Sababu 3 Kwanini Magufuli Anatumia Kiswahili kwa Wageni na Ngambo... na maana yake kwetu...

Sio Waafrika tu,

Hata wahindi, wachina, wajapan, Wadutch, etc

Lakini usisahau kuwa kuna vyuo vinaomba tu barua ya kutoka chuo ulichosoma , kama proof ya kuwa ulisoma masomo yako kwa lugha ya kiingereza.

Swali ni je Amewezaje kufaulu masomo yake pasipo kujua lugha ya kufundishia hayo masomo?

Lkn hao uliowataja hawajiiti ,,english speaking countries” kama Waafrika, hivyo wao ni sawa kufanya toefl kwa maana wana lugha zao, ila Waafrika mnajiita ,,english speaking” sasa kwa nini mfanye toefl (test of english as a foreign language) ?
 
Kuna watu wanadai eti UDSM ni chuo bora Tanzania wanachukua wanafunzi wenye IQ kubwa kuliko vyuo vyote Tanzania na wanatoa graduate wazuri kuliko graduate wa vyuo vingine, Sasa wenye uelewa wetu tunazidi kuwacheka tu maana ubora ni wa mtu mwenyewe sio wa chuo na huyo bora anaweza kuwa chuo chochote kile
 
View attachment 1112688
(picha na New Zimbabwe.com)​

Na. M. M. Mwanakijiji
Inawezekana zipo sababu kubwa tatu ambazo zimemfanya Rais Magufuli kuanza kutumia lugha ya Kiswahili anapokutana na wageni wa kigeni pale Ikulu au anaposafiri kwenda ng’ambo. Sababu hizo zikieleweka zinaweza kutudokeza kidogo kwanini yumkini Rais amefikia uamuzi huo. Naomba kupendekeza tu kuwa tunaweza tusizikubali sababu hizi na inawezekana zikaonekana si za msingi lakini zinaweza kuwa na maana kubwa kitaifa.
Sababu hizi tatu zaweza kuwa ni:
  • Ameamua kuitangaza na kuikuza lugha Kiswahili kimataifa.
  • Hajiamini kujieleza kw aufasaha katika lugha ya Kiingereza
  • Sababu zote mbili za a na b.
Kwa vile hakuna chombo chochote cha serikali kilichotoa taarifa za uamuzi na sababu ya Rais kutumia lugha ya Kiswahili kwa namna hii basi ni haki ya Watanzania kukisia sababu hizi hadi itakavyoelezwa vinginevyo. Ni bahati mbaya na makosa kuwa vyombo ambavyo vingeweza kutoa taarifa hizo hajifanya hivyo. Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Wizara ya Habari na Utamaduni, au hata Ofisi ya Rais wenyewe wangeweza kuwaeleza tu Watanzania sababu ya uamuzi huu. Kwa vile hawajafanya hivyo, na sidhani kama wanampango wa kufanya hivyo basi sisi wengine tumejipa uhuru na haki ya kudhania. Naomba niziangalie sababu hizi tatu na maana yake kwa taifa.
  • Ameamua kuitangaza na kuikuza lugha ya Kiswahili kimataifa.
Lugha ya Kiswahili ni lugha kubwa, inayoeweka na watu wengi zaidi Afrika kuliko lugha nyingine yeyote ya Kiafrika. Karibu nchi 14 za Kiafrika zina wazungumzaji wa aina ya lugha ya Kiswahili. Ukichukulia tu kwa haraka haraka kuwa watu wa Tanzania na Kenya peke yake ambao wanaelewa Kiswahili kwa kiasi unaona kuwa tayari karibu watu milioni 100 wanaelewa kwa namna Fulani lugha ya Kiswahili. Miaka ya karibuni tayari mataifa mengine ya Kiafrika yameanza kukipokea Kiswahili kama lugha rasmi mojawapo.
Hivyo, Rais anapotumia lugha ya Kiswahili anakipa jukwaa kubwa zaidi kuliko huko nyuma. Tulizoea kwa muda mrefu kuwa marais wetu wanapoenda nje hata kwa majirani zetu wanalazimika kuzungumza lugha ya Kiingereza. Kwamba, sisi Waafrika hatuna lugha inayotuunganisha watu (lingua franca) wote isipokuwa zile lugha za kigeni. Kiswahili kama lugha ya Kiafrika ni rahisi kutamkika kwani misingi yake ya maneno iko karibu katika lugha zote za kibantu na kwa kiasi kikubwa lugha nyingine za Kiafrika.
Kwa kutumia lugha ya Kiswahili Rais anaipa heshima lugha yetu; heshima ambayo inastahili. Hivi majuzi wakati Rais Donald Trump wa Marekani alipoenda Japan tuliona jinsi Waziri Mkuu wa Japan Abe Shinzo akizungumza Kijapani. Hili limetokea hata kiongozi huyo wa Marekani alipokutana na Rais wa China au wa Urusi. Kibarua ilikuwa ni kwa wakalimani kutafrisi kutoka lugha moja kwenda nyingine. Hili halikuwa jambo la ajabu.
Hivyo, pamoja na kuitangaza na kuikuza lugha hii Magufuli anaipa heshima ambayo inastahili. Kwamba, wazungumzaji wa Kiswahili hata wakiwa na vyeo vya juu kabisa wasijione duni mbele ya wageni. Mmoja wa washairi wakubwa kabisa – kama siyo mkuu kabisa – katika historia ya nchi yetu marehemu mzee Shaaban Robert aliwahi kuandika utenzi wake mashuhuri wa “Titi la Mama li Tamu”. Ubeti wake wa kufungulia Shaaban Robert aliandika:
Titi la mama litamu,hata likiwa la mbwa,
Kiswahili naazimu,sifayo iliyofumbwa,
Kwa wasiokufahamu,niimbe ilivyo kubwa,
Toka kama mlizamu, funika palipozibwa

  • Hajiamini katika kujieleza katika lugha ya Kiingereza
Kwa wale ambao tumepata nafasi ya kumsikia Rais Magufuli akizungumza Kiingereza ni wazi kuwa tunaweza kuona akifanya makosa ama katika matamshi, muundo au fasihi ya lugha ya Kiingereza. Makosa ambayo Magufuli anayafanya wengi ambao wanajifunza lugha ya Kiingereza au wamejifunza lugha hiyo ukubwani wanaweza kujikuta wakiyafanya. Hili ni kweli pia kwa wazungumzaji wa asili wa lugha ya Kiingereza. Makosa haya yanaitwa “common mistakes” au “Common errors” katika lugha ya Kiingereza.
Makosa haya ya lugha si ya kipekee kwa lugha ya Kiingereza. Kwa mtu anayejifunza lugha ya Kiswahili au lugha nyingine yeyote anaweza kujikuta akiyafanya mara kwa mara. Ama katika kutamka maneno au katika muundo na sarufi ya lugha hiyo. Kwa mfano kwa watu wengi wanaojifunza Kiswahili wanaweza kushangaa kuwa lugha yetu haina sana msisitizo katika herufi Fulani kama ilivyo katika lugha nyingine nyingi.
Sasa Magufuli inawezekana ameona watu wanamsema au anaonekana kama kituko kwa wageni pale anapovunja lugha ya Kiingereza hasa kwa vile ni msomi wa PhD. Hili linatuleta kwenye hoja nyingine ndani ya hoja hii kuwa kuwa msomi wa eneo Fulani haina maana mtu anaimudu lugha ya Kiingereza. Kiingereza cha kisomi (academic writing) mara nyingi si kigumu kama kile cha kujieleza. Hii ni kwa sababu lugha ya kisomi ina maneno yake na ni rahisi kufuata. Si kila msomi anaweza kuandika riwaya ya Kiingereza au insha ya kijamii kwa Kiingereza bila kupata shida ya maneno. Hili linatokea hata kwa wasomi kutoka nchi nyingine ambazo hawazungumzi Kiingereza kwa asili (native English speakers).
Sasa kama Magufuli anaona hajiamini kwa sababu ya makosa ya mara kwa mara – ambayo si ya ajabu sana – inawezekana kuamua kuzungumza Kiswahili ni salama na bora kwake kuliko kujionesha udhaifu wake wa lugha.
Ikumbukwe hili si tatizo la Magufuli tu. Wapo watu wetu wengi tu ambao wanaweza kuchanganya maneno ya Kiingereza kwenye Kiswahili (Kiswakinge) lakini hawawezi kuunda kauli zinazoeleweka za lugha ya Kiingereza. Na wengine hata Kiswahili kilichonyoka (kisichonganyana) na Kiingereza hawawezi kukitumia. Tumeona mambo haya Bungeni ambapo sharti mojawapo ni kuwa mgombea awe anaweza kujua lugha ya Kiingereza au Kiswahili. Tumeona watu wanaoomba kugombea Bunge la Afrika ya Mashariki wengine wakivunja maneno hadi unasikia kujing’ata ulimi! Lakini watu wale wale wanaweza kujieleza kwa Kiswakinge!
  • Mchanganyiko wa Sababu 2 za Kwanza
Inawezekana kabisa kuwa Rais ameamua kufanya hivi kutokana na sababu zote mbili kwamba anataka kuienzi, kuiheshimu na kuipa jukwaa kubwa lugha ya Kiswahili lakini vile vile yeye mwenyewe hayuko mzuri sana (kama Watanzania wengine wengi) kutumia lugha ya Kiingereza kwenye hadhara. Kama hili ni kweli basi hakuna aibu katika yote mawili; yote mawili yanaweza kuwa sababu za kutosha tu.
Hii ina Maana gani kwa taifa?
Swali kubwa la msingi ni je jambo hili lina maana gani kwetu kama taifa? Je, ina maana sasa Watanzania wasijifunze Kiingereza kabisa na wote wajifunze kila kitu kwa Kiswahili? Je, ina maana lugha ya Kiingereza si muhimu tena? Naomba kupendekeza mambo yafuatayo:
  • Ikumbukwe kuwa kama taifa na kama mtu mmoja mmoja hatuwezi kukwepa matumizi ya lugha ya Kiingereza. Kwanza kwa sababu mfumo wetu wa kiserikali unafuata kwa kiasi kikubwa mfumo wa Kiingereza lakini pili ni kuwa kwa vile lugha ya Kiingereza ndio lugha inayoiunganisha dunia. Sasa hivi ni vigumu kwenda mahali popote na kukosa kabisa mtu anayejua Kiingereza. Ni rahisi kupata mtu anayejua Kiingereza kuliko mtu anayejua lugha nyingine yeyote. Hivyo, Kiingereza hakikwepeki.
