Sababu ya kifo cha Steven Kibona na Gilman Rutihinda

Status
Not open for further replies.

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
5,712
10,209
Kibona alikuwa ni Waziri wa fedha, naye Rutihinda alikuwa ni Gavana wa Benki Kuu.

Hawa jamaa wazalendo, walikataa kuprint fedha na kuziingiza kwenye system kwani walijua wakifanya hivyo mfumuko wa bei na ugumu wa maisha ungeongezeka.

Bwana mkubwa kwa hasira za kukataliwa ombi lake akawapeleka India, waliporudi kutoka huko wote wakaanza kuumwa, na bwana mkubwa akatueleza kuwa wamelishwa vyakula vya Kihindi hivyo basi, walikumbwa na tumbo la kuharisha kwa sababu ya ugeni wa chakula cha Kihindi.

Hawakukaa muda mrefu, wakafa. Je ni kweli walidungwa sumu iuayo taratibu? Au ndio kifo chao kilikuwa chakawaida tu?
 
'Intelijensia' zilisema ni tatizo la kawaida tumbo kuleta tatizo unapokula vyakula usivyozoea!!!!
 
Kama kulikuwa na hilo la kuprint fedha zaidi sijui... lakini pia kulikuwa na lile la wazalendo hao kugomea (makadirio?) ya gharama za kifisadi za msafara wa rais wa wakati huo kwenda Rio de janeiro. Hilo pia lilimuudhi mno mkulu huyo.
 
Jamani siyo hivyo. Niliwahi kuongea na daktari mmoja wa Muhimbili alinidokeza kuwa wale watu walikuwa na NGOMAwakaenda nje kubadilisha damu, lakini kwa kuwa kipindi kile utaalam huo ulikuwa haujashamiri, mambo yakawaendea kombo. Kumbuka kuwa walikuwa wanafia nje na kuletwa maiti kama sijakosea.:msela:

Mkuu na watu wengine, katika matibabu ya HIV hakuna suala la kubadirisha damu. Nenda uendano hilo suala halipo kisayansi.

Tena kwa dawa za HIV zilizopo sasa, ikiwa mwathirika wa VVU anatumia vizuri dawa, unaweza usimpate kabisa mdudu wa HIV ndani ya damu isipokuwa katika baadhi ya cells zenye CD4+ maeneo yaliyofichika katika mwili.

Naamini kama kweli ulipewa taarifa kama hiyo, huyo mtu aliyekupa taarifa hiyo si daktari; na kama ni daktari basi ni daktari kihiyo maana taarifa alizokupa si sahihi.
 
Kibona alikuwa ni Waziri wa fedha, naye Rutihinda alikuwa ni Gavana wa Benki Kuu.
Hawa jamaa wazalendo, walikataa kuprint fedha na kuziingiza kwenye system kwani walijua wakifanya hivyo mfumuko wa bei na ugumu wa maisha ungeongezeka...

Kama kulikuwa na hilo la kuprint fedha zaidi sijui... lakini pia kulikuwa na lile la wazalendo hao kugomea (makadirio?) ya gharama za kifisadi za msafara wa rais wa wakati huo kwenda Rio de janeiro. Hilo pia lilimuudhi mno mkulu huyo.

Kimsingi naweza kukubaliana na sababu hizo mbili, kwa sababu katika siasa za Tanzania, ukipingana na matakwa ya wakubwa basi lolote linaweza kutokea. Kumbuka kwamba wizara ya fedha (na hazina pia) ni wizara nyeti sana kiasi kwamba iwapo utapishana kauli na wenye nchi, huenda likakupata lolote, ukichukulia kilichowapata Meghji, Mramba, Balali, Gray Mgonja, Liyumba na wengine.
Lisemwalo lipo!
 
