Rukwa wapongeza ziara za Rais Majuu!

Unayaongelea Rukwa Angalia Jiji la Dar wewe unafikiri linajijenga wenywe ?ni mafanikio ya safari za Jk mambo bado ndio kwanza kipindi cha kwanza sasa tusubiri kipindi chapili Nchi ataifanya kuwa new york ya Afrika utajaza mwenywe.

Mkuu, unapewa nini kwa kulamba viatu vya JK vizuri namna hii?
 
jamani vasco da gama USA kaenda mara ngapi na Ulaya Asia kaenda mara ngapi?

ziara ya kwenda studio inatufaisha nini watanzania? hii inaoenakana hakuwa na ratiba maalum....eti Obama aje bongo akatembelee Bongo records kwa P funky!!!

Yo YO mkuu ni kweli hakuwa na ratiba maalum na ndio maana ilibidi acancel kwenda Seattle ambako pia alikuwa anakwenda kuhutubia NGO moja!!
Hawa watu wa Rukwa msiwalaumu yote hiyo ni ignorance waliyonayo kwani hawajui kuwa hiyo barabara inajengwa kwa fedha za Millennium Challenge Account fedha ambazo upatikanaji wake ni nchi husika kukidhi masharti yaliyowekwa na serikali ya marekani na si Rais wa nchi kwenda kuomba msaada! Hence, u Vasco Dagama wa Jakaya haukuwaletea hawa wafipa barabara!!
 
Mkuu, unapewa nini kwa kulamba viatu vya JK vizuri namna hii?
Hawa ndio wapambe nuksi, eti anasema kipindi cha pili ataifanya Dar kuwa New York!! Kipindi cha pili kama Mwenyezi atampendelea atakuwa anatuibia tu hata fanya lolote yeye na wapambe wake na ndio maana watu wanamuomba Mwenyezi atuondoshee balaa la huyu bwana kupata kipindi cha pili!
 
Akhsante YoYo kwa kutuletea lihabari. Lakini ujue wazi kabisa kuwa limenitibua sana... Tunasafari ndefu sana katika nchi yetu kuyafikia maendeleo tunayo yatamani na kuyafikiria. Mods bora wabadilishe tu hiyo heading ku-reflect baadhi ya wana CCM wa Rukwa. Na aliyeandika na kuipa kichwa cha habari kana kwamba ni wananchi wote wa Rukwa anastahili kusurubishwa kinamna yake.
 
Hawa ndio wapambe nuksi, eti anasema kipindi cha pili ataifanya Dar kuwa New York!! Kipindi cha pili kama Mwenyezi atampendelea atakuwa anatuibia tu hata fanya lolote yeye na wapambe wake na ndio maana watu wanamuomba Mwenyezi atuondoshee balaa la huyu bwana kupata kipindi cha pili!

JK ni chaguo la Mungu nahakuna wa kubisha hilo, kwani hata katika uchaguzi wake umesibitisha hivyo wananchi walimpa kura zao kwa wingi kuliko uchaguzi wa rais yoyote yule katika historia ya TANZANIA .
 
Taarifa imesomwa na Mykt wa CCM Rukwa, hivyo kichwa cha habari kingefaa kuwa "Wana CCM Rukwa wawajia juu wanaobeza safari za Rais Kikwete nje" .

Hawa ndiyo viongozi wanaotegemewa!! Anafikiri Tanzania ni Rukwa tu. Hivi Rukwa hawawezi kupata kiongozi anayeweza ku analyze anagalau one step ahead ya huyu?
 
JK Atulie kwanza aache munkari wa kutembea anajidhalilisha mwenzie Mkapa alitengeneza pesa za kuchimbia bomba la kutoka victoria kwenda kahama na barabara ya kwenda mwanza kutokea dodoma na ya mtwara kutokea ikwiriri kulikuwa na pesa nying yeye,akadhibiti mfumuko wa bei tulinunua mkate shilingi mia tatu tangu mwanzo wa utawala wake mpaka mwisho,JK anazurura tuu weee kila mahala yupo,atulie bwana aendeshe nchi anaglia Dar haina hata eneo la bustani ,chafu kuliko kawaida,hakuna utawala wa sheria kabisa kila mtu anafanya anavyotaka, amezidi bwana apunguze aibu
 