  • Kwamba watu wetu wanapata shida kumudu lugha hii ni matokeo ya mambo mengi. Yawezekana kwa kiasi kikubwa ni suala la elimu na mfumo wetu wa elimu. Lugha ya Kiingereza nakumbuka ilianza kufundishwa toka darasa la tatu (sijui kama bado ni hivi). Sasa mtu anachukua Kiingereza toka darasa la tatu hadi la kumi na nne na bado hajamudu lugha hii ni shida. Ama walimu wetu, mitaala yetu au mfumo wetu mzima unahitai kuangaliwa. Na hili linahusu pia lugha ya Kiswahili yenyewe. Tumeona watu wanatoka Chuo Kikuu lakini wanapata shida kujieleza kwa Kiswahili hadi unaweza kuwaonea huruma!
  • Lugha kama somo jingine lolote lile linahitaji mtu kujifunza zaidi na kujiendeleza. Kosa kubwa ambalo naweza kuliona ni kuwa watu wanadhaniwa “wanajua” kiingereza kwa sababu wamepata shahada Fulani. Kwamba, kwa vile mtu ameenda chuo kikuu basi anadhaniwa anajua Kiingereza. Na hasa kwa vile anaweza kuandika kwa kutumia “templates” na msaada ya program za kusaidia kuandika. Ni muhimu mtu kujiendeleza yeye mwenyewe. Ikumbukwe kuwa hata kwenye nchi za wazungumzaji wa Kiingereza wa asili pia na wao wanawafundisha watoto wao Kiingereza sahihi. Kiingereza cha kuandika na kuzungumza vina misamiati tofauti na kile cha kisomi. Tuliosoma kwenye hizi nchi za wenzetu tunajua kabisa kuwa hata Chuo Kikuu baadhi ya masomo ya kwanza kwenye kozi ni yale ya kupandisha lugha kidogo. Masomo haya yanaitwa “English 101” ambayo ni kozi ya mhula wa kwanza kwenye vyuo vikuu vingi. Sasa kama wenyewe hawa wanatoa hizi kozi na zinaenda zaidi sisi wengine ambao Kiingereza ni lugha ya tatu au ya nne kwanini tusione umuhimu wa kuhakikisha mtoto kabla ya kwenda Chuo Kikuu anasoma Kiingereza tena? Hadi awe anaonesha uhimili (proficiency) ya lugha?
  • Ni muhimu kuanzia sasa kwa Wizara ya Mambo ya Nje au chombo husika kuhakikisha kuwa Rais anaenda na mkalimani wake ambaye anamudu Kiingereza. Asiwe mtu mwenye “mmh mmh, aah aah” nyingi! Isije kutokea lililotokea juzi Zimbabwe. Kwamba, Wizara na Ikulu hawakumuandaa mtu wa kufanya ukalimani ni jambo la aibu. Kwenye mambo haya ya kimataifa kuna taratibu za kuweza kumtumia mkalimani baada ya kuapa. Kwanini hakukuwa na mkalimani sielewi. Rais Magufuli na yeye asidhanie kuwa watu wataelewa Kiswahili kwa vile tu yeye anazungumza. Ni lazima atoe nafasi kwa mtu kumtafsiria. Japo atakuwa anaweza kuelewa mtu akizungumza kwa Kiingereza yeye bado anaweza kujibu kwa Kiswahili na mkalimani akatafsiri. Wapo Watanzania wengi ndani na nje ambao wanamudu lugha mbalimbali na ambao Rais anaweza kuwatumia.
Itoshe tu mimi kusema kuwa, sijaona tatizo lolote lile kwa Rais kuzungumza lugha ya Kiswahili kwa sababu yoyote ile. Kitu ambacho sikukipenda na hakikuwa na ulazima ni kuonekana kuwa upande wetu hatukujiandaa vizuri na kuwa Rais alizungumza Kiswahili bila kuwaandaa upande wa pili. Kuna teknolojia za kutosha hata za vyombo vya masikioni ambayo Rais anaweza kwenda navyo na wageni wahusika wakapewa wakati anazungumza na watu wetu wakatafsiri moja kwa moja. Kama tumeamua kuyavulia nguo maji, basi tujitumbukize kweli kweli siyo miguu tu! Ni matumaini yangu kuwa uamuzi wa makusudi, wa kina na wenye kuongozwa na sayansi utafanyika ili kuhakikisha kuwa lugha ya Kiswahili inaendelea kukuzwa lakini vile vile kuinua matumizi ya lugha ya Kiingereza. Si lazima tufanye uchaguzi wa kimojawapo na si kingine. Naamini kwa taifa letu kuendelea hivi viwili vinatakiwa viwe kama mapacha wanaofanana. Naamini katika kuharakisha maendeleo na kujiamini hatupaswi kuonesha uduni au ubora wa lugha moja dhidi ya nyingine na badala tuone kuwa lugha hizi kama walivyofanya nchi nyingine duniani zinaendana. Wachina wanajifunza Kichina na Kiingereza, Waarabu wanajifunza Kiarabu na Kiingereza, hata Wajerumaini na Wafaransa nao wanakifunza Kiingereza vile vile. Sasa kama hawa wenzetu walioendelea wanaona umuhimu wa lugha zao PAMOJA na lugha ya Kiingereza sisi tunachokihofia ni nini?
Magufuli ameonesha njia tu. Tutaifuata au tunaona aibu na kujiona duni?
Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com
mi lugha ya malkia ndo najiamini. hata navotongoza dame. kwa kisqahili lazima nifeli. akijichanganya kwenye lugha ya malikia ameliwa
 