Ipo siku every secrete will be revealed. I hope I will live to see that day
 
Kibona alikuwa ni Waziri wa fedha, naye Rutihinda alikuwa ni Gavana wa Benki Kuu.
Hawa jamaa wazalendo, walikataa kuprint fedha na kuziingiza kwenye system kwani walijua wakifanya hivyo mfumuko wa bei na ugumu wa maisha ungeongezeka.
Bwana mkubwa kwa hasira za kukataliwa ombi lake akawapeleka India, waliporudi kutoka huko wote wakaanza kuumwa, na bwana mkubwa akatueleza kuwa wamelishwa vyakula vya Kihindi hivyo basi, walikumbwa na tumbo la kuharisha kwa sababu ya ugeni wa chakula cha Kihindi.
Hawakukaa muda mrefu, wakafa. Je ni kweli walidungwa sumu iuayo taratibu? Au ndio kifo chao kilikuwa chakawaida tu?
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni...Ni kitu gani kilichomzuia Mwinyi kuwaondoa na kuwaweka wanaoweza kutimiza matakwa yake....Mbona Mrema akupelekwa huko India?
 
Hi habari imekaa ki-Mtikilatikila, miaka ya '90 wakati wa siasa za uzawa na mageusi tuliizungumza sana kama propaganda dhidi ya watawala wakati huo, mitaani Dar watu walifikia kuamini kuwa hawa watu waliuliwa kwa sumu hadi walioianzisha nao wakafikiri ni ukweli.

Ukweli ni kwamba hawa marehemu ni miongoni mwa waathirika wa mwanzo wa HIV na wakati ule uelewa haukuwa mkubwa na kulikuwa na unyanyapaa sana kiasa cha kudhania waheshimiwa viongozi hawawezi kudhaniwa haka kaugonjwa.
 
Jamani siyo hivyo. Niliwahi kuongea na daktari mmoja wa Muhimbili alinidokeza kuwa wale watu walikuwa na NGOMAwakaenda nje kubadilisha damu, lakini kwa kuwa kipindi kile utaalam huo ulikuwa haujashamiri, mambo yakawaendea kombo. Kumbuka kuwa walikuwa wanafia nje na kuletwa maiti kama sijakosea.:msela:

Please mkuu,
usidhalilishe taaluma za watu..waache madaktari wa ukweli wafanye kazi zao, usipeleke siasa huko, unless una solid evidence about misconduct kama ulivyowatuhumu hapo juu bolded..
Kuna wengi wanakesha kuokoa maisha ya binadamu; at the same time --wengine kwa sababu zao binafsi na kukosa utu--wanayaondoa
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni...Ni kitu gani kilichomzuia Mwinyi kuwaondoa na kuwaweka wanaoweza kutimiza matakwa yake....Mbona Mrema akupelekwa huko India?

Na kweli Mwinyi alitimiza matakwa yake baada ya kufa Rutihinda na Kibona kwani ndio wakati huo baada ya vifo vyao, akawateua Kighoma Alli Malima kuwa waziri wa fedha na Idris Rashid kuwa gavana wa benki kuu!!Huyu mzee alikuwa mchafu sana na ndiye aliyetuletea balaa zote hizi nchini mwetu na juu ya hayo anataka kumrithisha mwanae Hussein utawala wa nchi yetu; hilo haliwezekani waende wakale hizo pesa walizotuibia kupitia kwa Ladwa!!
 
Mkuu na watu wengine, katika matibabu ya HIV hakuna suala la kubadirisha damu. Nenda uendano hilo suala halipo kisayansi. Tena kwa dawa za HIV zilizopo sasa, ikiwa mwathirika wa VVU anatumia vizuri dawa, unaweza usimpate kabisa mdudu wa HIV ndani ya damu isipokuwa katika baadhi ya cells zenye CD4+ maeneo yaliyofichika katika mwili. Naamini kama kweli ulipewa taarifa kama hiyo, huyo mtu aliyekupa taarifa hiyo si daktari; na kama ni daktari basi ni daktari kihiyo maana taarifa alizokupa si sahihi.
Hata mimi nakuunga kwa miguu miwili na mikono miwili hilo suala la kubadilisha damu halipo na watu wengi wanaamini lipo ,kuna watu wanaweka ligi ya ubishi kuwa damu inabidilishwa hadi sasa,ni sawa na ule ubishi wa mkate na nini sijui kuku nani kilianza hadi jamaa wakaenda ku google kwa Francis teh teh
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom