RPC wa Dar es Salaam Muliro una Taarifa kuwa Mauwaji ya Kikatili kwa Madereva Bodaboda yamerejea tena?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,646
109,031
Ndani ya Wiki Moja nimetoka Kuhudhuria Misiba ya Madereva Bodaboda Wawili ( tena Vijana kabisa Masikini ya Mungu ) na Wote wameuwa Kikatili ( Kishalubela ) na Watu wanaowapora Pikipiki zao huku Wakiwatoboa na Kuwanyofoa Macho yao.

Muda huu huu kuna Mwana ( Rafiki ) nae ananiambia atachelewa kuja Maskani kwani anaenda Mazikoni kuna Dereva Bodaboda Kauliwa vibaya na Kuporwa Pikipiki ya Boss ( Taita ) wake.

RPC wa Dar es Salaam Muliro hebu anza sasa Kulifanyia hili Kazi kwani Madereva Bodaboda wako katika Mtihani mkubwa wa Kuuwawa Kishalubela ( Kikatili ) na Majambazi ambao hutumia Wanawake Warembo kama Chambo ili Kufanikisha azma zao hizo Ovu.

Na maeneo ambayo ndiyo HATARISHI kwa Bodaboda wengi Kuuwawa na Kuporwa Pikipiki ni Kunduchi Makaburini, Ununio, Tegeta Masaiti, Boko na Mbweni.

Nirudi Kwao Madereva Bodaboda ambao Wengi wao ni Marafiki zangu kwakuwa huwa wananisaidia Kunivushia Wake za Watu katika Uzinifu kuwa huku Kutekwa Kizembe na Kuuliwa Kikatili hivi huwa mnataka Wenyewe na tunapoelekea nitaanza hata Kuacha Kuhudhuria Misiba yenu kwakuwa huwa hamfuati Ushauri wangu mzuri Kaka yenu GENTAMYCINE Mimi.

Madereva Bodaboda wa Msasani CCBRT, Masaki Kona ya Slip Way ( Bakhressa ), Tegeta kwa Ndevu, Mbezi Beach Makonde, Boko Magengeni na Kawe kote nimeshawaambieni kuwa Ukikodiwa hasa mida ya Usiku na Mteja kisha ukamtajia Hela Kubwa na bado akakubali Kukulipa Shtuka upesi na jua kuwa huyo ni Israeli anataka kwenda Kukumaliza.

Nikaenda mbele na Kuwaambieni kuwa Ukikodiwa na Binti / Mwanamke Mrembo kisha muda Wote mkiwa njiani anaogea na Simu au Anachati anza Kushtuka na kuwa Makini kwani hapo Mipango ya Kukumaliza inaandaliwa kama si Kusetiwa.

Kwa jinsi GENTAMYCINE ninavyowapenda nikaenda mbele zaidi na Kuwaambia ukiona Umembeba Abiria ( hasa Mwanamke ) na mnakoelekea ni barabara ya Mapori na Giza ukiona anakuomba usimame mara moja akojoe ( asusu ) Wewe mkatalie na ikiwezekana mwambie aikojolee Pikipiki yako ( alipokaa ) na utaisafisha mbele kwa mbele ili Ujiokoe na Mtego wake lakini bado tu hamsikii.

Nikamalizia kwa Kuwaambieni kuwa ukiona Unakodiwa na Mteja unayemshuku basi Kisirisiri muombe Dereva Bodaboda Mwenzako hapo Kijiweni Kwako akufuate kwa nyuma ili hata kama Kukitokea chochote basi aweze Kukupa Msaada na Usiporwe Pikipiki na Kuuwawa Kikatili hivyo / hivi.

Leo nimeamua Kujitolea Kuwatetea hivi kwakuwa GENTAMYCINE naumia Mkifa wote nitakosa Bodaboda kwa Kuniletea Wake za Watu katika 'Mbanduano' kwani kwa jinsi nilivyoshibana nanyi na mnavyonipenda Kaka yenu kuna muda huwa mnaniletea hawa Mademu ( Wake za Watu ) bure kabisa bila Kunitoza chochote na hata ikitokea nawalipeni Chenu huwa mnakataa kabisa Kupokea.

Mwisho nawaombeni pia Chunguzaneni sana katika Vijiwe vyenu kwani kuna Uwezekano mkubwa baadhi yenu ni sehemu ya Kuchonga ( Kupanga ) Mipango ya Kutekwa na hatimaye Kuuliwa na Kuporwa hizo Pikipiki zenu mpya mpya na sijui kwanini zile Kongwe ( Nzee ) huwa haziporwi.

Kuweni makini na Jalini Usalama Ok?
 
Kuhusiana na hao warembo wanaotumika kama chambo, ukihisi anachati na watu mkiwa kwenye mwendo, na ukamtilia wasiwasi na labda uliwahi kusikia kwa watu kuwa huyu ni "informer", jifanye kama unampeleka halafu mbele kidogo tu piga U turn au pita njia nyingine na endesha kwa spidi kubwa rudi naye ulikotoka. Ukifika mlazimishe kwa vitisho aseme alikuwa anachati nini, na nani. Ukiona haeleweki mpeleke polisi. Anaweza akawa ndiye aliyechora michoro ya wote walioporwa na kuuwawa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akipiga kelele unataka mbaka au muibia?
 
Ujumbe mzuri sana ase lakini bodaboda na madem ni pete na kidole,hivyo ni ngum kwa bodaboda kushtukia mitego kama hyo
 
Back
Top Bottom