Rushwa Bungeni.. it has come to my attention...

Haya Vuvuzela linalia..... magoli ni bila bila hadi sasa, wananchi wamejaa ktk ma bar wakitazama luninga pasipo matumaini...Muda unayoyoma..
 
Solution ni kuukubali mfumo wa rushwa na kuuhalalisha. Watanzania wote tukiwa walarushwa basi rushwa itakosa mvuto na kufa kifo cha mende. Uadilifu sasa utachukua nafasi yake.

Hebu fikiria tu scenario ambapo kila mtanzania ni mlarushwa. Fikiria nchi ambamo wanunuzi wote wanatembea na pesa feki na wauzaji wote wanauza bidhaa feki. Patakuaje hapo?

Du ! naona U Mobutu, U Marcos(wa Phillipines) na hata Unyan'gau wa jirani zetu unatunyemelea, lakini ndo ukweli wenyewe.
 
Hii mijamaa ijifanye viziwi tu,ila wanatengeneza moto.Ukishawaka,hao watoto na wajukuu zao utawafikia tu hata kama watatudanganya kwamba wamefia huko Ulaya na Marekani.

Mimi siamini hata kidogo kwamba hili vuguvugu la hapa JF eti litaishia hivihivi,kuna siku kila mtu ataamua kuchukua maamuzi yake binafsi.Hii dhulma na malalamiko ya wananchi yote yanafika kwa Muumba,itafikia hali ya kuchoka na Mungu atupe Fursa,patakuwa hapatoshi.

Inakoelekea ni kule ambako kila mmoja atakata tamaa ya kuishi kutokana na umaskini wa kutupwa,then itakuwa mtu haoni hasara kutangulia kwa sababu hata kama akiendelea kuishi..muda si mrefu njaa,pressure,mtingo wa mawazo etc vitamuondoa tu hapa kwa dunia

Ila kwa kweli kuna watu wana roho mbaya katika ile nchi...they dont even rethink their decisions......,how can one be happy kwa dhulumu maisha ya watu namna hii.

Poa,tutafika tu.Kadri wanavyodhulumu ndivyo akili mpya zatujia vichwani mwetu.
 
Hii nchi ni yetu soote, lakini wenzetu wameamua kiula wao tuuu na watoto wao na jamaa zao......inauma sana jinsi Mwalimu alivyo hangaika kuijenga Tz leo hawa majambazi wanaibomoa kifisadi hivi?!
Sijui nani ataikomboa nchi yetu tena........au tu .................msituni?
 
Inavyoonekana watu wana machungu, itafikia mtu haoni haja ya kisahani chao cha kura atasema liwalo na liwe ila tuombe tusifike huko.
 
Squad la nzi.. linaandaa orodha kamili ya wale wote waliojiunga katika kupeana mapenzi na ufisadi! counting.... tik tak tik tak!
 
Squad la nzi.. linaandaa orodha kamili ya wale wote waliojiunga katika kupeana mapenzi na ufisadi! counting.... tik tak tik tak!

Afadhali Mzee, maana nilianza kuhangaika na kupenda kutoamini mada yako; kama rushwa iko bungeni sasa ni wapi hakuna? Majemadari wetu hawajashtukia hiyo rushwa hadi sasa, au ndio wamepoozwa....najua kitu kimoja kwa wanasiasa - UONGO na kuusifia UONGO! Na kina Mrema watakushikilia documentary materials za ofisini labda ni the so-called standing orders kujitetea kuwa waliokuwa wanafanya ni safi tupu,.. shida kwelikweli.
 
ukitaka kula vizuri shurti ule na wenzako

kuweka lami TZ ni mara mbili ya kenya, je hizi hela zote zinaenda wapi????
 
Rushwa iliyotembea na wale ambao tukiwaandika kuwa ndio wamepokea, wengine majina yao yatawaliza watu au kuwafanya wasikitike. Huu mfumo wa utawala wa kifisadi hauwezi kuondolewa kwa makubaliano mezani. Ni wakubomolewa tu.

Huyu Mrema lazima alindwe kwani asipolindwa anaweza kumwaga ugali na mboga juu ya kashfa ya barabara ya Bagamoyo mpaka Msata ambapo kuna ufisadi wa hali ya juu umetendeka!!
 
Squad la nzi.. linaandaa orodha kamili ya wale wote waliojiunga katika kupeana mapenzi na ufisadi! counting.... tik tak tik tak!

Nitashangaa kama wabunge 15 tu katika bunge zima kama wakiwemo kwenye hiyo orodha, 11 wa Chadema (nitahudhunika sana) na wengine kama wanne hivi wa CUF akiwemo Hamed rashid. Kwa kweli wengine hamna cha kushangaa kama walipewa za EPA hizi ni mtoto kabisa?

Machale yananicheza kuwa 11 imeingiliwa!
 
Kwani huyu Mrema kafanya nini haswa? mbona watu mnalaumu bila kuzungumza makosa yake. Kwa habari nilizozipata watuwengi hapo TANROADS hawampendi kwani amekuwa ni mtu anayesimamia haki .
 
Hayo magazeti yanayo andika juu ya huyu Mrema - This Day etc sii yenyewe ni ya hao mafisadi? Hapa tunaongelea sector yenye fedha nyingi sana - zaidi ya shs. trillioni moja kwa mwaka na nyingi ya hizo zinatoka moja kwa moja toka kwa wafadhili wa nje - mbona hatuwasikii hao wafadhili wakilalamika au kusimamisha/kupunguza misaada yao kama ufisadi ni kiasi wanavyoandika haya magazeti. Kila kukicha mikataba ya miradi mipya inatiwa saini kati ya Tanzania na benki ya dunia; ADB etc kujenga barabara mpya. Yote hii inasimamiwa na hao TANROADS! Kamati ya Miundo Mbinu ya Bunge inamsifiwa huyu Mrema katika ripoti yake. Haya Magazeti tunasikia mengine hayaja walipa wafanyakazi wake mishahara kwa miezi kadhaa! Inaweza kuwa issue hapa ni njaa katika waandishi wa habari ambao sasa wanalipwa na wakandarasi walionyimwa tenda na TANROADS. Tuwe more objective kwenye hili swala.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom