Rostam nusura ajiumbue

Nakuhakikishia siyo King Maker, he is not learned, but bright and smart, anza kuamka wewe, mwamshe baba na mama ili waamshe chama uone moto utakao waka humo ndani. Jamaa ni habari nyingine, kama Mkulu anabow down kwa huyu jamaa, naamini unakokwenda one day, you will too.

- Labda mkuu ungewasaidia kuwaamsha baba na mama yako kwanza,halafu ukajisaidia na wewe mwenyewe kabla ya kuwekeza kwenye kampuni ya Mwakyembe ili kushindana na huyu Kingmaker wako, si umeona mlivyoadhirika na unavyolalama kila kona!

Respect!

Wazee wa sauti ya umeme FMES!
 
Nakuhakikishia siyo King Maker, he is not learned, but bright and smart, anza kuamka wewe, mwamshe baba na mama ili waamshe chama uone moto utakao waka humo ndani. Jamaa ni habari nyingine, kama Mkulu anabow down kwa huyu jamaa, naamini unakokwenda one day, you will too.

Maneno mazito sana haya Mkuu nami nayaafiki kabisa.
 
Hili Riburushi kwa nini mnalionea aibu jamani?
Mnataka atutawale hadi kwenye familia zetu?Jamani inauma sana mi ngoja niende kwa bibi Swanga nampiga na kombora kali afie mbali atatunyanyasa mpaka lini?Kama mmeshindwa mi namloga.

Hili si Burushi ni Bamasinde toka Uajemi(Iran), maburushi yanatoka Baruchiland kule Pakistan. Limewanywa akili wanaCCM karibu wote sasa linatuburuza WaTAnzania wote.

Hivi Risasi moja ya AK47 ni Tshs ngapi huko Tanzania?
Hapa USA ni$1.00 tu ambayo ukienda hapo kwenye FastFood ya karibu hata French Fries ndogo hupati
 
Maneno mazito sana haya Mkuu nami nayaafiki kabisa.

- Hapana, humsaidii wala kumkomoi anybody, soon utakuja kugundua the truth kwamba kuna somebody aliyewekeza kwenye kampuni ya Mwakyembe, halafu huyo huyo akakimbilia kwa Nchimbi, kumpa info sasa guess what Nchimbi akazifikisha kwa Rostam, matokeo yake zikatoka gazeti la Mtanzania, na sasa shujaa wetu Mwakyembe amepunguzwa nguvu, na ndio maana ya maneno unayoyaita mazito, Bwa! ha! ha! ha! in the end ni sisi wananchi ndio tutalipia Maneno mazito sana.

Respect!

FMES
 
1.
Shisye nakuheshimu, naomba tuheshimiane, kwa vile hunijui, sikujui, our common denominator ni jamii forums, hizo interest zangu binafsi hapa ni zipi? Anipigie mimi simu kama nani?.

2.
Pasco:

Nakuhakikishia siyo King Maker, he is not learned, but bright and smart, anza kuamka wewe, mwamshe baba na mama ili waamshe chama uone moto utakao waka humo ndani. Jamaa ni habari nyingine, kama Mkulu anabow down kwa huyu jamaa, naamini unakokwenda one day, you will too.

- Very interesting, yaani kumbe unafahamu maana ya neno kuheshimiana, na kutojuana, pole sana mkuu!

William.
 
- Hapana, humsaidii wala kumkomoi anybody, soon utakuja kugundua the truth kwamba kuna somebody aliyewekeza kwenye kampuni ya Mwakyembe, halafu huyo huyo akakimbilia kwa Nchimbi, kumpa info sasa guess what Nchimbi akazifikisha kwa Rostam, matokeo yake zikatoka gazeti la Mtanzania, na sasa shujaa wetu Mwakyembe amepunguzwa nguvu, na ndio maana ya maneno unayoyaita mazito, Bwa! ha! ha! ha! in the end ni sisi wananchi ndio tutalipia Maneno mazito sana.

Respect!

