Rose Kamili amemsafisha Dr. Wilbrod Slaa. Hongera Rose Kamili na wenzako mliofanikisha hilo

Hii kutoka kwa kanoni ya ndoa ya kanisa katoliki ndani yake kuna vipingamizi vingi ila mie nime copy haka kakipengele ili wadau mtoe wasiwasi. kama sio mvivu tembelea link hii:CATHOLIC ENCYCLOPEDIA: Canonical Impediments

(c) public decorum (honestas publica), a legal anticipation of affinity; those who will be related by the consummation of marriage are already looked upon as related when they are betrothed or have only ratified the marriage contract. This impediment is as extensive as affinity, if it springs from a reception of the Sacrament of Matrimony; if it arises solely from betrothal it extends only to the first degree;

MkamaP, ulitakiwa usoma kwanza hapo kwenye red kabla hujaenda huko uliko-bold text. Na angalia neno linalotumika "affinity' au unata kusama linamaansha 'kurekebisha?
 
MkamaP, ulitakiwa usoma kwanza hapo kwenye red kabla hujaenda huko uliko-bold text. Na angalia neno linalotumika "affinity' au unata kusama linamaansha 'kurekebisha?

af·fin·i·ty(
schwa.gif
-f
ibreve.gif
n
prime.gif
ibreve.gif
-t
emacr.gif
)
n. pl. af·fin·i·ties1. A natural attraction, liking, or feeling of kinship.
2. Relationship by marriage.
3. An inherent similarity between persons or things. See Synonyms at likeness.
4. Biology A relationship or resemblance in structure between species that suggests a common origin.
5. Immunology The attraction between an antigen and an antibody.
6. Chemistry An attraction or force between particles that causes them to combine.

Mkuu mie hapa nilitaka kukuonyesheni kuwa kuna kufunga ndoa na kurekebisha ndoa. Hata hivyo sijaelewa unataka kusema nini zaidi.


 
af·fin·i·ty(
schwa.gif
-f
ibreve.gif
n
prime.gif
ibreve.gif
-t
emacr.gif
)
n. pl. af·fin·i·ties1. A natural attraction, liking, or feeling of kinship.
2. Relationship by marriage.
3. An inherent similarity between persons or things. See Synonyms at likeness.
4. Biology A relationship or resemblance in structure between species that suggests a common origin.
5. Immunology The attraction between an antigen and an antibody.
6. Chemistry An attraction or force between particles that causes them to combine.

Mkuu mie hapa nilitaka kukuonyesheni kuwa kuna kufunga ndoa na kurekebisha ndoa. Hata hivyo sijaelewa unataka kusema nini zaidi.

Kama hukuelewa uliniwekea hizo notes za nini? kwanza ziko nje ya context. Sijui knowledge kwenye mambo ya kanisa katoliki ikoje!
 
Ukijikita kusoma ukaachana na porojo haya mambo hayakupi shida. Ukisoma utagundua kwamba Padri Jean-Bertrand Aristide aliacha na akawa Rais wa Haiti mwaka 1991 na 1996. Askofu Fernando Lugo aliacha uaskofu na akawa Rais wa Paraguay kuanzia August 15, 2008 hadi wiki tatu zilizopita.

Ushabiki wa imani ya kidini ukiambatna na chuki dhidi ya ukatoliki ni mbaya sana. Lakini mwisho wa siku, kama mtoa hoja alivyosema, hushia kwa mpinga u-RC kuumbuka. Labda ni vyema kujiuliza why failure? Ni wazi kanisa Katoliki lina watu wanaotumia akili zaidi ktk kukabiliana na maisha duniani! Na hili ndilo linalowatofautisha na imani nyingine zote duniani!
 
Yaonekana huyu askofu mwenye sakata la kutiwa ndani kwa ufisadi wa kontena ni Bahalinha Aloysiuuuuus vile wakati ule akiwa jimbo la Geitha vile.
 