Acha ujinga wako wewe! Usitufanye Watanzania ni WAPUMBAVU kiasi hiki! UPUUZI MTUPU@ Eti nduli anakuza Kiswahili! Kama ni kukuza Kiswahili kwanini isiwe walio ndani ya Serikali wote wakiwa nje ya nchi waongee Kiswahili na siyo huyo dikteta peke yake? Kama huna cha maana cha kuandika ni bora ukae kimya badala ya kuonyesha ujuha wako hadharani ukidhani Watanzania ni wapumbavu wakubwa.
Karai kama kawaida yako
 
CCM kwa kuhamisha magoli hamjambo, Mr. Mmm unakumbuka uchaguzi wa 1995, Mkapa vs Mrema? Kigezo na propaganda kubwa ilikuwa kumdis Mrema kuwa hajui kiingereza, ataombaje misaada, ataongeaje na wageni wa kimataifa nk.

Mungu si Athumani kaamua kumleta kutoka upande huohuo asiyejua kiingereza lakini ana PHD, sasa propaganda zimehamia kuwa kiingereza si kitu maana wachina na north Korea wananguvu na hawaongei kiingereza!

Mmm ulivyojiunga na hao watu ni nadra malaik wa mbinguni kuanza kumtetea shetani, try hard mmm!
 
This is rubbish from a learned person like you! If this so-called "kukitangaza Kiswahili" is done by a person with a very good command of English like Professor "Lumumba" anyway, then your arguments would hold water. But with a person so poor in English, both spoken and written, then your thinking from a person of your level, allow me to call it "professorial" rubbish!
Karai la ufipa katika ubora wako.

Mnajdili lugha ya rais uchaguzi 2020 mtapigwa matakuja kulia tena hapa
 
Ukitaka kujua kiswahili ni janga, geuza hiyo simu yako itumie kiswahili badala ya kiingereza kisha uje hapa uchangie.
... ha ha ha! We jamaa! Umenikumbusha; linapokuja suala la simu hata bibi yangu kule kijijini ana-prefer version ya Kiingereza kuliko Kiswahili.
 
This is rubbish from a learned person like you! If this so-called "kukitangaza Kiswahili" is done by a person with a very good command of English like Professor "Lumumba" anyway, then your arguments would hold water. But with a person so poor in English, both spoken and written, then your thinking from a person of your level, allow me to call it "professorial" rubbish!

Well said. Hakuna kumung'unya maneno. Suala si uzalendo wala kutangaza Kiswahili. RAIS HAJUI KIINGEREZA, FULL STOP.
 
Kusoma hadi level ya PhD siyo guarantee kwamba kuwa utamudu kuongea kiingereza katika maongezi ya kawaida hasa kama hukitumii katika mawasiliano yako ya kila siku na ikiwa siyo lugha yako ya asili kama ilivyo kwetu bongo. Kwa sisi hasa tuliosoma masomo ya sayansi, tunaweza kuwa wazuri sana kwenye zile taaluma zetu hadi kuwa madaktari bingwa tusiweze kuongea kiingereza fluently lakini tunaweza kuwasiliana au kuwasilisha mada kwenye taaluma zetu kwa sababu academic writing and speaking ni tofauti na maongezi ya kawaida

Kwa mfumo wa elimu yetu hadi PhD ni masaa zaidi ya laki moja na nusu ya ku consume na ku Generate knowledge iliyo kwa Kingereza kwa kiasi kikubwa. Ukisema kati ya huo muda ni asilimia 1 tu ndio inatumika kwenye mambo ya shule (chini ya dk 15 kwa siku), unazungumzia masaa 1500. Ukiweka na consumption ya muziki, filamu, magazeti na habari kwa ujumla, interaction za kijamii, na interaction na Kingereza kazini, kuna tatizo somewhere.