FMES

Sichangii huu mjadala kwa nia ya kumtetea yeyote yule bali kutetea maslahi ya Tanzania na Watanzania. Hakuna ushahidi wowote wa Mwakyembe kuhusika na ufisadi dhidi ya Watanzania. Kuwa na share za thamani ya shilingi millioni 1 kwenye kampuni ambayo haijulikani lini itaanza usambazaji umeme kamwe siwezi kuuita huo kama ni ufisadi. Lakini kwa upande wa fisadi Rostam kishatufisadi Watanzania shilingi bilioni 240 (Kagoda 40 billioni na Richmond/Dowans bilioni 200) na juzi karibu ifikie bilioni 300 kama siyo Watanzania kusimama kidete kupinga ununuzi wa mitambo iliyochoka. Hilo la Mwakyembe kupunguzwa nguvu utalijua wewe na sijui huyo aliyempunguza nguvu ni nani na kafanya hivyo kwa faida ya Watanzania au ya mafisadi!!!mimi natetea maslahi ya Tanzania na Watanzania
 
Sichangii huu mjadala kwa nia ya kumtetea yeyote yule bali kutetea maslahi ya Tanzania na Watanzania. Hakuna ushahidi wowote wa Mwakyembe kuhusika na ufisadi dhidi ya Watanzania. Kuwa na share za thamani ya shilingi millioni 1 kwenye kampuni ambayo haijulikani lini itaanza usambazaji umeme kamwe siwezi kuuita huo kama ni ufisadi. Lakini kwa upande wa fisadi Rostam kishatufisadi Watanzania shilingi bilioni 240 (Kagoda 40 billioni na Richmond/Dowans bilioni 200) na juzi karibu ifikie bilioni 300 kama siyo Watanzania kusimama kidete kupinga ununuzi wa mitambo iliyochoka. Hilo la Mwakyembe kupunguzwa nguvu utalijua wewe na sijui huyo aliyempunguza nguvu ni nani na kafanya hivyo kwa faida ya Watanzania au ya mafisadi!!!mimi natetea maslahi ya Tanzania na Watanzania

- Anyways, ni maoni yako, ila ya kwangu ni kwamba Mwakyembe will never be the same, ile moral authority aliyokuwa akiongea nayo before haya hayajafichuliwa hatakuja kuwa nayo tena, hiyo ni political fact na hata yeye mwenyewe anajua hilo, sasa kilichoguswa hapo ni masilahi hasa ya taifa kwani waliomchokonoa unafikiri ni wajinga?

- I respect the man na ninaamini kwamba sio fisadi na hakufanya kwa nia mbaya, lakini mbele ya jamii jina limepungua nguvu na hasa katika vita vya mafisadi, huwezi kupigana navyo huku ukiwa na hata harufu tu ya mis-appropriate, tulioumia ni taifa sio anybody na ndio maana hasa ya masilahi ya taifa, ingawa na wewe una the way ya kuyaona masilahi ya taifa, ila kwangu mimi masilahi ya taifa yameguswa kutokana na kumpunguza nguvu Mwakyembe, maneno ya kwamba yeye na Rostam originally walitaka kuanzisha kampuni moja, lakini Rostam akakataa kuwekeza hela zake, ndio kila mmoja akaamua kuanzisha kampuni yake na sasa wanagombea uwanja wa umeme Singida, huwezi kusema kwamba politically sio damaging kwa jina la DK, tena yanapotokea Chadema.

- The damage is done, na sasa watakaolipia ni sisi taifa, yaani wananchi na hilo ndio hasa lilokuwa the goal ya mafisadi, that is how I see it lakini na wewe unaweza kuona tofauti ndio demokrasia at work.

Respect.

FMES
 
Maneno mazito sana haya Mkuu nami nayaafiki kabisa.

Asante BAK, ni kweli ni mazito na sio mazito tuu, bali pia yanaumiza. Ukweli unauma. Yaliyomuingia yamemuumiza lakini ukweli umemfikia hata kama ni ukweli mchungu. The King Maker was once the sweeter. CCM kwa kupenda vitamu, wakakamia vitamu. Then he turned bitter, they are left with no option 'to take the bitter with the sweet' na 2010, vitamu hivyo vitawatokea puani kwenye baadhi ya majimbo.
Kwa vile CCM wanamkumbatia sasa, mimi naamini, hata makuwadi opportunist wa CCM, ambao 2010 watajitupa kusaka ulaji, watajikuta lazima wamnyenyekee, hata kama humu kwenye JF wanajifanya wanauchukia sana ufisadi kwa kauli nzito huku kimoyomoyo wanatamani kufika juu nao wakajilie.

