Sabodo aichangia CHADEMA milioni mia moja

Wewe moyo wa huyu mtoaji unaujua?
kwani kuna binding agreements kwamba mtoaji msaada lazma alipwe fadhila? acheni woga jamani Chadema ikiwa na Slaa haiwezi kutetereka unaweza kutoa hela na ukaambiwa u-disappear
 
kwani kuna binding agreements kwamba mtoaji msaada lazma alipwe fadhila? acheni woga jamani Chadema ikiwa na Slaa haiwezi kutetereka unaweza kutoa hela na ukaambiwa u-disappear

Rudia kusoma post # 35 hapa

Ujue kwa nini ni vibaya kuruhusu vyama kuchangiwa michango mikubwa na vizito, pia jielimishe zaidi kwa nini nchi zilizoendelea ambazo zimekuwa na demokrasia ya vyama vingi kwa mamia ya miaka zina tough campaign finance laws.

The fact kwamba hamna binding agreement kwamba anayetoa msaada hatakiwi kulipwa fadhila haimaanishi lolote, haimaanishi kwamba mtoa msaada hataomba fadhila, na haimaaanishi kwamba mpewa msaada hatalipa fadhila.

Huwezi kusema kwamba kuacha mwanya wa rushwa ni sawa kwa sababu hamna binding agreement kwamba rushwa itatendeka. Huwezi kusema kulala mlango wazi ni sawa kwa sababu hamna binding agreement na maharamia kwamba waje kukuibia. Lazima vyama na civil society wote tuwe vigilant kuziba mianya yote ya rushwa, na campaign finance yetu ina mianya kibao ya rushwa. Hili halibishiki.

Rather than kuangalia kama kuna binding agreement inayoshurutisha mpokea msaada kulipa fadhila (a weak argument indeed, hii binding agreement ita serve nini sasa? kuhalalisha rushwa ?) kinachotakiwa kuangaliwa actually ni the opposite.

Kuwe na strict campaign finance laws, kuwe na a ceiling figure ambayo mtu mmoja anaweza kutoa katika a political campaign.

Hivi sisi nchi masikini kama Tanzania tunaachia individual atoe campaign contribution kuliko matajiri wa Marekani? Individuals hawa wakijisikia wanavinunua vyama tutasemaje?

Ona chart ya campaign contributions ceiling figures Marekani hapa

The FEC and the Federal Campaign Finance Law Brochure
 
Hapa ndipo JF watu wanapata nafasi ya kujionyesha kama wao ni wafuata principles regardless, au wanasema ufisadi ukiwa CCM tu.

Hili swala la vizito wachache kuchangia hela nyingi chama linanuka ufisadi popote utakapoliweka, CHADEMA au CCM. Sasa kama wakulu wengine wanaona mabaya yakiwa CCM tu, lakini yakiwa CHADEMA wanayafumbia macho, sawa.

Lakini mimi impartiality yangu hainiruhusu kufanya hivyo. Jambo linalonuka ufisadi litabaki kunuka ufisadi tu, likiwa CHADEMA au CCM.

Na wala sitachelea kubonda eti kwa sababu ni CHADEMA wamefanya na si CCM.

Can you imagine the outrage kama muhindi angepigwa picha anampa JK mchango wa shilingi milioni mia moja na kuwekwa hapa JF?

Where is that outrage hapa? Au mkuki mtamu kwa CCM, kwa CHADEMA mchungu ?
 
Kiranga,
Point moja unayosahau, ambayo mimi nafikiri ni muhimu, ni usiri wa mtoaji na kiasi wanachotoa. Mimi nisingekuwa na wasiwasi hata kidogo kama mhindi, kama ulivyosema, angepigwa picha akimpa Kikwete mchango wa chama. As long as tunajua ametoa kiasi gani, sina tatizo.
Tatizo langu linakuja pale fedha zinazotolewa zinakuwa siri ya chama. Kuna tetesi katika uchaguzi wa 2005 Iran ilitoa fedha kwa Kikwete, na ile kampuni ya Makaburu inayochimba Tanzanite, ilitoa mamilioni. Hizo mpaka leo zimebaki tetesi. CHADEMA walijitahidi kutangaza michango waliyopewa na matumizi yao 2005 na kuitaka CCM wafanye hivyo kukawepo kigugumizi upande wa CCM. Yote unayosema nakubaliana na wewe lazima kuwepo uwazi wa fedha zinazotolewa na kiasi kilichotolewa.
 
This requires more than just transparency, we surely need transparency, but we also need caps on these amounts.

The best thieves steal in broad daylight, usidanganyike na show za photo ops.