That said, research has shown mastery of languages, any language, to be an indicator of one's intelligence. I emphasise on any language because English tends to derail the discussion despite the fact that for us it is the low hanging fruit, easy considering the amount of it we are exposed to in our lifetime. A Tanzanian who speaks zulu or Italian, now that's impressive cause it shows he likely made a real effort.
 
Mbona Russia president, China president, Japan president, hawaongei kingereza wanapokuwa na Donald trump, hii kasumba ya kikoloni shida sana.

Ingekuwa kasumba ya kikoloni kama tungekuwa tunakitazama Kiarabu na kijerumani kama ambayo unakitazama kiingereza.
 
Katika Marais watano waliotawala Tanzania, mtaalamu wa kuongea kiingereza cha Kisiasa, kiuchumi, kidini na cha mitaani alikuwa Rais wa awamu ya kwanza Marehemu Mwalimu J.K. Nyerere.
huyu aliweza kuongea ung'eng'e kuliko Waingereza wenyewe na walikuwa wanmshangaa sana.Hayati Mwalimu Nyerere hata alipokuwa anaongea Kiswahili, alikuwa anaongea kwa kutumia Kiswahili chenye ufasaha wa halii ya juu.
Kwa hiyo kujua lugha na kuweza kuiongea kwa ufasaha ni KARAMA au KIPAJI cha mtu.
Bahati nzuri Kiswahili hata ukiongea broken hakuna mtu atakucheka au kushangaa lakini ukiongea kiingereza broken ni aibu mbele ya watu.
Kawaida Wanasayansi wengi huwa wanaongea kiingereza broken. Wanasayansi kitu muhimu kwao ni kujua fomula, Principal nk.
Rais wetu ni Mwanasayansi ,kwake kuongea kiingeresa fasaha cha Kisiasa, kiuchumi nk si kitu muhimu.
Kwa hiyo kama anaweza kuongea Kiswahili au Kisukuma kwa ufasaha na watu wakamuelewa au kukawa na mkalimani mzuri, anafanya jambo sahihi na lenye tija kwa kutumia Kiswahili badala ya lugha ingine.
Hata Rais Mwinyi alikuwa hapendi sana kutoa hotuba zake kwa kiingereza. Yeye alipenda sana kuongea Kiswahili kama anavyofanya Rais aliyeko madarakani.
 
Hayo yote mawili yanaenda pamoja, kutokujua na kuamua kuitangaza
Tatizo letu ni moja kila anaetaka kufanya kitu anaamua kufanya peke yake kama sheria yake pekee
Viongozi wote wamekuwa na kasumba hii ya kujiamulia kitu bila kushirikisha wengine na kuifanya kama sheria.

Elimu ya kusoma soma la kiingereza kuanzia la tatu halina faida yeyote kama lugha haifundishwi kwa masomo yote.
Na hii ndio unakuta mtu ana ufaulu mzuri kwa kukariri lakini alichofaulu kwa kingereza ukimwambia aiandike kwa kiswahili sidhani kama ataweza

Watu hawajiongezi kujifunza hata kwa kusoma magazeti na kuangalia tv
Practice inahitajika bila aibu we ongea tu
 
