Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,989
Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma limetoa ufafanuzi kuhusu Mtumishi wa Mungu Erick Manyanya (33) Mwinjilisti wa Kanisa la Country Living aliyeshikiliwa kwa tuhuma za kuwashawishi Wazazi kutowapeleka Watoto shule kwa kile alichodai Yesu anakaribia kurudi.
Wiki moja iliyopita, Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Ngollo Malenya aliagiza Muinjilisti huyo kutoka Kijiji cha Chengena ambaye pia alikuwa Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa ajili ya mahojiano zaidi.
Kipitia JamiiFoorums.com, Mdau aliyejitambulisha ni ndugu wa mtuhumiwa huyo amedai ndugu yao amepigwa na Askari Polisi na afya yake si nzuri pia amekwama kupata dhamana hadi watakapotoa Tsh. 200,000.
Malalamiko hayo soma hapa - Ndugu yetu aliyekamatwa kwa kuzuia Watoto kwenda shule mbona hapewi dhamana na Polisi?
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, ACP Marco Chilya amesema mtuhumiwa bado yupo chini ya Jeshi hilo na kufafanua zaidi.
“Upelelezi bado unaendelea, kuhusu kumpiga Askari ampige kwa interest gani? Kwanza kesi kama hizo zinashughulikiwa na Dawati la Jinsia ambao wapo friendly na wanajichanganya na jamii.
“Hakuna Askari ambaye anataka mtuhumiwa afie mahabusu, kama ni mgonjwa atapelekwa hospitali chini ya ulinzi, atatibiwa atarejeshwa kuendelea na mchakato wake wa kisheria.
“Hivyo, hakuna kitu kama hicho, ingekuwa labda ni jambazi amepora au ameiba na kuna kitu tunataka inawezekana nguvu ya ziada ingetumika lakini siyo huyo, labda kama alipigwa na ndugu zake kabla hajakamatwa."
Madai ya kukwama kwa dhamana
Kamanda anasema “Hakuna dhamana inayotolewa kwa laki mbili wala haitolewi kwa hela, kama ndugu wana changamoto waende kwa OCD, inawezekana kuna watu ambao si Askari wanataka kutumia nafasi hiyo kufanya yao kwa mgongo wa Polisi."
Pia soma = Namtumbo: Wazazi waacha kupeleka Watoto Shuleni wakiaminishwa Yesu Kristo anakaribia kurudi