Sababu 5 CCM Kushinda Uchaguzi 2015

Ingawa ni kweli CCM itashinda ila sababu zilizoletwa na mtoa maada si za CCM ya leo, nadhani mtoa maana kafunua malengo ya ccm wakati inaanzishwa kayaanika hapa, kwa kifupi CCM imepoteza dira na haina haijui inataka kufanya nini katika nchi hii, wanachojua viongozi wa ccm ni kuwa wanataka kushika dola tena sio kama chama bali watu binafsi kupitia chama.

Sababu pekee iliyopo kwa CCM kushinda ni kukosekana kwa upinzani wa kweli, upinzani umeingia kwenye mtego wa CCM kwamba ni wagomvi na wanahatarisha amani ya nchi. Sehemu kubwa ya wakina mama na wazee ambao ndio wapiga kura wa kweli wamekuwa waoga wa upinzani, Ukiajumlisha na CCM kugawa viapande vya khanga kwa kina mama na pombe za kienyeji kwa kina baba, kipi kitazua ushindi kwa CCM.
 
Kweli mtoa mada unachekesha sana. Mada yako ninailinganisha na mtu anayetoka kwenda kuiomba maiti imtolee damu.
 
Kama Mtanzania utaulizwa kuwa ni awamu ipi ambayo imefanikiwa sana jibu ni serikali ya kikwete awamu ya 4. wapo wajinga wanaoponda haya mafanikio lakini mhe.mbowe amesema mnyonge anyongwe lakini haki yake mpeni.wana jf.someni hutuba ya m.kiti wa ccm akifungua mkutano mkuu wa nane wa taifa wa ccm.
 
Ndugu zangu ni vizuri kuambiana mambo ya msingi haswa linapokuja swala la hatma ya Taifa letu.
Tanzania ni nchi ya kipekee duniani na watu wake ni wa kipekee pia, utu wetu , utanzania wetu huwezi pata sehemu nyingine. Watanzania ni watu wenye upendo, amani na mshikamano huwezi linganisha na nchi yoyote ile. Tumekuwa tukiishi siku zote kwa amani, kupendana na kushirikiana kabla na hata baada ya kuasisiwa taifa letu. Lakini baada ya kuingia siasa za upinzani nchini mwetu , kumekuwa na fikra zenye kuhatarisha amani yetu. Hatukatai upinzani, ndio maana kumekuwa na vyama vingi vya siasa nchini Tanzania. lakini kamwe hatutaruhusu amani yetu kupotea na siasa za kutubagua. Hadi hapa, Amani na maendeleo yaliyopoTanzania yametokana na uongozi wa chama cha mapinduzi. Kuanzia kwa wazee wetu waasisi, na viongozi wetu wakiongozwa na Mwenyekiti wetu, Rais wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete. Kwa siasa safi na uongozi makini, Sina budi kuzitaja sababu 5 kwa nini chama cha mapinduzi kitashinda uchaguzi wa 2015.

Moja; CCM imeweza kulinda na kudumisha Uhuru wa Nchi yetu na raia wake.
Muhimu kwa watanzania wote kukumbuka kwamba chama cha mapinduzi hakina udini wala ukabila kwa misingi hiyo kimeweza kudumisha amani na umoja wa nchi yetu.

Mbili; CCM imekuwa ya kwanza katika ushirikishwaji wa watanzania wote walio nje ya nchi katika kutoa mchango wao ili kuleta tija na maendeleo ya taifa letu.

Tatu; CCM imehakikisha kwamba Nchi yetu inatawaliwa kwa misingi ya kidemokrasia. Nchini Tanzania kuna demokrasia ya kutosha na hata kupitiliza. Mwananchi yoyote anao uhuru wa kuishi, kuabudu na kufanya maamuzi apendayo ili mradi sheria za nchi zinazingatiwa.

Nne; CCM haina ubaguzi, kila mtu anayo nafasi. Chama cha mapinduzi siku zote kimekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba Serikali na vyombo vyote vya umma vinatoa nafasi zilizo sawa kwa raia wote, wanawake na wanaume bila kujali rangi, kabila, Dini, au hali ya mtu.

Tano; CCM iko mstari wa mbele katika kuimarisha uhusiano mwema na Vyama vyote vya Siasa vya Nchi nyingine vyenye itikadi kama ya CCM ambavyo kweli vinapinga Ukoloni, Ukoloni Mamboleo, Ubeberu na Ubaguzi wa aina yoyote.