Kwenye thread moja nyuma niliwahi kukiri kuwa sio kila aliyeandikwa fisadi ni fisadi, na sio kila fisadi, ni fisadi mbaya, kuna mafisadi mwema kama alivyo baniani mbaya, kiatu chake dawa.

Lakini pia kuna wanao onekana sio mafisadi kumbe ni mafisadi tena hawa ndio mafisadi waovu kuliko wale wa epa maana wanafisidi from within katika mtindo wa kikulacho.

As 2010 is just around the corner, lets be patience, tutasikia mengi na tutaona mengi. Siye wengine yetu macho na masikio.
 
Sasa kidogo na mimi ndio naanza kupata picha ya ugomvi wa King Maker na Dr. Harry. issue siyo conflict of interest ni conflict ya kimaslahi. wote wanamiliki kampuni za kufua umeme majina karbu yafanane. mmoja ana eneo hana mkataba. mmoja ana mkataba hana eneo.
kwa maoni yangu, wote ni mafisadi.


Da hii kali.

Kwa hiyo mtu akiwa na mkataba hana eneo, au ana eneo hana mkataba, then, ..kwa mujibu wa JF pundit, ana qualify kuwa fisadi!!

Hapa inabidi tuanze kufanya juhudi ya kujuzana kiswahili sasa..duh!

Kaazi kwelikweli
 
Da hii kali.

Kwa hiyo mtu akiwa na mkataba hana eneo, au ana eneo hana mkataba, then, ..kwa mujibu wa JF pundit, ana qualify kuwa fisadi!!

Hapa inabidi tuanze kufanya juhudi ya kujuzana kiswahili sasa..duh!

Kaazi kwelikweli

Heshima mbele,
Nimewaita wote mafisadi only in this particular case. Mwenye mkataba, ameweza kupata mkataba baada ya kuwahakikishia Tanesco kuwa analo eneo, kumbe hana!.
Mwenye eneo, amefanya 'inside trading' kwa kujua ukipata eneo, unapata mkataba, hivyo akakimbia kimbilia kuanzisha kampuni ya wazalendo na kukimbilia kutafuta eneo, na akapata, katika safari ya kufuatilia mkataba, ndipo aliposhangaa mkataba kapewa mwenye eneo.

Cha muhimu kwa mwananchi ni umeme wa uhakika, cha muhimu kwa mfanya biashara ni mkataba, kupata eneo,
Fweza itaongea. Na mwenye eneo asiye na mkataba afanyenye?. Dawa ni kupiga kelele for public sympathy.
Hicho kilio cha public sympathy sio ili wananchi wapate umeme, bali uwezekano wa kukosa ulaji. Ndio maana conclusion yangu, wote mafisadi.
 
Heshima mbele,
Nimewaita wote mafisadi only in this particular case. Mwenye mkataba, ameweza kupata mkataba baada ya kuwahakikishia Tanesco kuwa analo eneo, kumbe hana!.
Mwenye eneo, amefanya 'inside trading' kwa kujua ukipata eneo, unapata mkataba, hivyo akakimbia kimbilia kuanzisha kampuni ya wazalendo na kukimbilia kutafuta eneo, na akapata, katika safari ya kufuatilia mkataba, ndipo aliposhangaa mkataba kapewa mwenye eneo.

Cha muhimu kwa mwananchi ni umeme wa uhakika, cha muhimu kwa mfanya biashara ni mkataba, kupata eneo,
Fweza itaongea. Na mwenye eneo asiye na mkataba afanyenye?. Dawa ni kupiga kelele for public sympathy.
Hicho kilio cha public sympathy sio ili wananchi wapate umeme, bali uwezekano wa kukosa ulaji. Ndio maana conclusion yangu, wote mafisadi.

Ukweli mbele,

Bado hoja yangu ipo palepale. Haijalishi nani ana mkataba au ana eneo au vyote viwili ( as I don't have a good background kuhusu contracts za huu mradi wa umeme wa nguvu za upepo), kinachonisumbua mimi ni kuhusu mitambo ya DOWANS na ni yupi baina ya hawa mabwana mwenye ka-historia ka ku-screw fedha za wavujajasho. Mradi huo wa Singida, wala haujaanza, na hata kama ni uwizi au ufisadi unawezaje kumkamata mtu kabla hajaiba?

