Rwanda yaandika barua UN kupinga kupelekwa Jeshi la SADC DRC. Yasema sio jeshi la kulinda amani bali kuivamia Rwanda na kuwafuta Watutsi wa Congo

Serikali ya Rwanda imenyooka sana kuhusu hili suala lakini sijui kwanini watu wanashindwa kuelewa.
20240219_035421.jpg
20240219_035424.jpg
 
Yao wanataka kugawa Kongo.
Ila ulikuwa mpango wa USA miaka ya 90. Na hicho ndicho kisababishi cha Second congo war. Baada ya kabila kugoma makubaliano ya kugawa congo. USA walimsupport Pk na kurudi drc kuanzisha vita ya pili , walikamata congo yote , ponea ya wacongo ilikuwa ni Angola chini ya general Joao de Matos.
Walikufa watu zaidi ya 5 million kule.
Tafuta "UN mapping report" ya congo utaona.
Berlin conference in modernity.
 
Kwanini waasi wa FLDR wasikae mezani na Kagame, ili waingizwe ndani ya Jeshi la Rwanda?. Halafu Tishekedi akaendelea kuwasafisha M23?, Kwa kupata msaada kutoka Tz?.
Kuna kipindi wakati Kikwete alipokuwa rais alitoa hili wazo. Kagame alimcharukia kidogo aanzishe vita na Tanzania.
 
Kumbuka Mtutsi yeyote akiwa DRC anaitwa Mnyarwanda na hilo nimelishuhudia Lumumbashi.

Rwanda wasikubali kuona tena Mauaji ya Kimbari dhidi ya Watutsi yatokee tena na sijui hizi chuki dhidi ya Watutsi sijui ni nani anayezisambaza.

Look ni kama Massai tukianza kuwaua Massai wa Tanzania unafikiri Massai wa Kenya watakaa watuangalie? Never!

Mimi nawasapoti sana Watutsi waliidhibiti GENOCIDE wakaijenga Nchi ya Rwanda na sasa hata Mgao wa Umeme hawana.
Mambo ya ndani ya Congo Rwanda inamhusu nini wewe libavicha?
 
FLDR wanafalsafa moja tu ambayo ni kuwamaliza Watutsi Rwanda rejea 1994 wanataka KUMALIZA KAZI waliyoianza mwaka 1994 na bado wanatembea na vile vitabu vya HUTU COMMANDMENTS.

Kwa upande mwingine M23 wanataka Serikali ya DRC irudi kwenye Meza ya mazungumzo kuliko kukodi Majeshi na kulalamika na kulalamika tena na tena na kuendelea kulalamika.
Sasa kwanini unataka waasi wa m23 waingizwe jeshi la congo kwanini kagame asiwachukue awaingize kwenye jeshi lake?
 
Ikiwa Congo Dr itamegwa na Kivu ikajitenga basi ushawishi kijeshi na kiuchumi wa Tanzania hapa East Africa utapungua kama sio kuisha kabisa. Natamani kumwona Samia ana declare FULL SCALE war na mamluki wa RDF waliopo Congo DR.
 
Rwanda imeandika Barua kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ikipinga upelekwaji wa Jeshi la SADC la kulinda amani kutoka Nchi za Afrika Kusini,Tanzania na Malawi kuwafurusha M23.

Kwenye Barua yake Rwanda inasema Jeshi Hilo sio neutral Bali ni Vikosi vya kwenda akusaidoa DRC na Burundi kufanikisha malengo Yao ya Kuivamia Rwanda na pia Kuwafuta Wakonhomani wenye Asili ya Kituwi.
View attachment 2906485

Ikumbukwe wiki za karibuni M23 imeongeza harakati zake za Vita Kwa kutumia silaha Kali.
View attachment 2906496View attachment 2906497

Swali
Nani alimpa Kagame kazi ya kuwalinda Watutsi wa DRC? Je hao ni Raia wa Rwanda au wa DRC?

Pili nini Lengo la Kagame kuwasaidia Watutsi wa DRC?

My Take
Bila kubadili Utawala pale Kigali hakuna amani itapatika huko Eastern DRC.👇👇

View: https://twitter.com/NewTimesRwanda/status/1758477584118026499?t=IXDjigoBEs8ynkhK3utFIw&s=19

Swala kwamba kuna wa Congo wenye asili ya kitusi sio hoja,zamani walikuwa wanaitwa wanyamurenge, DRC haiwatambui kama ni raia, sasa DRC inataka iwafukuze waende Rwanda, lakini ardhi Yao ibaki kuwa ya Congo! Fikiria useme wamasai wote warudi Kenya, uende Arusha, uwafukuze wote waende Kenya, Ila ardhi Yao ibaki TZ! Kama, huwataki,Rudisha Arusha kwa, Kenya ikiwa, na wamasai wake.
Rwanda inawatumia kuiba madini, na kuna wadau wakubwa, Makampuni makubwa ya madini, yanayopeleka siraha ili hii Vita isiishe. Kila simu na computer inayotengenezwa duniani, madini yantoka Congo,
Dawa hapa, ni kukata mirija inayowapa siraha M23, winda na ua wafadhili wao, kimya kimya,
 
Tishekedi aruhusu Jeshi la Rwanda limsaidie kuwasafisha Waasi wa FLDR halafu akae mezani na M23 ili waingizwe kwenye Jeshi la DRC lakini kukimbilia kuomba Msaada wa SADC bila ku deal na MZIZI WA FITINA ni kupoteza muda tu.
Yaani fisi unampa nafasi ya kulinda butcher?
Eti Kagame apewe jukumu la kuwaondoa M23, how?
Hivi wewe hujui M23 ni jeshi la Rwanda?
 
M23 wamekaa hotelini Kinshasa miezi minne kuitikia with wa serikali ya Congo kufanya majadiliano hakuna kiongozi aliyefika hata kuwasalimia ikabidi wajiondokee na madeni ya hotelini wakalipa wenyewe.
Hii ilikuwa ni baada ya mivutano ya muda mrefu huki wakigoma kulegeza masharti yasiyotekelezeka.
 
Hii Propaganda imechokwa. Fdlr waliopigana 1994 na kuishi maporini miaka na miaka ni wazee hawana nguvu za kupigana tena.Hao Fdlr wa sasa ni wahutu vijana waliozaliwa Congo,hawahusiki na yaliyotokea 1994 na ni haki yao kurudi Rwanda.Safari hii watarudi kwa mtutu kwa msaada wa ndugu zetu waha.
Nakushauri fanya utafiti wa kina kuhusu FDLR wanaopigana huko Eastern DRC ujiridhishe wanapigania nini.
 
Back
Top Bottom