Ndugu Nikupataje, nimekuelewa saana. Sisifii but watu waliowengi huwa wanatatizwa sana na habari nyingi zitokanazo na kanisa. Huwezi kuweka mvinyo mpya kwenye vyombo vya zamani unajua matokeo yake. Wakati wa ujio wa Papa nilikuwepo T.E.C. Dr. Slaa kwa nafasi yake ya Katibu wa T.E.C. na kashfa hizo angekuwa keshatolewa mapema asiendelee na matayarisho hayo. Kwa nini aliendelea hadi mwisho na Papa kuondoka nchini? He worked so hard those days. Ziara ikafana na kuwa historia hapa nchini. Nikupataje, unajua waliowengi wanamikashfa mingi. Sasa wanajitahidi kutafuta pa kutokea. Na hao wanaowatetea mafisadi lazima kwa namna moja ama nyingine wanafaidika na ufisadi huu na ndio wanaouliza maswali ya kitoto kama Slaa mumeo na mengineyo mengi.
 
slaa is beyond many...no wender he has done all these stuffs and yet he has followers
 
Dr. Slaa, badili dini uwe MWISLAMU........ Ongea na masheikh wew na huyo MUSHUMBUSI muwe waislamu.

Sisi tutakikaribisha vizuri sanaaaaaa......chonde, hukunhakuna shida hizo,ndoa tunakufungisha kiurahisi sanaaa!!!!""""""


Uliza mwenzako.JK ana.wake wangapi, anafaidi ile mbayaaaaaaa!!!!!!"""""
 
Na Dkt Slaa ameacha shughuli za kanisa tunamtegemea kuongeza rekodi ya kuwa rais Tz
Ukijikita kusoma ukaachana na porojo haya mambo hayakupi shida. Ukisoma utagundua kwamba Padri Jean-Bertrand Aristide aliacha na akawa Rais wa Haiti mwaka 1991 na 1996. Askofu Fernando Lugo aliacha uaskofu na akawa Rais wa Paraguay kuanzia August 15, 2008 hadi wiki tatu zilizopita.
 
Probelm ni kwamba kitabu kitakatifu hakijatoa ruksa ya DIVORCE and there is nobody to change that.

And there is no way padri akaenda kufunga ndoa kanisani. Ngoja tuone hayo mambo ya ndoa yamekaaje maana kuacha upadri ni kitu kimoja na kuoa ni kingine.
 
nakupongeza kwa kuandika makala ndefu lkn tatizo ni kwamba MAKALA YAKO INAKINZANA NA KICHWA CHA HABARI. kwanza theory ni mbili. hii ya rose siyo theory. ilijulikana kwa muda mrefu sn! sikuelewi unapo sema rose kumshitaki slaa ni kumpa ushindi! ushindi upi!? naona kama ni kumuumbua na kumshushia heshima. elewa kuwa mambo mengi yameibuka kuhusu suala la rose. inasemekana baada ya idadi wa wabunge wa viti maalumu kutoka kilmanjaro , arusha na manyara kuwa kubwa, slaa alishauriwa asimuweke rose kwenye viti hivyo lkn hakusikia. rose kamili amekua diwani wa ccm kwa miaka 10.inasemekana slaa alimpa ubunge ili kumfanya akae kimya kuhusu uhusiano wake na mama ishumbisha (sp).

hii inaonesha kuwa slaa anaweza kutoa na kupokea hongo. jambo la pili ni kwamba mtu ambae ni padri tena katibu wa baraza la maaskofu, kuratibu ziara ya papa na kupeana nae mkono eyapoti, huku anajua kuwa na kimada rose, haipendezi. kama ni kweli kuwa alifunga ndoa ya serikali mwaka 1997, hali ya kua ni padri, basi hana uchamungu hata chembe. mimi ni muumini wa kawaida lkn siwezi kuoa mwanamke serikalini! slaa sidhani kama kashfa hizi zinampandisha chati. vilevile kumuiiba mke wa ishumbisha ni jambo la aibu. above all amezaa naye. ana watoto 2 na rose, huyu mtoto wa uzeeni wa nini? sina HAMU WITH THIS FOOLISH SLAA!

