Fidel80
JF-Expert Member
- May 3, 2008
- 21,947
- 4,445
Hakimu Mkazi Kisutu, Addy Lyamuya alitoa hukumu kwa mwanamziki huyo pamoja na watoto wake kwa kutumia mawazo yake binafsi.
Katika rufani hiyo, Nguza (babu Seya) pamoja na watoto wake - Papi Ngunza, Nguza Mbangu na Francis Nguza - wameiomba mahakama hiyo, kupitia mwenendo mzima wa ushahidi uliopelekea wao kutiwa hatiani na kusababisha kuhukumiwa kifungo hicho.
Wakili Mabere Marando ambaye anawatetea washitakiwa hao, aliwasilisha hoja hizo mbele ya Jopo la Majaji watatu lililokuwa likiongozwa na Nathalia Kimaro pamoja na wenzake ambao ni Jaji Mbarouk Salim Mbarouk na Jaji Salum Massati.
Marando alidai kuwa Babu Seya alikuwa na mpenzi wake aliyemtaja kwa jina la Farida ambaye mara baada ya kuachana alimuambia kuwa atamkomesha ambapo alidai kuwa kunauwezekano kesi hiyo ikawa ni kisasi cha mwanamke huyo ambaye alitoa vitisho hivyo.
Aliendelea kudai kuwa kunauwezekano wa Farida kuwafundisha watoto hao wanaodaiwa kubakwa, kusema uongo Mahakamani ili kuweza kumfunga Babu Sey na wanawe kama kisasi alichodai kumlipia.
Awali Marando alidai Mahakamani hapo kuwa upande wa utetezi unaondoa sababu za kutaka rufani hizo ambazo ni sababu ya 1,2,3,5,6,7,8,11,14 na 15 ambapo alidai kuwa katika rufani hiyo wataanza na sababu namba tisa kutokana na misingi ya kisheria.
Alidai kuwa sababu hiyo inaeleza maelezo ya anayeitwa Mahakamani kwa ajili ya kutoa ushahidi ambapo alidai kuwa mujibu wa sheria za motto kutoa ushahidi Hakimu ananatakiwa kumuhoji kabla ya kutoa ushahidi wake ili aweze kuona kama motto anauelewa gani juu ya kiapo cha ushahidi.
Marando alidai kuwa katika rufani ya awali katika Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam, nchini ya Jaji Thomas Mihayo alisema kuwa utaratibu uliokuwa umetumiwa na hakimu aliyekuwa ametoa hukumu hiyo ilikuwa na makosa kutokana na watoto ambao walitoa ushahidi kutohojiwa kabla ya kutoa ushahidi wao.
Alidai kuwa mahojiano ya awali na mtoto anayetoa ushahidi ni ili kupata maamuzi na kujua kama mtoto anajua maana ya kiapo ambapo mahojiano hayo baina ya hakimu na mtoto yanatakiwa kuhojiwa.
"Kwa kutozingatia mambo hayo ushahidi ambao utakuwa umetolewa na mtoto huyo utakuwa batili na hauna maana yoyote," alidai Marando.
Aliongeza kuwa muelekeo wa Jaji Mihayo aliyesikiliza rufani hiyo kwa mara ya kwanza haukuwa mzuri kutokana na sheria mbalimbali alizozitumia kugongana ambapo alidai kuwa kutokana na hali hiyo Jaji huyo alifanya kosa kisheria.
Wakili huyo alidai kuwa mashahidi 10 kati ya tisa wa upande wa Jamuhuri ambao walitoa ushahidi wao hawakuapishwa wala kuangalia uwezo wao kama wanaelewa maana ya kiapo.
Pia alidai kuwa katika rufani iliyosikilizwa na Jaji Mihayo alisema kuwa hakimu aliyetoa hukumu hiyo kwakuangalia ushahidi wa pande mbili ambapo alidai kuwa Jaji huyo alikosea kwakua ushahidi wa utetezi haukuangaliwa vyema.