Tujue kitu kimoja, kwamba bila sheria watu hawalazimiki ku act in the best interest of all, wata act in their own best interest. Bila strict campaign finance laws hawa matajiri pamoja na viongozi wa vyama vya kisiasa hawalazimiki ku act in the best interest of the people, and can easily cut deal consciously or even get into temptations and be trapped unconsciously.

Hata baada ya strict campaign finance laws, inabidi tuwe macho sana tu, sembuse sasa hivi ambako hatuna hata hizo sheria ?

Mimi hii supposed transparency hainipi any level of comfort at all, kwa sababu ukweli unabaki kibopa akichangia shilingi milioni 100 anapata power sana chamani na anaweza kutaka kulipwa fadhila kwa namna yoyote, na CHADEMA wakishaonja utamu wa mamilioni ya michango who is to say how will they react ?

T.H White katika "The Once and Future King" aliandika "What is not forbidden is compulsory" . Tusipokataza huu mwanya wa rushwa katika michango ya kampeni, tutawalazimisha wafanyabiashara wote watumie mbinu za michango ya kampeni kwa njia za kutoa rushwa.
 
Hao wote wanao itwa mafisadi wamefisadisha nini?
Wamefisadi pesa zetu.
Je unajuwa kiundani kama kweli ni mafisadi?
Gazeti la Tanzania Leo walipoandika Fredirick Sumaye anamiliki account nje ya nchi alikwenda mahakamani na akashinda kesi,Gazeti likatakiwa kumlipa pesa na kumwomba radhi.Rostam ni mfadhali wa CCM ambaye ametajwa kwenye ufisadi wa aina mbali mbali,nini kina mzuia kufuata nyayo za Sumaye?
 
wakuu naweza kuonekana kama nimeachwa nyuma kidogo
naomba kuuliza swali dogo, huyu bwana Sabodo anamiliki makampuni yapi vile
ama biashara zipi kwa sababu nimekuwa nikimsikia kwenye michango
 
Wewe moyo wa huyu mtoaji unaujua?
Kwani wewe unaujua moyo wake, ndiyo maana nimesema mioyo ya watu inatofautiana na ndiyo maana kajitokeza tofauti na wengine, jamani tumuache Sabodo tusimuwekee moyo wa kudhania.
 
Kwani wewe unaujua moyo wake, ndiyo maana nimesema mioyo ya watu inatofautiana na ndiyo maana kajitokeza tofauti na wengine, jamani tumuache Sabodo tusimuwekee moyo wa kudhania.

Apparently wewe huujui na mimi siujui.

Which is more of a reason to legislate campaign finance na kuachana na mediocrity ya kusema "tumuachie Sabodo". Unasema " tusimuwekee moyo wa kudhania" ? Tusimuwekee moyo wa kudhania indeed, tumuwekee regulations zitakazotupa uhakika kwamba hawezi kununua influence katika vyama vya siasa bila kuvunja sheria.

Kwa mfumo wetu wa sasa tajiri yeyote anaweza kununua influence katika chama chochote bila kuvunja sheria, tena akapiga picha na rais au mwenyekiti wa chama na kuiweka katika gazeti front page. Hatuna campaign finance laws. This is a tragedy.

Lakini kwa watu wengine ufisadi ni kuchangia mihela CCM tu, ukichangia CHADEMA hamna ufisadi.
 
Kavunja sheria gani?
 
Kavunja sheria gani?

Inaonekana wewe mgumu wa kuelewa sana.

Malalamiko yangu yote hapa yanazunguka the fact kwamba nchi yetu haina sheria za campaign finance, na kwamba mtu yeyote mwenye hela anaweza kuja kununua influence katika chama chochote na kupiga picha na mwenyekiti wa chama chochote cha siasa au hata rais ambaye naye ni mwenyekiti wa CCM, na kuanika picha hizi kwenye front pages za magazeti na hata mtandaoni, kuzidisha influence hiyo.

Si kila kitu kinachopigiwa kelele ni lazima kiwe uvunjaji wa sheria, ndiyo maana tuna bunge ili vinavyohitaji kutungiwa sheria vitungiwe. Ukiweka standards zako katika sheria utakuwa na standards zilizo chini sana, kwa sababu vipi kesho bunge likisema "rushwa" yote inahalalishwa kama "takrima" na isijali ukweli kwamba matajiri watakuwa na access kubwa zaidi kwaa vitu na huduma ?

Kitu kutokuwa na sheria ya kukikataza hakuna maana kwamba ni sawa kufanyika (sheria zina loopholes kibao za vitu ambavyo hatujavifikiria bado) na kitu kuwa sheria kukikataza hakuna maana kwamba ni kitu kizuri (kina Martin Luther King Jr. waliandamana kupingana na sheria dhalili zilizokataza watu weusi kukaa viti vya mbele kwenye mabasi.