Labda unieleweshe, Rose Kamili yeye ansema kuwa kwa kuwa aliwahi kuzaa na Slaa na kuishi nae basi kiserikali tayari ni mumewe. Sio kwamba walifunga ndoa, lbda hili inabidi tutafiti zaidi.
 
Labda unieleweshe, Rose Kamili yeye ansema kuwa kwa kuwa aliwahi kuzaa na Slaa na kuishi nae basi kiserikali tayari ni mumewe. Sio kwamba walifunga ndoa, labda hili inabidi tutafiti zaidi.

Unajua watanzania wamekuwa na uvivu kubwa wa kusoma kiasi kwamba inatisha. Kitu ambacho ni cha kusoma kwenye vitabu tukageuza neno likawa ni kutafiti (research).

Imefika mahala sasa hata neno research limepoteza essence yake kwa sababu kitu kidog tu mtu anakimbia na kusema anaenda kukifanyia research.

Mwanafunzi wa Form two akisoma Physics kwa kutumia Abbot na Nelkon utamwita anafanya research kwa sababu anapekua vitabu!

Hebu tuache uvivu wa kusoma, tuone kama kuna mtu atakatiza kudanganya hiki au kile.
 
Si ajabu Hiyo ni kesi ya janja janja. Rose ana nia njema sana na Slaa. Hiyo kesi ni gia yao kupata jukwaa la kusafishia majina yao. Huenda Huyu mama atatumia mbinu za Hilary kumsfashisha "mumewe" kikamilifu . Na Slaa nae atamsafisha Rose ili watengenenezeane njia!!!
 
Mimi napenda kuamini kwamba kama kuna watu wawili - mmoja akisema "kuku" na mwingine akaisema "siyo kuku ni bata" - mimi mtu wa tatu niliyesikia siwezi, kwa kutegemea kauli hizo mbili, niseme aliyesema "kuku" kakosea. Hivyo, kwa Rose kusema alichosema na kwa vile hatujasikia akikisema tangu walipoachana na Dr Slaa na amekuja kukisema leo siwezi, kama ninataka kuwa neutral, kuamini kama ni kweli au si kweli. Mahali ambapo hatuna sababu ya kuamini kuwa ni kweli ni lazima tu'suspend judgement' ili kujiridhisa.

Mambo ya ndoa yana mambo mengi sana wakati mwingine unachokisikia siyo kile kilichofanyika. Nasema hivi kwa sababu nilishafanya utafiti kwa watu ambao ndoa zao zimevunjika nikajifunza mambo mengi. Niliongea na watu 400 uso kwa uso. Nilitumia miezi 2. Nilikuwa naanza asubihi hadi jioni. Habari nilizozipata ni "amazing". Kuna mfano mmoja niutumie bila kutaja wahusika na kwa kubadilisha mazingira. Ndoa x ilivunjika. Mume alidai sababu ilikuwa y. Mke alidai sababu ilikuwa z na watu waliowafahamu (ikiwa ni pamoja na ndugu) walidai sababu ilikuwa w. Hivyo, majibu yakawa matatu y, z na w. Sasa nani kati ya hao alisema ukweli au sababu zote tatu zilikuwa kweli?

Kuhusu 'theories' unazosema ni kwamba, hakuna maisha ambayo yana'attract speculations' kama maisha ya upadri na utawa. Na 'speculations' nyingi zinahusu fedha (wizi), pombe (ulevi) na wanawake/wanaume (uasherati). Kuna mfano mmoja wa padri x. Ilidaiwa kuwa ana lala kwa mke wa mtu na waumini wakasema wana ushahidi wa kuona kwa macho yao na wakasema wataenda kutoa ushahidi kwa askofu. Habari zikawa habari na kukaundwa kamati ya kwenda kuonana na askofu kuhusu jambo hilo baya.

