ROSTAM: Dowans ndiyo Richmond

Mzalendo Mkuu

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
735
191
Mwizi siku zake ni Arobaini. Siku zote imekuwa siri lakini hatimaye amekuja kujulikana mmiliku wa Dowans. Jambo moja la kushangaza ni kuwa kwenye gazeti la Mtanzania Rostam anasema Dowans ndiyo kampuni iliyoleta mitambo kwa haraka na kuzalisha umeme wa bei nafuu zaidi! Hapa ninashanga kwa kuwa Mitambo ililetwa na Richmond naye Rostam anasema mitambo ililetwa na Dowans. Kwake Rostam Richnomond na Dowans ni kitu kimoja? Nchi inakwenda wapi hii?
 
Inawezekana alichanganywa akili mpaka akajisahau. safi sana
 
Hivi jamani kweli Kikwete hafahamiani na Rostam Aziz?Maana juzi kauongopea uma wa watanzania kuwa hawajui dowans na wala wao dowans hawamjui yeye.NI AJABU NA KWELI LAKINI IMETOKEA HAPA TANZANIA, RAIS WA NCHI KUWAONGOPEA RAIA WAKE WAPATAO MILION 40 MCHANA KWEUPE
 
Jinsi Kikwete alivyosema hawajui Dowans, iko siku mtasikia anasema hajui kama kuna mgao wa umeme
 
Hivi jamani kweli Kikwete hafahamiani na Rostam Aziz?Maana juzi kauongopea uma wa watanzania kuwa hawajui dowans na wala wao dowans hawamjui yeye.NI AJABU NA KWELI LAKINI IMETOKEA HAPA TANZANIA, RAIS WA NCHI KUWAONGOPEA RAIA WAKE WAPATAO MILION 40 MCHANA KWEUPE
Huyo ndio mkwere tatizo la gari ni engine yeye anaenda kununua tairi mpya
 
do kumbe siku zote tunaangaika mmiliki mwenyewe yupo asante sana kwa kutujuza hilo ila iko siku mwana wa adamu atakuja kuwahukumu mafisadi
 
Ni kweli JK hawajui Dowans,ila anawajua Ricmonds,hao ndiyo walioingia mkataba na siyo Dowans hii ndiyo habari ya kubadili majia ya kampuni leo Mobitel,kesho Buzz keshokutwa TIGO au CELTEL - ZAIN - AIRTEL kumbe kampuni ni ileile,watueleze ukweli hawa wasituchanganye kwani kuna mkataba wa DOWANS au ni wa RICMONDS au kubadili majina kuficha madhambi kwa kutumia majina tofauti.Hivi TANESCO na BUNGE nani zaidi ROSTAM yuko bungeni kuchunguza udhaifu wa Bunge na serikali yake na kutafuta pa kupatia fedha huyu yupo kimaslahi zaidi.Hivi hizo Almasi anazochota huko mwadui hazimtoshi? umewahi kusikia kiwanda cha kukata almasi kilichokuwa Iringa? naamini hakipo je hizo almasi hazipo?huyu jamaa hana chembe ya uzalendo wala siamini kama ni mtazania tamaa ya namna hii kutaka wewe ndiyo uwe na fedha kuliko serikali inatisha.dawa yake ipo jikoni siku wa TZtutakapoamka lazima aziteme zote
 
Choooooonde choooonde!!!!!!! usije ukajichukulia sheria mikononi
 
baada ya jk kuiongelea dowans afu akaona wabongo hawajareact na yeye ameanza kujitangaza polepole,...nyoka anajiondoa magamba mwishowe atakuwa na ngozi mpya...huu ndo wakati wa kumshambulia huyu fisadi...alimtuma jk aongee kwanza ili hewa iwe nyepesi kidogo
 
Richmond/ Dowans ni kitu kimmoja,Sio kweli kwamba Viongozi wa juu serikalini hawajui mmiliki.Na kwanini serikali inamuogopa Dowans na kutelekeza wananchi wake?Je Dowans ni muhimu kuliko wananchi?
 
Je ni kweli Kikwete hamjui Dowans????????????? Ila anamjua Rostam Aziz ambaye alifinance kampeni zake za uchaguzi wa 2005; na akamteua kuwa Mhazini wa CCM pindi alipokuwa Mweneyekiti wa Chama hicho. Kwa Kikwete huo ndio ukweli. Rostam yeye anasema Hajutii kuhusika na DOWANS. Kikwete muda wote akiwa swahiba wa Rostam na Lowasa unafikiri atawaumbua wenzie??? Kulindana mpaka kieleweke. Si unajua sisi ndio sisi na huyo mwenzetu!!!!. Kwa Lowasa ilikuwa ajali ya Kisiasa!!!!!!!!!!!!!!!!!. Kwa Dowans hawajui. Kesho tutasikia mengi na makubwa. Nawahimiza wanaharakati wakaze buti. Waswahili husema la kuvunda halina ubani na mwenye macho haambiwi tazama. Sasa tumeona na tunajua. Tutafakari ili tuchukue hatua. Hatima ya Nchi hii imo mikononi mwetu hasa wazalendo.
 
Mwizi siku zake ni Arobaini. Siku zote imekuwa siri lakini hatimaye amekuja kujulikana mmiliku wa Dowans. Jambo moja la kushangaza ni kuwa kwenye gazeti la Mtanzania Rostam anasema Dowans ndiyo kampuni iliyoleta mitambo kwa haraka na kuzalisha umeme wa bei nafuu zaidi! Hapa ninashanga kwa kuwa Mitambo ililetwa na Richmond naye Rostam anasema mitambo ililetwa na Dowans. Kwake Rostam Richnomond na Dowans ni kitu kimoja? Nchi inakwenda wapi hii?

wamerogwa hao.

JK alisema haijui Dowans, lakini tumetumia umeme wao.
 
Back
Top Bottom