Paparazi Muwazi
JF-Expert Member
- Dec 23, 2007
- 310
- 79
- Thread starter
- #181
Naona hatimaye Waraka huu umeletwa JF. Huu ndio Waraka alioandika Balillle na kumpa Mzee Yusuph Halimoja, ndio waraka ambao Chacha Amekuwa akipita katika vyombo vya habari kutoa hoja zake akiusoma.
Katika waraka huu mtaona ule mkakati niliowadokeza wa kumweka Mbowe mwenyewe kikaangaoni, hii ilikuwa ni baada ya mkakati wa mwanzo wa kumng'oa kwanza Dr Slaa kushindwa.
Katika waraka huu Kamati ya Mziray imetajwa, mtakumbuka niliwaeleza siku za nyuma kuhusu hili. Hii ndio njia mpya ya Wagawe, Uwatawale inayoendelea.
Na katika taarifa hii Balille anafanya spinning sasa kuwa ripoti hii iliminywa toka mwezi Disiemba kumbe ukweli ni kuwa ni Mwenyekiti wa Kamati Bwana Mziray ndiye ambaye katika vikao vyote vya kamati kuu vilivyofuata hakutaka kuleta ripoti yake mpaka Mkakati na Rostam wa kumtoa Dr Slaa Dodoma Juni 28 akaipeleka ripoti hiyo Dodoma siku moja kabla ya kikao ili ripoti hiyo isipitie kwenye sekretariati kama zilivyo nyaraka nyingine za kamati kuu.
Kabla ya kuipeleka ripoti hiyo Dodoma alishatoa ripoti hiyo kwa Rostam, Kaborou, Ballile na Halimoja. Ndipo Kaborou akamsaidia Chacha kuandika waraka wa kumpinga katibu mkuu ambao mwanzoni ulikuwa utoke kwa jina lake lakini baadaye akaamua utoke kwa jina la Yusuph Halimoja kwa wajumbe wote wa kamati kuu. Ballile naye akajiandaa kuchapa ripoti hiyo Mtanzania ndio maana habari ya Mtanzania ya Juni 29 kama nilivyowadokoza siku chache zilizopita ilikuwa na taarifa za ripoti hii kuwa ilimkandamiza Dr Slaa(hiki ndicho Ballile alitaraji kitokee lakini hakikutokea). Badala yake taarifa ya wazee ndio ikachukua uzito na hatimaye ikapelekea Chacha kusimamishwa.
Sasa kuhusu taarifa ya Mziray, pamoja na kuwa ilifika dodoma bila kupitia sekretariati mwenyekiti Mbowe akiamini katika demokrasia alikubali ijadiliwe(kwa mujibu wa wachambuzi hili lilikuwa kosa la kisiasa la mbowe).
Taarifa hiyo ilijikita katika kusema CHADEMA kuna ubaguzi wa ukabila, elimu na dini. Kwamba CHADEMA inapendelea zaidi wasomi katika kugawa nafasi za utumishi makao makuu na hata viti maalumu. Pia taarifa ili eleza kuhusu ukabila kwa kutumia takwimu zilizotajwa hapo juu.
Mjadala ulipoanza ikabainika kwamba Kamati ya Mziray iliandika taarifa za uwongo kabisa na majungu kwa kutoa takwimu na hoja za uwongo. Kura zikapigwa na wajumbe 29 wa Kamati Kuu wakaikataa hiyo taarifa kama si nyaraka ya chama(total dismissal). Wajumbe wawili tu wakapiga kura za ndio, Mwenyekiti wa kamati Mziray na mjumbe wa Kamati Mzee Shilembi wa Shinyanga. Hata wajumbe wengine wawili wa kamati hiyo waliikataa ripoti hiyo, Katibu wa Kamati mama Sophia Khatau alipiga kura ya hapana na Wakili Mbogoro Mjumbe wa kamati naye alikataa kwa kuwa hakushiriki kwenye vikao vya Kamati. Mjumbe mmoja toka Pemba wa Kamati hiyo alifariki kabla ya Kamati kuwasilisha kazi yake.
Sasa kwa kuwa Mkakati wa Rostam kuichafua CHADEMA hususani Dr Slaa ulijikita katika ripoti hiyo na walitarajia kuwa ndio njia ya kumuondoa Dr Slaa, wakafanya kikao tarehe 29 Dodoma na kukubaliana kati ya Ballile na Rostam kwamba waitoe ripoti hiyo bado pamoja na kuwa imekataliwa na ili isionekane ni Rostam Rai na Mtanzania zijikite katika kumnukuu Chacha Wangwe akizungumzia ripoti hiyo kuwa ni maoni ya wanachama, na gazeti la Majira liichape ripoti yote kama ilivyo.
Ripoti hiyo iliandaliwa na Mziray katika kile kinachoitwa Kamati imewahoji viongozi na wanachama 42 wa CHADEMA. Alipotakiwa kuwasilisha majina ya waliohojiwa na Kamati kuu akasema wamewahoji viongozi 31 tu na alipotakiwa kutoa majina yao hakuwa nayo, ila Bwana Mziray alikiri mbele ya kikao cha Kamati Kuu ya Chama hicho kuwa kati ya aliowahoji ni pamoja na Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi bwana Kaborou.
Kikao cha jana pamoja na mambo mengine kilikubaliana kwamba Rostam atoe fedha za ziada kwa ajili ya ripoti hiyo kusambazwa nchi nzima kwa ajili ya kumchafua Dr Slaa na CHADEMA.
Kama nilivyowaahidi, nitawaletea taarifa kuhusu kikao cha kesho kadiri nitakavyozipata
PM