RPC wa Mwanza ACP Liberatus Barlow auawa na wanaodaiwa ni majambazi!

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa Mwanza Injinia Everest Ndikillo amesema kuwa Kamanda Barlow alikuwa anatoka katika kikao cha harusi na ndugu yake aitwaye Sembeli Maleto kilichokuwa kinafanyika katika Hotel ya Florida na kisha kumpeleka mwanamke aitwaye Dorcas Moses Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Nyamagana maeneo ya barabara ya Kona ya Bwiru kwenda Kitangiri.

"Walipofika getini kwa Mama Dorcas mara waliwaona watu wawili wakiwa wamevaa makoti ya Polisi-Jamii, Mama Dorcas alimuuliza Kamanda Barlow kama anawafahamu Kamanda akasema kuwa hawa na watu wa ulinzi wa Jamii wako doria." Alieleza Mkuu wa Mkoa.

Aliongeza kusema: "Mara wale watu waliongezeka na kuwa sita wakaanza kama kuzozana wao kwa wao na ndipo Kamanda alipowauuliza kuna nini, Mmoja wao akajibu hakuna kitu na ikapelekea Kamanda kutaka kutoka nje ila wale watu watatu wakaizingira gari ya Kamanda Barlow aina ya Rav 4. Kamanda Barlow alipoona kama hali hewa inabadilika alichukua redio call ili aweze kuwa taarifu askari na ndipo wale jamaa walipompiga risasi kichwani nakupelekea kifo chake."

Taratibu za mazishi ya Kijeshi bado zinaendelea na nyumbani kwa marehemu ambapo watu mbalimbali wako katika hali ya majonzi sana. Mke wa Kamanda Barlow yuko Dar es Salaam na anatarajia kufika Mwanza.

Mpaka sasa Polisi wanamshikilia mtu mmoja aitwaye Dorcas kwa ajili ya Mahojiano huku uchunguzi mkali ukiendelea kuhusiana na kifo cha kamanda Liberetus Barlow.
Shukran kwa taarifa mkuu,sasa ni Dorothea ama ni Dorcas?

Na huyo "mtu mmoja" anayeshikiliwa na polisi anayeitwa Dorcas ndiye huyo huyo aliyekuwa naye wakati wa tukio?

Kwasababu mara wamu address kama "mwalimu Dorcas",halafu tena "mama Dorcas", na mwishowe tena "mtu anayeitwa Dorcas".Yani hakuna flow inayoonyesha kwamba wana nia ya kuulewesha umma ukweli.

Sijui kwanini hawa watu huwa hawawezi kutoa taarifa zisizokuwa na mizengwe na utata.

Halafu kila mtu anaongea lake,thread kama hii ilitakiwa ifungwe hadi kuwe updates za kueleweka,maana kuna wanaodai mara hana mke,mara ana mke,mara mke yuko anaishi Dar!Mara mke wake alifariki!duh!
 
Tunasubiri majibu zaidi kuliko maswali tuliyo nayo kutoka Jeshi la Polisi, lakini kwa ufupi tu ni kuwa, binafsi najiuliza hivi hakuna mkono wa maofisa wa jeshi hilo mkoani Mwanza? maana nasikia kati ya makamanda wa polisi waliokuwa makini katika kazi, huyu Barow alikuwa miongoni mwao. Hakutaka mchezo kazini na zipo taarifa wapo maofisa wake waliokuwa hawapendi misimamo yake ya kikazi. Manumba tunakusubiri kwa hamu na ripoti yako!
 
mkuu hapo kwenye red. hiyo ndo inaitwa intelejinsia
 
mkuu hapo kwenye red. hiyo ndo inaitwa intelejinsia

Ni mwalimu Doroth Moses wa shule ya Msingi Nyamagana ambaye ndiye alikuwa naye kwenye gari toka kikao cha arusi katika Hotel ya Florida. Na huyu ndiye anaeshikiliwa na polisi mpaka sasa ka uchunguzi zaidi.
 
Tunasubiri majibu zaidi kuliko maswali tuliyo nayo kutoka Jeshi la Polisi, lakini kwa ufupi tu ni kuwa, binafsi najiuliza hivi hakuna mkono wa maofisa wa jeshi hilo mkoani Mwanza? maana nasikia kati ya makamanda wa polisi waliokuwa makini katika kazi, huyu Barow alikuwa miongoni mwao. Hakutaka mchezo kazini na zipo taarifa wapo maofisa wake waliokuwa hawapendi misimamo yake ya kikazi. Manumba tunakusubiri kwa hamu na ripoti yako!
Hivi si kulikuwepo na Kamnda Ntobi once upon a time?

Kama ni kweli unayosema,sitoshangazwa,maana polisi nao ni majambazi,ama kwa maana nyingine,kuna wanaoshirikiana na majambazi.

Halafu pia ikija kwenye "Pale pahala",wanakuwa wadhaifu mnoo!Hata kimada wa RPC ama OCD anatisha wananchi nyau na hata askari wa chini wanawasikiliza vimada hao.Na uombe Mungu usiingie kwenye anga ya kimada utakoma ubishi.Huwa wanafanya wanavyotaka na huwa wanajulikana na mji/jiji zima kuwa pale ni pahala pa Kamanda na wanachoamuwa wao nacho ni kama amri ya kamanda mwenyewe.

Tanzania hovyo bana.Nilishalala ndani siku tatu na marafiki zangu kwa amri ya kimada wa kamanda Chiko,kisa tulikuwa tunajimwaga kwenye hoteli ambayo huwa wanakulana uroda na kimada alikuwa around nyakati hizo mida ya jioni,so hataki vijana maeneo hayo kwani yeye alikuwepo hapo na akasikia maongezi yetu pale muhudumu aliposema huyo kimada yuko hapo,sisi tukawa tunasema hatuna shida naye na kwamba hata kazi ya polisi ni kulinda usalama wa raia.

Tuliswekwa ndani na mdhamana tukakataliwa na walitaka kutupa kesi eti ya madawa ya kulevya.Mdhamana tukiuliza kwanini hatupewi,tunaambiwa ni amri kutoka juu!Ilkuwa ijumaa, na mdhamana ilikuwa hadi jumatatu.Bongo hovyoo!
 
Back
Top Bottom