View attachment 70958
Source: Vijimambo
Plagiarism is an offense.
Jifunze kumtambua source.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Ongezea na ile ya kuwalipia ticket za ndege Wazamiaji waliopo Marekani waje nyumbani kuja kusalimia na kurudi kuendelea na box oyee.

Matola
Inaonekana una hasira ya maisha hao sio wazamiaji ni wakazi halali; wanakuja Tanzania mara nyingi sikulaumu huwafahamu ndio sababu unaropoka ovyo.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Tanzania hakuna chama cha Upinzani ila bali ni vyama vya kidini wewe Christian Democratic Movement aka Chadomo.Chini ya katibu wa baraza la Maaskofu padri mla vya watu Slaa.Mkishika hii nchi ujue yesu karudi

We unajua udini tu...longofya sana wewe....acheni udini hapa tujadili mambo yamaendeleo ya nchi yetu nani kakuambia utukuze dini za waarabu na wazungu afrika? Acha kuwa mtumwa wewe...
 
CCM ni baba wa vyama Tanzania hatahivyo inatakiwa itoe darasa kwa vyama vingine ambavyo vinaendeshwa kwa sura za kidini na kikanda wakiwa na lengo la kutugawa wananchi; vyama hivi vimejaa mapungufu:-

1. CUF - Uislam na Ukanda wa Pwani
2. Chadema - Ukristo na Ukanda wa Kaskazini na Uchaga

kwa hiyo wewe ndo mama wa vyama, unaweka kitu kisichokuwa na miguu hapa unatuambia hao walio CCM hawanba dini na mahali watokapo?
 
Matola
Inaonekana una hasira ya maisha hao sio wazamiaji ni wakazi halali; wanakuja Tanzania mara nyingi sikulaumu huwafahamu ndio sababu unaropoka ovyo.

Chama
Gongo la mboto DSM
Hao ni Wazamiaji tu, wote waliondoka Bongo kwa Non Immigrant Visa ya miezi 3 kipindi hicho, na hakuna hata mmoja ambaye aliomba Working Viza acha kuona kila aliye Bongo basi ni saa 7 usiku.
 
Hao ni Wazamiaji tu, wote waliondoka Bongo kwa Non Immigrant Visa ya miezi 3 kipindi hicho, na hakuna hata mmoja ambaye aliomba Working Viza acha kuona kila aliye Bongo basi ni saa 7 usiku.

Wengine waliwin lotto wameandoka bongo wakiwa status; pamoja yote wamerekebisha mambo tatizo lipo wapi? Hata wewe ulipoondoka Kamchukumu lengo lilikuwa kumsalimia dada Dar kwa mwezi tu ukaamua kulikita Dar; kwa mantiki wewe ulikimbia Bukoba na kulikita Dar na wahusika walikimbia Bongo na kulikita DC kutafuta maisha sasa tatizo lipo wapi?

Mtu aliyewin lotto hawezi kujishughulisha na upuuzi wa CCM Marekani na kusubili ticket za dezo ndio arudi nyumbani kusalimia, mnatia aibu sana kama maisha magumu rudini nyumbani muongeze nguvu kazi.

Mkurugenzi wa VOA Swahili ni Mtanzania na kuna watu kama kina John Mashaka hawa hata siku moja hawawezi kuvizia hizo ticket za dezo ndio warudi nyumbani.
 
Katika watu unayemjua ni John Mashaka na mkurugenzi wa VOA Mwamoyo Hamza? Mbona watanzania wengi tu wametulia; hao wote waliosafiri wanakuja sana bongo tatizo wewe upo Tabata kwa shemeji huwajui; ugumu wa maisha Marekani si urahisi wa bongo!

Hao nimetoa mfano tu, najuwa wapo wezi kama kina Othman Njaidi, Max Shimba nakadhalika, na wapo Wazee wa box oyee $20 per hour.
 
Hao nimetoa mfano tu, najuwa wapo wezi kama kina Othman Njaidi, Max Shimba nakadhalika, na wapo Wazee wa box oyee $20 per hour.

Matola
Unalipwa kiasi gani bongo? $20 kwa saa sio mbaya

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mimi silipwi, mimi ndio nalipa Wafanyakazi wangu, simply am Business Man......

Matola
Acha matumizi mabaya ya lugha wewe ni mchuuzi tu bado hujawa mfanyibiashara kulipa vibarua ndio unataka kujigeuza mfanyibiashara?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom