Rukwa wapongeza ziara za Rais Majuu!

Yo Yo

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,217
1,706
Naiweka ki BAK style yaani copy bin paste....

Wana-Rukwa: Wanaodai Rais Kikwete
anasafiri sana wameishiwa hoja
. Mkoa huo wasema kuwa hao ni watu wa kupuuzwa tu
. Wasema kuwa safari za Rais zimeuwezesha mkoa kupata barabara ya kwanza kubwa ya lami

Na Mwandishi Maalum
MKOA wa Rukwa umewalaani watu wanaosambaza madai kuwa safari za Rais Jakaya Kikwete nje ya nchi hazina faida na kuwa amekuwa anatumia muda wake mwingi nje ya nchi badala ya kushughulikia matatizo ya ndani.


“Tunawalaani kabisa wanaosema kuwa ukienda nje unapoteza wakati,” imesema sehemu ya taarifa ya Mkoa wa Rukwa iliyotolewa na wana-Rukwa usiku wa jana, Jumatano, Mei 27, 2009, kwenye Hoteli ya Kilimanjaro-Kempiski mjini Dar Es Salaam.


Wana-Rukwa walieleza msimamo wao huo katika hotuba ya shukurani iliyosomwa na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo, Hypolite Matete katika hafla kubwa ya uchangiaji elimu katika mkoa huo.


Kiasi kikubwa cha jumla ya sh bilioni 1.9 zilichangwa ama kuahidiwa katika hafla hiyo ambako Rais Kikwete alikuwa mgeni rasmi na alisaidia katika kunadi baadhi ya vitu, ili kutunisha mfuko huo wa elimu wa mkoa huo, unaojulikana kama Mfuko wa Elimu wa Mwalimu Nyerere.


Akiwashukuru waliochangia harambee hiyo, Mwenyekiti Matete alimwambia Rais Kikwete kuwa mkoa wa Rukwa unawaalani wote wanaodai kuwa safari zake za nje hazijailetea Tanzania manufaa.


Matete alisema kuwa bila safari za namna hiyo na uhusiano wa karibu wa Rais Kikwete na aliyekuwa kiongozi wa Marekani, Rais George W Bush wala Tanzania isingepata fedha za ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 230 kwa kiwango cha lami kutoka Tunduma hadi Sumbawanga chini ya msaada wa Serikali ya Marekani kupitia shirika lake la MCC.


“Tunakushukuru Mheshimiwa Rais kwa kuuwezesha Mkoa wa Rukwa kuunganishwa kwa barabara ya kwanza muhimu ya lami na mkoa mwingine. Tunakushukuru kwa kuendeleza kilimo na kuinua kipato cha wakulima katika Mkoa wa Rukwa,” alisema Matete na kuongeza:


“Kwa sababu ya upatikanaji wa mbolea, mbegu bora kwa wakati, na mpango wa Stakabadhi Ghalani kipato cha wakulima wetu kimeongezeka. Ni kilimo tu kinachoweza kubadilisha maisha ya watu wetu kwa sababu asilimia 80 ya Watanzania wanaishi kwa kutegemea kilimo. Sasa tunaamini fika kuwa dhamira ya Serikali yako ya maisha bora kwa kila Mtanzania itatekelezwa.”


Mwenyekiti huyo alisema: “Watu wanaosema kuwa unazurura kwa kutafuta wawekezaji wa kuja kuinua uchumi wa Tanzania ni watu wameishiwa hoja. Tusisumbuke nao. Endelea kuhangaika kwa sababu maendeleo hayana mwisho.”
Mwenyekiti huyo alikuwa anatoa shukurani kufuatia hotuba ya Rais Kikwete ambaye mbali na kuelezea maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Tunduma hadi Sumbawanga, pia alielezea jitihada za Serikali yake katika ujenzi wa barabara nyingine za mkoa wa Rukwa.


Alisema Rais Kikwete katika hotuba yake: “Nafurahi kusema kwamba jitihada za ujenzi wa barabara ya lami ya kilomita 230 kutoka Tunduma hadi Sumbawanga ni ajenda yetu kuu. Tumehangaika nayo siku nyingi lakini sasa mchakato wa kuanza ujenzi unaendelea vizuri…Nimeahidiwa kuwa zabuni zitakuwa tayari Agosti ama Septemba 2009, na kazi ya ujenzi inatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwaka huu au mwanzoni mwa mwaka jana.”


Aliongeza Rais Kikwete: “Kwa barabara za ndani ya mkoa, tunayo misaada kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya ukarabati na uimarishaji wa barabara ya kilomita 230 kutoka Sumbawanga hadi Mpanda, na barabara ya kilomita 87 kutoka Chala mpaka Katongoro hadi Kilando.”


Aliongeza: “Serikali ya Denmark nayo imekubali kusaidia ujenzi wa kilometa 148 za barabara kutoka Kilyamatundu hadi Muze. Mpango wa upanuzi wa bandari ya Kasanga katika Ziwa Tanganyika unafanywa na Mamlaka ya Bandari.”
“Lakini bado watu wengine wanatuambia tunazurura tu,” alisema Rais bila kuingia katika undani wa kauli yake hiyo.


Hata hivyo, watu wachache pamoja gazeti moja la Mwananchi jana na leo limeandika habari za kuonyesha kuwa ziara za Rais nje ya nchi hazina faida na kuwa Rais Kikwete anatumia muda mwingi nje ya nchi.


Mwananchi limeandika habari hiyo jana likikariri makala iliyochapishwa katika jarida la Economist la Mei 7.


Pamoja na Mwananchi kuandika habari hiyo siku 20 tokea ziandikwe kwenye jarida hilo, halikuchapisha undani wa kweli kweli wa makala hiyo uliokuwa unasifia mafanikio ya Serikali ya Rais Kikwete katika masuala mengine.


Makala ya awali ya Economist inasisitiza kuwa kutokana na mafanikio hayo ya utendaji wa Serikali ya Rais Kikwete, hakuna shaka kuwa Rais huyo atachaguliwa tena kwa kishindo katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.


Shutuma hizo za Rais kusafiri nje, zimekuwa zinatolewa kila mara Rais Kikwete anapokuwa na safari za Marekani na wala siyo kuhusu safari nyingine.

Nimeitoa kwenye blogu ya salva ikulumawasiliano.blogspot.com
 
Last edited by a moderator:
He! it has come to this? Yaani Rukwa wamepata barabara kwa sababu ya safari za Mwungwana? Long live Vasco Da Gama.
 
Shutuma hizo za Rais kusafiri nje, zimekuwa zinatolewa kila mara Rais Kikwete anapokuwa na safari za Marekani na wala siyo kuhusu safari nyingine.
jamani vasco da gama USA kaenda mara ngapi na Ulaya Asia kaenda mara ngapi?

ziara ya kwenda studio inatufaisha nini watanzania? hii inaoenakana hakuwa na ratiba maalum....eti Obama aje bongo akatembelee Bongo records kwa P funky!!!
 
Ignorance tu ya watu wa Rukwa!

MCA nchi nyingi tu wamepata pesa kule kwa kutimiza masharti na sii lazima kuenda US mara 6 kama JK!
 
He! it has come to this? Yaani Rukwa wamepata barabara kwa sababu ya safari za Mwungwana? Long live Vasco Da Gama.

Pia safari zake zimeifanya nchi kutambulika zaidi kuliko hata wakati wa kambarage,ni Kiongozi aliyebahatika hilo tulishukuru hapa TZ naweza hata kumuita OBAMA wa Afrika .
 
Unatoka Rukwa?

Unayaongelea Rukwa Angalia Jiji la Dar wewe unafikiri linajijenga wenywe ?ni mafanikio ya safari za Jk mambo bado ndio kwanza kipindi cha kwanza sasa tusubiri kipindi chapili Nchi ataifanya kuwa new york ya Afrika utajaza mwenywe.
 
Unayaongelea Rukwa Angalia Jiji la Dar wewe unafikiri linajijenga wenywe ?ni mafanikio ya safari za Jk mambo bado ndio kwanza kipindi cha kwanza sasa tusubiri kipindi chapili Nchi ataifanya kuwa new york ya Afrika utajaza mwenywe.
Duh hii mpya.. Dar kuwa NY ya Afrika.. itachukua miaka 200 kufikia hata Maputo!
 
"lakini bado watu wengine wanatuambia tunadhurura tu" jkwalker...

message sent...ukirusha jiwe gizani ...atakayeguna mh!! limempata!!

tunaamini kelele zetu hapa na za wengine zinamfikia......!!

misaada sio muarubaini wa umaskini wetu ...!! ni lazima tulenge kwenye kujitegemea......hata kama siasa ya ujamaa na kujitegemea hamuitaki .basi tuwe na siasa ya KUJITEGEMEA!!!
 
Unayaongelea Rukwa Angalia Jiji la Dar wewe unafikiri linajijenga wenywe ?ni mafanikio ya safari za Jk mambo bado ndio kwanza kipindi cha kwanza sasa tusubiri kipindi chapili Nchi ataifanya kuwa new york ya Afrika utajaza mwenywe.

Ebwana wee huyu jamaa kakoleza kimpumu nini maana sijawahi kusikia wala kuona
pumba kama hii,kwenye mtandao.
 
Taarifa imesomwa na Mykt wa CCM Rukwa, hivyo kichwa cha habari kingefaa kuwa "Wana CCM Rukwa wawajia juu wanaobeza safari za Rais Kikwete nje" .
 
Pia safari zake zimeifanya nchi kutambulika zaidi kuliko hata wakati wa kambarage,ni Kiongozi aliyebahatika hilo tulishukuru hapa TZ naweza hata kumuita OBAMA wa Afrika .

JK kaingia kabla ya Obama so kwa nini Obama asiwe JK wa Marekani? Kuhusu Jk kuwa Obama wa Afrika unajua mwenyewe vigezo ulivyo tumia kuwa linganisha.
 
Unayaongelea Rukwa Angalia Jiji la Dar wewe unafikiri linajijenga wenywe ?ni mafanikio ya safari za Jk mambo bado ndio kwanza kipindi cha kwanza sasa tusubiri kipindi chapili Nchi ataifanya kuwa new york ya Afrika utajaza mwenywe.

This is what I call day time dreaming. Ufisadi wote huo Dar iwe kama New York lini? Ni nini alicho badilisha kuhusu Dar mpaka sasa hivi ili mtu ambae hajatua Dar miaka mitano kweli aone tofauti? Anyway sijui kwa nini hata naji sumbua kujibu, sawa mkuu Dar itakua New York ya Afrika karibuni, kwani kuna tatizo bana.
 
Lengo la kila Mtanzania mwenye nia njema na taifa hili ni kuona maendeleo kwenye sekta ya elimu, afya, barabara, maji etc, lakini kwa nguvu hizi za harambee kubwa kubwa kwa kipindi cha mwaka mmoja kuelekea uchaguzi; napata hofu michango yote isije ikaishia kwenye kampeni na kusudio rasmi lisitimizwe.
 
lengo la kila mtanzania mwenye nia njema na taifa hili ni kuona maendeleo kwenye sekta ya elimu, afya, barabara, maji etc, lakini kwa nguvu hizi za harambee kubwa kubwa kwa kipindi cha mwaka mmoja kuelekea uchaguzi; napata hofu michango yote isije ikaishia kwenye kampeni na kusudio rasmi lisitimizwe.


good thinking/good vision....thanks
 
...Yaani kuahidiwa tu kwamba barabara ya Tunduma-Sumbawanga itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami kuanzia mwisho wa mwaka huu, ishakuwa "tunawalaani kabisa wanaosema ukienda nje unapoteza tu wakati" ?? Si angalau ndugu zetu wasubiri imalizike kujengwa kwanza?? Hivi wanajua kuwa hizo hela za hio barabara zinaweza zikachomekwa mahali pengine wakati wowote na wao wakaishia kuisikia lami kwenye redio tu?
 
Pia safari zake zimeifanya nchi kutambulika zaidi kuliko hata wakati wa kambarage,ni Kiongozi aliyebahatika hilo tulishukuru hapa TZ naweza hata kumuita OBAMA wa Afrika .

Obama Rais wa Marekani ni mzalendo anaeipenda nchi yake na ndio maana sio fisadi wala hawalindi mafisadi!!
 
Back
Top Bottom