Askofu aliposikia hivyo, ilibidi achukue hatua. Padri huyo alikuwa wa shirika na siyo wa jimbo. Mapadri wa shirika wanakuwa chini ya 'major superior' na si askofu. Mapadri wa jimbo ndio wako chini ya askofu. Sasa alichokifanya askofu ni kutoa taarifa kwa mkuu wa shirika la yule padri akisema hamtaki jimboni mwake akidai ndani ya siku mbili awe ameshaondoka parokiani.

Padri akafunga mizigo yake kwenda shirikani kwao ili mkuu wa shirika aamue kifanyike nini. 'Most probably' ilikuwa kumrudisha kwao (nchi anakotoka). Habari zikawafikia watu wengi na hata yule mama. Maskini! Kumbe gari la padri lilikuwa linafanana na gari la mume wa yule mama, ambaye alikuwa akifanya kazi Afrika Kusini na akawa amekuja likizo kwa wakati huo. Na gari lake alikuwa akilipaki nje maana nyumba yao ilikuwa haina uzio ila ilikuwa kama mita 100 hivi kutoka barabara kuu.

Sasa waumini walipokuwa wanaona lile gari waliamini ni gari la yule padri. Kumbe haikuwa hivyo. Lilikuwa la mume wa yule mama. Baada ya ukweli kubainika wale waumini walijiona hawafai maana walitoa "ushahidi wa kudhania" - haukuwa na ukweli wowote ingawa wakati wanaongea na askofu walidai "wana ushahidi wa kuona kwa macho yao".

Mimi niseme, ukweli wa mambo ya Rose Kamili na Dr Slaa wanayajua wao kwa undani kuliko jinsi tunavyoweza ku'speculate'. Na kwa vile baadhi yetu 'speculations' ndizo zinazonoga kuliko ukweli, nawaomba tuendelee ku'speculate'!

Upupupu masaburi tu.
 
Kabla ya July 2007 ni wachache sana walikuwa wakiithamini Habari ya sababu za Padri Wilbrod Slaa kuacha utumishi wake wa upadri. Binafsi hadi kufikia mwaka 2007 nilikuwa na theory kama tatu zote toka vyanzo Tofauti vikieleza ni sababu gani ilimfanya Dr. Slaa akaachana na shughuli za kanisa.

Theory ya kwanza niliyoisikia ilikuwa ni kwamba amempa mwanamke mimba na hivyo yeye mwenyewe akaamua kuachana na mambo ya misa akaomba kurudi uraiani ili akajenge familia yake. Theory hii mimi nilisikia katikati ya mwaka 2006

Theory ya pili niliambiwa kuwa alipokuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu (TEC) alifanya ufisadi wa hali ya juu. Ufisadi wenyewe ni ule wa kula hela za ujio wa Pope John Paul II hapa nchini September 1990 na hivyo Kanisa likamuondoa. Theory hii niliisikia mwishoni mwa mwaka 2007 baada ya yeye kutangaza list ya mafisadi pale Mwembeyanga.

Theory ya tatu niliyoisikia huwa siisikii ikisemwa hadharani ni kwamba Dr. Wilbrod Slaa alikorofishana na askofu mmoja ambaye ninalihifadhi jina lake. Ugomvi haukuanza na huyo askofu. Bali ni kwamba huyo askofu alikuwa na ndugu yake pale TEC na huyo ndugu alikuwa ni mmoja wa wakuu wa kitengo cha misaada kiitwacho CARITAS.
Tatizo likawa kwamba yule jamaa wa CARITAS akawa anatumia jina la Kanisa na misaada ile kupitisha maslahi yake kama vile makontena. Padri Wilbrod Slaa kama Katibu wa TEC akagundua hilo na akachukua hatua za nidhamu kwa huyo jamaa.

Kumbe ambalo Padri Slaa hakujua ni kwamba yule jamaa hakuwa peke yake, alikuwa anashirikiana na askofu huyo ambaye jimbo lake liko kanda ya ziwa Victoria. Askofu yule akapata habari ya kusimamishwa yule staff wa CARITAS. Akamjia juu Padri Slaa.

Padri Slaa akakataa shinikizo la kumrudisha yule fisadi wa CARITAS na hivyo majibizano yakawa makali kati ya Slaa na yule askofu. Ikaonekana wazi kwamba kumbe yule askofu yuko team moja na yule jamaa wa CARITAS.

Kwa sababu mali za CARITAS ni zinasimamiwa na TEC basi hapa katibu wa TEC yaani Padri Slaa akaona huyu naye ni mtuhumiwa mwingine anayepaswa kuwajibika tena kwa ubishi wake. Hivyo, Padri Slaa akaamua Polisi wamweke ndani askofu yule kwa kushiriki ule ufisadi na yule jamaa wa CARITAS.

Kitendo cha askofu kuwekwa ndani kikawashtua na wakawasiliana haraka japo enzi hizo simu za mkononi hazikuwapo lakini Kanisa lina mawasiliano mengi tu wakati huo. Ndipo maaskofu wakati huo wakaingilia na askofu mwenzao akatoka rumande. Hivyo, askofu wa Kanisa Katoliki Tanzania akawa ameonja adha ya kuwekwa ndani kwa muda wa masaa! Rais wa TEC wakati huo akiwa Mrehemu Askofu Samba wa Musoma akaingilia kati na ikaamuriwa kwamba Padri Wilbrod Slaa amefanya utovu wa nidhamu kumweka askofu ndani. Na hili likamuudhi Dr. Slaa akaamua kuachana na utumishi ambako wengi kimakosa huita kuachana na upadri.

Hizi ndizo theory tatu nilizowahi kusikia kuhusiana na sababu za Dr. Slaa kuacha upadri. Narudia kueleza, theory zote hizi ninazijua tangu mwaka 2007.

Sasa tuje kuzichambua theory hizi. Theory ya kwanza imenichukua miaka mingi kuiamini kwani sikuwa namjua Rose Kamili kwani niliambiwa kwamba mwanamke mwenyewe ni mzungu wala si Rose Kamili. Sasa niliposikia kuwa Rose Kamili ni mke wa Dr. Slaa basi nikaanza kutoipa nafasi hiyo theory.

Theory ya pili ya kufisadi hela za Pope sikuwa na vigezo vya kuipinga. Lakini sikushangaa ilipoanza kutumiwa na wanasiasa mfano ni Stephen Wasira alivyoitumia kwenye kampeni ya uchaguzi mdogo huko Arumeru. Lakini hatimaye aliyekuwa Rais wa TEC hadi mwezi uliopita yaani Askofu Jude Thaddaeus wa Mwanza alikana hadharani kwamba Dr. Slaa hajawahi kutuhumiwa wizi wa hela za ujio wa Papa.

Theory ya tatu kwamba Dr. Slaa alimweka ndani askofu nimekuwa nikibishana na wenzangu wengi. Ukweli wanaoijua huwa tunatofautiana na handling ya issue hiyo lakini siyo event. Mtu mwingine kabisa ambaye nilidhani haijuia aliwahi kunieleza kwamba baada ya Dr. Slaa kumweka ndani yule askofu akalalamika kwa Askofu Anthony Mayala wa Mwanza. Mimi nimekuwa nikipinga na kuuliza iweje Dr. Slaa ashitakiwe kwa Askofu wa Mwanz wakati yeye hakuwa Padri wa Jimbo la Mwanza na alikuwa wa Jimbo la Mbulu?

Ninapowauliza hivyo wanakosa majibu. Lakini kukosa majibu maana yake ni kwamba tunakubaliana kwamba Dr. Slaa alimweka ndani yule askofu lakini tunatofautiana kujua hatua zilizofuata.

