RPC Morogoro akana polisi kutumia risasi za moto

RPC Moro si anajifanyaga mbabe. sasa mbona anaanza kujitia kidole mwenyewe? Idiot!
 
Kuhusu mauji ya raia asiye na hatia askari wa morogoro si waadililifu wameanza kulalamikiwa toka kitambo
 

Attachments

  • Barua ya afande.jpg
    Barua ya afande.jpg
    77.5 KB · Views: 82
Kwa hiyo aliyerusha hiyo risasi ni mojawapo ya wale vijana walioandaliwa na Nape kwenda kuvuruga mkutano wa Chadema?
 
Huyo reporter wa BBC hamna kitu. Nimemsikia akiripoti jana, hakuna hata swali moja aliloulizwa na mwenzie wa studio aliloweza kujibu.

Alikuwa anakariri tu maelezo aliyopewa na RPC bila kubalance story. Hata akiulizwa, anatoa majibu aliyonayo kichwani bila kujibu swali.

No wonder matukio mengi ya TZ hayaripotiwi na BBC.

Kwa hadhi ya BBC, anaishusha sana. Kwa ufupi, hamna kitu.
 

KWAMBA askari polisi mjini Morogoro juzi walimuua kwa risasi kijana mmoja na kujeruhi wengine wawili wakati walipokuwa wakidhibiti maandamano ya wafuasi wa Chadema, ni taarifa ambazo zimetusikitisha sana na kutoa picha kwamba nchi yetu hakika bado ina safari ndefu kuelekea kwenye demokrasia ya kweli na utawala bora.


Tunasema nchi yetu bado ina safari ndefu kufikia vigezo vya demokrasia na utawala bora kutokana na matukio mengi makubwa tunayoshuhudia mara kwa mara katika sehemu kadhaa nchini. Aghalabu yamekuwapo matukio ya vifo na uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu unaotokana na matumizi mabaya ya silaha na madaraka kwa upande wa Jeshi la Polisi. Mifano ya hali hiyo ya kusikitisha ni nyingi, lakini yatosha tu kusema hapa kwamba jeshi hilo kwa kiasi kikubwa limeshindwa kuelewa dhana ya ulinzi wa raia na haki ya mtu kuishi, ikiwa ndiyo dhima na dira kuu inayoliongoza jeshi hilo.

Yapo maeneo ambayo jeshi hilo limefanya vizuri na sisi tumekuwa msitari wa mbele kulimwagia sifa kila linapostahili kupongezwa. Lakini jeshi hilo limelaumiwa kwa mambo mengi ambayo hatuwezi kuyaorodhesha yote katika safu hii kutokana na ufinyu wa nafasi. Moja ya malalamiko makubwa ambayo yamekuwa yakielekezwa kwa jeshi hilo ni jinsi ambavyo limekuwa likivinyanyasa vyama vya upinzani na kuegemea kwa chama tawala. Miaka 20 tangu kuanzishwa kwa siasa za vyama vingi nchini, Jeshi la Polisi limekuwa halionekani kuvitendea haki vyama vya upinzani na limekuwa linavunja sheria ya mwaka 1992 ambayo ilianzisha vyama hivyo.

Kwa mfano, jeshi hilo limekataa kuelewa au kutambua kwamba sheria hiyo ya vyama vya siasa haitoi mamlaka kwa jeshi hilo kutoa vibali kwa vyama hivyo kufanya shughuli za siasa, yakiwamo maandamano, mikutano ya ndani na ya hadhara na shughuli nyingine zozote za kisiasa. Sheria inasema kuwa, ili shughuli hizo zifanyike kwa amani na utulivu, lazima vyama hivyo vilitaarifu rasmi Jeshi la Polisi ndani ya saa 48 kabla ya kufanyika kwa shughuli hizo ili jeshi hilo litoe ulinzi. Lakini katika hali ya kushangaza, jeshi hilo limejipachika mamlaka ya kuratibu shughuli za vyama hivyo kwa kutoa au kukataa kutoa vibali vya kufanyika kwa shughuli hizo.

Swali ambalo limekuwa likiulizwa na wananchi wengi ni kuhusu sababu za jeshi hilo kutoa vibali pasipo pingamizi kwa vikundi vinavyoandamana au kufanya mikutano ya hadhara kuipongeza Serikali na viongozi wake? Kama kweli ajenda ya jeshi hilo siyo ya siri na inaendeshwa kwa dhamira safi, inakuwaje halifanyi hivyo kwa vyama vya upinzani ambavyo vimesajiliwa kisheria au vikundi vya wanaharakati vinavyotetea haki za kijamii? Inakuwaje basi vyama vya upinzani na vya kiharakati vikataliwe kuendesha shughuli zake kwa kisingizio cha kutokuwapo polisi wa kutosha kulinda shughuli hizo, lakini polisi wa kusha, tena wenye magari yaliyosheheni silaha za kivita wanapatikana kuzuia shughuli hizo zisifanyike?

