Sabodo aichangia CHADEMA milioni mia moja

Wana-JF:
Mfanyabiashara maarufu nchini na kada wa CCM, Mustafa Sabodo amekichangia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Shs 100 milioni kwa ajili ya kampeni ya uchaguzi. Akikabidhi hundi hiyo kwa M'Kiti wa Chadema Freeman Mbowe, Sabodo alisema pamoja na yeye kuwa ni mwanachama wa CCM, lakini ameamua kuchangia CHADEMA kuendeleza upinzani wa kweli nchini na kuongeza kuwa Chadema ni chama cha upinzani kilicho makini.

Chanzo - ITV Bulletin 8.00 pm today.
 
Angekichangia chama tawala angeitwa fisadi... siasa bana... nachoka kabisa!
Kuna mtu yoyote ametoa mchango mkubwa CCM akaitwa fisadi watu wakashindwa kuonyesha ufisadi wake hapa?Kama yupo tupe jina na ushahidi.
 
Ahahahaa-hii imeonyesha jinsi gani hata vyama vya siasa vinahitaji msaada pia ktk utendaji wa kazi.Well done
 
Kuna mtu yoyote ametoa mchango mkubwa CCM akaitwa fisadi watu wakashindwa kuonyesha ufisadi wake hapa?Kama yupo tupe jina na ushahidi.
Hao wote wanao itwa mafisadi wamefisadisha nini? Je unajuwa kiundani kama kweli ni mafisadi?
 
Ngoja niwasikilize kwanza wakubwa mtoe comment zenu maana najua watu watakuja na mengi hapa. Ngoja kwanza tuwasikilize kabla hatujatoa lolote midomoni mwetu.
 
tunawahitaji akina sabodo wengi zaidi, kwa ajili ya maendeleo ya kweli ya demokrasia nchini
 
Vyama vyote, vilivyo madarakani na vya upinzani, viogope kuchangiwa michango mikubwa na watu wachache. Chama kinapochangiwa mchango mkubwa na mtu mmoja kuna hatari kubwa ya kununuliwa na kukosa uhuru wa maamuzi.
 
Kiranga,
Mbona hili bwawa lilishapasuka siku nyingi? Huwezi kulirudisha jini kwenye chupa.
 
Hongera sana Sabodo kwa moyo ulioonyesha, maendeleo ya jamii hayana itikadi Mungu akubariki na akuzidishie maradufu na akupe afya njema.

Nafikiri kuna watu wengi tu walio na moyo wa Sabodo lakini wanasita kujitokeza kwa sababu mbalimbali. Lakini pole pole ndio mwendo kuna siku na wao wataelewa umuhimu wa vyama mbadala kwa jamii na kujitokeza kuvisaidi kwa wazi.
 
Ama kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni... rafiki na mshirika mkuu wa Jeetu Patel anachangia chama makini chenye kupinga ufisaid Chadema!

Tuliwaambia hapa kila mwana siasa wa Bongo ana bei yake mkabisha haya sasa....
 
Kiranga,
Mbona hili bwawa lilishapasuka siku nyingi? Huwezi kulirudisha jini kwenye chupa.

It is not so much kulirudisha jini kwenye chupa as it is ku state first principles tu. Every action has an equal and opposite reaction, there is no free lunch in the known universe, especially kutoka kwa ndugu zetu hawa.

Kama hii situation inaweza kuwa repaired, legality yake na swala zima la campaign finance legislation linasemaje etc, hayo ni maswala mengine.

Vyama imara huendeshwa kwa grassroot organizations, sio kwa kuwa na michango mikubwa ya vizito wachache.

Kesho keshokutwa kizito atakuwa ana interest zake za kibiashara atawaomba wabunge wa CHADEMA wamfanyie hisani fulani kwa kutumia privileges zao za kibunge wataona haya kumkatalia kwa kuangalia mchango wake mkubwa, tutakwazana hivi hivi jamani. Ni hilo tu ninalohofia.
 
