Kenya: Jaji Mkuu awataka Watumishi wa Mahakama kuendelea kutekeleza majukumu yao Kikatiba bila kuogopa wala kuzingatia yaliyosemwa na Rais Ruto

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Viongozi wa Kisiasa Kenya akiwemo Katibu Mkuu wa Jubilee, Jeremiah Ngayu Kioni awanadai Rais William Ruto ana njama ya kupunguza ukali wa kitengo cha Mahakama ili apitishe Sheria zinazokiuka Katiba bila pingamizi

Jeremiah anadai kuwa Rais Ruto ana njama iliyojificha inayohisisha kuongeza kwa Muhula wa Urais bila Pingamizi kutoka kwa Mahakama.

Katika barua ya Ndani iliyoandikwa na Jaji Mkuu, Martha Koome kwenda kwa Watumishi wa Mahakama amewataka Watumishi hao kuendelea kutekeleza majukumu yao Kikatiba bila kuogopa wala kuzingatia yaliyosemwa na Rais Ruto

Koome amesema “Ofisi yangu na Tume ya Utumishi wa Mahakama zimeweka wazi kwa vyombo vingine vya dola na kwa umma kwa ujumla kwamba njia sahihi ya kupinga uamuzi wa mahakama ikiwa mtu hajaridhika ni kukata rufaa au kuomba mapitio katika mahakama ya juu zaidi. Kuwashambulia majaji na Afisa wa Mahakama waliofanya uamuzi hadharani kunadhoofisha maadili yote ya utaratibu wetu wa Kikatiba,”

"Mashambulizi au maoni kama hayo yanapotolewa kuhusu masuala ambayo yanasubiri korti yoyote pia yanakiuka sharti la mahakama ndogo ambalo ni derivative ya kanuni ya sheria na kwa hivyo ni msingi wa msingi wa kitaifa na kanuni ya taifa letu, kama ilivyoelezwa katika Ibara ya 10 ya Katiba."

Vilevile Rais wa Chama cha Wanasheria nchini humo, Eric Theuri ametoa wito kwa Wanasheria nchini humo kujitokeza na kuandamana ili kupinga matamshi yake Rais William Ruto kuwa hatazingatia maamuzi ya Mahakama

Rais William Ruto alidai kuwa utendaji kazi wa Mahakama umeingiliwa na Mafisadi wanaopania kukwamisha kutekelezaji wa Sera za Serikali ya Sera Kwanza, hivyo ataanza kupuuza maamuzi ya Mahakama yanayoenda kinyume naye. Aliongeza kuwa kuna Mawakili na Majaji ambao wanashirikiana na Mafisadi nchini ili kukwamisha mipango ya Serikali ikiwemo Mpango wa Nyumba za Bei nafuu na ule wa Bima ya Afya

Chama cha Wanansheria kinaandaa maandamano ya amani kuanzia wiki ijayo ili kulinda Uhuru wa Mahakama. Rais wa Chama hicho amesema katika maandamano hayo watasoma na kuonesha Kiapo ambacho kila Wakili wa Mahakama Kuu ya Kenya amekula Kulinda Utawa wa Sheria, Uhuru wa Mahakama na Katiba ya Nchi

Wanasheria sasa Wanamtaka Rais Ruto kutumia njia muafaka kuwasilisha Ushahidi Mahakamani

IMG_8815.jpeg
 
Hiyo ndiyo Kenya, Kiranja wa Demokrasia Afrika Mashariki!

Hata Rais anakaripiwa😃
 
Back
Top Bottom