Utaona kwamba kama kulikuwa na juhudi ya wanasiasa kupeleleza habari za Dr. Slaa kule TEC basi hakika hii theory ya tatu hata kama wakiijua hawataweza kamwe kuitangaza. Kwa nini hawataweza? Kwa sababu Padri kumweka ndani askofu ni kweli unaweza kujenga hoja kwamba ni utovu wa nidhamu. Lakini kizazi cha sasa hakiishii hapo. Watu watauliza sababu ya kujua kwa nini askofu awekwe ndani.

Umati ukipogundua kwamba kumbe Dr. Slaa alimweka askofu kwa sababu ya ufisadi wa CARITAS basi maana yake ni kumpandisha chati zaidi kwamba kumbe Dr. Wilbrod Slaa alianza vita ya ufisadi tangu akiwa kanisani na mafisadi wa huko walimkoma.

Nimesema zote hizi tatu ni theory. Narudia tena kusema hii ya tatu sijawahi kuisikia kwenye vyombo vya habari ila ninaisikia tu kwa wachache sana wanaopenda kujishughulisha na mambo ya Kanisa Katoliki. Tunaijadili kwenye meseji zetu, kwenye vigenge vyetu na inaishia huko.

Lakini zile thoery mbili zimashamwagwa magazetini na wote mnajua.

Nilioongea hapo juu ni history sasa tuje kwenye hoja ya leo. Juzi, Rose Kamili anakuja na hoja mahakamani akisema kuwa alifunga ndoa na Dr. Wilbor Slaa June 18, 1987. Hapa maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba haijulikani kama iko siku Pope John Paul II atakuja kuitembelea Tanzania.

Sanasana kila nchi na kila jimbo mwaka huo walikuwa na mikikimikiki ya kuadhimisha mwaka wa Mama wa Yesu uliotangazwa na Papa huyu January ya mwaka huo.

Mnaopenda nyimbo za Bikira Maria mnakumbusha kipindi hiki ndipo zilitoka kwa wingi na zinavuma hadi leo. Ndiyo ilikuwa kazi kuu ya Kanisa wakati huo.

Sasa, kama Dr. Slaa alifunga ndoa ya kiserikali tarehe hiyo kwanza hapa unapaswa kujiuliza maswali mengi. Je, idara iliyofungisha ndoa hiyo haikujulishwa kwamba huyo mfunga ndoa ni padri wa Kanisa Katoliki? Binafsi ninajua kuwepo kwa mahusiano ya siri kwa mapadri na maaskofu dunian na wanawake lakini ndoa ya siri tena imesajiliwa hii ni habari niliyojifunza.

Tuendelee kuchambua. Pope John Paul II alipokelewa na Rais Ali Hassan Mwinyi pale airport September 01, 1990. Airport iko D'Salaam basi kikanisa askofu aliyemkaribisha alikuwa ni wa Jimbo la D'Salaam yaani Laurian Cardinal Rugambwa akiwa na Msaidizi wake (Coadjutor) aitwaye askofu Polycarp Pengo.
Katibu wa Baraza la Maaskofu aliyekuwaepo ni Padri Wilbrod Slaa.

Hii maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba Pope alikuja nchini ikiwa ni zaidi ya miaka mitatu huku Padri Wilbrod Slaa akiwa kweny endoa na Rose Kamili. Kumbe, wakati sisi tunajua kwamba Katibu wa TEC yuko kwenye jopo la kumkaribisha Pope mwenzetu Rose Kamili anaona kwamba mumewe wa ndoa anamkaribisha Pope tena ndoa yenye watoto wawili tayari.

Rose Kamili amewasilisha mahakamani maelezo kwamba kitendo cha Dr. Slaa kuzaa naye na kufunga ndoa June 18, 1987, kilimfanya aanze taratibu za kuondoka kwenye nafasi za upadri. Hapa Rose Kamili anatufunulia ukweli ambao hatukuujua. Ukweli uliotufanya tuogelee katika kila mtu na theory yake. Wasira alikuwa na theory moja wakati mimi nilikuwa na theory tatu nimezitaja hapo juu.

