Sababu 3 Kuonyesha Kwamba Richmond ni Mali ya Rostam Zatajwa!

kazi kweli kweli wajameni, hii ndio tanzania na hawa ndio viongozi wetu
 
...katika Tanzania hii nakulilia wanaotaka mambo yatendwe ni wengi, ila wanaothubutu kutenda ni wachache!!
 
Mnalia na RA wakati kuna munene yupo nyuma yake mnaogopa kumrushia mawe

Hapa atulii na mtu bali tunatafuta wahusika. Huyo mnene unayemsema kuwa tunaogopa kumrushia mawe ni ni Raisi wa Tanzania kupitia chama cha mapinduzi - Jakaya Mrisho Kikwete. Ametajwa mara nyingi humu JF kuwa amewekwa mfukoni mwa RA na do maana ameshindwa kuchukua hatua stahili juu ya Mafisadi.
Maadamu RA ndiye anaye onekana zaidi (amewaficha hao wengine mfukuni/tumboni), ndo maana tunamtafuta ili tuwapate hao wengine. TUKIMPASUA TUMBO, HAO WOTE WALIOJIFICHA NDANI MWAKE TUTAWAPATA. Tunacho fanya ndicho hicho.

"Follow the river and you will find the sea"
 
Buchanan, Nashukuru bora umeileta hiyo, kuna jamaa wako special humu kwa ajili ya Dowans, juzi tulibishana nikawaeleza soma hiyo Mwanahalisi na wenyewe wananikazania nisome Mtanzania. Na sasa hivi watakuja!!
Hawa waliopo humu kwa ajili ya Dowans tafadhali wakae na kutambua huu ujambazi una mwisho, hata Mobutu Seseko aliyekuwa ananunua majeshi ya Ubelgiji na ufaransa ulifika mwnisho na akatimka
 
Hawa waliopo humu kwa ajili ya Dowans tafadhali wakae na kutambua huu ujambazi una mwisho, hata Mobutu Seseko aliyekuwa ananunua majeshi ya Ubelgiji na ufaransa ulifika mwnisho na akatimka

Mwisho wao ni lini, na mbona unachelewa kufika wakati taifa linaangamia? ama tutaendelea kuungoja mpaka kiama wakati nchi inakwisha?
 
Buchanan, Nashukuru bora umeileta hiyo, kuna jamaa wako special humu kwa ajili ya Dowans, juzi tulibishana nikawaeleza soma hiyo Mwanahalisi na wenyewe wananikazania nisome Mtanzania. Na sasa hivi watakuja!!
Mtanzania ni gazeti linalomilikiwa na New habari 2006 ambayo ni kampuni ya Rost tamu sasa ndo imepewa kazi ya kusafisha hilo.
 
Kubenea Kiboko
Not bad kwa kijana illiterate from Kirongwe village in Mafia amabaye hajui difference between peace talks na peace process
haya endeleeni

Na wasemaje kuhusu Boss wa Usalama Rashid Othman na Waziri wake Sophia Simba! Mbele ya Kubenea hawa hawaoni ndani.
 
Kikao cha juzi juzi cha wana-CCM Mjini Dodoma kimeibua mambo mengi! Kwenye kikao hicho ilidaiwa kwamba wakati Mbunge wa Nzega, Mh Selelii akiongea kwa makini na kwa kujiamini huku kukiwa na kimya kikuu ambacho kama sindano ingedodoka ungeisikia, Mh Selelii baada ya kumtoa jasho Rostam Aziz kwa kutoa ushahidi kuwa alikuwa mmiliki wa Richmond alimgeukia mbunge wa Ukonga, Mh Makongoro Mahanga ambaye alidai Ripoti ya Richmond (maarufu kama Ripoti ya Dkt Mwakyembe) ilikuwa feki, eti kwa sababu Kamati Teule haikumshirikisha Rais Kikwete ambaye "kama angeelezwa angemwokoa Lowasa!"

Lakini Mh Selelii alihoji, kama Ripoti ilikuwa feki inawezekanaje Rais aliyepewa taarifa hiyo kabla ya kufikishwa bungeni akaiamini? Kuhusu Kamati teule kutokumshirikisha Rais Kikwete, Selelii alisema kabla ya Kamati Teule kuwasilisha ripoti yake bungeni ilikabidhi ripoti kwa Rais!

"Mnaleta umbea hapa eti Rais hakujua haya. Rais tulimpa ripoti hii kabla ya kuiwasilisha bungeni!" Alisema Selelii kwa hasira na kwa taratibu mno. Baada ya kumaliza kumuumbua Mahanga Selelii alimgeukia Sophia Simba ambaye alituhumu Kamati teule kuwa ilimuonea Lowasa na kumvua nguo Anne Kilango na mumewe John Malecela! Selelii alisema kuwa yaliyotolewa hayakustahili kutolewa kwenye kikao hicho bali kwenye kitchen party-ni mambo ya mtu binafsi!

"Sophia Simba amesema hapa kuwa Lowasa ni mwanamme namba moja, ni mwanamme wa shoka! Akimaanisha kwamba wanaume wote akiwamo Rais, Waziri Mkuu, Wabunge na madiwani sio kitu. Mimi sikubaliani naye. Labda kama ni mwanamme wa shoka katika masuala mengine." Alisema Selelii kwa kujiamini! SOURCE: MwanaHALISI, tr 11-17/11/2009, uk 2.
 
This is the conflict of the millionaires club...yote majizi tu haya.
 


1. Selelii alisema kuwa yaliyotolewa hayakustahili kutolewa kwenye kikao hicho bali kwenye kitchen party-ni mambo ya mtu binafsi!

2. "Sophia Simba amesema hapa kuwa Lowasa ni mwanamme namba moja, ni mwanamme wa shoka! Akimaanisha kwamba wanaume wote akiwamo Rais, Waziri Mkuu, Wabunge na madiwani sio kitu.

3. Mimi sikubaliani naye. Labda kama ni mwanamme wa shoka katika masuala mengine." Alisema Selelii kwa kujiamini!


SOURCE: MwanaHALISI, tr 11-17/11/2009, uk 2.

- Saafi sana, unajua hata kule US, wale DEA yaani Drugs Enforcement Agents wanapotaka kuwakamata wauza Drugs, huwa na wao huwa wanashuka chini na kujifanya wauza Drugs ndio the only way ya kuwapata hawa criminals in their own game.

- Kumjibu Sophia ni lazima ushuke kwenye level yake, kama Seleli, alivyofanya hapa saafi sana.

Respect.


FMeS!
 
- Saafi sana, unajua hata kule US, wale DEA yaani Drugs Enforcement Agents wanapotaka kuwakamata wauza Drugs, huwa na wao huwa wanashuka chini na kujifanya wauza Drugs ndio the only way ya kuwapata hawa criminals in their own game.

- Kumjibu Sophia ni lazima ushuke kwenye level yake, kama Seleli, alivyofanya hapa saafi sana.

Respect.


FMeS!

Selelii nimemkubali, haumi maneno, anatoa vitu black n white! Kwenye gazeti mojawapo la leo, TZ Daima kama sikosei, JK amesema kuwa kuna baadhi ya mawaziri hatamaliza nao awamu hii ya kwanza, ie kabla ya uchaguzi mkuu ujao! Sijui nani hao ambao wanatishiwa nyau so far!
 
Kwenye listi ya makamanda, Mhe. Seleli ni mmoja wa makamanda wa ukweli ninaowaaminia ambao hawajazungukwa na kiwingu chochote cha uchafu.
 
Hivi jamani Watanzania tuna laana? Huyu Muirani ameshika viongozi wetu wapi jamani? Kwa kweli vitu vinavyotokea Tanzania vinanipa kichefuchefu sana. Ilikuwaje mpaka Rostam akafika katika hiyo status aliyo nayo? Does it mean kwamba nchi ni kama kakampuni kake? Waafrika! Nahisi wajukuu zetu watafukua makaburi yetu waangalie tulikuwa watu wa namna gani.
Naomba kuwakilisha.
 
Kwenye listi ya makamanda, Mhe. Seleli ni mmoja wa makamanda wa ukweli ninaowaaminia ambao hawajazungukwa na kiwingu chochote cha uchafu.

Mafisi-adi wanawazushia kila leo uwongo makamanda wetu! Mimi sioni Lowasa atanyanyukaje kisiasa hata kama akifurukuta vipi? Ndio maana mafisi-adi yanadai eti ripoti kama ingekabidhiwa kwa JK kwanza kabla ya kusomwa bungeni, JK angemwokoa Lowasa! Hizo sio dalili za maji kuzidi unga?
 
tutapiga kelele weeee.na ndio maana mukulu anasema kelele za malngo hazimnyimi usingizi mwenye nyumba...tumeshaongea sana mambo haya na hakuna la maana tunalo achieve mwishowe tunaonekana wendawazimu tu..facts zote ziko wazi ,cha ajabu hata bunge lenyewe linashindwa ku deal na hii issue sembuse sisi..
 
Kubenea kiboko!

Kubenea kiboko kwa lipi..to me he is just mpayukaji tu.toka kaanza kupiga makelele what happened?si alikuwa kibaraka na kumpamba sana kikwete wakati wa uchaguzi huyu au!! ukiboko wake unatoka wapi..njaa tu inamsumbua
 
Back
Top Bottom