Ama kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni... rafiki na mshirika mkuu wa Jeetu Patel anachangia chama makini chenye kupinga ufisaid Chadema!

Tuliwaambia hapa kila mwana siasa wa Bongo ana bei yake mkabisha haya sasa....
Kanda2,
Habari za siku nyingi. Naona umeadimika sana hapa JF. Lakini mwenzako MS amekuwa akikuwakilisha vilivyo.
 
It is not so much kulirudisha jini kwenye chupa as it is ku state first principles tu. Every action has an equal and opposite reaction, there is no free lunch in the known universe, especially kutoka kwa ndugu zetu hawa.

Kama hii situation inaweza kuwa repaired, legality yake na swala zima la campaign finance legislation linasemaje etc, hayo ni maswala mengine.

Vyama imara huendeshwa kwa grassroot organizations, sio kwa kuwa na michango mikubwa ya vizito wachache.

Kesho keshokutwa kizito atakuwa ana interest zake za kibiashara atawaomba wabunge wa CHADEMA wamfanyie hisani fulani kwa kutumia privileges zao za kibunge wataona haya kumkatalia kwa kuangalia mchango wake mkubwa, tutakwazana hivi hivi jamani. Ni hilo tu ninalohofia.
Kiranga,
Unachosema ni kweli kabisa. Na kwa hili tupo ukurasa mmoja. At least CHADEMA wamekuwa wawazi kuhusu wachangiaji wao tangu uchaguzi wa 2005. CCM hawajataja hata siku moj fedha zao zinatoka wapi. Kwa hili tuwapongeze. Sasa kwa next step ni kuchukua hatua kama walivyofanya hapa Marekani, kuweka limit ya michango ya matajiri, au ya kampuni, na michango hii ijulikane wazi, si kwa upinzani tu bali hata kwa chama tawala ambacho mpaka sasa kimekataa kutaja wachangiaji wake na kiasi kilichotolewa.
 
It is not so much kulirudisha jini kwenye chupa as it is ku state first principles tu. Every action has an equal and opposite reaction, there is no free lunch in the known universe, especially kutoka kwa ndugu zetu hawa.

Kama hii situation inaweza kuwa repaired, legality yake na swala zima la campaign finance legislation linasemaje etc, hayo ni maswala mengine.

Vyama imara huendeshwa kwa grassroot organizations, sio kwa kuwa na michango mikubwa ya vizito wachache.

Kesho keshokutwa kizito atakuwa ana interest zake za kibiashara atawaomba wabunge wa CHADEMA wamfanyie hisani fulani kwa kutumia privileges zao za kibunge wataona haya kumkatalia kwa kuangalia mchango wake mkubwa, tutakwazana hivi hivi jamani. Ni hilo tu ninalohofia.
Kiranga usihofu sana, mioyo ya watu inatofautiana si kila mtu atoaye hungojea karama zimrudie kuna wale wenye mioyo ya tenda wema uende zako usisubiri.........
 
Kada wa CCM aichangia CHADEMA Sh 100 milioni

Monday, 12 July 2010

sabodo.jpg

Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe (wa pili kushoto) akipokea hundi ya Sh 100 milioni jijini Dar es salaam kutoka kwa Mfanyabiashara maarufu nchini na kada wa CCM, Mustafa Jaffar Sabodo huku katibu mkuu wa chama hicho Dr Willibrod Slaa akishuhudia

Geofrey Nyang’oro

VYAMA vya upinzani sasa vinaweza kuwa vimepata matumaini mapya ya vyanzo vya fedha baada ya mfanyabiashara maarufu nchini na kada wa CCM, Mustapha Sabodo kutoa mchango wa Sh100 milioni kwa Chadema.Sabodo, ambaye anaendesha biashara za aina mbalimbali, pia atakuwa tayari kukichangia chama hicho fedha wakati mwingine wowote, kwa mujibu wa mfanyabiashara huyo.

Mchango huo ambao umewekwa bayana unafungua ukurasa mpya kwa vyama vya upinzani ambavyo vimekuwa vikisumbuliwa na ukata wa fedha kutokana na kutokuwa na vyanzo vya fedha.

Vingi vinategemea ruzuku, lakini mgao wao ni mdogo kutokana na kuingiza wabunge wachache bungeni na kutopata kura za kutosha kwenye kinyang'anyiro cha urais.

Wakati CCM ikifaidi ruzuku kutokana na kufanya vizuri kwenye uchaguzi, wafanyabiashara wamekuwa wakimimina misaada na michango yao kwa chama hicho tawala, wengi wakionekana kuwa na hofu ya kuchangia kwenye vyama vya upinzani huku wale wanaothubutu wakifanya hivyo kwa usiri mkubwa.

"Hii ni historia mpya katika siasa za vyama vingi nchini," alisema mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya kiasi hicho cha fedha iliyofanyika nyumbani kwa Sabodo Upanga jijini Dar es salaam.

"Ni wajibu wa wafanyabiashara wakubwa kuona umuhimu wa kusaidia vyama vyote makini nchini bila kuwa na ubaguzi wala woga.

“Kwa kweli tunakushukuru sana... Mzee ameonyesha njia, naamini itakuwa mfano kwa wengine wenye uwezo.”

Mbowe alisema mara nyingi ni vigumu kwa wafanyabiashara wakubwa wa kada ya Sabodo kuchangia kwa uwazi vyama vya upinzani kwa kiasi kikubwa kama hicho cha fedha na kutaka kitendo hicho kuigwa na wafanyabiashara wengine.

Akizunguza kwenye hafla hiyo, Sabodo alisema pamoja na kuwa mwanachama wa CCM anapenda kuona upinzani nchini unaimarika.

“Kambi ya upinzani ikiimarika na kupata wabunge wengi, hili litasaidia kuimarisha demokrasia nchini na kuliletea taifa maendeleo ya kweli,” alisema Sabodo ambaye muumini mkubwa wa siasa za Mwalimu Julius Nyerere.

Sabodo alifafanua kuwa kuongezeka kwa wabunge wa upinzani bungeni ni jambo la muhimu katika kuweka upinzani kwa CCM na kusukuma gurudumu la maendeleo kwa wananchi wake.

Katika hafla hiyo ambayo pia aliahidi kuendelea kukichangia chama hicho, Sabodo aliitaka Chadema kuongeza nguvu katika harakati zake za kisiasa na kumuelezea katibu wake mkuu, Dk Willibrod Slaa kuwa ana uchungu wa kweli na Watanzania.

Naye Dk Slaa alitoa shukrani zake kwa Sabodo huku akidokeza kuwa mchango huo utatumika katika vipaumbele vitakavyopangwa na chama wakati wa mkutano wa kamati kuu uliopangwa kufanyika Julai 20.

Alitaja baadhi ya mikakati hiyo kuwa ni ya kuimarisha chama kama Operesheni Sangara na utekelezaji wa mikakati ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 31.

“Nawaomba Watanzania wengine wa kada na uwezo mbalimbali kuchangia Chadema ili kuondokana na ukiritimba wa chama kimoja kwa kuwa ni hatari kwa maendeleo na usalama wa nchi kama michango yote iielekezwa kwa chama hicho pekee,” alisema Dk Slaa.

Dk Slaa alitumia nafasi hiyo kuviomba vyombo vya dola kuacha kuwatisha Watanzania wenye mapenzi mema wanaochangia vyama mbadala kama Chadema kwani kufanya hivyo ni kuhujumu taifa na kukwamisha maendeleo.

Chadema bado haijamtaja mgombea urais baada ya mwenyekiti wake, Mbowe kuamua kugombea ubunge.

Source: Mwananchi
 
Kiranga usihofu sana, mioyo ya watu inatofautiana si kila mtu atoaye hungojea karama zimrudie kuna wale wenye mioyo ya tenda wema uende zako usisubiri.........

Wewe moyo wa huyu mtoaji unaujua?
 
Back
Top Bottom