View attachment 1112688
(picha na New Zimbabwe.com)​

Na. M. M. Mwanakijiji
Inawezekana zipo sababu kubwa tatu ambazo zimemfanya Rais Magufuli kuanza kutumia lugha ya Kiswahili anapokutana na wageni wa kigeni pale Ikulu au anaposafiri kwenda ng’ambo. Sababu hizo zikieleweka zinaweza kutudokeza kidogo kwanini yumkini Rais amefikia uamuzi huo. Naomba kupendekeza tu kuwa tunaweza tusizikubali sababu hizi na inawezekana zikaonekana si za msingi lakini zinaweza kuwa na maana kubwa kitaifa.
Sababu hizi tatu zaweza kuwa ni:
  • Ameamua kuitangaza na kuikuza lugha Kiswahili kimataifa.
  • Hajiamini kujieleza kw aufasaha katika lugha ya Kiingereza
  • Sababu zote mbili za a na b.
Kwa vile hakuna chombo chochote cha serikali kilichotoa taarifa za uamuzi na sababu ya Rais kutumia lugha ya Kiswahili kwa namna hii basi ni haki ya Watanzania kukisia sababu hizi hadi itakavyoelezwa vinginevyo. Ni bahati mbaya na makosa kuwa vyombo ambavyo vingeweza kutoa taarifa hizo hajifanya hivyo. Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Wizara ya Habari na Utamaduni, au hata Ofisi ya Rais wenyewe wangeweza kuwaeleza tu Watanzania sababu ya uamuzi huu. Kwa vile hawajafanya hivyo, na sidhani kama wanampango wa kufanya hivyo basi sisi wengine tumejipa uhuru na haki ya kudhania. Naomba niziangalie sababu hizi tatu na maana yake kwa taifa.
  • Ameamua kuitangaza na kuikuza lugha ya Kiswahili kimataifa.
Lugha ya Kiswahili ni lugha kubwa, inayoeweka na watu wengi zaidi Afrika kuliko lugha nyingine yeyote ya Kiafrika. Karibu nchi 14 za Kiafrika zina wazungumzaji wa aina ya lugha ya Kiswahili. Ukichukulia tu kwa haraka haraka kuwa watu wa Tanzania na Kenya peke yake ambao wanaelewa Kiswahili kwa kiasi unaona kuwa tayari karibu watu milioni 100 wanaelewa kwa namna Fulani lugha ya Kiswahili. Miaka ya karibuni tayari mataifa mengine ya Kiafrika yameanza kukipokea Kiswahili kama lugha rasmi mojawapo.
Hivyo, Rais anapotumia lugha ya Kiswahili anakipa jukwaa kubwa zaidi kuliko huko nyuma. Tulizoea kwa muda mrefu kuwa marais wetu wanapoenda nje hata kwa majirani zetu wanalazimika kuzungumza lugha ya Kiingereza. Kwamba, sisi Waafrika hatuna lugha inayotuunganisha watu (lingua franca) wote isipokuwa zile lugha za kigeni. Kiswahili kama lugha ya Kiafrika ni rahisi kutamkika kwani misingi yake ya maneno iko karibu katika lugha zote za kibantu na kwa kiasi kikubwa lugha nyingine za Kiafrika.
Kwa kutumia lugha ya Kiswahili Rais anaipa heshima lugha yetu; heshima ambayo inastahili. Hivi majuzi wakati Rais Donald Trump wa Marekani alipoenda Japan tuliona jinsi Waziri Mkuu wa Japan Abe Shinzo akizungumza Kijapani. Hili limetokea hata kiongozi huyo wa Marekani alipokutana na Rais wa China au wa Urusi. Kibarua ilikuwa ni kwa wakalimani kutafrisi kutoka lugha moja kwenda nyingine. Hili halikuwa jambo la ajabu.
Hivyo, pamoja na kuitangaza na kuikuza lugha hii Magufuli anaipa heshima ambayo inastahili. Kwamba, wazungumzaji wa Kiswahili hata wakiwa na vyeo vya juu kabisa wasijione duni mbele ya wageni. Mmoja wa washairi wakubwa kabisa – kama siyo mkuu kabisa – katika historia ya nchi yetu marehemu mzee Shaaban Robert aliwahi kuandika utenzi wake mashuhuri wa “Titi la Mama li Tamu”. Ubeti wake wa kufungulia Shaaban Robert aliandika:
Titi la mama litamu,hata likiwa la mbwa,
Kiswahili naazimu,sifayo iliyofumbwa,
Kwa wasiokufahamu,niimbe ilivyo kubwa,
Toka kama mlizamu, funika palipozibwa
  • Hajiamini katika kujieleza katika lugha ya Kiingereza
Kwa wale ambao tumepata nafasi ya kumsikia Rais Magufuli akizungumza Kiingereza ni wazi kuwa tunaweza kuona akifanya makosa ama katika matamshi, muundo au fasihi ya lugha ya Kiingereza. Makosa ambayo Magufuli anayafanya wengi ambao wanajifunza lugha ya Kiingereza au wamejifunza lugha hiyo ukubwani wanaweza kujikuta wakiyafanya. Hili ni kweli pia kwa wazungumzaji wa asili wa lugha ya Kiingereza. Makosa haya yanaitwa “common mistakes” au “Common errors” katika lugha ya Kiingereza.