" Katika nyaraka rejea zilizotumiwa na hakimu aliongeza mawazo yake binafsi kutokana na kupingana na maelezo ya mashahidi, katika ukurasa wa 532 mstari wa saba katika hukumu hii, hakimu anapingana na shahidi aliyejitambulisha kwa jina la Lubaba ambaye mama yake ni Mzaramo na baba yake Mkongo.
"Lakini katika maelezo ya hakimu anaonyesha kijana huyo ni Mzaramo wakati si kweli, hiyo yote inaonyesha jinsi gani hakimu alivyokuwa akiweka mawazo yake binafsi," alidai Marando.
Marando alidai kuwa kwa muda wa miaka 30 ambayo amefanya kazi ya uwakili hajawahi kuona hukumu ya namna hiyo ambayo hukumu inatolewa kwa kufuata mawazo ya hakimu badala ya ushahidi wa pande mbili.
Aliendelea kudai kuwa hakuna ushahidi ambao ulionesha mshitakiwa wa pili alibaka au kulawiti kabla au baada ya kufanya safari zake za kimuziki katika mikoa ya Mwanza na Arusha ambapo alisema kuwa hakimu aliweza kuweka mawazo yake binafsi ili kuwezesha mshitakiwa huyo kuwa na hatia ya kumfunga gerezani.
"Mbali na hayo mshitakiw ahuyo wa pili alidai kuwa kati ya Agosti na Septemba alikuwa akirekodi albamu yake na mwanamuziki Lady Jee dee , lakini badala ya hakimu kuandika maelezo hayo na matokeo yake aliandika ‘So what?'," alidai wakili huyo.
Alidai kuwa hakimu huyo hakuandika maelezo ya mashahidi wa upande wa utetezi na badala yake aliandika idadi ya mashahidi ambao walifika kutoa ushahidi wa upande wa utetezi ambapo wakili huyo alihoji hali hiyo iliyofanywa na hakimu huyo.
Wakili huyo alidai kuwa kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa na watoto ambao wanadaiwakufanywa vitendo vya ubakaji na kulawitia walitaja baadhi ya watu ambao hawakuweza kuitwa na upande wa mashitaka kufika Mahakamani kwa ajili ya kutoa ushahidi wao.
Alidai kuwa watoto hao walimtaja Mangi ambaye anauza duka ambalo lipo karibu na nyumbani kwa Babu Seya ambaye anadaiwa kuona watoto hao wakati wakiingia na kuchukuliwa na mshitakiwa huyo wa kwanza na pia anadaiwa kusikia wakati watoto hao wakilia wakati wakifanyiwa vitendo hivyo.
Pia mbali na Mangi pia ilidai kuwa watoto hao walimtaja dada na bibi ambao walikuwa wakikutwa katika nyumba hiyo ambapo Marando alihoji kutokuitwa kwa watu hao kufika kutoa ushahidi ili kuweza kuthibitisha madai hayo.
"Kitu cha kushangaza zaidi ni madai ambayo yalitolewa kuwa watoto hao walifanyiwa vitendo hivyo tarehe 11 Oktoba wakati siku hiyo ilikuwa ni Jumamosi na pia mshitakiwa wa kwanza alikuwa amekamatwa na katika maelezo ya watoto hao inadaiwa kuwa walikuwa wakifanyiwa vitendo hivyo wakati wakitoka shule.
"Je siku hiyo ya jumamosi mbona haikutajwa wakati maelezi yanadai kuwa walifanyiwa siku za katikati ya wiki, Jamuhuri ingeweza kufanya uchunguzi ili kuweza kubaini mtu ambaye aliweza kuwabaka watoto hao na si kama jinsi inavyodaiwa," alidai.
Alidai kuwa baadhi ya shahidi mtoto alishindwa kumtambua Babu Seya na mwingine alikanusha kubakwa na mshitakiwa wa 3 na 4 ambapo alidai kuwa hakimu aliandika kuwa kutokana na watoto hao kujuana alihisi kuwa ni lazima watoto hao walibakwa licha ya watoto hao kutothibitisha.