Vilevile Dr. Harry, kama ulivyopenda kumwita, ameamua kumbana 'fisadi mwenzake' asitutie ktk hasara nyengine kwenye DOWANS, hili kwangu ni jambo la kheri, na sidhani kama hiyo nayo inaingizwa kwenye kapu la ufisadi.
 
Ukweli mbele,

Bado hoja yangu ipo palepale. Haijalishi nani ana mkataba au ana eneo au vyote viwili ( as I don't have a good background kuhusu contracts za huu mradi wa umeme wa nguvu za upepo), kinachonisumbua mimi ni kuhusu mitambo ya DOWANS na ni yupi baina ya hawa mabwana mwenye ka-historia ka ku-screw fedha za wavujajasho. Mradi huo wa Singida, wala haujaanza, na hata kama ni uwizi au ufisadi unawezaje kumkamata mtu kabla hajaiba?

Vilevile Dr. Harry, kama ulivyopenda kumwita, ameamua kumbana 'fisadi mwenzake' asitutie ktk hasara nyengine kwenye DOWANS, hili kwangu ni jambo la kheri, na sidhani kama hiyo nayo inaingizwa kwenye kapu la ufisadi.
Nakubaliana na wewe, 'between the two devils, choose the lesser' kwa vile ya dowans sasa ni wimbo, naomba nisiendeleze kuuimba utapanda chart mpaka utahit.
Pia nazidi kuitetea ile hoja, kuwa fisadi siyo fisadi tuu, kuna fisadi mwema, huyu anauma huku anapulizia, kama CCM walipokea msaada wa mabilioni ya fisadi kufanyia kampeni, wao CCM hawana kosa na kwao huyo ni fisadi mwema kama alivyo kwa wananchi wa Igunga ambao kila kilio chao kinasikilizwa kwa kuingiza mkono mfukoni na kugawa masalia ya mafao ya Epa na Dowans.

Pia naunga mkono vitendo vyovyote vya ufisadi wenye lengo jema la kumkomboa mwananchi huku pia ukichumia tumbo lako.

Nimeisoma kwa makini falsafa ya Ujamaa wa Mwalimu ya binadamu wote ni sawa na nia yake ya dhati kwenye Azimio la Arusha.
Pia nimelisoma Azimio la Zanzibar kuhusu viongozi kumiliki mali ambalo linaendana na hali halisi ya tulipo sasa kwenye uchumi wa soko. Kwa lugha nyingine ni ubepari.

Pia naungana na Mwalimu kuwa 'Ubepari ni Unyama' kwangu ubepari ni ufisadi kwa kuwanyonya wengine ili mmoja anehemeke. Kwa tafsiri yangu, Mabepari wote ni mafisadi ndio maana nilishaangaa mpiga debe mkuu dhidi ya ufisadi wa Richmond ni kuwadi wa ufisadi tarajiwa wa powerpool!.
Namalizia kuwa sina chuki na mafisadi na utajiri wao, bali nawaheshimu wajamaa wa kweli na umasikini wao japo binafsi si mmoja wao maana mimi niko kwenye lile kundi la wengi la 'ukikipata, kitumie' kwa kutumia falsafa ya 'The end justifies the means'.
 
- Anyways, ni maoni yako, ila ya kwangu ni kwamba Mwakyembe will never be the same, ile moral authority aliyokuwa akiongea nayo before haya hayajafichuliwa hatakuja kuwa nayo tena, hiyo ni political fact na hata yeye mwenyewe anajua hilo, sasa kilichoguswa hapo ni masilahi hasa ya taifa kwani waliomchokonoa unafikiri ni wajinga?