Badala ya kulikemea jeshi hilo kwa kuvunja sheria na kukandamiza demokrasia, chama tawala na Serikali yake mara zote vimekuwa vikikaa kimya, huku vikichekelea pembeni na kuliacha jeshi hilo likitekeleza kile kinachodaiwa na vyama vya upinzani kwamba ni kutekeleza maagizo kutoka juu. Pengine ndiyo sababu kila mara jeshi hilo linaposababisha vifo vya raia kwa kisingizio cha kudhibiti maandamano ambayo hayana vibali vya polisi, Serikali hujitokeza na kulipongeza jeshi hilo kwa kusimamia sheria

Hivyo ndivyo ilivyokuwa jana. Akizungumzia tukio la Morogoro ambapo juzi mji huo na viunga vyake viligeuka uwanja wa mapambano, ambapo polisi waliua mtu mmoja kwa risasi wakati wakidhibiti maandamano ya wafuasi wa Chadema, Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi alisema polisi walikuwa wanatekeleza wajibu wao, huku akiwataka viongozi wa vyama vya siasa kufuata sheria.Polisi waache matumizi mabaya ya silaha


 
Kulikuwa hakuna sababu ya kutumia nguvu kubwa kudhibiti waandamanaji hata kama hawakuruhusiwa kwani hawakuwa na silaha. Polisi kutumia silaha za moto halafu wasema hawakutumia wakati kuna mtu kafa inasikitisha sana sana. Huku kuua raia bila sababu za msingi kutaisha lini?
 
Ni katika taarifa ya habari ya ITV ya jana Tar 28/08/2012, Shigela alisema kuwa haingii akilini kuona polisi wanasemwa kuwa ndio waliomuua mtu pale Morogoro asiyekuwa mhusika hata kidogo katika maandamano ya CHADEMA, wakati waliovaa magwanda walikuwa wanaonekana na wasidhurike na risasi hizo, Shigela akasema kuwa huo ni mchezo mchafu wa CHADEMA.

Kwa kauli hii ilinipa maswali mengi ya kujiuliza katika CD hii ya Shigela na mtazamo wake kuhusu Polisi na Serikali, kwani ailiingia akili kupigwa kwa Ulimboka ? na polisi kumleta mtu anayesemekana mkenya katika mazingira ya utata? iliingia akilini kuawa kwa mfuasi wa CHADEMA pale Igunga? iliingia akilini mauaji yaliyofanywa na Zombe? ilingia akilini kwa kupigwa kwa wabunge wa CHADEMA pale Mwanza? ilingia akilini kupigwa na kuawa kwa raia pale Songea waliokuwa wakienda kutaka kauli ya mkuu wa wilaya ? iliingia akilini kwa mauaji yaliyofanywa kule Arumeru.

Kwa mujibu wa SHIGELA ni mauaji ya Morogoro tuu ambayo hayaingii akilini na hivyo jibu rahisi kama mauaji hayaingii akilini mwa SHIGELA muhusika ni CHADEMA. Kwa kauli ile inadhihirisha kuwa mauaji yaliyopita yaliingia akilini mwa SHIGELA.
 
Tatizo la mbumbumbu shigera alitaka kuona wavaa magwanda ndiyo waliouwa!
 
Ni katika taarifa ya habari ya ITV ya jana Tar 28/08/2012, Shigela alisema kuwa haingii akilini kuona polisi wanasemwa kuwa ndio waliomuua mtu pale Morogoro asiyekuwa mhusika hata kidogo katika maandamano ya CHADEMA, wakati waliovaa magwanda walikuwa wanaonekana na wasidhurike na risasi hizo, Shigela akasema kuwa huo ni mchezo mchafu wa CHADEMA.

Kwa kauli hii ilinipa maswali mengi ya kujiuliza katika CD hii ya Shigela na mtazamo wake kuhusu Polisi na Serikali, kwani ailiingia akili kupigwa kwa Ulimboka ? na polisi kumleta mtu anayesemekana mkenya katika mazingira ya utata? iliingia akilini kuawa kwa mfuasi wa CHADEMA pale Igunga? iliingia akilini mauaji yaliyofanywa na Zombe? ilingia akilini kwa kupigwa kwa wabunge wa CHADEMA pale Mwanza? ilingia akilini kupigwa na kuawa kwa raia pale Songea waliokuwa wakienda kutaka kauli ya mkuu wa wilaya ? iliingia akilini kwa mauaji yaliyofanywa kule Arumeru.

Kwa mujibu wa SHIGELA ni mauaji ya Morogoro tuu ambayo hayaingii akilini na hivyo jibu rahisi kama mauaji hayaingii akilini mwa SHIGELA muhusika ni CHADEMA. Kwa kauli ile inadhihirisha kuwa mauaji yaliyopita yaliingia akilini mwa SHIGELA.

Na mimi nilimsikiliza, hapo kwenye red inaonyesha kuwa kwa mawazo yake polisi wangewaua kwanza magwandwa kwa sababu ndio wana hasira nao. kwa hiyo anatetea kuwa huyo aliyeuawa, itakuwa si polisi walihusika.
labda shigela atueleze; CDM walikuwa na silaha wakati wanaandamana? maana marehemu aliuawa kwa risasi, nani waliokuwa na risasi kati ya CDM na polisi?
 
na hivi unde RPC wa Morogoro ametangaza kuwa matokeo ya post mortem yanaonyesha kuwa kijana alifariki kutokana na kupigwana kitu kizito kichwani na sio risasi
 
hili lijamaa na limustach lake huwa linlopoka tu, eti kijana kijana gani sura limemkomaa na limustach kama kambale?
 
Ina maana polisi wapo kuuwa wenye magwanda tu? Hawa viongozi ndio anaowasema lowasa.
 
Na mimi nilimsikiliza, hapo kwenye red inaonyesha kuwa kwa mawazo yake polisi wangewaua kwanza magwandwa kwa sababu ndio wana hasira nao. kwa hiyo anatetea kuwa huyo aliyeuawa, itakuwa si polisi walihusika.
labda shigela atueleze; CDM walikuwa na silaha wakati wanaandamana? maana marehemu aliuawa kwa risasi, nani waliokuwa na risasi kati ya CDM na polisi?

Unajua mimi nilivyomuelewa Shigela ni kwamba yeye na uzezeta wake anajaribu kuaminisha watu kuwa ni mwana CDM ndiye alifanya mauaji yale ili tu CDM isingizie serikali kuwa inaonewa kwa watu wake kuuliwa hovyo, sitaona ajabu yoyote hapo Polisi Morogoro watakapokuja na mtuhumiwa (huenda akawa ni mwana CDM) anayefanana na Mtuhumiwa wa Ulimboka, najaribu kwenda nje ya Box na kufikiri kuwa kuna mpango mahususi ndani ya serikali ya kuua watu kadhaa ili kuinusuru image ya CCM kwa kuelezea watanzania kuwa Chadema ni watu wa fujo na wauaji, WHY?

Hebu tuangalie nyuma tukianzia na Arusha, Igunga, Mwanza, Arumeru etc, mauaji hayakomi, watuhumiwa wa mauaji hawajakamatwa Wala kufunguliwa file la uchunguzi, Bungeni akina Mnyika wakitaka kuulizia wanaambiwa kesi ipo mahakamani, Hata hii ya Morogoro wataweka mshitakiwa feki chap chap ili lisiongelewe ktk Bunge linalokuja, Ni kitu cha ajabu kidogo pale mkuu wa Polisi Morogoro anaposhindwa kuelezea straight kuwa deceased aliuwawa na Bullet wound, kwanini hakupenda kusema vile wakati hata sie tulioona picha tu tulilitambua hilo?

Kwanini apige chenga wakati ni Obvious hata kwa mwananzengo wa Dutwa kule Bariadi angeweza kusema kuwa donda ni la risasi? Bado naamini 99% kuwa kijana yule ametumika kama Guinea pig wa propaganda za CCM same like mauaji ya Ndago - Iramba yaliyofanywa na vijana waliopelekwa kule na hayawani mmoja wa huko huko. Msisahau kuwa Igunga walimwagia mtu wao Acid kwa malengo yaleyale na hii sasa wanatumia mbinu zilezile kwa lengo lilelile....
 
The people have nowhere to run to, all opposition parties are weak except perhaps the Chadema, which seeks to maintain the status quo as far as income gap is concerned. The CCM is looting the country. Then this calls for a street uprising. Rise Tanzanian, Rise! Let's stand up to these thieves! It's now or never.
 
Back
Top Bottom