Rostam aibukia kanisani!

Mambo ya kiroho ni magumu sana

DHAMBI zote zasameheka isipokua tu ile ya kumdharau ROHO MTAKITIFU

Kama Baba mwenyewe na Mwana mtakatifu ni sawa ama Wakuu kuliko Roho Mtakatifu, kwa nini hiyo iwe ndio dhambi isiyosameheka?

Na kwa nini kuwe kuna dhambi isiyosameheka?
 
Rostam Ni Muislam Huu Ni Unafiki Analake Jambo Anatoa Rushwa Kumba Spika Kwa Mlango Wa Nyumba.wana Kkkt Chukueni Hela Hiyo Mungu Kampa Uwezo Wakuja Kuleta Hela
Anajipendekeza Kwa Spika

Spika asikubali!
Mbona hakwenda kanisani kwa MWAKASEGE?
Ama aliogopa nini? Inabidi akaombewe na mapepo yatoke maana anasema kuhusu amani kupotea na huku kila mtu akijuwa wazi kuwa yeye ni namba moja kwenye UFISADI na ndio anayetaka tuipoteze amani hiyo kwa kueneza udini na ukabila kwa kutumia makada wa ccm pamoja na MAPANDIKIZI YAO!
 
Kama Baba mwenyewe na Mwana mtakatifu ni sawa ama Wakuu kuliko Roho Mtakatifu, kwa nini hiyo iwe ndio dhambi isiyosameheka?

Na kwa nini kuwe kuna dhambi isiyosameheka?

Kwani Rostam kaenda kuomba msamaha ama ametoa pesa na kusema AMANI IOMBEWE KWA TAIFA?

Sasa mtuhumiwa top aje kutoa milioni saba kanisani na huku akisema amani iombewe,je alishawaambia waumini hao kuwa ni kwanini kutuhumiwa kwake ni upotevu wa AMANI?
Na ndio maana msimamo wangu ni kwamba...WAZIRUDISHE PESA HIZO HADI RIPOTI ZITAKAPOSOMWA NA UAMUZI KUTOLEWA NA BUNGE!
 
Tusichanganye mambo ya SIASA na KIROHO

Hukumu zote ziwe za kisiasa (yaliyo yake kaizar) Na hukumu za kiroho (Mungu) tumuachie yeye.

Kukataa zaka tayari ni hukumu ya kiroho inamaana hapo huyo Pasta kasimama nafasi ya MUNGU kumhukumu RA.

Enyi watu wa mataifa kuweni waelevu kama NYOKA
 
Tena nawaembieni muombapo jifungieni ktk vyumba vyenu kwani Baba aliye juu awaona na hakika mkifanya hivyo sara zenu zitapokelewa.
 
Hapana...Ujumbe ulioambatana na fedha ndiyo fedheha!
Unakumbuka Rudy Giulliani alipozikataa pesa za Sultan wa Saudi Arabia kwasababu tu ya kauli yake kuwa marekani bado wanahitaji kuwa makini?
Pale pale ground ZERO Giulliani akazikataa dola milioni kumi za Prince!
 
Tena nawaembieni muombapo jifungieni ktk vyumba vyenu kwani Baba aliye juu awaona na hakika mkifanya hivyo sara zenu zitapokelewa.

Msingi wa haki uko kwenye sheria na si kanisani!
Huko kanisani ni politics tu!
Sheria ni mahakamani na bungeni....Huko chachi ni mwendo ule ule wa kujisafisha!
Walianza na ukabila na udini ukagoma...Sasa ni ziara za makanisani na misikitini...Subirini muone..Mambo ni tight kwani JK mwenyewe yuko huko G8 summit na akishatoka huko na majibu ama maamuzi ya ripoti zote!
Kama ni wote wameguswa basi watajiuzulu..Kwani tumeshawapa ushauri na wamegoma!
 
Ni lile anaposali Spika Samwel Sitta... (KKKT Kinondoni).

Aichangia kwaya Tshs Milioni 7...

Amalizia na kuwaomba waumini kuiombea nchi kwani iko kwenye kipindi kibaya cha watu kutafutana uchawi na kuonesha hali si shwari nchini.

Zaidi tusubiri kutoka vyombo vya nyumbani kwani walikuwepo wengi. Wasipoandika tutaandika!

Makanisa nayo kwa kukumbatia majambazi ndio wenyewe, hivi kuna haja gani ya kupokea michango ya watu kama Rostam?

Makanisa hayo hayo yanamweka viti vya mbele fisadi Mkapa. Pia walisema JK katumwa na mungu, makanisa siku hizi yamegeuka kuwa biashara. Ni aibu kweli kweli.
 
