RPC Morogoro akana polisi kutumia risasi za moto

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,371
Katika hatua ya kushangaza, RPC wa Morogoro amekana askari wake kutumia silaha za moto wakati wa kuzima maandamano ya chadema yaliyofanyika mkoani Morogoro leo.Alisisitiza polisi kupiga mabomu ya machozi tu.

Source:Mahojiana ya kamanda huyo na kituo cha TV cha chanel ten wakati wa taarifa ya habari ya saa moja usiku huu.
 
Kwa mujibu wa mwandishi wa BBC Eric Nampesya,RPC wa moro bw Shilogile kaeleza kuwa wao wametumia mabomu ya machozi na si silaha za moto hivyo wanafanya uchunguzi wa kifo cha bw ally mfuasi wa chadema.NIMEKUMBUKA MANENO YA DR SLAA JUU YA HUJUMA YA KUBAMBIKWA MATUMIZI YA SILAHA KUHUJUMU M4C MORO.
 
So anazungumziaje kijana Ally aliyekufa kwa kupigwa risasi ya moto? au risasi imetoka kwa silaha ya wana cdm
 
Wanafanya uchunguzi kuona risasi ilitoka ktk SMG(bunduki zimilikiwazo na polisi) ama labda ni bastola inayoweza kuwa ya mtu mwingine?
 
Sheria ichukue mkondo wake. Hata kama haki itapatikana 2015 tujue wote wanachukuliwa hatua. Akiwemo mkuu wa polisi
 
Bomu analijua yeye,ssi tunajua yeye anafanya nini na askari wake wamefanya nini. Iwe bomu au risasi tunajua wameamua kuua
 
Wana JF

Nimesikiliza sauti ya RPC wa Morogoro akiongea na Times FM sasa hivi anasema polisi haijatumia risasi hata moja Morogoro na badala yake wametumia mabomu ya machozi tu na kwamba hata aliyefariki leo hawezi kusema kapigwa na risasi maana huenda amefariki kutokana na jeraha la BOMU LA MACHOZI.

Nimepigwa na Butwaa na kauli hii ya RPC.
 
Labda ndo walitumia zile silaha zao za manjiro ili ionekane sio polisi. Du akili ka za kuku!!
 
Aache usanii wake,yeye ajiandae ipo siku atapelekwa The Hague,asifikiri CCM itakuepo kumtetea. Mpanda ngazi hushuka!
 
upuuzi sana wana cheza na uhai wa mtu? Wanaleta usanii kwenye maisha ya watu damu ya ally itakwenda nao
 
Yaani kweli unaweza kuwaambia wananchi kitu kama hiki kweli? RPC? Kweli. Sasa inatosha.
 
hayo mabomu ukiligwa nalo nina kuua maana nakumbuka hapa arusha lilivunja dirisha na kuchoma vitu vilivyokuwemo huko lakini cha ajabu tuliambiwa chadema ndiyo tumechoma..
 
hakika polisi wetu ni waongo sana........polisi wa tanzania kila kukicha wanaua wananchi kwa risasi
 
Wana JF

Nimesikiliza sauti ya RPC wa Morogoro akiongea na Times FM sasa hivi anasema polisi haijatumia risasi hata moja Morogoro na badala yake wametumia mabomu ya machozi tu na kwamba hata aliyefariki leo hawezi kusema kapigwa na risasi maana huenda amefariki kutokana na jeraha la BOMU LA MACHOZI.

Nimepigwa na Butwaa na kauli hii ya RPC.

YES! Maafande wamenunuliwa, ulitegemea ajibu nn? Akili ndogo unatawala akili....... Asante mungu cjawahi kuwaamini polisi, pathetic force
 
kwani mabomu ya machozh yanaua. Kwanini asiende kukagua mwili wa marehemu ili ajiridhishe kama ni bom au risasi.?
 
Hivi nchi hii tunaelekea wapi hivi inaposemekana polisi hawajasoma ndo hivi? mtu ameuawa kwa risasi yeye anakana hivi hata kama akili zako ni ndogo ndo zinakuwa ndogo kupitiliza. Mungu atawahukumu wote mliotenda udhalimu huu na wote waliowatuma na wanaoshabikia uhovu huu.
 
Back
Top Bottom