Kwa mafisadi Mwakyembe will never be the same kwa sababu kawaanika hadharanimna wengine wakamwaga unga tena wa kazi za juu sana katika nchi yetu hadharani ndiyo maana wanafanya kila jitihada kutaka kumchafua lakini hadi hii leo sijaona chochote kile kinachoonyesha kwamba Mwakyembe naye ni fisadi. Kumbuka fisadi Edwards Hosea Mkuu wa PCCB na Mwanasheria Mkuu wa serikali walipewa kazi ya kuchunguza mkataba wa Richmond kabla ya Mwakyembe na timu yake. Wakaja na ripoti iliyojaa uwongo wa hali ya juu kwamba mkataba wa Richmond haukuwa na ufisadi wowote bali kulikuwa na kasoro ndogo ndogo za kiutendaji. Watanzania tukaikataa ripoti ile na ndiyo kuundwa tume ya Mwakyembe ambayo iligundua ufisadi wa fisadi Rostam kulipwa bilioni 200 yena kwa kutumia uwongo wa hali ya juu kwamba kampuni yake HQ yake ipo Houston, Texas na wana uzoefu mkubwa wa kuzalisha umeme. Kumbe ilikuwa ni kanyabwoya tu ya kutufisadi Watanzania. Yaliyofuatia baada ya ripoti hiyo wote tunayajua na sina haja ya kuyarudia.


- - I respect the man na ninaamini kwamba sio fisadi na hakufanya kwa nia mbaya, lakini mbele ya jamii jina limepungua nguvu na hasa katika vita vya mafisadi, huwezi kupigana navyo huku ukiwa na hata harufu tu ya mis-appropriate, tulioumia ni taifa sio anybody na ndio maana hasa ya masilahi ya taifa, ingawa na wewe una the way ya kuyaona masilahi ya taifa, ila kwangu mimi masilahi ya taifa yameguswa kutokana na kumpunguza nguvu Mwakyembe, maneno ya kwamba yeye na Rostam originally walitaka kuanzisha kampuni moja, lakini Rostam akakataa kuwekeza hela zake, ndio kila mmoja akaamua kuanzisha kampuni yake na sasa wanagombea uwanja wa umeme Singida, huwezi kusema kwamba politically sio damaging kwa jina la DK, tena yanapotokea Chadema.

Nimekuuliza Mwakyembe kapunguzwa nguvu na nani? Kivipi? Na je kupunguzwa nguvu kwa Mwakyembe ni kwa maslahi ya Taifa au ya Mafisadi? Kivipi? Tafadhali fafanua.

Mpaka sasa hivi hatujaona ushahidi wowote unaonyesha kwamba Mwakyembe alitaka kufungua kampuni pamoja fisadi Rostam. Pia kutaka kufungua kampuni na mtu hakuonyeshi kama ni ufisadi kwa sababu kwanza hatujui ni mwaka upi walitaka kufungua kampuni hiyo pamoja. Labda wakati huo ufisadi wa Rostam ulikuwa bado haujajulikana kama ilivyo sasa. Kumbuka miaka michache tu iliyopita fisadi Rostam alikuwa anakaa meza moja na akina Mkapa na Kikwete kupanga mikakati mizito ya chama cha mafisadi ikiwemo ya uchaguzi. Mpaka hapo tutakapopata ushahidi unaojitosheleza kuhusu nia ya Mwakyembe kutaka kufungua kampuni na fisadi Rostam hizi zitakuwa ni hearsay tu za kutaka kumpaka matope kiboko ya mafisadi.


- - The damage is done, na sasa watakaolipia ni sisi taifa, yaani wananchi na hilo ndio hasa lilokuwa the goal ya mafisadi, that is how I see it lakini na wewe unaweza kuona tofauti ndio demokrasia at work.

Respect.

FMES

Kwangu mimi bado Mwakyembe kwa wengi wetu ambao hatujaona ushahidi wa kutosha ni mtu safi ambaye ameweka mbele maslahi ya Taifa ukilinganisha na fisadi Rostam, Mkuu wa PCCB na Mwanasherai Mkuu walioandika ripoti ya uongo kwamba katika mkataba wa Richmond hakukuwa na ufisadi wowote bali ni kasoro ndogo ndogo za kiutendaji. Mtu kuingia na Serikali mkataba kwa kutumia info za uwongo na kulipwa shilingi bilioni 200 halafu hakuzalisha hata tone ya umeme. Juu ya hayo Wataalamu wa TANESCO waliishaur serikali kutoingia mkataba na kampuni hiyo maana kuna vitu vingi vya kuthibitisha utaalamu wao vilikuwa vinakosekana. Kwa mafisadi ni kweli Mwakyembe is damege goods, lakini kwa Watanzania wengi tunaotetea maslahi ya nchi bado tunamuona ni shujaa kwa kuanika uozo chungu nzima kuhusiana na mkataba wa Richmond/Dowans ambao kamwe tusingeyajua yaliyojiri kama siyo ujasiri wa Mwakyembe na kamati yake maana na wao wangeweza kuandika the same report kama iliyoandikwa na Edwards Hosea na Mwanasheria Mkuu wa serikali lakini wakaweka maslahi ya nchi mbele na kuamua kufanya kweli. Hapa chini nimekuwekea ushahidi zaidi wa mabilioni ambayo fisadi Rostam hajayarudisha kama alivyotakiwa, kama akishindwa kuyarudisha basi tutaishinikiza serikali kwamba mitambo ile michakavu ni halali yetu hivyo itaifishwe