Kumbe wakati tunaona Padri Slaa anachacharika nchi nzima kuandaa ziara ya Pope basi leo ndiyo tumefunuliwa na kujulishwa kwamba hapohapo alikuwa na process nyingine ya kuanza kuachana na upadri.

Leo nimeona picha za wabunge wa CCM yaani Esther Bulaya, Sofia Simba wakimkubatia Rose Kamili bungeni leo. Siwezi kusema ni kumpongeza au kumfariji au ilikuwa ni issue nyingine. Lakini kama kuna watu nyuma ya Rose Kamili binafsi ninaona kwamba ni walewale ambao hawajui kwamba unapopambana na jambo linalohusisha Kanisa Katoliki basi inabidi ama tukuhurumie au tuone ulivyo na akili nyingi sana hapa duniani.

Kwani wengi hapa duniani ambao hujikuta wamegusa mambo yanayoguswa na Kanisa Katoliki wameishia kuumbuka kwa sababu ya ujinga wao kutojua mengi yanayohusiana nalo. Na wasipojirekebisha wataendelea kuumbuka tu.

Hili la Rose Kamili tayari ninauona ni ushindi kwa Dr. Slaa na kilio kwa wote waliomtafuta kwa scandal za tangu akiwa Kanisani.

Kwa sababu hadi dakika hii kuna wanaocheka wakidhani Dr. Slaa kaumbuka, lakini kwa kweli Rose Kamili katurahisishia kazi kubwa kutujulisha kwamba ni nini kilimfanya Padri Wilbrod Slaa aache upadri na aingine mtaani. Bahati nzuri Rose Kamili haongei bila ushahidi.

Sisi wengine wote na yote tuliyosema hayana ushahidi. Binafsi hadi sasa, niliamini zaidi theory ya kumweka ndani yule askofu kuliko theory zote. Lakini ukiniuliza ushahidi nitakwama, hadi siku yule askofu akisema au Dr. Slaa akisema au hata askofu yeyote akisema, kitu ninachoamini haitatokea.

Niliwahi kumsikia Dr. Slaa kwamba afadhali wamsingizie kwamba alikosana na baadhi ya maaskofu hapo angetetemeshwa kidogo na tuhuma hizo. Pia mlioangalia mdahalo kwenye TV siku mbili kabla ya uchaguzi wa 2010, Dr. Slaa alieleza wazi kwamba alipokuwa TEC, contena lilikuwa likija kwa kutumia jina la kanisa alikwua anaingilia na kwa kusaidian na Usalama wa Taifa walikuwa wanalipiga mnada.

Kwa mimi muumini wa theory ile niliona kana kwamba anautaja mgogoro ule lakini kwa jinsi ambavyo si rahisi kwa mtu baki kuulewa.

Hivyo, nahitimisha kwa kusema kwamba Rose Kamili amemsafisha Dr. Wilbrod Slaa hata kama kuna watu akili yao leo inashangilia kitendo cha Rose wakati akili zao hizohizo zilishangilia tuhuma za Stephen Wasira kule Arumeru kwamba Dr. Slaa alitimuliwa upadri kwa sababu ya kufisadi hela kwa ziara ya Pope John Paul II.

Hongera sana Rose Kamili. Kama kuna wenzio nyuma ya hili naomba uwafikishie hongera zangu kwao hata kama kila mtu katika Jamii Forum atanipinga kwa hili.

Hizo ni research questions, naona zote zinaweza kutoa majibu sahihi. Hiyo ya Rose Kamili kufunga naye ndoa inawezekana ni ndogo zaidi ya hizo zingine kwa sababu pamoja na kufunga ndoa haiukumzuia yeye kuendelea na upadri wake. Nadhani hizo theories zingine zina nguvu zaidi.
 
Back
Top Bottom