Sababu 3 Kuonyesha Kwamba Richmond ni Mali ya Rostam Zatajwa!

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,199
1,969
Katika Gazeti la MwanaHALISI, tr 11-17/11/2009 inasemekana mbunge wa Nzega, mh Lucas Selelii wakati wa Kikao cha CCM Dodoma alieleza sababu tatu (3) zifuatazo kwamba Richmond (Development Company LLC) ni mali ya Rostam Aziz: 1. Alitafuta nyumba kwa ajili ya matumizi ya ofisi ya Richmond (Development Company LLC) na alilipia pango la nyumba hiyo! 2. Jopo la Waandishi wa Habari mashuhuri kwa ajili ya kuisafisha Richmond (Develpment Company LLC) baada ya vyombo vya habari kuanza kueleza utata wa mkataba lilitafutwa na Rostam Aziz ili kupoza makali! "Tumezungumza na waandishi wa habari hawa mmoja baada ya mwingine na wote wametuthibitishia hili," alisema Selelii. Majina ya waandishi hao ni Gideon Shoo, Jimmy Mdoe na Salva Rweyemamu ambaye sasa ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais! 3. Fedha za Dowans (ambayo iliirithi Richmond Develpment Company LLC kwa shinikizo toka Wizara ya Nishati na Madini chini ya Karamagi) zilihamishiwa katika akaunti ya Caspian (ya Rostam Aziz), Rostam Aziz alikuwa akifuatilia mwenyewe fedha hizo hazina! Source: MwanaHALISI, tr 11-17/11/2009, uk. 2.
 
Na yeye ndiye alikuwa akiilipa M.A. Kharafi kazi za ukandarasi na aliwatisha kwamba wao ndio wenye serikali kabla ya Kharafi kutishia kwenda mahakamani ndipo Rostam akaamua kuwalipa fedha alizotaka kuwadhulumu. Lakini akaamua kuwaondoa na kuipa kampuni "yake" ya Caspian kazi badala ya Kharafi. Sehemu kubwa ya makubaliano ya Dowans yalifanywa na Rostam na ndiye aliyemuomba Brig. Suleiman Al Adawi, kuokoa jahazi. Rostam hawezi hata kwa sentimeta moja kuikwepa Richmond. ANAHUSIKA na mengine ni silaha za AKIBA.
 
Watanzani bwana inawachukua miaka mingapi kubaini muiran Rosti tamu ni gaidi wa uchumi wa Tanzania.
 
Watanzani bwana inawachukua miaka mingapi kubaini muiran Rosti tamu ni gaidi wa uchumi wa Tanzania.

Hili gazeti la MwanaHALISI ndio limenifumbua macho leo kuhusu uhusika wa RA na Richmond/Dowans!
 
Buchanan, Nashukuru bora umeileta hiyo, kuna jamaa wako special humu kwa ajili ya Dowans, juzi tulibishana nikawaeleza soma hiyo Mwanahalisi na wenyewe wananikazania nisome Mtanzania. Na sasa hivi watakuja!!
 
Ingewezekana kuazima sheria za China japo kwa mwezi mmojatu, kuna watu nchi hii majina yao yangefutika milele.
 
Huwa najiuliza hili swali , Je Tanzania kuna kiongozi wa kuweza kuwakomboa wana nchi katika maswala haya ya UHUJUMU UCHUMI ?

Rais wetu moja kwa moja tunajua hana uwezo huo..!
 
Katika Gazeti la MwanaHALISI, tr 11-17/11/2009 inasemekana mbunge wa Nzega, mh Lucas Selelii wakati wa Kikao cha CCM Dodoma alieleza sababu tatu (3) zifuatazo kwamba Richmond (Development Company LLC) ni mali ya Rostam Aziz: 1. Alitafuta nyumba kwa ajili ya matumizi ya ofisi ya Richmond (Development Company LLC) na alilipia pango la nyumba hiyo! 2. Jopo la Waandishi wa Habari mashuhuri kwa ajili ya kuisafisha Richmond (Develpment Company LLC) baada ya vyombo vya habari kuanza kueleza utata wa mkataba lilitafutwa na Rostam Aziz ili kupoza makali! "Tumezungumza na waandishi wa habari hawa mmoja baada ya mwingine na wote wametuthibitishia hili," alisema Selelii. Majina ya waandishi hao ni Gideon Shoo, Jimmy Mdoe na Salva Rweyemamu ambaye sasa ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais! 3. Fedha za Dowans (ambayo iliirithi Richmond Develpment Company LLC kwa shinikizo toka Wizara ya Nishati na Madini chini ya Karamagi) zilihamishiwa katika akaunti ya Caspian (ya Rostam Aziz), Rostam Aziz alikuwa akifuatilia mwenyewe fedha hizo hazina! Source: MwanaHALISI, tr 11-17/11/2009, uk. 2.

Si kwamba hakuna ushaidi wa RA kuhusika katika RICHMOND ila ni nani wa kumchukulia hatua? Viongozi wote wa ngazi za juu akianzia na Rais, mawaziri, Mahakama na wanasheria wote wapo mfukoni mwa RA, na kwa sehemu kubwa yeye ndiye aliye waweka kutokana na pesa za ufisadi huo. Yeye ndiye anaye wapangia viongozi waseme ni ndo maana viongozi wameshikwa na kikigumizi katika kuchukulia ahtua na hii ndo inayosababisha makundi ndani ya CCM na serikali yake.
 
Hizi kelele za watanzania kama hawato kuja kuzifanyia kazi zinaweza kuja kuwaletea mashaka makubwa sana mbeleni..!!
 
Kubenea Kiboko

usiku anavuta mshiko kwa Rostam alfajiri anamlipua kwenye gazeti lake

the technique aliyokuwa akimfanyia Lowassa, usiku anavuta akikosa matangazo ya serikali kwenye gazeti wiki nzima ana mli[ua kwenye gazeti

Not bad kwa kijana illiterate from Kirongwe village in Mafia amabaye hajui difference between peace talks na peace process

lakini kwanini tusijikumbushe aliyotuambia mzee Mugongo Mugongo sometimes back hapa JF:

3. Saed Kubenea – Stan Katabalo impostor, only without the education, the sophistication, the principles and steely determination for which Katabalo is remembered for. A little Kingmaker in the making, if only he would be aware that he needs to stop being a pawn in the great political game. He gets direct congratulatory calls from Sumaye, Magufuli, Butiku, Warioba and others whenever his paper comes out. He is welcome at Salim A. Salim house. This is such an awesome achievement for a person who is half-schooled and who has never read any major literary work of non-fiction (and who might not get this joke). That our politicians would embrace Kubenea, who still milks the "acid incident", speaks of the level of their desperation to smear each other (in the name of "saving the country").

haya endeleeni
 
Mkuu huko China si mchezo ukituhumiwa tu kwa ufisadi, mwenye unaisalimisha roho yako kwa muumba
 
Kubenea Kiboko

usiku anavuta mshiko kwa Rostam alfajiri anamlipua kwenye gazeti lake

the technique aliyokuwa akimfanyia Lowassa, usiku anavuta akikosa matangazo ya serikali kwenye gazeti wiki nzima ana mli[ua kwenye gazeti

Not bad kwa kijana illiterate from Kirongwe village in Mafia amabaye hajui difference between peace talks na peace process

lakini kwanini tusijikumbushe aliyotuambia mzee Mugongo Mugongo sometimes back hapa JF:

haya endeleeni
Ok ya Kubenea tumeyasikia...na ya kwako je?
 
lisemalo lipo na kama lipo....yote ya nini?...jamani nchi yetu na viongozi wetu wenyewe....tufanye kama korea au chini kama fisadi adhabu ni kunyongwa mpaka kufa.....watakoma na itakuwa fundisho...wanatusumbua mjina hapa....
 
Mnalia na RA wakati kuna munene yupo nyuma yake mnaogopa kumrushia mawe
 
GT ndo wale wanao mtetea rostam......ndo mnalazimisha watu wasome gazeti la mtanzania?? lol tumekwisha wagundua.
 
Kubenea Kiboko

usiku anavuta mshiko kwa Rostam alfajiri anamlipua kwenye gazeti lake

the technique aliyokuwa akimfanyia Lowassa, usiku anavuta akikosa matangazo ya serikali kwenye gazeti wiki nzima ana mli[ua kwenye gazeti

Not bad kwa kijana illiterate from Kirongwe village in Mafia amabaye hajui difference between peace talks na peace process

lakini kwanini tusijikumbushe aliyotuambia mzee Mugongo Mugongo sometimes back hapa JF:

haya endeleeni

GT Acha wivu wa kuku! Wewe pamoja na elimu yako hata siku moja huwezi bahatika kupeana mikono na watu mashuhuri kama Salim Ahmed! Salim!
 
Huyu Rweyemamu anastahili kuendelea kuwepo Ikulu kweli? Ndio maana kauli zake huwa hazieleweki anapotoa statement mbalimbali za Ikulu, mtawajua kwa matunda (kauli) yao!
 
Back
Top Bottom