Kwa hiyo kuuliza "kuna sheria gani imevunjwa" quite apart from being an absolving statement on the part of CHADEMA na huyu Sabodo, actually inaweza kuwa ndiyo outrage yenyewe kama nilivyo irepresent issue hapo juu.

Quite apart from absolving the parties kwa sababu hamna sheria iliyovunjwa, the fact kwamba hamna sheria iliyovunjwa ndiyo outrage yenyewe.

Ni kama vile unaenda sehemu nyumba ya mtu ambayo inatakiwa kuwa na usalama wa kutosha, halafu unakuta wamelala mlango wazi (mlango wazi hapo ni kwamba kuna uwazi wa rushwa) halafu unapouliza "nyie mbona mnalala mlango wazi, hamuogopi kuibiwa?"

Jibu unalopewa ni "Kwani tumevunja sheria gani kulala mlango wazi? Katika vitabu vyetu vya usalama hatukatazi kulala mlango wazi"

Ukisikia nyumba iko hivi ujue hawana security policy.

Nchi ambayo haina campaign finance laws za kukataza uncapped contributions au inayoruhusu outrageous contributions haiwezi kusema kwamba iko serious katika vita dhidi ya rushwa.

Chama kinachokibali mihela yote hii kutoka kwa mfanyabiashara mmoja, kama alivyosema mkuu mmoja hapo juu kabla yangu, kinapoteza moral authority yote ya kusema ufisadi na rushwa katika uchaguzi.

Worse still, mfanyabiashara mwenyewe hata si mwanachama wao. Wengine tunaweza hata kusema officially CHADEMA imehongwa na CCM mchana kweupeeeee.
 
It would make much more sense kwa hizo hela wanazopeleka ziteketezwe kwene white elephants, wangezipeleka kwene vikundi vya uzalishaji mali walau hata kama mikopo it would make much difference.

Miafrika bana..
 
Usitumie hoja ya nguvu kunilazimisha nikuelewe hata sioni cha kuelewa tumia nguvu ya hoja ueleweke.

Hakuna hoja ya nguvu hapo, wewe ni mgumu wa kuelewa, kubali tu.

Mimi nilishaeleza kwamba outrage ni the fact that hatuna campaign finance laws.

Nilisema

Kwa mfumo wetu wa sasa tajiri yeyote anaweza kununua influence katika chama chochote bila kuvunja sheria, tena akapiga picha na rais au mwenyekiti wa chama na kuiweka katika gazeti front page. Hatuna campaign finance laws. This is a tragedy.

Wewe ukaenda ku quote post hiyo hiyo niliyosema kwamba outrage ni the fact that we do not have campaign finance laws, ukauliza "kuna sheria gani imevunjwa".

Kavunja sheria gani?

Hivi unajiona una uelewa kamili wewe kweli?
 
Hivi sisi nchi masikini kama Tanzania tunaachia individual atoe campaign contribution kuliko matajiri wa Marekani? Individuals hawa wakijisikia wanavinunua vyama tutasemaje?

Ona chart ya campaign contributions ceiling figures Marekani hapa

The FEC and the Federal Campaign Finance Law Brochure
Hivi kweli Kiranga unaishi Tanzania au Marekani, unataka kuleta sheria za uchaguzi wa Marekani sijui chart campaign contributions ceiling figures tutaziweza kweli?, halafu nani ai control hiyo chart Kiravu au Tendwa au NEC you must be joking, this is Tanzania and that is US.

Sheria zetu tu hizi bado zinatupa shida halafu tuanze kuazima advanced election laws, my friend we are still too young to adopt(not adapt) each and every thing from abroad, tusiwe kama dodoki kufyonza kila kitu. Tuimarishe kwanza sheria zetu za uchaguzi tulizonazo kama ile ya wafadhiri wa vyama kuwa transparent, mfano mzuri ni kama huu alioonyesha Sabodo kwa kweli anastahili pongezi.

Kwa watanzania naowajua mimi kwenye michango iwe ya harusi, fees nk ni heri kuwawekea minimum limit kuliko kuweka maximum limit, maana najua maxima limit itaji set yenyewe kutokana na hali ya maisha yalivyo.

Respect.
 
Hivi kweli Kiranga unaishi Tanzania au Marekani, unataka kuleta sheria za uchaguzi wa Marekani sijui chart campaign contributions ceiling figures tutaziweza kweli?, halafu nani ai control hiyo chart Kilavu au Tendwa au NEC you must be joking, this is Tanzania and that is US.

