Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,483
- 40,010
Habari toka kwa ka'nzi' ni kuwa mshiko wa nguvu umekuwa ukitembezwa kwa muda sasa kuwalainisha watendaji mbalimbali serikali na Bungeni ili kuhakikisha kuwa mabadiliko ya haraka hayatokei Tanroads. Kama wachunguzi wetu walivyoliibua suala la ATCL ambalo nalo hadi leo bado linabebwa, Tanroads vile vile hakutafanyika mabadiliko wakati wowote karibuni. Sababu kubwa ambayo imehakikishiwa ni mlolongo wa zawadi na vituliza midomo (kama vuvuzela) ambavyo baadhi ya wanasiawa wamepatiwa au kujipatia.
Hivi sasa inaonekana mlolongo huu umefika hadi Majumba yote mawili makuu! Watu wamekatiwa fedha taslimu na wengine vitu mbalimbali huku wengine wakiahidiwa zaidi huko mbele ya safari.
Ka nzi kanadokeza kuwa katika hili msaidizi mmoja wa Rais yuko karibu kwa namna ya kutisha na mambo yanayoendelea aidha kwa baraka za huyo Rais au akimwacha gizani lakini akilitumia jina lake (Rais). Hadi hivi sasa kwa uhakika ni kuwa licha ya kelele nyingi kwenye magazeti kuhusu Tanroads na ushahidi wote wa kubebwa na kukiukwa kwa taratibu mbalimbali Bw. Mrema hang'oki na watu wajifunze kuishi hivyo hivyo naye. Kama ilivyokuwa vigumu kumng'oa Mataka pale ATCL ni vigumu kumng'oa Mrema Tanroads bila ya kumtafutia mahali pengine pa "kuchumia" taifa. Ni ugumu ule ule ulioko Bandari kama ulivyokuwepo TAnesco.
habari kwa ufupi ndiyo hiyo, mkitaka kwa urefu.. subirini turudi mitamboni siku chache zijazo.