RPC wa Mwanza ACP Liberatus Barlow auawa na wanaodaiwa ni majambazi!

Eti kapigwa risasi na majambazi?...kwa hiyo wameshafanya uchunguzi na kujua ni majambazi? Wamepora nini? Hivi RPC si anakuwa na mlinzi...je naye ameuawa...hivi si jeshi hili lililouwa majambazi watano juzi...vipi intelijensia juu ya mipango ya mauaji ya RPC Mwanza?

Hivi huyu Mwema ndio alikuwa interpol Nairobi? Mbona TZ hatuishi mambo ya vioja?

Kila nafsi itaonja mauti. Pole kwa familia ya marehemu!
 
Maswali:
  1. Je, alikuwa peke yake ndani ya gari? Kwa nini?
  2. Kwa nini kikao cha harusi kifanyike hadi saa 7 usiku wakati sheria inakataza kufunguz baa zaidi ya saa 4 na nusu usiku?
  3. Huyo "dada" yake amehojiwa juu ya uhusiano wao na watu wengine?
  4. Je, mezani kwake kulikuwa na masuala gani aliyokuwa akiyafuatilia?
  5. Je, kuna biashara zozote ambazo marehemu amekuwa akiendesha; peke yake au akishirikiana na wabia? Ni akina nani hao? Je kuna ugomvi wowote wa kibiashara baina ya marehemu na wabia wake?
  6. Je, kuna uhusiano wowote kati ya kifo cha marehemu wa mahasimu wa kisiasa jijini Mwanza? -ndani ya CCM? baina na wapinzani CCM/Polisi?
  7. Kwa nini polisi haijawachukulia "majambazi" waliojaribu kuwaua Wabunge wa CDM?
  8. Je, kuna wakati polisi wamekuwa wakiwatumia "majambazi" kuwashughulikia watu wanaodhaniwa kuwa wabaya wa polisi?
Bila IGP/DCI kujibu maswali haya kwa ufasaha, ni vigumu kuamini kuwa the system is not 'hiting from back.'
 
Du kumbe hii habari nzito hapa JF!!!!!!!
There are currently 1391 users browsing this thread. (524 members and 867 guests)
 
Naona umeanza kutumia lugha ya kikristo hapo chini kwanini usitumie ile Lugha iliyotumiwa kwenye kile kitabu kilichokojolewa?

There are few thousands of words to fit description of your state of mind and i would really like like to type them out-but I STIL LIKE MY MEMBERSHIP HERE.
 
Wanakuwa Busy mno kuhaikia ccm badala ya kuangalia suala la ulinzi wa Raia na mali zao sasa hili ni Anguko kuu.

Nchi yeyote inapo shindwa kusimamia sheria mwisho wake huwa hivi, hatuwezi kujua hao waliotenda hayo mauaji wanafikiksha ujumbe gani lakini hapa tunaamini sasa hata zile taarifa za Kova za intelijensia huwa ni za uongo kwnini wameshindwa kuilinda Roho ya kiongozi mwenzao? ikiwa intelijensia yao kwenye mashambulio ipo juu?

Ama intelijensia yao hutoa taarifa kwenye mikutano ya Chadema tuu?

Barlow alitoka wapi saa nane za usiku? ni vikao gani vya Harusi hufanyika Muda huo?

Na alikuwa akiendesha mwenyewe, ama alikuwa na Dereva?

Nashawishika kusema haya,

Kutokana na Mambo yanayo endelea sasa lazma waziri Nchimbi na Amiri mkuu wafumue JESHI LA POLISI NA KULIUNDA UPYA..............
 
wangeanza na Andengenye, Shilogile na huyu Kamhanda..shenzi zao kabisa malipo ni hapa hapa duniani

Plzzz tuwe mioyo ya kibinadam haijalish nan kafanyiwa, bt pia ukae ukijua hakna kiongozi mzuri polisi km Andengenye, bt kifo cha Mh. huyu co cha kushangilia hata kidogo, fikiria y wamemfanyia hivi na baada ya hapo what next kwa raia na polisi? pengine majambaz hawapumui kwasbb yake!!!!! plz sumtym tuache ushabiki uco na mantiki~!
 
Nasikitika kutokana na mauaji ya huyu RPC ambaye namjua tukiwa Chuo Kikuu. Hata Kifo cha Mwandishi Mwangosi, na wengine wote waliouwawa na kuteswa vinanisikitisha sana.

Nasikitika jinsi mtu unavyolelewa, unakuwa unasomeshwa na unakuwa na mafanikio kielimu. Hata hivyo kuchagua kazi inakuwa ni changamoto kubwa katika dunia yetu hasa bara la Afrika na TZ. Kazi ya upolisi ni nzuri iwapo eneo unalofanyia linaamini na kuzingatia sheria na haki za binadamu.

Katika Mazingira yaliyojaa uonevu kwa wanyonge na kila mtu mwnye nguvu anakuangalia wewe umlinde mwenye nguvu hata kama ana makosa ni sawa na kuwa motoni! Wenzetu ulaya wana msemo kuwa ukitaka kuwa kwenye pepo ya Ulaya kutana na polisi wa Kiingereza. Polisi ambao kwao mhalifu hushughlikiwa kwa umakini kirafiki huku haki zake za kibinadamu zikizingatiwa. Yaani ukimwona Polisi ni usalama kweli na ndio kimbilio la watu wote. Unadhifu wa uniform zao unashabihiana na mioyo yao na utendaji kazi mzuri ambao hautiliwi mashaka.

Sisemi kuwa ndugu yetu huyu alichagua kazi ambayo si nzrui, isipokuwa wote mtakubaliana nami kuwa mazingira yaliyopo hivi sana yanawalazimisha wenye madaraka wasio na hofu ya Mungu kuingia kwenye uchafu. (Ni lazima nikiri kuwa sijui utendaji wa Marehemu ulivyokuwa kwa maana mimi niliingia kwenye fani nyingine; na kuwa hata sisi wengine ni wahanga wa hali hiyo katika fani tulizochagua kuutumikia Umma) nimekuwa namsikia sana kwenye vyombo vya habari.

Siku hizi kazi nyingi ikiwemo Polisi zimeharibiwa na kugeuzwa vichaka vya wahalifu, watoa rushwa, wala rushwa, mafisadi na uchafu mwingine. Katika Jamii yetu kama una madaraka na huna hofu ya Mungu, unaweza kuyatumia utakavyo kuwadhalilisha wanyonge ili mradi usimguse mwenye fedha au madaraka. Hakuna nafasi ya kuwatumikia wanyonge kwa haki; na kwa maana hiyo ukisimamia haki na kuwapa haki wanyonge, basi wewe utasulubiwa na kutolewa kafara na wale wenye nguvu wasiomwogopa Mungu kwa maana kwa kufanya hivyo unazuia wadhalimu wao kujirusha na madaraka yao kujipatia hata kile wasichostahili.

Ukiwa na roho ndogo na wewe unaweza kuingia katika mtego huo kwani hiyo ni kazi rahisi. Tuendelee kuwa na moyo mkuu... Huenda Ndugu yangu huyu alipojiunga na kazi hii alikuwa na nia nzuri ya kutumikia watu wake lakini akakuta mazingira magumu ambayo yeye mwenyewe kwa kutumia akili zake ninazozijua na roho yake asingeweza kubadilisha hali iliyopo.

Hata sisi wengine tumeshindwa tunaugulia rohoni tu kuwa tumeingia na ari kubwa ya kuinua hali ya nchi yetu lakini tunashuhudia tukizeeka huku hali ikizidi kuwa ngumu na hata kuona kuwa nia na juhudi za binafsi zimekuwa kama tone la maji katika Bahari ya Hindi. Kila mara hujiuliza ni nini hatma ya Taifa letu; Wananchi wanyonge. Watoto wetu na Wajukuu zetu tuwaachie wosia Gani?

Nakumbushwa kuwa hakuna kukata tamaa na tuendelee kuwahudumia Watanzania wenzetu popote tulipo kwa haki heshima na uadilifu wa hali ya juu. Iko siku hali hii itakuwa historia iwapo wote tutasimama kwa pamoja na kulenga kurudisha heshima ya nchi yetu na watu wetu.
 
Back
Top Bottom