Makosa haya ya lugha si ya kipekee kwa lugha ya Kiingereza. Kwa mtu anayejifunza lugha ya Kiswahili au lugha nyingine yeyote anaweza kujikuta akiyafanya mara kwa mara. Ama katika kutamka maneno au katika muundo na sarufi ya lugha hiyo. Kwa mfano kwa watu wengi wanaojifunza Kiswahili wanaweza kushangaa kuwa lugha yetu haina sana msisitizo katika herufi Fulani kama ilivyo katika lugha nyingine nyingi.
Sasa Magufuli inawezekana ameona watu wanamsema au anaonekana kama kituko kwa wageni pale anapovunja lugha ya Kiingereza hasa kwa vile ni msomi wa PhD. Hili linatuleta kwenye hoja nyingine ndani ya hoja hii kuwa kuwa msomi wa eneo Fulani haina maana mtu anaimudu lugha ya Kiingereza. Kiingereza cha kisomi (academic writing) mara nyingi si kigumu kama kile cha kujieleza. Hii ni kwa sababu lugha ya kisomi ina maneno yake na ni rahisi kufuata. Si kila msomi anaweza kuandika riwaya ya Kiingereza au insha ya kijamii kwa Kiingereza bila kupata shida ya maneno. Hili linatokea hata kwa wasomi kutoka nchi nyingine ambazo hawazungumzi Kiingereza kwa asili (native English speakers).
Sasa kama Magufuli anaona hajiamini kwa sababu ya makosa ya mara kwa mara – ambayo si ya ajabu sana – inawezekana kuamua kuzungumza Kiswahili ni salama na bora kwake kuliko kujionesha udhaifu wake wa lugha.
Ikumbukwe hili si tatizo la Magufuli tu. Wapo watu wetu wengi tu ambao wanaweza kuchanganya maneno ya Kiingereza kwenye Kiswahili (Kiswakinge) lakini hawawezi kuunda kauli zinazoeleweka za lugha ya Kiingereza. Na wengine hata Kiswahili kilichonyoka (kisichonganyana) na Kiingereza hawawezi kukitumia. Tumeona mambo haya Bungeni ambapo sharti mojawapo ni kuwa mgombea awe anaweza kujua lugha ya Kiingereza au Kiswahili. Tumeona watu wanaoomba kugombea Bunge la Afrika ya Mashariki wengine wakivunja maneno hadi unasikia kujing’ata ulimi! Lakini watu wale wale wanaweza kujieleza kwa Kiswakinge!
  • Mchanganyiko wa Sababu 2 za Kwanza
Inawezekana kabisa kuwa Rais ameamua kufanya hivi kutokana na sababu zote mbili kwamba anataka kuienzi, kuiheshimu na kuipa jukwaa kubwa lugha ya Kiswahili lakini vile vile yeye mwenyewe hayuko mzuri sana (kama Watanzania wengine wengi) kutumia lugha ya Kiingereza kwenye hadhara. Kama hili ni kweli basi hakuna aibu katika yote mawili; yote mawili yanaweza kuwa sababu za kutosha tu.
Hii ina Maana gani kwa taifa?
Swali kubwa la msingi ni je jambo hili lina maana gani kwetu kama taifa? Je, ina maana sasa Watanzania wasijifunze Kiingereza kabisa na wote wajifunze kila kitu kwa Kiswahili? Je, ina maana lugha ya Kiingereza si muhimu tena? Naomba kupendekeza mambo yafuatayo:
  • Ikumbukwe kuwa kama taifa na kama mtu mmoja mmoja hatuwezi kukwepa matumizi ya lugha ya Kiingereza. Kwanza kwa sababu mfumo wetu wa kiserikali unafuata kwa kiasi kikubwa mfumo wa Kiingereza lakini pili ni kuwa kwa vile lugha ya Kiingereza ndio lugha inayoiunganisha dunia. Sasa hivi ni vigumu kwenda mahali popote na kukosa kabisa mtu anayejua Kiingereza. Ni rahisi kupata mtu anayejua Kiingereza kuliko mtu anayejua lugha nyingine yeyote. Hivyo, Kiingereza hakikwepeki.
  • Kwamba watu wetu wanapata shida kumudu lugha hii ni matokeo ya mambo mengi. Yawezekana kwa kiasi kikubwa ni suala la elimu na mfumo wetu wa elimu. Lugha ya Kiingereza nakumbuka ilianza kufundishwa toka darasa la tatu (sijui kama bado ni hivi). Sasa mtu anachukua Kiingereza toka darasa la tatu hadi la kumi na nne na bado hajamudu lugha hii ni shida. Ama walimu wetu, mitaala yetu au mfumo wetu mzima unahitai kuangaliwa. Na hili linahusu pia lugha ya Kiswahili yenyewe. Tumeona watu wanatoka Chuo Kikuu lakini wanapata shida kujieleza kwa Kiswahili hadi unaweza kuwaonea huruma!