Duu,

Wafipa wametuonea wivu sisi Wanyamwezi kwa kujipendekeza kwa Rostam Ngosha Aziz. Wakasema kama Igunga wametoa kali ya kumsifia RA, sisi ngoja twende mbali zaidi na tumsifie Kikwete. Ila lazima tulaani mashambulizi kwake. Wakachambua na kupata humuhumu ndani ya JF kama sikosei, wakaamua kuchukua BOENG 747 na kulijaza mafuta na kwenda nalo......... Yes, "MLAANIWE JF KWA KULAUMU SAFARI ZAKE MUUNGWANA...."
Lidumu Bakuri la Matonya.......
Adumu Rostam Aziz.....
Udumu Ufisadi......
Wadumu Wahindi.............
Wadumu vibaka wa madini .........
Idumu CCM............
Idumu tabia ya KUJIKOMBA!!!!!.......
Lidumu giza nene linalotukumba WADANGANYIKA......
 
Tunaitaji watumishi kama hawa ;hata kama wanahisiwa kutumia vibaya fedha bado wanawakumbuka watu wa chini;wa madhabahuni ale madhabahuni
 
Attachments

  • Rukwa.jpg
    Rukwa.jpg
    14.8 KB · Views: 38
tehe tehe raisi anakwenda nchi za watu kuhutubia NGO....aibu hizi......jaamni hivi hizi safari ni yeye vasco da gama anazipanga au ni watu wake? alafu yeye safari zake ni marekani tu....
 
Ukitaka kumfahamu fika Mwingira angalia channel yake ya Trenet hauhitaji masimulizi. Jamaa ni player kweli na anazidi kupata wafuasi wanaopenda mahubiri ya mipasho
 
Taarifa imesomwa na Mykt wa CCM Rukwa, hivyo kichwa cha habari kingefaa kuwa "Wana CCM Rukwa wawajia juu wanaobeza safari za Rais Kikwete nje" .

Kwame Nkrumah... asante sana... lakini mimi naenda mbali zaidi... kichwa cha habari kingefaa kuwa "Mwenyekiti wa CCM Rukwa awajia juu wanaobeza safari za Rais Kikwete nje"
 
Ukitaka kumfahamu fika Mwingira angalia channel yake ya Trenet hauhitaji masimulizi. Jamaa ni player kweli na anazidi kupata wafuasi wanaopenda mahubiri ya mipasho

Hizo pesa amezitoa wapi, katika mfuko wa sadaka ya waumini wake? Nao wamemruhusu agawe pesa hivyo?
Je, amezilipia kodi ya serikali?
Au ni mchezo uleule wa 'uponyaji recycling' unaingia kenye money recycling?
Yetu macho; tusubiri historia itasema.
 
Mimi siwaelewi kabisa, huyu jamaa katoa milioni 10 thats it!

Chenge ameziweka wapi zake??
 
kuna watu wa kuwaonea huruma jamani! Rukwa, si Tanzania hii ni TANGANYIKA
 
Kwame Nkrumah... asante sana... lakini mimi naenda mbali zaidi... kichwa cha habari kingefaa kuwa "Mwenyekiti wa CCM Rukwa awajia juu wanaobeza safari za Rais Kikwete nje"
Hata waliochangia hapa kuwaponda wana-Rukwa bila kuisoma habari vizuri nao wameingia kwenye kundi la ignorants !! Taarifa inasomwa na maybe iliandaliwa na Mwenyekiti wa CCM Rukwa, nyie mnawaponda wana Rukwa wote, hamuoni kwamba ninyi ni sawa na huyo mwenyekiti?
 
hii imetungwa tu na Salva, thats what they do to create a perception kwamba ana support kubwa ya wananchi...wanatumia uchafu uchafu tu kama huu na redet...mtasikia kesho mkoa mwingine wazee wanamuunga mkono kwa kitu kingina...etc etc..
 
Hata waliochangia hapa kuwaponda wana-Rukwa bila kuisoma habari vizuri nao wameingia kwenye kundi la ignorants !! Taarifa inasomwa na maybe iliandaliwa na Mwenyekiti wa CCM Rukwa, nyie mnawaponda wana Rukwa wote, hamuoni kwamba ninyi ni sawa na huyo mwenyekiti?
hii habari nimeitoa kwenye blogu ya ikulu....kwa maana inatoa taarifa za uhakika za ikulu...imeandikwa kama ilivyo......soma hata gazeti la mtanzania la leo...
 
Back
Top Bottom