Aliongeza kuwa katika kielelezo kilichotolewa na Hospitali ya Mwananyamala kilidai kuwa mtoto mmoja aliambukiza Kisonono ambapo washitakiwa hao kupitia mawakili wao waliomba kwenda kuwapima washitakiwa hao ili kuweza kuona ni mshitakiwa yupi aliyekuwa amemuambukiza ugonjwa huo wa zinaa.
Alidai kuwa licha ya ombi hilo upande wa Jamuhuri ulikataa kuwapeleka washitakiwa hospitali kwa ajili ya kuweza kuwapima ugonjwa huo ambapo alidai kuwa mtoto mwingine katika maelezo yake alidai kuwa alilazimishwa na Babu Seya kumkamua vipele vilivyokuwa katika sehemu zake za siri vilivyokuwa vikitoa usaha na maji.
Hata hivyo wakili huyo alidai kuwa upande wa Jamuhuri haukuwa tayari kuwafikisha watuhumiwa hao katika kituo cha afya ili kuweza kuthibitisha madai hayo yaliyokuwa yamedaiwa.
"Mshitakiwa wa nne ambaye alikuwa ni mwanafunzi naye pia anadaiw akushiriki katika vitendo hivyo lakini upande wa Jamuhuri haukuwahi kumuita Mkuu wa shule ya sekondari ya Mbezi ambayo alikuwa anasoma ili kuweza kuthibitisha kama mwanafunzi wake alikuwa hafiki shule.
"Lakini mambo yote hayo hayakuweza kufanywa wakati kila mmoja anaelewa kuwa muda ambao anatoka mwanafunzi huyo watoto hao wanakuwa tayari hawapo lakini hazikuweza kufanyika jitihada mbalimbali," alidai.
Alidai kuwa katika jarada la kesi hiyo, mashitaka mawili yalikuwa yakiingiliana ambapo shitaka moja lilidai kuwa watoto hao walifanyiwa vitendo hivyo Oktoba ambapo shitaka jingine lilidai kuwa watoto hao walifanyiwa vitendo vinvyo kwanzia April hadi Oktoba.
Alidai kuwa katika maelezo ya mashahidi hakuna shahidi aliyedai kuwa alifanyiwa vitendo hivyo kati ya Aprili hadi Julai na kwamba kwa kipindi hicho ambacho kimetajwa mshitakiwa wa 2 na 3 walikuwa wakishinda katika kambi yao ya mazoezi ya FM Academy.
Naye wakili wa upande wa Jamuhuri uliokuwa ukiongozwa na Justuce Mlokozi alikili watoto hao kutorekodiwa na pia kutofanyiwa kiapo ambapo alidai kuwa Mahakama iliegemea ushahidi wa Jamuhuri na kwamba hata kama kulikuwa na makosa madogomadogo yanaweza kutibika chini ya sheria namba 388 ya mwenendo wa mashahidi.
Mlokozi alidai kuwa waliamua kuwaleta watoto katika ushahidi huo kutokana na wao ndio walikuwa walengwa zaidi na wakati wakifanyiwa kitendo hicho hakuna watu wengine waliokuwa wakiona.
Aliendelea kudai kuwa kuhusu kutofautiana kwa miezi katika jarada la kesi hiyo alidai kuwa hakukuw ana tarehe maalum ambayo watoto hao wlaifanyiwa vitendo hivyo na kwamba walikuwa wakifanyiwa kwa nyakati tofauti.
Aliongeza kuwa kuhusu kusafiri kwa mshitakiwa wa 2 alidai kuwa hiyo si hoja kuwa hajatenda kosa ambapo alidai kuwa anaweza kuwafanyia kipindi ambacho anakuwa hapa jijini Dar es Salaam na kudai kuwa kuhusu Farida haiwezekani kuwafundisha watoto wote kusema uongo kama inavyodaiwa na utetezi.
Mjisomee maelezo hayo hapo juu hawa wanatoka kumbe sheria zilipindishwa.