  • Lugha kama somo jingine lolote lile linahitaji mtu kujifunza zaidi na kujiendeleza. Kosa kubwa ambalo naweza kuliona ni kuwa watu wanadhaniwa “wanajua” kiingereza kwa sababu wamepata shahada Fulani. Kwamba, kwa vile mtu ameenda chuo kikuu basi anadhaniwa anajua Kiingereza. Na hasa kwa vile anaweza kuandika kwa kutumia “templates” na msaada ya program za kusaidia kuandika. Ni muhimu mtu kujiendeleza yeye mwenyewe. Ikumbukwe kuwa hata kwenye nchi za wazungumzaji wa Kiingereza wa asili pia na wao wanawafundisha watoto wao Kiingereza sahihi. Kiingereza cha kuandika na kuzungumza vina misamiati tofauti na kile cha kisomi. Tuliosoma kwenye hizi nchi za wenzetu tunajua kabisa kuwa hata Chuo Kikuu baadhi ya masomo ya kwanza kwenye kozi ni yale ya kupandisha lugha kidogo. Masomo haya yanaitwa “English 101” ambayo ni kozi ya mhula wa kwanza kwenye vyuo vikuu vingi. Sasa kama wenyewe hawa wanatoa hizi kozi na zinaenda zaidi sisi wengine ambao Kiingereza ni lugha ya tatu au ya nne kwanini tusione umuhimu wa kuhakikisha mtoto kabla ya kwenda Chuo Kikuu anasoma Kiingereza tena? Hadi awe anaonesha uhimili (proficiency) ya lugha?
  • Ni muhimu kuanzia sasa kwa Wizara ya Mambo ya Nje au chombo husika kuhakikisha kuwa Rais anaenda na mkalimani wake ambaye anamudu Kiingereza. Asiwe mtu mwenye “mmh mmh, aah aah” nyingi! Isije kutokea lililotokea juzi Zimbabwe. Kwamba, Wizara na Ikulu hawakumuandaa mtu wa kufanya ukalimani ni jambo la aibu. Kwenye mambo haya ya kimataifa kuna taratibu za kuweza kumtumia mkalimani baada ya kuapa. Kwanini hakukuwa na mkalimani sielewi. Rais Magufuli na yeye asidhanie kuwa watu wataelewa Kiswahili kwa vile tu yeye anazungumza. Ni lazima atoe nafasi kwa mtu kumtafsiria. Japo atakuwa anaweza kuelewa mtu akizungumza kwa Kiingereza yeye bado anaweza kujibu kwa Kiswahili na mkalimani akatafsiri. Wapo Watanzania wengi ndani na nje ambao wanamudu lugha mbalimbali na ambao Rais anaweza kuwatumia.
Itoshe tu mimi kusema kuwa, sijaona tatizo lolote lile kwa Rais kuzungumza lugha ya Kiswahili kwa sababu yoyote ile. Kitu ambacho sikukipenda na hakikuwa na ulazima ni kuonekana kuwa upande wetu hatukujiandaa vizuri na kuwa Rais alizungumza Kiswahili bila kuwaandaa upande wa pili. Kuna teknolojia za kutosha hata za vyombo vya masikioni ambayo Rais anaweza kwenda navyo na wageni wahusika wakapewa wakati anazungumza na watu wetu wakatafsiri moja kwa moja. Kama tumeamua kuyavulia nguo maji, basi tujitumbukize kweli kweli siyo miguu tu! Ni matumaini yangu kuwa uamuzi wa makusudi, wa kina na wenye kuongozwa na sayansi utafanyika ili kuhakikisha kuwa lugha ya Kiswahili inaendelea kukuzwa lakini vile vile kuinua matumizi ya lugha ya Kiingereza. Si lazima tufanye uchaguzi wa kimojawapo na si kingine. Naamini kwa taifa letu kuendelea hivi viwili vinatakiwa viwe kama mapacha wanaofanana. Naamini katika kuharakisha maendeleo na kujiamini hatupaswi kuonesha uduni au ubora wa lugha moja dhidi ya nyingine na badala tuone kuwa lugha hizi kama walivyofanya nchi nyingine duniani zinaendana. Wachina wanajifunza Kichina na Kiingereza, Waarabu wanajifunza Kiarabu na Kiingereza, hata Wajerumaini na Wafaransa nao wanakifunza Kiingereza vile vile. Sasa kama hawa wenzetu walioendelea wanaona umuhimu wa lugha zao PAMOJA na lugha ya Kiingereza sisi tunachokihofia ni nini?
Magufuli ameonesha njia tu. Tutaifuata au tunaona aibu na kujiona duni?
Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com
Andiko lako ni refu mno kwa mTz kama Mimi, mi nimeenda moja kwa moja kuchagua hill la katikati, Asante sana.
 
Naona unajaribu kuficha madhaifu ya Mfalme ya kutokujua vizuri Kiingereza.
Unafikiri labda hili tatizo nimeliona leo; ni tatizo la msingi kwa Watanzania wengi. Lakini kutokujua vizuri Kiingereza haina maana mtu hajui anachozungumza au anachotaka kuzungumza. Sasa kwanini asizungumze kwa lugha anayoweza kujieleza vizuri? Ila nina uhakika angekuwa anaruhusiwa kujieleza kwa Kisukuma tungekiona cha moto...
 
We knew this already...

Labda utuambie kwa analysis yako most probably ipi ndio hasa sababu inayomfanya hivyo!

Nachohisi mimi binafsi...ni sababu ya pili...

Hajui kuongea Kiingereza maana hata Kiswahili chenyewe hajui kabisa!
 
Back
Top Bottom