Sheria zetu tu hizi bado zinatupa shida halafu tuanze kuazima advanced election laws, my friend we are still too young to adopt(not adapt) each and every thing from abroad, tusiwe kama dodoki kufyonza kila kitu. Tuimarishe kwanza sheria zetu za uchaguzi tulizonazo kama ile ya wafadhiri wa vyama kuwa transparent, mfano mzuri ni kama huu alioonyesha Sabodo kwa kweli anastahili pongezi.

Kwa watanzania naowajua mimi kwenye michango iwe ya harusi, fees nk ni heri kuwawekea minimum limit kuliko kuweka maximum limit, maana najua maxima limit itaji set yenyewe kutokana na hali ya maisha yalivyo.

Respect.

Let's just be honest.

1. Wabongo wengitunapenda wafadhili, tuko radhi godfather mmoja atoe mchango mkubwa hata kama anahatarisha uimara wa chama. Ukiwaambia watu kupenda penda wafadhili wakubwa ni kuuza chama wanakuona mbaya.

2. Namba moja hapo juu inasababishwa kwa wingi sana na kutegeana.Abdulhalim kauliza hapo juu nani kachangia chama chake, watu kimyaa.Kila mtu anasubiri wahindi wachangie milioni mia. Kazi tarumbeta nyingi wakati contribution ya logistics na tangibles hamna.

3. Kabla hata hatujajaribu kuweka campaign finance laws na kuona challenges ziko wapi tushaanza kuwa defeatists, tunashindwa vita kabla hata hatuja fire a single shot. Now I realize this may not be a piece of cake, but we shouldn't be afaraid to start at least a gradual process, the way you sound inaonekana unaogopa kabla hata ya kuanza.

Muhindi anatafuta jinsi ya kununua influence wewe unamwambia maximum limit ajiwekee mwenyewe, halafu kesho uankuja kupigia kelele ufisadi hapa. Hilarious.

Kama hutaki kuiga watu vunja vyama vingi basi, urudi kwenye chama kimoja, upige kura ya ndiyo au siyo.

Si hatuwezi kuiga vya wenzetu bwana?

Sio una half step, mara unataka kuiga halafu hapo hapo ukiwekewa standards unajitia hatuwezi kuiga. Kama tunataka democracy na kupiga vita rushwa campaign finance laws ni lazima.

Kama democracy na kupiga vita rushwa si muhimu basi hakuna haja ya campaign finance laws wala hata vyama vingi.

Huwezi kulala mlango wazi, halafu mtu akaja kukwambia dunia iliyoendelea siku hizi watu hawalali milango wazi, kuna wizi kila pahala binadamu hawaaminiani, wewe unasema usilete habari za Marekani.

Kesho keshokutwa kwa mfano mkisikia Sabodo kapenyeza maswali yatakayompa business advantage kwa wabunge wa CHADEMA waende kuuliza kwenye floor ya bunge mtasema ufisadi? Bada ya kutetea michango hii ya kifisadi?

Au mnataka mpaka muhindi wa watu awape viloba vya unga wabunge wa CHADEMA wampitishie VIP lounge ndiyo mjue kwamba Kikwete alivyokuwa anasema "kula uliwe" alikuwa hatanii?
 
It appears watu wengi humu hawamfahamu Sabodo such that anaonekana ni fisadi tu. Nna swali kwa wanaforum ni fisadi gani tena wa kidosi amewahi kununua ukurasa mzima wa magazeti Guardian, Daily news, Nipashe, Mwananchi na si mara moja kuikandia serikali pia CCM na sera zake??????????
 
1. Wabongo wengitunapenda wafadhili, tuko radhi godfather mmoja atoe mchango mkubwa hata kama anahatarisha uimara wa chama. Ukiwaambia watu kupenda penda wafadhili wakubwa ni kuuza chama wanakuona mbaya.

2. Namba moja hapo juu inasababishwa kwa wingi sana na kutegeana.Abdulhalim kauliza hapo juu nani kachangia chama chake, watu kimyaa.Kila mtu anasubiri wahindi wachangie milioni mia. Kazi tarumbeta nyingi wakati contribution ya logistics na tangibles hamna.

Ukweli bana ni kwamba waTZ ni ma-voyeur na wafuata upepo tu na ndio maana mabadiliko ya dhati itakuwa vigumu sana kutokea.

Tz hakuna structures za kueleweka za vyama na civil groups za ukweli zinazoweza kueka kweli msimamo dhidi ya tabaka tawala. Matokeo yake watu wanageukia hizi top down approach za kutaka kwenda ofisi kuu au bungeni kana kwamba ndio only way ya kulichagiza tabaka tawala. Hakuna structures za watu ku-own and to feel belonging to certain groups. Ndio maana wanashangilia ufadhili na kufadhiliwa. The common voyeurs and wafuata upepo do not own ANYTHING. ZERO.
 
Back
Top Bottom