Have a lovely and enjoyable Weekend :)


~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~

Siri ya wizi mkubwa Richmond

Mwandishi Wetu Januari 28, 2009

Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo
Watimka na mabilioni ya walipa kodi

Walichotewa kabla hata ya kazi

WAKATI Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akisubiriwa na wabunge kuwasilisha taarifa ya Serikali kuhusu utekelezaji wa mapendekezo ya Bunge kuhusu kampuni ya Richmond Development, kampuni hiyo iliyorithiwa na kampuni ya Dowans, ilitokomea na zaidi ya Sh. bilioni 23, Raia Mwema imebaini.

Kinyume cha maelezo yaliyowahi kutolewa na baadhi ya viongozi wakuu serikalini katika Bunge, kwamba Richmond haikuwahi kupewa fedha za Serikali, ukweli ni kwamba kampuni hiyo ilichotewa zaidi ya Sh. bilioni 30 (Dola 30,696,598 za Marekani).

Kiasi hicho ni sawa na asilimia 35 ya gharama ya kodi ambayo msingi wake ulikuwa kufanikisha mchakato wa ufunguaji wa hati ya muamana (letter of credit) kati ya kampuni hiyo na Benki ya Biashara.

Malipo hayo ya asilimia 35 ni utekelezaji wa makubalino yaliyofikiwa awali, kati ya Serikali na wawakilishi wa kampuni ya Richmond Development.

Uchunguzi wa Raia Mwema umebaini kuwa baada ya kupewa kitita hicho cha zaidi ya Sh bilioni 30, Richmond ilipewa masharti ya kurejesha fedha hizo serikalini katika malipo ambayo yangefanyika kwa awamu tatu.

Hesabu zilizofanywa ni kwamba Richmond ilitakiwa kurejesha serikalini dola 1,279,044 za Marekani (zaidi ya Sh bilioni 1.3), kila mwezi, lakini katika mikupuo (awamu) mitatu.

Hesabu hizo zinabainisha kuwa kama makubaliano hayo yangefanyika bila ukorofi au kasoro yoyote, Richmond ingefanikiwa kurejesha serikalini fedha ilizopewa katika miaka miwili. Kwa tafsiri nyingine ni kwamba, Richmond ingelipa deni hilo serikalini ndani ya muda wa uhai wa mkataba wake na Serikali, ambao ni miaka miwili.

Lakini uchunguzi zaidi wa Raia Mwema umebaini kuwa malipo ya awali yalipaswa kuanza kufanyika Novemba, mwaka 2007. Hata hivyo, kutokana na utata wa kampuni ya Richmond hasa kwa upande wa uwezo wake kiteknolojia na utendaji, kampuni hiyo iliuza shughuli zake kwa kampuni nyingine binafsi ya Dowans.

Imebainika kuwa wakati mchakato wa uuzaji wa shughuli za kampuni hiyo kwa Dowans unafanyika, Richmond ilikuwa haijarejesha fedha ilizopewa na Serikali na kwa kuwa Dowans ndiyo iliyobeba mikoba, ilipaswa kuendeleza urejeshaji huo wa fedha.

Kutokana na hali hiyo ya fedha za Serikali kubaki kwa 'wawekezaji' hao waliopasiana mpira wa uwajibikaji, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kupitia timu ya watalaamu wa sheria, ilichunguza mkataba kati yake na Richmond ambao ulirithiwa na Dowans.

Taarifa ya timu ya wanasheria wa TANESCO ilibaini kuwa mkataba huo hauna nguvu za kisheria na kuamuru uvunjwe. Mkataba ukavunjwa rasmi Agosti mosi, mwaka 2008.

Hata hivyo, wakati mkataba huo unavunjwa uchunguzi wa Raia Mwema umebaini kuwa fedha zilizopaswa kurejeshwa Serikali hazikuwa zimerejeshwa zote.

Imebainika kuwa fedha zilizorejeshwa hadi mkataba unavunjwa ni jumla ya dola 7,674,186 za Marekani (zaidi ya Sh bilioni 7.7), huku dola za Marekani 23,022,412 (zaidi ya Sh. bilioni 23) zikibakia kwa Richmond na mrithi wake Dowans.

Taarifa zaidi za kiuchunguzi zinaeleza kuwa kutokana na hali hiyo Bodi ya TANESCO pamoja na uongozi wa shirika hilo umekwisha kuchukua hatua.

Hizo ni pamoja na maagizo ya Bodi ya TANESCO kwa uongozi wa shirika hilo kuchukua hatua zinazostahili kuhusu deni hilo na kutokana na maagizo hayo, uongozi wa TANESCO ulilazimika kutoa taarifa rasmi serikalini ili hatimaye ijulikane namna fedha hizo zitakavyorejeshwa.

Uchunguzi zaidi umebaini kuwa ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imechunguza mchakato huo na kubaini kuwa Serikali ilitoa fedha hizo kwa Richmond.

Ofisi hiyo ya CAG, katika taarifa yake ya ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka ulioishia Desemba 31, mwaka 2007, imeweka bayana kuwa fedha hizo bado hazijarejeshwa serikalini.

"Tunafahamu kutokana na taarifa za uongozi kwamba mkataba kati ya TANESCO na Dowans ulivunjwa Agosti mosi, 2008. Matokeo yake ni kwamba kiasi cha fedha kilichotolewa na kutakiwa kurejeshwa kinaweza kuwa hasara kwa TANESCO au Serikali," inaeleza sehemu ya waraka rasmi wa ofisi ya CAG kwa serikali ambao Raia Mwema imeuona.

Kampuni ya Richmond Development ilipewa zabuni tata na Serikali kuagiza mitambo ili kuzalisha umeme wa dharura nchini.

Aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa
Kutokana na utata wa zabuni hiyo, Bunge lililazimika kuunda Kamati Teule kuchunguza na kubaini upungufu ambao hatimaye ulimgharimu aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na mawaziri Nazir Karamagi na Dk. Ibharim Msabaha waliojiuzulu Februari 2008.

Mbali na viongozi hao kujiuzulu, Kamati ya Bunge iliwasilisha mapendekezo 23 yanayohitaji kufanyiwa kazi na Serikali. Mapendekezo hayo ni pamoja na kuwawajibisha baadhi ya watendaji wa Serikali na baadhi ya vyombo nyeti, akiwamo Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Dk. Edward Hosea pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika.

Katika mkutano wa Bunge ulioanza wiki hii, Serikali inatarajiwa kuwasilisha taarifa yake kuhusu utekelezaji wa mapendekezo hayo. Taarifa hiyo inatarajiwa kuwasilishwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

 
Na Alfred Lucas

Mwanahalisi~Maslahi ya taifa Mbele

MFANYABIASHARA na mbunge wa Igunga, Rostam Aziz amesitisha uchapishaji magazetini wa taarifa yake ya kukana tuhuma za ufisadi.

Taarifa iliyokuwa inakwenda kwa njia ya tangazo, ilikuwa inakana kuhusika kwake na kampuni ya kufua umeme kwa njia ya upepo ya Wind East Africa Limited.

Kampuni hii inatuhumiwa kupora ardhi ya wananchi katika kijiji cha Kisasida, mkoani Singida na taarifa zinasema tayari watu wameanza kuhamishwa kwa nguvu kama inavyofanywa kwenye maeneo yenye migodi ya madini mbalimbali.

Taarifa zinasema uhamishaji watu kwa nguvu unafanywa kwa msaada wa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Parseko Kone.

Hata hivyo, madai hayo yamekanushwa vikali na Kone akisema, "Mimi sijaenda huko na wala si kazi yangu kuhamisha watu. Kuna watu hapa wanafanya siasa na wanadhani kwamba mimi ni kikwazo katika kufanikisha malengo yao."

