Ruto: Tutatoa bajeti kubwa kwa Mahakama ili isimamie Demokrasia, Uhuru na Haki

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Kutoka uwanja wa Kasarani
Septemba 13, 2022



Rigathi Gachagula - Naibu Rais
Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagula amesema kuwa nchi hiyo haitaingilia uhuru wa watu katika kuwasiliana.

Amewataka wakenya kuzungumza kwa uwazi pasipo kuogopa kuwa Serikali itaingilia mawasilano yao. Aidha, amewaondoa wasiwasi wakosoaji wa Serikali hiyo kuwa watakuwa salama kwani huo ni uhuru wao wa msingi.

Maskini hawataburuzwa na maafisa wa Serikali kwa namna yoyote ile.

William Samoei Ruto - Rais
Kusimama hapa mbele yenu ni uthibitisho kuwa Mungu yupo. Nimesimama mbele yenu kama kijana maskini wa kijijini aliyebahatika kuwa Rais.

Mahakama na vyombo vyetu vya dola vimetushangaza sana. Vilipitia kipindi kigumu kisicho zungumzika, lakini walivuka salama. Jambo hili linapaswa kupongezwa.

Washindi wa uchaguzi huu ni wananchi wote wa Kenya. Tumetoka mbali kwenye safari ya uhuru wetu kama taifa, kwa sasa tunaweza kusema kuwa tumekaribia kufika nyumbani.

Nitafanya kazi na wakenya wote pasipo kujali walimpigia nani kura. Kwa vijana wadogo waliojaribu kushindana lakini hawajapata nafasi ya kushinda nawatia moyo, mwaka 1992 nilianza safari yangu ya siasa nikiwa kama ninyi. Msikate tamaa.

Mimi ni mfano wa vijana wapambanaji. Kumtumikia Mungu, kufanya kazi pasipo kuchoka pamoja na kuziamini ndoto zako ndiyo njia pekee ya kukufanya ufanikiwe.

Serikali yangu itaheshimu maamuzi ya mahakama. Tutatoa bajeti kubwa kwa mahakama ili iendeshe demokrasia na haki kwenye nchi hii. Leo hii nitateua Majaji 6 wa mahakama ya juu ili kuonesha dhamira yangu njema, na kesho nitawaapisha.

Bajeti ya Jeshi la polisi inapaswa kuondolewa kwenye ofisi yangu. Sheria ya kubadilisha jambo hili niikute leo ofisini kwangu nisaini ili mkuu wa polisi apewe mamlaka kamili ya kusimamia fedha zao. Hapa tunataka kuongeza uhuru wa jeshi letu, wafanye kazi pasipo kuingiliwa na Serikali.

Bei ya mbolea tunakwenda kuipunguza, kuanzia wiki ijayo watu waende kununua kwa nusu bei. Tunataka ipatikane kwa urahisi kwa wakulima wetu.

Tunataka kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira, pia tutajenga mifumo rafiki kwa watu kujiajiri na kufanya biashara.

Deni la taifa lazima tuanze kulipunguza, wiki chache zijazo tutakaa tuone tunaanzaje kulipa madeni haya. Hata hivyo, tunapaswa pia kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kuinua uchumi wetu. Naomba tulipe kodi.

Mfuko wa bima ya afya tunaenda kuuangalia upya, pia mfumo wa elimu yetu tutauangalia upya. Nitaunda timu ya kukusanya maoni juu ya namna ya kutengeneza mtaala mpya wa elimu yetu.

Serikali yangu itapambana na mabadiliko ya hali ya hewa. Tunataka kuhakikisha kuwa afya zetu pamoja na mazingira kwa pamoja vinabaki salama.

Tupo tayari kushirikiana na taasisi zote za kimataifa kwenye kupambana na majanga ya kidunia. Nawakaribia waje tufanye kazi pamoja.

Naahidi kumfanya kila mkenya ajisikie fahari. Nitafanya kazi kwa bidii, kwa wakenya wote bila kujali wanatoka wapi au walimchagua nani. Tujenge nchi moja, tukumbatie vipaji na karama za watu wetu.

Kwa jiani zetu msiwe na wasiwasi, jioneni kuwa bado mnaye rafiki wa kweli. Karibuni Kenya.
 
Nasikia jamaa anataka kuongoza ki-ccm... Mama atakuwa amempa ABCDE..
20220913_114248.jpg
 
Haya mengine ni mapicha picha Nasubiria mwelekeo wa hotuba yake ya kwanza sijuini lini.
 
Ngoja mahakama ianze kutoa maagizo yanayopinga maamuzi ya serekali yake alafu tuone atafanyaje.

Naona Rais ameamuru bajeti ya polisi iwache kusimamiwa na Ofisi ya Rais na iende kwa usimamizi wa inspekta generali wa Polisi.

Tayari hapa naona kakosea, jambo kama hili ni lazima bunge ligeuze sheria, mtu akienda mahakama na kupinga uamuzi huu, mahakama itakua haina budi ila kupinga uamuzi wa Rais hapo ndo ataanza kuona labda nisiwaongezee bajeti hawa watu ambao wanapinga maamuzi ya serekali yangu
 
Ngoja mahakama ianze kutoa maagizo yanayopinga maamuzi ya serekali yake alafu tuone atafanyaje.

Naona Rais ameamuru bajeti ya polisi iwache kusimamiwa na Ofisi ya Rais na iende kwa usimamizi wa inspekta generali wa Polisi.

Tayari hapa naona kakosea, jambo kama hili ni lazima bunge ligeuze sheria, mtu akienda mahakama na kupinga uamuzi huu, mahakama itakua haina budi ila kupinga uamuzi wa Rais hapo ndo ataanza kuona labda nisiwaongezee bajeti hawa watu ambao wanapinga maamuzi ya serekali yangu

Kuna vitu vingine vinafanywa na executive orders na si lazima tena urudi bungeni.
 
Back
Top Bottom