Msingi wa haki uko kwenye sheria na si kanisani!
Huko kanisani ni politics tu!
Sheria ni mahakamani na bungeni....Huko chachi ni mwendo ule ule wa kujisafisha!
Walianza na ukabila na udini ukagoma...Sasa ni ziara za makanisani na misikitini...Subirini muone..Mambo ni tight kwani JK mwenyewe yuko huko G8 summit na akishatoka huko na majibu ama maamuzi ya ripoti zote!
Kama ni wote wameguswa basi watajiuzulu..Kwani tumeshawapa ushauri na wamegoma!

Kanisa halifuati sheria za dunia hii ,kanisa sheria zake kofi la kushoto mpe la kulia pia,akikunyanganya shati mwachie na joho pia.

MIsingi ya haki ni UPENDO wapendeni adui zenu ,maana mkipendana ninyi kwa ninyi nao wapendana wao kwa wao na tofauti yenu na wao itakua ipi??
 
Rostam anajaribu kujiosha lakini hiyo sabuni haitaweza kumtakasa kabisa. Kitu ambacho kitaweza kumtakasa ni yeye kujisalimisha mahakamani hata kama kesi itakuwa haijafunguliwa dhidi yake. Auambie umma kupitia mahakama uchafu wote ambao amekuwa akifanya yeye na washirika wake, aombe msamaha, arudishe pesa zote I mean ZOOOOTE kwa watanzania. Kisha hasijitetee kupunguziwa kifungo, JAJI ndio ataangalia sasa huyu mtu anastahili kifungo cha miaka 20 au zaidi. Akifika jela watanzania au wairan wenye nia njema na yeye watamtumia mtumishi wa Mungu huko gerezani ili amsaidie katika sala za kutubu kwa Mungu. Watanzania tutamsamehe kwa kumlambisha miaka 20 au zaidi iwapo atakubali kurudisha pesa zetu na kueleza upupu wake wote.
 
Kanisa halifuati sheria za dunia hii ,kanisa sheria zake kofi la kushoto mpe la kulia pia,akikunyanganya shati mwachie na joho pia.

MIsingi ya haki ni UPENDO wapendeni adui zenu ,maana mkipendana ninyi kwa ninyi nao wapendana wao kwa wao na tofauti yenu na wao itakua ipi??

Kwa mantiki hiyo unawataka waumini wamchaguwe tena ili aendeleze ufisadi kwa kutumia huo mfano wa sheria ya dini ya kuachiana na joho?

Yani sasa washaachiwa mali zote za nchi...Na hivyo milioni saba ni kibao na sasa upande wa pili wa shavu ni upi huo?

Na shati ndio kiwira na Richmond...Joho itakuwa nini tena?

Ama kibao ndio ufisadi? Hakuna upande mwingine wa shavu wa kupiga na hakuna joho la kumwachia mnyang'anyi!

Wametuacha uchi na yatima...Hawawezi kutupora kingine chochote na hatuna kingine cha kuwapa zaidi ya uhai wetu ambao hata hivyo inavyoelekea wanataka tuamini kuwa uko mikononi mwao na si mikononi mwa Mungu.

Milioni saba zitatupa amani? Ama utazilinganisha na mabilioni ya dola walizokwapua? Milioni saba si ela ya kula tu kwa watu kama yeye?

Jibu ni BIG NO!

Je Migodi yetu na mali nyingine ikiwa ni pamoja na mabilioni ya dola vitatupa amani...

Jibu hapa ni BIG YES...ONLY KAMA TUKIZIKA TOFAUTI ZETU ZA KIDINI NA KIKABILA NA ADUI YETU KUWA MMOJA....MFISADI!
ni saa ya UHURU!
 
Yaliyo ya Kaizar mpeni kaizar na yake Mungu mpeni Mungu.

RA mhukumuni kwa sheria zenu za kikaizar Na msimulazimishe Pasta amuhukumu kwa sheria ya Mungu
 
Yaliyo ya Kaizar mpeni kaizar na yake Mungu mpeni Mungu.

RA mhukumuni kwa sheria zenu za kikaizar Na msimulazimishe Pasta amuhukumu kwa sheria ya Mungu

Sheria za Mungu ndizo makanisa wanazozifuata kama hawawezi kuzitekeleza basi wanakuwa ni wanafiki maana mahubiri yao na matendo yako yametofautiana kama usiku na mchana.
 
Sheria za Mungu ndizo makanisa wanazozifuata kama hawawezi kuzitekeleza basi wanakuwa ni wanafiki maana mahubiri yao na matendo yako yametofautiana kama usiku na mchana.