Alisema, kampuni zinazodaiwa kugombea eneo awali zilikuwa kampuni moja. "Hizi kampuni awali zilikuwa moja. Zimegawanyika kutokan na sababu zao binfasi," alisema Kone katika mahojiano na gazeti hili kwa njia ya simu.

Wananchi waliohojiwa katika eneo anapotaka kujenga mradi, wamesema kampuni ya Wind East Africa Limited haijawahi kuwalipa hata senti tano kama fidia.

Tayari kampuni ya Rostam imepewa mkataba na Shirika la Umeme nchini (Tanesco) kwa njia ya upendeleo. Wameingia mkataba bila kuwa na miliki ya ardhi.

Hata hivyo, katika taarifa yake aliyositisha uchapishaji wake, Rostam anamtuhumu mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa kuwa anampakazia kwa kudai kuwa anamiliki kampuni ya Wind East Africa Limited.

Taarifa hiyo (MwanaHALISI inayo nakala), inasema anazushiwa na kwamba hahusiki na kampuni hiyo, bali imekuwa kawaida ya Dk. Slaa na washirika wake kumchafua yeye kwa kumpachika tuhuma zinazomhusisha na kampuni zilizokumbwa na kashfa za ufisadi.

Dk. Slaa anamtuhumu Rostam kuwa ni fisadi mkubwa, na kwamba ni mmiliki wa kampuni ya Kagoda Agriculture Limited iliyochota zaidi ya Sh. 40 bilioni kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Hata hivyo, Rostam hajakana kumiliki Kagoda.

Rostam pia hajakana taarifa zilizohusu andishi la wakili wa Mahakama Kuu, Bhydinka Michael Sanze kuwa aliitwa na Rostam ofisini kwake 50 Mirambo, jijini Dar es Salaam , kusaini nyaraka zilizowezesha Kagoda mabilioni kutoka BoT.

Katika andishi hilo la wakili Sanze, Rostam anatajwa kuwa ndiye kinara wa mpango wa kuchota mabilioni ya shilingi kutoka Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya BoT akitumia Kagoda.

Ni katika andishi hilo ambamo Rostam anadaiwa kuwahusisha rais mstaafu Benjamin Mkapa, katibu mkuu wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Philip Mangula na aliyekuwa Gavana wa BoT, Dk. Daud Ballali.

Wakili Sanze anaeleza kuwa Rostam, Peter Noni na Bered Malegesi walimthibitishia (yeye Sanze) kuwa Rostam alikuwa kwenye kikao ambapo Mkapa alitoa maelekezo kwa gavana Ballali kutoa fedha hizo kwa Rostam, kupitia Kagoda, kwa ajili ya shughuli za uchaguzi ndani ya CCM.

"Rostam mwenyewe alisema, ‘system yote inajua,'" anaeleza Sanze. Hata katika taarifa aliyotaka ichapishwe katika vyombo vya habari, Rostam hakukana Kagoda.


Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Karatu juzi, Dk. Slaa alisema ana uhakika kampuni ya Wind East Africa Limited ni mali ya Rostam akishirikiana na aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowassa.

"Sikiliza bwana. Hii ni kama Kagoda. Kwenye nyaraka za usajili hakuna wanapoonekana. Lakini katika baadhi ya nyaraka nilizonazo, wanaonekana wamesaini vitu mbalimbali na kutumia anuani ya kampuni ya Rostam wakati wa kusajili.

"Nawasubiri wakane. Nitawaumbua maana nimejiandaa kikamilifu. Mimi si mtu wa kukurupuka na Rostam anajua hivyo," anasema Dk. Slaa.

Anasema bado anaamini kuwa hakuna mgongano wa maslahi, isipokuwa ufisadi unaofanywa na Rostam Aziz na rafiki zake, wakisaidiwa na mkuu wa mkoa wa Singida.

Dk. Slaa anasema akina Rostam wanataka kuzalisha umeme wakati hawana eneo. "Hicho ndicho chanzo cha ugomvi wao na Dk. Mwakyembe (Harrison Mwakyembe, Mbunge wa Kyela)."

Alisema, "Nimekwenda Singida. Naufahamu vema mradi unaodaiwa. Nimeongea na wanakijiji Singida na viongozi wao. Kina Mwakyembe wanataka kuwakomboa wananchi, lakini kina Rostam wanataka kuwakandamiza.
Brother BAK long time upo salama ??
 
Back
Top Bottom