Askofu Malasusa: Sijalelewa kuwa Kinyume na Serikali, Sijalelewa kutoitii Serikali

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,990
142,007
Mkuu wa Kanisa la KKKT baba askofu Dr Alex Malasusa amesema alipochaguliwa tu Muumini mmoja alimtumia salamu za pongezi na kusema " mitaani Watu wanasema wewe uko Karibu sana na Serikali"

Askofu Malasusa amesema hawezi kukataa ukaribu wa na Serikali kwa Sababu hukulelewa kwenda Kinyume au kutoitii Serikali

Askofu Malasusa amesema Hayo mbele ya viongozi wakuu wa Serikali na mihimili ya DOLA yaani Rais Samia, Spika Dr Tulia, JM Prof Juma, Katibu Mkuu wa CCM Dr Nchimbi, Waziri wa mambo ya Ndani na RC Chalamila

Source Upendo TV
 
Hana jipya huyu nae, ndio maana nina miaka miwili na zaidi nasali nyumbani tu au online, nasikitika sana sana ameniharibia sana kuhusu maisha yangu ya KKKT
 
Hatimaye zile tuhuma kwamba huyu ni Mamluki ndani ya kanisa leo amezithibitisha mwenyewe

Screenshot_2024-01-21-14-02-58-1.png
 
Chaguo letu walutheri lilikuwa dr.benson bagonza ila wakafanya Yao baada ya kuona TEC wanapeleka moto Sasa dhehebu la pili kwa waumini wengi ilibidi lishikiriwe kwa namna yoyote na mkumbuke Dr.Bagonza na kadinali Rugambwa ni marafiki walioshibana fikiria huo moto
 
Hana jipya huyu nae, ndio maana nina miaka miwili na zaidi nasali nyumbani tu au online, nasikitika sana sana ameniharibia sana kuhusu maisha yangu ya KKKT
Mimi nimeamua kuabudu mizimu kabisa kwa upuuzi wa KKKT kuongozwa na kada wa CCM na afisa kipenyo
 
Baadhi ya dondoo kwenye hotuba zake:-

1. Sikulelewa kuipinga Serikali.

2. Njooni tusemezane. Tusemezane (dialogue) tukiwa na neno.

3. Kama angetafutwa wa kufaa kuwa Mkuu wa Kanisa basi mimi Malasusa nisingechaguliwa.

4. Rais uchaguzi mdogo 2024 tuufanye ufanikiwe.

5. Amani na mshikamano wa kitaifa.

6. Ninaipenda sana serikali yangu.

7. Rais suala la ndoa za jinsia moja tuachia Kanisa.

8. Amzawadia rais kwa kuhudhuria kwenye ibada iliyomsimika kuwa Mkuu Mpya wa KKKT Tz.

Tathmini.
Hotuba yake imemshushia Askofu Dr. Benson Kalikawe Bagonza wa Dayosisi ya Karagwe kitu kizito utosini.

Aidha, hotuba imempa Bagonza angalizo kutathmini nafasi yake ya criticism kipindi hiki ambacho yeye Malasusa anaenda kuliongoza Kanisa.

Malasusa ni kijana wa mjini Bagonza ni kijana wa shambani, kuvumiliana kunahitajika kwa mustakabali na maslahi mapana ya Kanisa na taifa.

Bagonza alikuwa Askofu Juni 15, 2003. Alikuwa Msemaji Maarufu kwenye Makanisa ya Lutheran Western Illinois kwa miaka 7 alipokuwa akisoma katika chuo cha Wartburg Seminary Dubuque.

2020 aliamua kujiimarishia ulinzi binafsi kufuatia kuhisi hakuwa salama.

Malasusa alikuwa Askofu Aprili 17, 2004 na sasa Mkuu wa Kanisa mara 2. Anajuwa kuchanga karata na kujipatia dume zote. Ni Banker hivyo anajuwa hesabu vizuri.

Asilimia kubwa ya wafuasi wa Kanisa hawakukubaliana na Malasusa kurudi kwenye Ukuu wa Kanisa na ikadhaniwa amefanikiwa kwa mkono wa serikali.

Nijuavyo mimi, Kanisa ni Watchdog wa serikali kama lilivyo mhimili wa Bunge. Kanisa pia limepewa jukumu adhimu na MUNGU la kusahihisha utendaji na mwelekeo wa serikali ili amani idumu kazi ya MUNGU isonge mbele.

Malasusa hakuongelea yafuatayo ambayo Bagonza hasingeyaacha:-

Ugumu wa maisha.
1. Sukari 1kg 5,000/
2. Nyama ya ng'ombe 1kg 12,000/
3. Nyama ya nguruwe 1kg 13,000/
4. Nguruwe na ng'ombe wanachuana mtanange wa bei.
5. Samaki 1kg 10,000/ baada ya Ziwa Victoria na Tanganyika kufungwa.
6. Usalama wa Chakula hususan ugavi na bei kutokuwa himilivu.
7. Pengo kubwa la kipato.
8. Uhaba wa nishati unaohujumu jitihada za wananchi kujikwamua na umaskini.

Maridhiano ya kisiasa.
1. Madai ya Katiba Mpya.
2. Mabadiliko ya Sheria ya Uchaguzi.
3. Misighishano ndani ya vyama iliyosababisha kesi Mahakamani.
4. Changamoto za Siasa za Kanisa (Church Politics).

Nini tathmini yako.
 
Mkuu wa Kanisa la KKKT baba askofu Dr Alex Malasusa amesema alipochaguliwa tu Muumini mmoja alimtumia salamu za pongezi na kusema " mitaani Watu wanasema wewe uko Karibu sana na Serikali"

Askofu Malasusa amesema hawezi kukataa ukaribu wa na Serikali kwa Sababu hukulelewa kwenda Kinyume au kutoitii Serikali

Askofu Malasusa amesema Hayo mbele ya viongozi wakuu wa Serikali na mihimili ya DOLA yaani Rais Samia, Spika Dr Tulia, JM Prof Juma, Katibu Mkuu wa CCM Dr Nchimbi, Waziri wa mambo ya Ndani na RC Chalamila

Source Upendo TV

Haelewi mana ya haki,aendeles kuwa upande wa madhalimu ni uchaguzi wake.
 
Back
Top Bottom