Sheria za Mungu ni kuwa HAKIMU mtoa hukumu ni yeye tu yani Mungu na sheria yake nyingine ni Usihukumu maana kipimo chahukumu ukitoacho ndicho hichohicho utachopimiwa.Na akohoji wakiona je kijiti kilicho ndani ya jicho la rafiki yako yumkini ktk jicho lako kuna boriti??
 
Jamani kazi ipo! Ufisadi hadi makanisani! Hivi hawa watu wa kanisa la Kinodnoni wanatupa mfano gani????? Hivi wameshindwa kumwamini mungu wao kuwa atawaletea hizo fedha mpaka wanasafisha mafisadi! Huyo mchungaji kwa kweli awajibishwe. Kanisa ya kanisa lazima ifanywe na waumini, na kama waumini hawafanyi basi hapo hakuna uhai wa kanisa!!!!
 
Habari za Kitaifa Habari zaidi!
Rostam aliangukia Kanisa
Mwandishi Wetu
Daily News; Monday,July 07, 2008 @00:01

Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz amesema taifa liko katika wakati mgumu katika siasa na jamii na ameomba watu watumie makanisa kulirejesha katika mstari sahihi. Rostam alitoa kauli hiyo Dar es Salaam jana katika sherehe ya uzinduzi wa albamu ya kwaya ya Amkeni ya Usharika wa Kinondoni wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), ambako alikuwa mgeni rasmi.

Alisema waumini wa dini hawamtuhumu mtu, hawamshutumu, hawapendi wenye wivu na wenye chuki bali wanapenda haki na hivyo ni vizuri wakaitumia fursa hiyo kuliombea taifa. "Nawashukuru kwa kunialika kuwa mgeni rasmi leo hii…ni ishara kwamba mmeamua kupuuza vijimaneno na upuuzi wa vijiweni.

Nafurahi kuwa miongoni mwenu….hamtuhumu, hamshutumu, hampendi wenye wivu na wenye chuki, mnapenda haki. Ninao watoto watatu na nataka niwalee katika misingi hii,'' alisema Rostam huku akishangiliwa na umati wa watu waliofurika katika hafla hiyo. Alisema inasikitisha kuwa katika zama hizi watu wanachukiana hadi kufikia hatua ya kuzushiana uchawi na kuombeana vifo.

"Tutumie makanisa kukemea vitu hivi ili kurejesha taifa katika mstari ulio sahihi,'' alisema. Mbunge huyo ambaye katika siku za karibuni jina lake limekuwa likitajwa katika mijadala mbalimbali bungeni alisema licha ya matatizo ya kisiasa yanayolikabili taifa sasa, kuna matatizo ya jamii ambayo alisema ni vizuri yakashughulikiwa kama ya ndoa kuvunjika, kuongezeka kwa watoto wa mitaani, madanguro, kukithiri kwa matumizi ya dawa za kulevya na mengine yanayoongeza mmomonyoko wa maadili.

Katika hafla hiyo Rostam alitoa mchango wa Sh milioni tano kuchangia seti za vyombo vya muziki za kwaya ya Amkeni na jenereta yenye thamani ya Sh milioni 2.6. Mwaka 2005 Aziz alichangia ujenzi wa jengo la Kanisa hilo ambalo sasa linatumika kama sehemu ya Chuo Kikuu cha Tumaini.
 
Sheria za Mungu ni kuwa HAKIMU mtoa hukumu ni yeye tu yani Mungu na sheria yake nyingine ni Usihukumu maana kipimo chahukumu ukitoacho ndicho hichohicho utachopimiwa.Na akohoji wakiona je kijiti kilicho ndani ya jicho la rafiki yako yumkini ktk jicho lako kuna boriti??

Sheria zilizowekwa zikiwa ni za Watu...Then ni sheria za Mungu!
Kama ni HAKI...Then HAKI ni SHERIA!
Sauti ya watu ni sauti ya Mungu.
Hatuwezi kusema kama kipindi hiki ni kile cha Musa jangwani!
Sheria zote za Duniani zimetokana na AMRI KUMI ZA MUNGU!
Sasa Sheria ndio haki kwa Mtanzania aliyopewa na MUNGU NA si MILIONI SABA NA VITISHO!
 
Wanatuibia mabilioni halafu pesa hizo hizo wanazotuibia wanazitumia kujijengea majina na sifa ambazo hawastahili. Huyu RA ni wa kuogopa kama ukimwi, yeye kishakuwa tajiri wa kupindukia kupitia ufisadi alioufanya sasa anaona maji yamemfika ya shingo anazitumia pesa hizo hizo alizozipata kwa njia za haramu kujitafutia umaarufu asiokuwa nao. Watanzania tusimuonee huyu aibu bali lazima tumwambie ukweli bila kuficha.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom