alichonionesha siji kusahau,,niliogopa sana nikamwomba anisamehe. Zaidi anaheshimu madhehebu yote na dini zote, kimsingi ni wa pekee.
Natamani ushee kidogo kile Mungu alikuonyesha ili nasi tujifunze
 
Mwakasege ni Mtumishi wa Mungu kweli kweli. Mwaka 2002 pale Dodoma Warutheri wenzake wa mtaani kwetu walianza kumsema vibaya kuwa anapenda sana sadaka na anakula peke yake. Na mimi nikaingiwa na hayo mawazo mabaya nikaanza kumchukia. Mungu alichonionesha siji kusahau,,niliogopa sana nikamwomba anisamehe. Zaidi anaheshimu madhehebu yote na dini zote, kimsingi ni wa pekee.
Ukitaka kula pesa bila jasho ni kuchezea akili za watu. Kwanza watishietishie dhambi, kifo,msiba,jehanamu lenye ziwa la moto na maneno kama 'litakapokutokea' na mengi,mengi ya aina kama hiyo.
Usibadilishe maandishi ya vitabu vya madhehebu husika,wala kuongeza neno. Bali fasiri kwa lugha na sauti ya jaziba. Kula mayai ulegeze koo, sauti nzito itoke.
Watu watakuja wenyewe aidha kuchangia, kukutegemeza au kukutunza na misadaka ya kushindana nani katoa zaidi.
Kama ulikuwa haujajenga,utanunuliwa kiwanja na waumini,pia wataanzisha ujenzi wao wenyewe kwa umiliki wa jina lako.
Kama hauna gari, watajichanga wanunue,lakini kwa umiliki wa jina lako.
Kama unasomesha watoto shule za kata, utaombwa wakupelekee watoto zako wakasome kwenye shule za "Accademy". Tusisahau kubadilishiwa makochi ya sebuleni kwako kila baada ya siku90.
Sasa, ukitaka ku-"update" ulaji wako, weka waigizaji wa kushuhudia "miujiza" kila utoapo "neno" kwenye mimbari. Usiwalipe cha maana, wagawie "masalia". Hawana pa kwenda kwa kuwa ulishawasoma na kuwaelewa kuwa ni watu legelege wasiopenda kumenyeka na kula vya jasho lao.
Pia weka ma-"campainner" wako kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, kama humu jf na kwingineko kwa ustadi mkubwa, nikuhakikishie, lazima utaula mwanangu na maisha yako yatakuwa mazuri na bora kabisa, kuliko yale ya ahera ya baadae.
 
Back
Top Bottom