Rose Kamili awalipua Anna Abdallah, Mudhihir Mudhihir na mke wake kwa ufisadi

Kwa sababu ya passion ya kuzalisha, kusambaza na kutoa habari, nitakuwekea hapa chini. Lakini hata hivyo nafikiri kama wewe ni mvivu wa kusoma, basi automatically unakuwa ni mvivu wa kufikiri, conclusion yake ni kwamba umejiondolea sifa ya kuwa Great Thinker. Karibu usome hapa;

9.1 Bodi ya Korosho na Matumizi Mabaya ya Fedha za Wakulima
Mheshimiwa Spika, kwa kukazia hoja ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, naomba nitoe mfano wa Bodi ya Korosho jinsi inavyowanyonya wakulima wa Korosho katika Mikoa ya Lindi, Mtwara,Pwani na Ruvuma kwa kujilipa posho nyingi na marupurupu mengine huku wakiwaacha wakulima wa korosho wakiteseka na kuhangaika huku na huko kama kondoo wasio na mchungaji bila kutatua matatizo yao.

Mheshimiwa Spika
, bodi ilipokea kiasi cha shilingi bilioni 2 kati ya mwezi Oktoba 2011 na Januari 2012 kutokana na ushuru wa mazao ya nje(Export levy) ya korosho kwa msimu wa 2010/2011. Kiasi hicho kilikuwa ni kwa ajili ya shughuli za kuendeleza tasnia ya Korosho nchini.

Mheshimiwa Spika,
kwa masikitiko makubwa fedha hizo hazikutumika kufanya shughuli kama ilivyotarajiwa na badala yake zilitumika kugharamia vikao vya bodi ya wakurugenzi na safari za viongozi (management ya bodi) ambazo hazijaleta tija kwa tasnia nzima kama ilivyokusudiwa.

Mheshimiwa Spika, hayo yanapata ushahidi kutokana na matumizi ya kulipa posho kwa wajumbe wa bodi wanaounda Kamati ya ajira na uwekezaji ambayo wajumbe wake ni wanne, lakini aliwekwa na mke wa mjumbe katika malipo.

Mheshimiwa Spika, kwa kikao cha siku moja kilichofanyika tarehe 29/11/2011 wajumbe wa bodi hiyo walilipwa posho kama ifuatavyo:

1. Mh. J. Bwanausi – Mjumbe wa Bodi: Huyu alilipwa jumla ya shilingi 1,550,000/=, ikiwa shilingi 750,000/= ni posho ya kawaida (Per diem) na shilingi 800,000 ni "working session" kama ilivyoandikwa kwenye fomu ya malipo.

2. Mh. Anna M. Abdallah – M/Kiti wa Bodi ya Wakurugenzi: Huyu alilipwa jumla ya shilingi 1,800,000/= kwa mchanganuo ufuatao: Posho ya kikao shilingi 500,000/=, Usafiri shilingi 300,000/= Posho ya kawaida (Per diem) shilingi 900,000/= na Usafiri Dar es Salaam shilingi 100,000/=

3. Mh. Jerome Bwanausi – Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi: Huyu alilipwa kwa mara nyingine tena kwenye kikao hicho hicho jumla ya shilingi 1,550,000/= ikiwa posho ya kikao ni shilingi 400,000/=, Usafiri wa Ndege shilingi 300,000/=, Posho ya kawaida(Per diem) shilingi 750,000/= na Usafiri Dar es Salaam shilingi 100,000/=

4. Mh. Mudhihir M. Mudhihir – Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi: Huyu alilipwa jumla ya shilingi 1,550,000/= ikiwa posho ya kikao ni sh. 400,000/=, Usafiri wa Ndege sh. 300,000/= Posho ya Kawaida(Per diem) sh. 750,000/=, Usafiri Dar es Salaam sh. 100,000/=

5. Mrs. Mudhihir M. Mudhihir – Mke wa Mh. Mudhihir M. Mudhihir: Huyu alilipwa jumla ya shilingi 875,000/= kwa mchanganuo ufuatao: Posho ya kikao sh. 200,000/=, Usafiri sh. 300,000/= Posho ya kawaida (Per diem) sh. 375,00/=

Mheshimiwa Spika,
Jumla ya fedha zote zilizolipwa (kwa watu watano) katika kikao hiki cha wakurugenzi wa Bodi ya Korosho cha tarehe 29/11/2011 ni shilingi 7,325,000/=

Mheshimiwa Spika, licha ya matumizi ya fedha hizi kuwa hayana tija kwa kuwa matatizo ya wakulima wa korosho hayajapatiwaufumbuzi hadi sasa, utaratibu walioutumia wajumbe hawa kujipatia fedha hizi una dalili za kifisadi ndani yake. Hii ni kwa sababu mke wa Mh. Mudhihir M.Mudhihir ambaye si mjumbe wa kikao aliingia kwenye kikao na kulipwa posho. Utaratibu uliotumika kumlipa mke wa Mudhihir haueleweki na hata viwango vilivyotumika kukokotoa malipo yake pia havifahamiki.

Mheshimiwa Spika, dalili ya ufisadi mwingine katika bodi hii, ni kwa Mjumbe wa bodi Mh. Jerome Bwanausi kulipwa posho hiyo mara mbili. Katika fomu za malipo kwa Mh. Bwanausi, fomu moja ameandika jina lake kwa kifupi yaani J. Bwanausi na tarehe ya kuchukua fedha ameandika ni tarehe 28/11/2011 wakati katika fomu ya pili ya malipo ameandika jina kamili yaani Jerome Bwanausi na tarehe ya kuchukua fedha kaandika 29/11/2011.

Mheshimiwa Spika, mazingira kama hayo, yanaibua hisia kuwa Mh. Bwanausi alijipatia fedha hizo kwa njia ya udanganyifu na hivyo kuwaaminisha watu kuwa alitumia nafasi yake kama mjumbe wa bodi ya korosho kuchukua fedha za wakulima wanyonge wa korosho.

Kambi ya upinzani, tunaitaka serikali kutoa majibu juu ya bodi hizi za mazao na utaratibu wa kulipana posho ukoje?Aidha tunamtaka mkaguzi na mthibiti Mkuu wa serikali kufanya ukaguzi maalum (special audit) kwenye matumizi ya bodi hii .
Duh, harafu mijitu inakazana CDM wanataka sifa za bure bure, wanachokifanya CDM nikuwafungua watu macho! Hili la kufungua macho watu likishapita, nadhani mnafahamu kinachofuata.
 
ingesaidia sana ungechuja yale ya msingi sio kila mtu ana muda wa kusoma taarifa ndefu.

kile uchokiona kina maslahi ya wengi kuliko kingine kwenye taarifa hiyo ungetupa na sisi.

Niko busy sina muda wa kusoma.
wewe kama huwezi kusoma potezea, kwani lazima usome? imewekwa hotuba yote jinsi ilivo chambua mwenyewe acha uvivu! ushauri mwingine download uwe unasoma kidogokidogo yumkini utaambulia mawili matatu!
 
ingesaidia sana ungechuja yale ya msingi sio kila mtu ana muda wa kusoma taarifa ndefu.

kile uchokiona kina maslahi ya wengi kuliko kingine kwenye taarifa hiyo ungetupa na sisi.

Niko busy sina muda wa kusoma.
Hakuna anayekulazimisha wewe kusoma.. yeye kaweka, wewe chagua unachotaka kusoma.. vipi wewe??!! Acha porojo mama!! ebo!!
 
Mheshimiwa Spika, kwa namna ya kipekee napenda kumshukuru Kiongozi wa Kambi ya Upinzani na Mwenyekiti wa Chama makini cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Makamanda wenzangu wa chama hiki makini cha watu. Aidha napenda kuwashukuru Watanzania wote wenye mapenzi mema na nchi yetu.


KUMBE YALE YALIYOKO MAHAKAMANI NI HUYO MKUU NDIO ANAYECHEZA NAYO? UBARIKIWE SANA KAMNDA MBOWE KWA UAMUZI WAKO HUU WA BUSARA SILAA HATUFAI ENDELEEN KUMUWEKA UCHI ILI ARUDI KANISANI TUJE KUKEMEA MAPEPO YAKE

Wachungaji "fake" utawatambua hata kwa maneno yao tu, huitaji kusubiri vitendo.
Sina sababu ya kutoamini kwamba hao kondoo wa Bwana unaowaongoza unawapeleka motoni, na katika hili unahitaji kuombewa kwakuwa una pepo mchafu. Pepo tokaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!
 
Duh, harafu mijitu inakazana CDM wanataka sifa za bure bure, wanachokifanya CDM nikuwafungua watu macho! Hili la kufungua macho watu likishapita, nadhani mnafahamu kinachofuata.

Hii imenikumbusha kauli ya kamanda Kigaila kwamba ccm ni nyumba ya mapanya; baba mwizi, mama mwizi, mtoto mwizi, shangazi mwizi, mjomba mwizi, babu mwizi, bibi mwizi, shemeji mwizi, wifi mwizi, mjukuu mwizi hata na binamu naye mwizi.

sasa hili nalo waseme liko mahakamani halipaswi kuzungumzwa bungeni!!
 
Mr. & Mrs.Mwizihiri Mwizihiri wala msiogope hizi pokopoko za hapa jf,kula mali nchi hii haina mwenyewe. Msisahau kuomba uraia wa Marekani kwani saa ya ukombozi haiko mbali.
 
Back
Top Bottom